Sunday, September 30, 2012

Mchungaji Dr. Emmanuel Kandusi, manusura, mwathirika ahudhuria kongamano la saratani ya tezi dume Washington DC

Katika picha ni Dr. Kandusi akimkabidhi magazeti ya MAN Rais na Mwanzilishi wa Prostate Health Education Network Ndugu Thomas Ferington. Ndugu Farrington naye ni manusura, mwathilika na mhanga wa saratani ya tezi dume.
…………………………………………..
Mchungaji Dr. Emmanuel Kandusi, manusura, mwathirika na mhanga wa saratani ya tezi dume (prostate cancer) na mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus campaign akiwa Washington DC nchini Marekani kwenye Kongamano (Summit) la saratani ya tezi dume linaofanyika katika jengo la Maseneta wa Marekani Russell Hall Capitol Hill.
Katika kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa na waathilika na wanaharakati wa saratani ya tezi dume na baadhi ya Maseneta na Wabunge (Members of Congress) ulijadili pamoja na mambo mengi umuhimu wa kutoa elimu katika jamii juu ya saratani ya tezi dume na umuhimu wa kutoa tiba ya kisasa kwa watu wote na mahali popote.

Kongamano liliohudhuriwa na washiriki takribani mia moja, liliandaliwa na shirika la hiari Prostate Health Education Network la Marekani na lenye makao makuu huko Boston. Shirika hilo linakazia “Knowledge is the best defense against prostate cancer”.
Kongamano liligundua kuwa kwa kutoa elimu katika jamii utawezesha kupunguza magonjwa ya saratani (prevention is better than cure) kwa watu wengi. Watu wakielimika na kupata elimu juu ya hali hatarishi, umuhimu wa kubadili maisha yao kwa kula vyakula asilia, kufanya mazoezi, kujiepusha na utumiaji wa tumbaku wa aina yote, kupiga vita unene hatarishi itapunguza sana watu kupata saratani.
Hii itaokoa nguvu kazi na kuokoa pesa nyingi ambazo zinaweza kutumika kwa maendeleo mengine.

TANZANIA KUTENGA BILIONI 30 KWA AJILI YA KUENDELEZA KILIMO



TANZANIA KUTENGA BILIONI 30 KWA AJILI YA KUENDELEZA KILIMO

Na Rose Kitosio,ARUSHA

TANZANIA imetenga kiasi cha shilingi bilioni 30 kwa ajili ya
kuendeleza kilimo hasa kuwainua wakulima wa vijijini ambao
wanakabiliwa na changamoto kubwa ya wataalamu na maafisa ugani  wa
kilimo .

Hayo yalisemwa jana na waziri wa kilimo chakula na ushirika Tanzania
Christopher Chiza alipokuwa akifunga mkutano wa wadau wa sekta ya
kilimo  wa mapinduzi ya kijani uliomalizika jana  mjini hapa.

Alisema kuwa tanzani a bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya
kukosekana kwa  wataalamu wa kilimo hali inayopelekea wakulima
wadogowadogo hasa wa vijjiini kulima kilimo cha mazoea ambacho hakina
tija kwao .

Aidha alifafanua kuwa kutokana na changamoto hiyo ya kukosekana kwa
wataalamu wa kilimo wakiwemo  maafisa ugani imekuwa ni sababbu kubwa
ya Tanzania kutofikia katika malengo yake muhimu waliyojiwekea hasa
katika sekta ya kilimo .

“Tanzania bado tunakabiliwa na changamoto ya wataalamu wa kilimo na
hii inasababisha wakulima kuendelea tu na  kilimo ambacho hakina tija
yeyote kwao  hivyo hii bajeti tuliyoitenga tutahakikisha wakulima
wanafikiwa na elimu ambayo itawafanya wapige hatua katika kilimo na
pia kupukana na kilimo cha mazoea”alisema Chiza

Kutokana na hali hiyo waziri chiza alisema kuwa kutokana na bajeti
ambayo Tanzania imetenga watahakikisha kuwa maafisa ugani na wataalamu
watapatikana wa kutosha ili iweze kutolewa  elimu ya kutosha kwa
wakulima ambao wanalima kilimo cha mazoea ili waweze kuondokana na
hali hiyo.

Kwa upandea wake waziri wa maji profesa Jummane  Magembe alisema kuwa
kwa sasa kuna uharibifu wa vyanzo vya majiunaotokana na kuchoma misitu
kwa ajili a kilimo ,mila potofu ,uwindaji,kufyeaka maeneo ya vyanzo
,kuchoma mkaa  hivyo kusababisha kutokea kwa mabadiliko ya tabia nchi
ambayo yamekuwa yakiathiri kilimo  cha Tanzania.

Magembe aliongeza kuwa ni vema watanzania wakajikita zaidia katika
kutumia nishati ambazo hazichangii kuleta uharibifu wa mazingira kama
vile nishati ya umeme wa jua ambapo endapo wananchi watatumia nishati
hizo ni wazi kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi hayatakuwepo tena

WENYE UELEWA FINYU, WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA WAPENI MUDA WA ZIADA ILI WAFIKE KWENYE KIWANGO BORA CHA ELIMU



Na Queen Lema, MERU

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki Bw Joshua Nassari, ameishauri Serikali hasa kwa Mkoa wa Arusha kuhakikisha kuwa inaweka mikakati zaidi hasa kwa wanafunzi ambao wanakabiliwa na changamoto ya kuwa na uelewa mdogo, pamoja na kushindwa kusoma na kuandika kupewa muda wa ziada na fursa nyingi zaidi za muda wa masomo ili kuweza kupunguza idadi hiyo ambayo itapunguza changamoto hiyo ambayo inaikabili shule nyingi sasa.


Alisema kuwa kwa sasa wanafunzi ambao hawajui kusoma na kuandika pamoja na wale wenye uelewa mdogo huwa wanaachwa kama walivyo huku muda wa masomo nao ukiwa unaendelea hali ambayo ndiyo inayochangia hata maendeleo hafifu ya Elimu kwa baadhi ya wilaya hapa nchini

Bw Nassari aliyasema hayo wakati wa maafali  tisa ya darasa la saba katika shule ya Fikiria Kwanza  Usa river  wilayani Meru Mkoani hapa mapema jana ambapo pia alisema kuwa ipo haja ya Serikali kuendelea kuwekeza zaidi katika masuala ya Elimu hasa kwa wanafunzi ambao wanakabiliwa na changamoto kama hiyo mkoani hapa.

“tusilie kila siku elimu elimu bali  tunapaswa kuangalia changamot ambazo zinaikabili sekta hiyo tena hasa katika wasiojua kusoma na kundika pamoja na wale wenye uelewa finyu lakini kama wanafunzi hawa tutakuwa tunawaacha kama hasara ya mzazi basi tutakuwa tunaongeza idadi ya Mambumbu ila kama tutaweka  Nia hata kwa kuwapa walimu kazi ya ziada ya kuwafundisha hawa watoto basi kiwango cha elimu kitakuwa kwa kiwango kikubwa sana’aliongeza

Alisema kuwa mbali na changamoto ambazo zinaonekana kuwa chanzo cha kusababisha elimu hasa ya Mkoa wa Arusha kuwa chini pia Serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa inaangalia zaidi shule za Kata kwani nazo zimekuwa shule ambazo zinasahaulika sana na kusababisha hata aina ya elimu ambayo inatolewa ndani ya shule hizo kuwa ni elimu duni sana huku asilimia kubwa ya watanzania wakiwa wanategemea elimu kutoka ndani ya shule hizo

“kwa upande wa Vijijini shule hizi ni tegemeo kubwa sana kwa jamii lakini sasa hapa inaonekana baadhi ya watendaji wa Serikali kukwepa  majukumu yao na kusababisha mfumo wa elimu hizi kuwa chini lakini kama wangekuwa wanazitatua kero mbalimbali basi hata idadi ya watoto wenye uelewa finyu na wale wasiojua kusoma na kuandika nayo ingepungua sana na hivyo kukuza hata kiwango cha elimu ya Meru na Mkoa wa Arusha kwa Ujumla”aliongeza  Bw Nassari

Hataivyo Mkurugenzi mtendaji wa shule hiyo ya Fikiria kwanza Bi Necta Lema alisema kuwa ili kuboreesha suala zima la elimu hapa nchini kwa ujumla nazo shule mbalimbali zinatakiwa kutatua kero za elimu ambazo zipo sanjari na kuhakikisha kuwa wanajiwekea taratibu za kuwapa Motisha walimu mara kwa mara ili kuongeza hata kiwango cha ufaulu kwa haraka sana

Bi Lema alibainisha kuwa kwa sasa zipo baadhi ya shule ambazo zinawasahau sana walimu katika kuwapa Motisha hali ambayo inawafanya walimu wa shule hizo kuweza kufundisha kwa njia ya mazoea tofauti na pale ambapo walimu watakapotangaziwa Motisha kuweza kufundisha  kwa ufanisi wa hali ya juu ili kuwa mfano mzuri kwa shule na hata mbele ya wanafunzi.

“Motisha kwa walimu ni jambo jema sana kwani sisi tayari mpaka hapa tumeshajaribu kuweza kufanya hivyo na matunda tumeyaona hivyo ni jukumu la kila mkuu wa shule kuhakikisha kuwa mbalina kukazania elimu bora lakini kuwa mbunifu na ubunifu huo utachangia sana kuweza kuongeza hata idadi ya wanafunzi ambao wanafranya vema zaidi “aliongeza Bi Lema

WAMILIKI, WAKUU WA SHULE WATAKIWA KUWA MFANO MZURI WA UTUNZAJI WA MAZINGIRA




WAMILIKI, WAKUU WA SHULE WATAKIWA KUWA MFANO MZURI WA UTUNZAJI WA MAZINGIRA



Na Queen Lema, ARUSHA

WAMILIKI na Wakuu wa shule mbalimbali kwa kanda ya kaskazini wameombwa kuwa mabalozi wazuri wa mazingira kwa kuhakikisha kuwa wanawapa fursa wanafunzi mbalimbali kuwa mabalozi  na waelimisha rika kuhusiana na Mazingira ili kuendelea kuhifadhi  mazingira ambayo yanaharibiwa kila mara kuanzia ngazi ya shule.

Mratibu wa shirika la Roots and Shoots la mkoa wa Arusha Bw Japhet Mwanangombe alitoa wito huo wakati wa maafali ya pili kwa waelimishaji rika 191 ambao wameitimu kwa kupata elimu ya sekondari pamoja na elimu ya uelimishaji rika mapema jana.

Alisema kuwa kwa sasa pamoja na kuwa wamejikita kuhakikisha kuwa kila shule inakuwa na vitalu kwa ajili ya kuwaelimisha wanafunzi umuhimu wa kuhifadhi mazingira lakini bado kuna baadhi ya walimu wamekuwa kikwazo kikubwa kwa kutowapa wanafunzi fursa mbalimbalin za kupambana na uharibifu wa mazingira.

Kufuatia hali hiyo alisema kuwa inachangia sana wanafunzi kukosa haki yao ya msingi hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana baadhi ya wanafunzi hao kuwa maadui wa mazingira badala ya kuwa marafiki wa mazingira kwa maslahi ya maisha yao ya baadaye na jamii ambazo zinawazunguka

“tunachoomba ni kuwa baadhi ya wamiliki wa shule pamoja na wakuuu wa shule ambao bado wanaona suala la kuwa na elimu ya mazingira si rafiki sana kwao kwa kweli wanakosea kwani wanasababisha sana hawa wanafunzi wawe na maadui wa mazingira kwa kuharibu hata vyanzo mbalimnbali lakini kutokana na hali hiyo kama shule itashirikiana na taasisi mbalimbali kama yetu  basi watachangia sana ufanisi katika suala la mazingira”alisema

Pia alisema,nazo shule ambazo zipo pembezoni mwa miji nazo hazipaswi kukaa bila ya kuwa na elimu ya mazingira hasa katika mchakato mzima wa Upandaji wa vitalu ndani ya shule zao wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatafuta elimu hiyo kwa haraka sana kwani hali hiyo ya ukosefu wa elimu ya mazingira ambayo inaanzia kuanzia ngazi ya Shule inasababisha sana  mazingira ya Vijijni kuendelea kuharibiwa.

Katika hatua nyingine alisema kuwa Shirika hilo limejipanga kuhakikisha kuwa linaendelea kuzalisha waelimisha Rika wengi zaidi hasa kwenye suala zima la Mazingira kwani mpaka sasa zaidi ya waelimisha Rika 235 wa  wilaya  22 za Kanda ya Kaskazini wameshanufaika na elimu hiyo ambapo hata hali ya uharibifu wa mazingira nayo imepungua ndani ya shule mbalimbali tofauti na hapo awali

“leo hawa Vijana wameitimu ambao pia ni wahitimu wa darasa la saba na kidato cha nne lakini pia wanaelimu hii sasa sisin tunachokifanya ni kuhakikisha kuwa tunawatuma ndani ya wilaya zetu 22 ili wakapunguze huko tatizo la uharibifu wa mazingira ambao unafanywa na baadhi ya wanajamii kutokana na uhaba wa elimu”aliongeza Bw Joseph

Kwa upande wa wahitimu wa uelimishaji rika ambao wameitimu kwa kupata elimu hiyo kwa zaidi ya miaka minne walisema kuwa pamoja na kuwa wamefanikiwa kupata elimu hiyo kwa uraisi sana lakini navyo vijiji hasa vya nje ya Miji vinatakiwa kuhakikisha kuwa wanawatumia ili kupunguza athari mbalimbali ambazo zinajitokeza mara kwa malra ndani ya jamii.

MWISHO

VYAMA VYA SIASA ARUSHA VYATAKIWA KUTOA ELIMU YA URAIA NA DEMOKRASIA KWA VIJANA ILI KUEPUSHA UHARIBIFU WA MALI

VYAMA VYA SIASA ARUSHA VYATAKIWA KUTOA ELIMU YA URAIA NA DEMOKRASIA KWA VIJANA ILI KUEPUSHA UHARIBIFU WA MALI


Na Queen Lema, ARUSHA
VYAMA vya siasa hasa kwa mkoa wa Arusha  vimeombwa kuhakikisha kuwa vinatoa elimu ya Uraia pamoja na umuhimu wa demokrasia  kwenye siasa kwani kutokana na hilo asilimia kubwa ya Vijana wanaharibu sheria hizo bila kujua na kutambua kuwa wanafanya kosa
Hayo yameelezwa na Bi Cristanta  Mwinyi ambaye ni Katibu wa CCM Kata ya Ngararenaro wakati akiongea na vyombo vya habari mara  baada ya kuvamiwa na vijana wa  Chama cha demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)na kuharibu mali zenye thamani ya zaidi ya Laki tano
Bi Mwinyi alisema kuwa pamoja na kuwa wamevamiwa na vijana hao wenye itikadi tofauti hapo juzi bado kuna nafasi kubwa sana ya kuweza kuhakikisha kuwa vijana hao wanajua na kutambua maana halisi ya Demokrasia
Aliongeza kuwa vijana hao ambao si mara ya kwanza kufanya matukio kama hayo wanafanya hivyo kwa kujua kuwa wanashabikia baadhi ya vyama na kuharibu mali ya chama kingine wanavunja hata sheria na taratibu za nchi na pia ni chanzo hata cha mauji ambayo hayana  tija kwa jamii
Alifafanua kuwa endapo vyama vya siasa vingekuwa na tabia ya kuwaonya vijana wake kuacha kuharibu au kufanya fujo kwa vyama pinzani basi siasa ya mkoa wa Arusha ingekuwa inaenda vema tofauti na sasa ambapo siasa imegeuka kama uwanja wa mapambano makali kutokana na itikadi kali
“hawa vijana wanapotoka katika mikutano yao si mara mara ya kwanza kuharibu ofisi hii sasa kama wataendelea hivi kuharibu mali za ofisi hii ni wazi kuwa ipo siku na vijana wetu nao watainuka na hawatakubali na hayo yatakuwa ni mauji ya hali ya juu sasa ni wakati wa Vyama vya siasa kuhakikisha kuwa wanaliangalia suala hili kwa undani sana ili kuepusha madhara kama hayo”aliongeza Bi Mwinyi
Alifafanua kuwa endapo kama Siasa itaenda kistaarabu hasa pale ambapo baadhi ya vijana hao watakuwa wamepata elimu ya Uraia na Demokrasia basi itachangia kwa kiwango kikubwa sana hata kuweza  kuwapa wananchi wengine fursa ya kutumia Demokrasia vema tofauti na pale wenye itikadi moja kwenda nyingine kwani uharibifu huo nao unachangia sana hata Umaskini.
MWISHO

Friday, September 28, 2012

AGRA and SIDA sign US$ 10 million grant agreement to boost Africa-based agricultural entrepreneurs







AGRA and SIDA sign US$ 10 million grant agreement to boost Africa-based agricultural entrepreneurs


Arusha, Tanzania, September 28, 2012 – The Swedish International Development Cooperation Agency (Sida) and of the Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA) announced a US$10 million grant to support the development of Africa-based innovations to boost African agricultural growth.  Mr. Henrik Riby, Representative, Sida and Mrs. Jane Karuku, President of AGRA formalized the agreement this week in a signing ceremony at the African Green Revolution Forum in Arusha. 

The grant, awarded by Sida, will be directly channeled to the African Agribusiness Window of African Enterprise Challenge Fund (AECF), a fund hosted by AGRA.  Administered by the AECF, the grant will enable Africa-based entrepreneurs to submit new and innovative business solutions to accelerate the development of the agricultural sector in Africa. 

Between 10-12 winners will be selected and provided with funding to develop their ideas into practical projects that are both commercially viable and will have a broad developmental impact on the rural poor.  The projects will have a significant focus on the empowerment of women and environmental sustainability.

The grant is part of SIDA’s program area focused on inclusive business and pro-poor economic growth, with investments that must significantly contribute to poverty reduction and rural development.  The grant is expected to benefit at least an additional 60,000 households (300,000 people) with extra income, employment, market access and transfer of know-how.

“We know that a more effective and professional agriculture sector can make a real difference for millions of people living in poverty in sub-Saharan Africa, “said Henrik Riby, SIDA. “By sharing the financial risks of private investments in agribusiness, we hope to encourage new sustainable ways of raising rural incomes.”

The African Enterprise Challenge Fund is an important contributor to AGRA’s goals and strategy, and its impact will be enhanced with this grant from the Swedish International Development Cooperation Agency,” said Jane Karuku. “These projects benefit millions of Africa’s rural poor in very practical ways such as jobs, increased income, knowledge transfer and market access.”
About SIDA
Sida, the Swedish International Development Cooperation Agency, is a government agency under Sweden’s Ministry for Foreign Affairs. Sida's goal is to contribute to making it possible for poor people to improve their living conditions.



NAIBU WAZIRI ASHIKWA NA BUTWAA JUU YA MALIPO YA MKANDARASI UWANJA WA NDEGE KISONGO


NAIBU WAZIRI ASHIKWA NA BUTWAA JUU YA MALIPO YA MKANDARASI UWANJA WA NDEGE KISONGO 

NA ASHURA MOHAMED,ARUSHA

Naibu waziri wa Uchukuzi mhandisi dkt.Charles Tizeba ameiagiza mamlaka ya Viwanja vya ndege(TAA) kukaa pamoja na mkarandarasi wa kampuni ya Harising and Sons ili kukubalina namna ambavyo wanaweza wakafanya marekebisho ya kipande cha barabara cha mita 420 ili mkandarasi huyo aweze kumaliziwa malipo yake.

Ameyasema hayo mara baada ya kufanya ukaguzi katika barabara hiyo ya kurushia na kutua ndege iliyopo ndani katika kiwanja kidogo cha ndege kilichopo kisongo nje kidogo mwa jiji la Arusha.

Dkt.Tizeba amesema kuwa ni vyema kama pande hizo mbili zikakaa pamoja ili kupata muafaka kwa kuwa Mhandisi Mshauri alipendekeza marekebisho yafanyike baada ya msimu wa mvua kumalizika na wamiliki wa viwanja wanahitaji marekebisho yasisubiri msimu kumalizika.

Aidha amefafanua kuwa endapo pande hizo mbili zitakubaliana basi ni wazi kuwa mkandarasi atapatiwa fedha zake zote zilizobakia ambapo amesema kuwa mpaka sasa tayari ameshapatiwa malipo kwa asilimia 60 tu.
naibu waziri wa uchukuzi amesema kuwa mradi huo tayari umeshakamilika kilichokuwa kinasubiriwa ni makabidhiano tu ambapo mkandarasi anaona amefanya kazi vizuri huku mwenye kiwanja anaona hajakamilishiwa uwanja wao.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya viwanja vya ndege injinia White Majula amesema kuwa kuotokana na ubovu wa miundombinu uliokuwepo mamlaka ya viwanja vya ndege imekuwa ikifanya ukarabati wa barabara ya kuruka na kutua ndege kwa kiwango cha lami ambapo kwa mwaka 2011-2012 wamekarabati meta 420 kwa kiwango cha lami ili kukamilisha urefu wa meta 1620 zilizopo.

Pia ametaja baadhi ya changamoto ambazo bado zinahitaji kupatiwa marekebisho mara moja kuwa ni pamoja na Mwiingiliano wa barabara ya magari Arusha-Minjingu na miundo mbinu ya kiwanja ambayo imejengwa ndani ya eneo la kiwanja hivyo kutishia usalama wa kiwanja ambapo licha ya kujadiliwa na Mkoa wa Arusha,TAA,TANROADS na Wizara ya Uchukuzi, bado suala la kuhamisha barabara hiyo halijapatiwa ufumbuzi.

Lakini hata hivyo Injinia Majula amesema kuwa kutokuwepo kwa jengo la Abiria kumeathiri huduma ya kiwanja kutokana na ufinyu wa bajeti,Mmlaka ya Viwanja vya Ndege inaendelea kutafuta wabia kupitia sekta binafsi ili kufanikisha mpango huu.

Kiwanja cha ndege cha Arusha kilianzishwa mwanzoni mwa miaka ya 1950,kikiwa kinamilikiwa na mjasiriamali wa kizungu na kilimilikishwa rasmi serikalini mwishoni mwa miaka ya 1960 ambapo kina barabara moja ya kuruka na kutua ndege ya kiwango cha lami yenye urefu wa meta 1620 na upana wa meta 30 inayotumika kwa ndege zenye ukubwa na uwezo wa kubeba abiria 70 mfano ATR 72.

Mwisho…………………………….

mkutano wa mapinduzi ya kijani wajadili hatma ya wakulima wadogo barani afrika






ALIYEOKO KUSHOTO NI BI BELINDA BILLGATE WAKATI WA KATI NI RAISI JAKAYA KIKWETE, NA WA KULIA NI BW KOFF ANNAN KATIKA PICHA YA PAMOJA MARA BAADA YA KUFUNGUA RASMI MKUTANO WA MAPINDUZI YA KIJANI KWA NCHI ZA AFRIKA MAPEMA JANA, PICHA NA GLADNESS MUSHI, ARUSHA






Na Queen Lema, ARUSHA

KOFFI ANNAN AWATAKA VIONGOZI WA NCHI ZA BARA LA AFRIKA KUHAKIKISHA KUWA WANAPA FURSA MBALIMBALI WAKULIMA WA VIJIJINI ILI KUPUNGUZA ONGEZEKO LA WATU MIJINI

ALIYEKUWA katibu mkuu wa umoja wa Mataifa bw Koffi Annan amewataka viongozi mbalimbali katika nchi za bara la afrika kuhakikisha kuwa wanawajengea wakulima hasa wa vijijini uwezo wa kulima kwa kujiamini ili kuweza kupunguza wimbi kubwa la watu wanaokimbilia zaidi mijini

bw Annan aliyesema hayo leo (Jana) wakati alipokuwa akiongea na vyombo katika mkutano wa mapinduzi ya kijani unaondelea mjini hapa

Aidha bw Annan alifafanua kuwa asilimia kubwa ya wakazi wa vijijini wanakimbilia zaidi mijini kutokana na kukosa misaada ya kilimo huku hali hiyo nayo ikichangia kwa kiwango kikubwa sana ongezeko la watu

Aliongeza kuwa endapo kama viongozi hao watafanikiwa kuwaboreshea wakulima hata maslahi ya kilimo basi watachangia sana hata kuondokana na tatizo la machafuko mbalimbali ambayo yanaendelea kutokea ndani ya nchi mbalimbali za bara la Afrika kutokana na uhaba wa cahakula

'kama hawa viongozi wa bara la Afrika wakidhamiria sana hasa kwa wakulima wale wa vijijini kuhakikisha kuwa wanawapa fursa mbalimbali ambazo sehemu nyingine hamna basi watachangia kwa kiwango kikubwa sana hata kuweza kuweka uhakika wa chakula ndani na nje ya nchi zao lakini kama watakuwa hawawapi fursa basi watachangia sana hata kuweza kuwadidimiza wakulima hao wa chini'aliongeza bw Annan

Katika hatua nyingine alisema kuwa kwa sasa ni muda wa bara la Afrika kuhakikisha kuwa mafanikio kuelekea kufikia malengo ya millenia yanaendelea kuwa ya kuhamsisha zaidi mageuzi ya kilimo ili kuweza kuimarisha hata uchumi wa kijamii kwani kilimo hasa kwa bara la Afrika lina uwezo huo

Mbali na hayo alisema kuwa kwa muda huu ni vema kama kukawa na ushirika bunifu miongoni mwa sekta za Umma na zile binafsi ambapo kupitia sekta hizo zitachangia kwa kiwango kikubwa sana kutoa njia ambazo zinaweza kusaidia kufikia mafanikio ya kilimo hasa vijijini.

Awali Waziri wa kilimo chakula na ushirika hapa nchini bw christopher chizza alisema kuwa kwa sasa nchi ya Tanzania ina mikakai mingi sana ya kuhakikisha kuwa inaboresha kilimo chake kwa kutoa fursa mbalimbali za Kilimo ambacho kina uwezo wa kubadilisha hata Uchumi wa nchi

Bw chizza alifafanua kuwa Serikali ya Tanzania kwa sasa imeweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa wakulima wengi wa sasa wanatumia zaidi kilimo cha Umwagiliaji ambacho ni kilimo cha kudumu tofauti na kilimo cha kutegemea zaidi msimu wa mvua ambao mara nyingine unabadilika badilika na kusababisha hasara kwa wakulima na watumiaji wa mazao mbalimbali

"kwa sasa tumehakikisha kuwa tumejiwekeza zaidi katika aina ya kilimo cha umwagiliaji ambacho ndicho ,kinachoweza kubadilisha hali za wakulima wetu na sisi kama Serikali tumejipanga kuhakikisha wakulima wote wanakubali hili ili kuweza kuinua hata aina ya kilimo chetu'aliongeza bw Chizza.

MWISHO


KAMPENI ZA CHADEMA KWA KATA ZA DARAJA MBILI NA BANGATA KUANZA OCTOBER 3


KAMPENI ZA CHADEMA KWA KATA ZA DARAJA MBILI NA BANGATA KUANZA OCTOBER 3

Na Mery Kitosio, ARUSHA

CHAMA cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) kinatarajia kuanza rasmi kampeni zake katika kata za daraja mbili manispaa ya Arusha  na kata ya Bangata Wilayani Meru mkoani Arusha ambapo kampeni hizo zinatarajiwa kuwa kuanza rasmi October tatu na kuongozwa na  ya aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini Goodbles Lema na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari

Hayo yamelezwa mjini hapa na Katibu wa mkoa wa chama hicho  Amani Golugwa jana ambapo alisema kuwa mpaka sasa wameshafanikiwa kupata wagombea watakosimama katika kinyanganyiro hicho ambacho kitahusisha vyama mbalimbali vya siasa kwa mkoa wa Arusha.

Golugwa alisema kuwa ndani ya chama hicho wamesharidhia wagombea wawili kuweza kusimama ambao ni bw Prosper Msofe ambaye atasimama kama mgombea Udiwani kwa tiketi ya chama hicho  katika kata ya daraja mbili huku kata ya Bangata Meru nayo ikiwakilishwa na Erick Samsoni ambapo pia kampeni za kuchukua kata hizo nazo zitaendeshwa kwa njia ya kitaalamu na kidemokrasia sana.

“hawa watu wawili mpaka sasa chama kimeshawapa baraka zote za kuweza kugombea kwa kata hizi mbili lakini kwa sasa tunatarajia kuhakikisha kuwa kamwe demokrasia ya watanzania haibakwi na baadhi ya viongozi walafi na badala yake tutahakikisha kuwa kila mtu anatumia vema demokrasia yake ili kupata haki zake za msingi”aliongeza  Golugwa

Hataivyo aliongeza kuwa ndani ya kampeni hizo ambazo zinatarajiwa kuanza wiki ijayo chama hicho kamwe hakitamvumilia kiongozi yoyote yule ambaye atakuwa anatoa Rushwa ya aina mbalimbali zikiwemo Rushwa za kutumia magari ya Serikali ndani ya kampeni na badala yake kiongozi atakayefanya hivyo watamuhisha na Rushwa na hivyo chama hicho kitasimamia ukweli kwa kuwafikisha ndani ya Magareza

Awali alisema kuwa mbali na kuanza rasmi kampeni kwa kata za Daraja mbili na Bangata pia chama hicho kimelazimikka kuwapa waraka muhimu chama cha Wananchi Cuf juu ya mapungufu mbalimbali ambayo yanaendelea kutokea katika mji wa Arusha hasa katika harakati zao za mikutano ya Hadhara ambayo inaendelea ndani ya Mji wa Arusha

Golugwa alisema kuwa chama hicho kimekuwa kikitoa malalamiko kadhaa  baadhi ya wanachama wa Chadema wamewafanyia vurugu huku vurugu hizo zikihusishwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini bw Goodbless Lema hali ambayo inasababisha muendelezo wa Siasa chafu ambazo ndizo chanzo kikubwa sana cha ubakaji wa  Demokrasia hadharani.

“Sisi kamwe hatuwezi kuwafanyia hawa Cuf vurugu kwa kuwa tunajua kuwa hilo ni suala la uvuinjifu wa amani ndani ya nchi yetu na kwa maana hiyo tunapenda kuwaambia kuwa tunawapenda na pia tunawakaribisha ndani ya mji wa Arusha ila wasitafute visngizio vya hapa na pale ila watafute hoja ambazo zinajenga na kuimarisha hata Maslahi ya Nchi”alibainisha  Golugwa

Mbali na hilo katibu huyo pia alisema kuwa Cuf inatakiwa kuhakikisha kuwa inakuwa na Matamko ambayo yanalenga kumkomboa Mtanzania na wala sio kuwa na matamko ambayo hayana tija mbele za jamii kama ambavyo wamefanya kupitia Kwa Naibu  Mkurugenzi wa habari uenezi na haki za binadamu, Abdul Kambaya ambaye alitoa matamko ambalo lilikuwa na matisho na lugha isiyofaa kwa nchi na jamii za kitanzania

MWISHO

JAJI NYERERE ASISITIZA WANANCHI KUJITOKEZA KATIKA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Na Ashura Mohamed,Arusha

JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Jaji Aisha Nyerere,amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuweza kujitokeza kwa wingi katika kutoa maoni juu ya katiba mpya.

Aidha mashirika,taasisi zilizo za kiserikali au zisizokuwa za kiserikali kutumia nafasi zao kuisaidia serikali kuhamasisha umma juu ya umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika mchakato huo.

Jaji Nyerere aliyasema hayo juzi mjini hapa wakati alipokuwa akizindua vitabu vya uwajibikaji wa makampuni kwa jamii pamoja na kitabu kinachohusu haki za jamii katika maeneo ya uwekezaji,uzinduzi ulioenda sambamba na maadhimisho ya miak 17 ya Kituo cha sheria na haki za binadamu(LHRC).

“Napenda niwakumbushe watanzania kuwa kwa sasa taifa letu lipo katika mchakato wa kutunga katiba mpya,mchakato huu upo katika hatua za mwanzo kabisa ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi,hivyo kwa kuzingatia hayo napenda kuwahimiza ninyi na raia wengine kushiriki kikamilifu kikamilifu kutoa maoni yenu”

“Kituo cha sheria na haki za binadamu pamoja na watu wengine wenye nafasi na uwezo wa kutoa elimu kwa uumaa kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima,mnapaswa kutumia vema nafasi zenu”alisema na kuongeza
Jaji huyo alisema kuwa watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali hivyo wanapaswa kuungwa mkoni kwani utetezi wa haki za binadamu ni wajibu wa jamii nzima.

“Watetezi wa haki za binadamu wanaweza kuisaidia serikali katika uendelezaji na kulinda haki za binadamu na ni nafasi pekee kutengeneza misingi imara ya kuwatetea na kuwalinda watetezi wa haki za binadamau na kuna nafasi nzuri kama wakati huu wa mchakato wa kuhakikisha kuwa haki za binadamu na matamko mbalimbali ya kimataifa yanaridhiwa na kuwekwa katika katiba mpya kwani hii itakuwa na mchango mkubwa sana katika kulinda haki za binadamu na watetetzi wa haki hizo”alisema Jaji Nyerere

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Dk.Hellen Kijobisimbo alisema kuwa baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa ziliwakabili katika kutekeleza majukumu yao ni pamoja na sheria kwua kandamizi,hata wanapokuwa wanapokuwa wanamsaidia mtu kisheria,sheria zimekuwa zikiwakandamiza.

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni tatizo la mfumo wa mahakama ambapo mashauri yamekuwa yakichukua muda mrefu hadi kukamilika,wasaidizi wa kisheria kutokutambulika.
Dk.Hellen aliongeza kuwa vyombo vya dola navyo vimekuwa ni tatizo kwao kwani wakati mwingine wao wakiwa katika majukumu yao ya utetezi,vyombo vya dola vimekuwa vikiwaona wao ni wapinzani wakati wao ni wasaidizi wa serikali.

Naye Mratibu wa Kitengo cha uwajibikaji wa makampuni na mazingira(LHRC) Wakili Flaviana Charles akizungumza wakati wa uzinduzi wa vitabu hivyo alisema kuwa sheria ya uwekezaji hapa nchini haina vifungu vyenye kutoa wajibu wa wawekezaji kwa wananchi jambo linalosababisha jamii kutokunufaika na miradi ya uwekezaji inavyotekelezwa katika maeneo husika.

Aliongeza kuwa ukosefu wa sheria inayosimamia uwajibikaji wa makampuni kwa jamii umepekelea kuwepo kw augumu wa kuzichukulia hatua za kisheria kampuni zinazoshindwa kutimiza wajibu wake kwa jamii,ambayo imesababisha uwepo kwa migogoro isiyoisha ndani ya jamii.

WAMACHINGA WAGAWANA MAENEO KAMA NJUGU KILOMBERO

NA WAANDISHI WA UPAKO WA HABARI, ARUSHA

KUNDI la wa machinga mjini arusha leo wamevamia eneo la la
wazi lilopo ngarenaro na kujigawia tayari kwa kufanya biashara.

Kundi hilo la wamachinga limevamia eneo hilo ambalo lilikuwa
limezungushiwa mabati kwa kipindi cha
muda mrefu kilichopo ngarenaro jijini hapa wakidai kuwa eneo hilo ni la
serekali hivyo wanaenda hapo hapo kufanyia biashara maana wao wenyewe ni
serekali tosha.



Gazeti hili la nipashe lilifika eneo la tukio na kushughudia
wananchi hao wakiwa wanajigawia sehemu za biadhara huku wengine wakiwa wameanza
kuchimba kwa ajili ya kujenga vibanda vyao.

Wakiongelea tukio hilo baadhi ya wafanyabiashara hao
walisema wameamua kuchukuwa hatua hiyo kutokana na kukosa sehemu za
kwenda kufanyia biashara zao kwani eneo walilopewa
la uwanja wa NMC ni lidogo haliwatoshi wafanyabiashara wote.



Mmoja wa wafanyara
hao aliyejitambulisha kwa jina la Emanuel mushi alisema kuwa wao wamechukuwa
hatua hiyo kutokana na kitendo cha kukosa eneo la kufanyia biashara katika
kiwanja cha nmc huku mkandasi ambaye
amepewa tenda hiyo ya kuwagawia maeneo akiwa awazungusha.

Aidha alisema kuwa wameamua kufanya au kuchukuwa hatua hii
ili serekali ijue machinga arusha hawana mahala pa kwenda na wawaangalizie sasa
sehemu ya kuwaweka ili wafanyie biashara zao



Alisema kuwa wamesubiri kwa muda mrefu na tangu waambiwe
wanagawiwa eneo hilo hawajapatiwa na wamekuwa wakizungushwa tu bila ya
mafanikio yoyote hali ambayo inawafanya wao kuishi kama ndege.



,,leo asubuhi sisi tuliokuwa tumeweka vitu vyetu hapa nje ya
soko la ngarenaro tumefatwa tukafukuzwa kamamaubwa kibaya zaidi watufukuze
wakiwa wametupa sehemu ya kwenda lakini hawajatupa sehemu ya kwenda
wanatupeleka peleka na tulivyoona hivyo na ili eneo tunaliona wazi kila siku
tukaamua kuvamia ili tukae hapa,,alisema Mama rosemary mollel

Waliongeza kuwa sababu ingine ya kutoka katika uwanja huo ni
pamoja ya kuwa uwanja huo hauna miundo mbinu ya kutosha ikiemo choo kitu
ambacho ni tatizo kubwa sana kwa afya zao.

,,unajua eneo lile ni dogo kiukweli ni robo ya wamachinga tu
ndo wameingia katika eneo lile kibaya zaidi askari wanaotufata kutufukuza
tukiwauliza tuende wapi wanasema mtajua wenyewe kila tukaapo wanatufukuza
kibaya zaidi wanatuambia kuwa swali kama hilo msiniulize maana wakati mnakuja
kutoka vijijijini kwenu hamkututaarifu kwakua mlikuja kimnya kimnya basi
ondokeni ivyo ivyo kama ulivyokuja ,,alisema Lukas Seneu.



Machinga hao waliongeza kuwa serekali hii imekuwa ikifanya
kazi kwa kuwakomoa kwani wanadhani kuwa machinga wengi ni chadema hivyo
wanavyofanya hivi wanawakomoa kitu ambacho sio cha kweli na walibainisha kuwa
viongozi hao wa serekali wanawatesa hivi ili warudi kijijini lakini walisema
watapigana mpaka mwisho wake waone

Juhudi za kumpat a kaimu mkurugenzi wa jiji kuzungumzia swala hili
ziligonga mwamba kwani
ofisini hakuwepo na simu zake zote zilikuwa hazipo hewa.

RAISI KIKWETE ASISITIZA SERIKALI KUBORESHA VITUO VYA TAFITI ZA KILIMO ILI VITAFITI MAZAO MBALIMBALI YA KILIMO


RAISI KIKWETE ASISITIZA SERIKALI KUBORESHA VITUO VYA TAFITI ZA KILIMO ILI VITAFITI MAZAO MBALIMBALI YA KILIMO

Na Queen Lema,ARUSHA

RAISI Jakaya Kikwete amezitaka Nchi za bara la Afrika kuhakikisha kuwa zinaboresha vituo mbalimbali vya utafiti wa kilimo kwani kama kila kituo kitafanya vema tafiti zake basi zitachangia kwa kiwango kikubwa sana kuweza kuimarisha Kilimo na kukifanya kiwe cha kisasa zaidi ndani ya nchi mbalimbali ambazo bado mpaka sasa zinakabiliwa na changamoto kubwa ya kilimo duni

Raisi Kikwete aliyasema hayo jana(LEO)wakati akifungua mkutano wa wadau wa mapinduzi ya kijani ya  kilimo kwa nchi mbalimbali za Afrika(AGRA) ambapo alisema kuwa bado sekta ya kilimo katika nchi mbalimbali inakabiliwa na changamoto kubwa sana hali ambayo inatakiwa kutatuliwa kwa haraka sana kupitia vituo mbalimbali vya utafiti wa Kilimo

Alifafanua kuwa kwa sasa kunaitajika sana mapinduzi hasa kwenye taasisi za utafiti kwani hizo ndizo zitakazochochea sana mabadiiliko ya kilimo kutokana na uitaji mkubwa sana ambao upo ndani ya nchi mbalimbali kwa bara la Afrika

Pia alisema kuwa kama vituo hivyo vya tafiti vitapewa kipaumbele basi pia vitachangia kwa kiwango kikubwa sana kuweza kupunguza changamoto mbalimbali ambazo zinakabili sekta hiyo ya kilimo pamoja na wakulima ambao wanaitaji msaada mkubwa sana hasa wa wataalamu wa kilimo ambao wanatokea katika vituo hivyo vya utafiti.


"kwa sasa tuhakikishe kuwa tunajipanga ilivyo kwa kutoa kipaumbele kwa vituo hivi vya utafiti na hivi vituo navyo vinatakiwa kuhakikisha kuwa vinajiwekeza zaidi kwa kuwa bunifu na kutafiti hata mazao zaidi ya mawili kwa mwaka na kama Serikali zetu zitasimamia hivyo basi ni wazi kuwa zitchangia sana hata ongezeko la chakula na vipato vya wakulima hao kwa wingi sana"aliongeza  Dkt Kikwete

Katika hatua nyingine pia alisema kuwa  ili kukuza na kuimarisha sekta ya Kilimo hapa nchini na barani Afrika kwa ujumla wadau mbalimbali wa Kilimo wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatoa mafunzo na elimu zaidi kwa wakulima hasa wale wa vijijini kwani kutokana na uhaba wa elimu asilimia kubwa ya wakulima wanafanya kilimo cha mila na desturi huku hali hizo zikiwa zinachangia kwa kiwango kikubwa sana kudidimiza mazao na kusababisha hata ukosefu wa chakula.

"kama tutawapa hawa wakulima wetu vipaumbele kwa kusisitiza zaidi elimu, na maitaji mengine kwa ajili ya kuboresha kilimo basi wataweza kupiga hatua kubwa sana kutokana na baadhi yao hawana elimu huku jambo hilo likiwa linachangia sana kilimo duni pamoja na umaskini miongoni mwa jamii za wakulima"aliongeza Dkt Kikwete

Naye aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa bw Koffi Annan alisema kuwa ni vema kama  wadau wa sekta binafsi na sekta za umma wakahakikisha kuwa wanawekeza zaidi katika Kilimo ambapo kama watafanikiwa kufanya hivyo basi watachangia kwa kiwango kikubwa sana kuimarisha zaidi kilimo sehemu mbalimbali duniani na hali hiyo itachangia hata uchumi wa Nchi zao
 `
Bw Annan alizitaka Serikali za Nchi za Afrika nazo kuhakikisha kuwa nazo zinakuwa miongoni mwa wawekezaji wakubwa katika kilimo sanjari na kuwa bunifu katika kuwasaidia wakulima wadogo na wakubwa  hasa kwenye maitaji yao muhimu ambayo mara nyingine wanayokosa huku hali hiyo ikifanya kilimo kiweze kudorora na kushindwa kufikia malengo yake mbalimbali.

MWISHO

Tuesday, September 25, 2012

TUME YA KUDHIBITI UKIMWI YASHAURIWA KUONGEZA KASI

 Na Mustafa Leu. ARUSHA

TUME ya taifa ya kudhibiti Ukimwi nchini Tacaids, imeshauriwa  kuongeza kasi zaidi ya mapambano hayo   dhidi ya maambukizi mapya  kwa kutoa elimu  zaidi  kwa jamii iweze kuchukua hatua za kujiepusha  na maambukizi na kusathiri nguvu kazi ya taifa inayotegemewa.

Hayo yameelezwa jana na Afisa tawala mkoa wa Arusha, Exaud Mwanga,alipokuwa akifungua kikao cha siku moja cha viongozi wa madhehebu ya dini mkoani Arusha  kuhusu mwitikio na usahiriki wao  katika mapambano ya ugonjwa wa ukimwi  kilichoaandaliwa na tume ya taifa ya kudhibiyi ukimwi nchini Tacaids.

Mwanga, amesema kuwa serikali inatambua juhudi kubwa  zinazofanywa na madhehebu ya dini  kwa kushirikiana na tacaids   na wadau wengine kwa kutoa ushauri wa kiroho kwa watu waishio na ukimwi ushauri unaowawezesha waliokwisha ambukizwa kuishi kwa matumaini ..

Amesema mchango unaotolewa na madhehebu ya dini  katika kupunguza ongezeko la maambukizi ya ukimwi  ni mkubwa sana ,pamoja na mchango huo kuwa mkubwa bado mahitaji ya elimu ni makubwa  hasa ngazi za kata, vijiji na jamii  na familia yanahitajika ili kupunguza ongezeko la maambukizi mapya  ambapo kwa mijini kiwango cha maambukizi ni asilimia 8.7 na vijini ni asilimia 4.7

Awali Kamishina wa tume ya ukinmwi nchini Askofu mstaafu wa KKKt, Peter Lukumbusho Mwamasika , amesema taasisi za dini  zina wajibu mkubwa  kutoa misaada ya kimalezi, kiafya, kielimu, kiushauri,  kisheria  kwa waathirika  ambao ni waumini wao  ili waepuke kupata maambukizi mapya.

Amesema taasisi hizo za dini  lazima zitambue kuwa zina wajibu wa kuwatunza  yatima na wajane  wasiokuwa na uwezo ambao wanatokana na vifo vya ukimwi ili kuwaanzishia miradi ya kiuchumi na kuachana na tabia ya  kuwaombea dua na kuwaacha waende zao  bila kuwawezesha

Amewaambia viongozi hao kuwa Tacaids ina jukumu kubwa la kuhamasisha watu waeleze mahitaji yao kuhusu mapambano dhidi ya ukimwi  na kuwaepushia kupata maambukizi mapya na kupitia Tacaids, serikali inzifikia taasisi za dini ili ziweze kusaidia kutoa elimkwa wananchi kuhusu madhara ya ukimwi na hatua za kuchukua ili kujikinga na maambukizi mapya.

mwisho

KAMISHENI YA AFRIKA KUSIMAMIA USIKILIZAJI WA KESI ZA MAUAJI YA KIMBARI RWANDA


KAMISHENI YA AFRIKA KUSIMAMIA USIKILIZAJI WA KESI ZA MAUAJI YA KIMBARI RWANDA

Na Nicodemus Ikonko, Hirondelle, Arusha 

Arusha, September 25, 2012(FH) – Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) imehitimisha majadiliano na Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (ACHPR) ili kusimamia usikilizaji wa kesi za mauaji ya kimbari zinazopelekwa kusikilizwa nchini Rwanda.

‘’Hali iliyopo sasa ni kwamba ICTR kupitia ofisi ya Msajili imeshahitimisha majadiliano na ACHPR kusimamia usikilizaji wa kesi,’’ Msemaji wa Mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa, Roland Amossouga aliliambia Shirika la Habari la Hirondelle Jumanne.

Aliongeza kwamba,’’Hati ya makubaliano hayo itatiwa saini hivi karibuni na baada ya hapo ACHPR ndipo itaanza rasmi kazi yake ya kusimamia kesi ya (Jean) Uwinkindi nchini Rwanda.’’

Wafanyakazi wawili wa ICTR waliteuliwa Aprili mwaka huu kama wasimamizi wa muda wa kesi ya Uwinkindi, huku ACHPR ikisubiriwa kukamilisha makubaliano na ICTR kufanya kazi hiyo. ACHPR ina majukumu ya kulinda na kukuza haki za binadamu ikiwa ni miongoni mwa kazi zake.  

Wakati ukitolewa uamuzi wa kuhamishia kesi ya Uwinkindi kwenda Rwanda Juni 2011, Majaji walimwelekeza Msajili wa Mahakama ICTR kuingia katika mkataba wa maandishi na ACHPR ambao utaeleza wazi maslahi, fedha zinazohitajika na mambo mengine muhimu ambayo yatafanya taasisi hiyo kuweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Kwa mujibu wa majaji ‘’ACHPR itatakiwa kuwasilisha ripoti ya mara kwa mara kila baada ya miezi mitatu juu ya hali ya mwenendo wa kesi kwa Rais wa ICTR kupitia kwa Msajili wake, wakati kesi itakapoanza kusikilizwa hadi hapo itakapohitimishwa ikiwa ni pamoja na hatua ya rufaa kwa mshitakiwa na pia katika hatua ya kusimamia adhabu itakayotolewa, kama itakuwepo.’’

Majaji waliridhika kuwa hatua ya Kamisheni hiyo kusimamia mwendendo mzima wa kesi utatoa hakikisho kwamba ukiukwaji wowote wa haki ya mshitakiwa katika mwenendo wa kesi yake utapelekwa mbele ya Rais wa ICTR mara moja ili hatua za kurekebisha zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kufikiria kuiondoa kesi hiyo kusikilizwa mbele ya mahakama za Rwanda.

ICTR tayari imeridhia kesi nane kwenda kusikilizwa nchini Rwanda. Uwinkindi, ambaye ni mchungaji alihamishiwa nchini Rwanda Aprili 19, 2012, akiwa ni mshitakiwa wa kwanza wa ICTR kesi yake kwenda kusikilizwa nchini humo.

Nje ya Uwinkindi, kesi nyingine zilizohamishiwa nchini Rwanda ni pomoja na mtuhumiwa ambaye bado anashikiliwa na ICTR na kiongozi wa zamani wa wanamgambo wa Interahamwe, watuhumiwa sita ambao bado wanasakwa, wakiwemo mameya watatu, polisi mmoja, afisa wa zamani wa jeshi na meneja mmoja wa mgahawa. Hata hivyo kesi nyingine mbili bado zipo mbele ya Mahakama ya Rufaa zikisubiri uamuzi.

wanafunzi wa ilboru waandamana



Joseph Ngilisho,Arusha


WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Ilboru iliyopo Arumeru mkoani Arusha,wameandamana katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha,wakishinikiza mkuu wao wa shule ,Jovinas Mutabuzi aondolewe kwa madai kwamba amekuwa akichangia kudorora kwa elimu shuleni hapo.

Wakitoa madai yao leo mbele ya mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo,majira ya saa 2 asubuhi ,wamemtuhumu Mutabuzi kwenda kinyume na utaratibu wa shule hiyo ikiwemo kuwatimua ovyo walimu wao wanaodai walikuwa wakiwafundisha vizuri,kuwanyanyasa na matumizi mabaya ya fedha za shule.

Aidha wamebainisha kuwa mkuu huyo ameshiriki kuwagawa wanafunzi  kiitikadi za kidini  na kisiasa, kuwatoza faidi ya shilingi 150,00 hadi 190,000 pindi wanapotenda kosa ikiwemo kuchelewa wanapokuwa likizo ama wanapo kuwa na ruhusa ya kwenda kanisani ama msikitini.

Madai  mengine ni ufujaji wa fedha za umma zinazotolewa na wahisani ama wadau wa elimu wakishirikiana na mhasibu wa shule hiyo,ukarabati duni wa shule,miundo mbinu mibovu,wizi wa mali za umma,bodi ya shule isiyoeleweka,kudorora kwa taaluma,matumuzi mabaya ya fedha  na wanafunzi kudhalilishwa.

Akiongea kwa niaba ya wenzake kiongozi wa serikali ya wanafunzi hao(HP),Didas Mselle alimtaka mkuu huyo wa mkoa kuwapatia jibu la mara moja juu ya utekelezaji wa madai yao ikiwemo kumwondoa  mkuu wa shule hiyo kwani hawamtaki.

Alisema  wamekuja katika ofisi hiyo ya mkuu wa mkoa kwa lengo moja la kupata utatuzi wa madai yao ambayo wamedai yamekuwa ya muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi huku wanafunzi hao wakiendelea kunyanyasika na kusababisha baadhi yao kushuka kielimu kutokana na ufundishwaji mbovu huku idadi kubwa ya walimu wakitimuliwa mara kwa mara.

Wanafunzi hao wameenda m,bali zaidi wakimtuhumu Mutabuzi,kuiendesha shule hiyo kibabe kwa sheria zake huku akitumia simu yake ya mkononi kama M pesa ya kutumiwa fedha zinazotokana na adhabu ya wanafuzi hao.

‘’kwanza tunashangaa shule yetu inaakaunti tatu lakini mkuu wetu anaataka tumtumie fedha kwenye namba ya simu ya mhasibu wake hili suala haliwezekani kabisa kwani hata risiti hatupewe’’alisema

Akijibu hoja hizo mkuu huyo wa mkoa, aliwasihi wanafunzi hao kuacha jaziba na kurudi shuleni kuendelea na vipindi vya masomo kwani  hoja zao zitafanyiwa kazi na kwa kiasi kikubwa zimeonekana kuwa za msingi.

‘’mmekuja hapa kwa lengo la kuwasilisha kero zetu sasa tumezisikia ,tumezichukua na tunazifanyia kazi,rudini shuleni tutatuma viongozi wetu kufuatilia madai yenu na kuyapatia ufumbuzi ikiwemo kusikiliza upande mwingine’’alisema Magesa Mulongo.

Naye mkuu huyo wa shule hiyo,Jovinas Mutabuzi alipotafutwa kwa njia ya simu ya mkononi ili kujibu tuhuma hizo alisema kuwa madai hayo hayana msingi wowote na yamejaa uchochezi na kueleza kuwa wanafunzi hao wanamsukumo wa kisiasa na mara nyingi wamekuwa wakishiriki matendo maovu na  wanapokemewa ikiwemo kupewa adhabu wanasema wananyanyaswa .

Wanafunzi hao waliweza kutawanywa na askari polisi waliowaamuru warondoke na kurudi shuleni baada ya amri ya mkuu wa mkoa kuitoa ,hata hivyo hakuna vurugu yoyote iliyotokea.
Mwisho.

mbunge Anjela Kairuki,amehaidi kuwasadia waongoza utalii



Na  Mustafa  Leu,  Arusha.

MBUNGE wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia kundi la wafanyakazi, Anjela Kairuki, ameahidi kuwasaidia waongoza utalii kupata stahili zao mbalimbali ikiwemo kuboreshewa maslahi na kuondokana na manyanyaso wanyaopata kutoka kwa wamiliki wa kampuzi za utalii.

Kairuki, ametoa ahadi hiyo jana baada ya kumalizika kwa kikao cha pamoja na Waongoza utalii katika hotel ya Naura, ambapo waongoza utalii hao walitoa kilio kwa mbunge huyo kutokana na manyanyaso wanayopata ikiwemo kulipwa ujira mdogo wa shilingi 80,000 kwa mwezi na kupewa posho ndogo ya shilingi kati 10,000 na 1500 ya   kujikimu wawapo safarini katika mbuga za wanyama  na kulala kwenye Hoel zisizokuwa na viwango huku wakila chakula kibovu..

Kairuki, ambae ni naibu waziri wa Katiba na Sheria,  alisema ameenda  kuwasilikiliza kama mbunge na kwa kutambua kuwa ametokana na  kundi la wafanyakazi hivyo atawasaidia ili kuona manyanyaso yanatoweka na waweze kufanya kazi kwa ufanisi ili kuboresha sekta ya utalii nchini.

Amesema  anasikitishwa na viwango wanavyolipwa kutokana na kazi ngumu ya kuongoza watalii wawapo mbugani  huku wakiwa hawana mikataba ya hiari ya ajira kama sheria ya kazi mpya ya mahusiano kazini ya mwaka 2004  inavyoelekeza kila mwajjiri awe na mkataba wa hiari na mfanyakazi wake ili aweze kupewa stahili zake.

Amesema atahakikisha kuanzia sasa atashirikiana na waziri wa kazi na vijana,waziri wa Maliasili na Utalii, kusimamia makampuni hayo  uwepo wa mikataba ya hali bora ya wafanyakazi wa makampuni ya utalii na sekta zingine ili kuywaondolea manyanyaso

Kwa upande wao waongoza utalii hao kupitia Chama chao cha Tanzania Tour guides associatio, TTGA ,walimwambia waziri kuwa hawana mikataba ya ajira, wanalipwa maslahi duni, hawana bima na wakipata ajali hufukuzwa kazi   hivyo wanaomba iwepo sheria ya kuwalinda na kuwabana waajiri.

Wamesema tatizo ni makampuni mengi ya Utalii nchini kumilikwa na baadhi ya mawaziri na viongozi wa serikali hivyo kuwafanya wao wasiweze kulipwa ujira mzuri na hawana pa kupeleka malalamiko yao.

Wamesema kuwa waongoza watalii ndio mabalozi wazuri wa kuelezea utalii hapa nchini kwa sababu wanatumia 80% ya muda wakiwa na watalii mbugani wanatoa maelezo sahihi kwa wageni  na wageni huwa wanapokwena makwao huwa wanarejea na kuleta wageni wengine.

Wamesema Sekta inayoongoza kwa utalii hapa nchini ni ya uopiga picha hivyo sekta hiyo ni muhimu lazima ipewe thamani zaidi .Maeneo mengine waliyolalamikia ni kufungwa kwa baadhi ya njia ndani ya hifadhi hivyo kuwasababishia usumbufu, ubabe wa askari wa hifadhi, kutozwa faini  hawaruhusiwi kula meza moja na wageni wawapo porini kitendo ambacho ni cha ubaguzi na dharau kwao .

Baadhi ya Hotel kutoa chakula kibovu, malazi duni matandiko yamechakaa vitanda vibovu vyumba visivyofaa kulala binadamu.kulipwa ujira mdogo huku wamekabidhiwa magari ya mamilioni ya fedha
```````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````

Thursday, September 20, 2012

DKT ASHA MIGIRO KUWA MGENI RASMI BARAZA LA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA

Na Queen Lema ,Arusha

ALIYEKUWA naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa Dkt Asha Rose Migiro
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kuzindua baraza la viongozi wakuu wa
serikali za mitaa la Afrika Mashariki linalotarajiwa kuzinduliwa mjini
arusha kuanzia septembaer 24 ambapo mkutano huo utaudhuriwa na mawaziri
wa serikali za mitaa na viongozi wa juu wa serikali za mitaa kutoka nchi zinazounda
jumuiya ya afrika mashariki.

Hayo yalielezwa na mkuu wa kitengo cha mawasiliano kutoka Ofisi ya Waziri
Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) bi Rebecca Kwandu
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mjini hapa.



Alisema kuwa kupitia mkutano huo utaweza kuwawezesha viongozi wakuu wa
serikali za mitaa wa nchi wananchama kuzindua baraza la viongozi wakuu wa
serikali za mitaa la Afrika Mashariki yaani “The East African Local
Government Forum” ambapo kupitia baraza hilo wataimarisha utendaji wa
serikali za mitaa na utekelezaji wa dhana ya ugatuaji wa madaraka kwa umma
kwa lengo la kuleta maendeleo endelevu katika kanda ya afrika mashariki



“tunatarajia kukutana mjini hapa kwa lengo la kuwawezesha viongozi wakuu
kuzindua baraza la viongozi wakuu wa serikali za mitaa la afrika mashariki
ili kuwawezesha kufanya kazi kwa pamoja katika kuimarisha utendaji wa
serikali za mitaa hii itawasaidia kwa kiwango kikubwa kudumisha umoja
katika hata utendaji wa kazi zao”alisema bi Rebecca.



Aidha alieleza kuwa kupitia mkutano huu viongozi wa Serikali za Mitaa
watapata nafasi nzuri ya kubadilishana uzoefu kuhusu namna ya uwakilishi wa
wananchi unavyofanyika kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa kama vyombo vya
Uwakilishi wa wananchi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.



Alisema kuwa mkutano huo utazihusisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda. ambapo pia nchi
za Visiwa vya Comoro na Sudan ya Kusini zimealikwa kushiriki.

Aidha aliwataja washiriki wengine wa mkutano huo ni wadau wa maendeleo
ambao ni Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Mfuko wa
Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNCDF) na Shirika la Maendeleo la
Ujerumani(GIZ).


MWISHO

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA MAPINDUZI YA KIJANI


na gladness mushi,arusha

TANZANIA inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa jukwaa la mapinduzi
ya kijani Afrika utakaofanyika kuanzia septemba 26 hadi septemba 28
mjini Arusha utakaokutanisha viongozi mbali mbali wa kimataifa
ambao watajadili namna ya kuchukua hatua katika kuboresha usalama wa
chakula duniani .

Aidha katika mkutano huo viongozi hao wataweza kujadili sera ya
mapinduzi ya kilimo na uchumi wa Afrika ,njia za kukuza masoko pamoja
na namna ya kubadilisha mfumo wa kilimo.


Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Rais wa umoja wa
mapinduzi ya kijani Afrika (AGRA) bi Jane Karuku alisema kuwa
mkutano huo ni hatua inayofuata katika kuendeleza bara la Afrika
kupata ufumbuzi katika masuala ya usalama wa chakula.

Karuku alisema kuwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo katika
kukuza sekta ya ukuaji wa kilimo inawakilisha uchunguzi uliofanywa
katika wilaya ya kilombero mkoa wa morogoro juu ya njia bora za
kilimo.


Alieleza kuwa uchunguzi huo uliwezesha uzalishaji wa mahindi kwa
wakulima wadogo wa wilaya hiyo kuongezeka kutoka tani 1.5 hadi 4.5 kwa
hekta ,ambapo kwa upande wa mavuno ya mpunga yaliongezeka kutoka tani
2.5 hadi tani 6 hali iliyopelekea Tanzania kupata fursa hii ya kuwa
mwenyeji wa mkutano huo.


Aidha alisema kuwa jukwaa hilo litatoa nafasi ya kujadili namna bora
ya kuendeleza mipango ya uwekezaji wenye tija kwa ajili ya kuongeza
maendeleo ya kilimo barani Afrika pamoja na kujadili namna bora ya
kuunganisha nguvu ya jamii na sekta binafsi katika kuboresha usalama
wa chakula duniani


Aliongeza kuwa jukwaa hilo pia litaweza kujadili na kutafuta njia bora
za kuboresha kilimo barani Afrika na kuwawezesha wakulima wadogo
wadogo kushirikiana na vyama vya ushirika na wadau wengine ambapo
mjadala huo utatoa njia bora za matumizi ya rasilimali na kukabiliana
na changamoto zinazowakabili mamilioni ya wakulima barani Afrika.


“Wakulima wadogo wadogo ni kitovu kwa yale yote tuyafanyayo hivyo
mtazamo wetu ni kuwapatia wakulima wa afrika dhana za kilimo
wanazohitaji ili waweze kukua zaidi na kuongeza kipato chao na
watatuongoza katika kupata mafanikio mazuri”Alisema bi Jane.

WATU ZAIDI YA 500 WAMEFARIKI DUNIANI MKOANI ARUSHA KUTOKANA NA AJALI

WATU ZAIDI YA 500 WAMEFARIKI DUNIANI MKOANI ARUSHA KUTOKANA NA AJALI

Na Queen Lema, ARUSHA
IMEELEZWA kuwa kutokana na changamoto mbali mbali za uasalama barabarani kwa mkoa wa arusha zimesababisha zaidi ya watu 441 kupoteza maisha kutokana na ajali za magari huku watu zaidi 120 nao wakipoteza maisha kwa ajili ya ajali za pikipiki kwa kipindi cha januari 2010 hadi agost 2012.

Hayo yalielezwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani kwa mkoa wa arusha bw Mwakyoma Marison wakati alipokuwa akizungumza na wadau mbali mbali wa usalama barabarani katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama kwa mkoa wa arusha mapema jana.

Alisema kuwa ajali hizo zimetokana na vyanzo mbali mbali ambavyo vinafahamika na jamii ya mkoa wa arusha ambapo ni pamoja na uzembe wa madereva, uzembe wa watembea kwa miguu,ubovu wa magari, ubovu wa barabara pamoja na chanzo kikubwa cha ajali ambazo ni mwendo kasi
Alibainisha kuwa hali hizo zimekuwa ni changio kubwa sana la ajali za barabarani ingawaje kikosi cha usalama wa barabara kimejipanga kihakikisha kuwa kuanzia sasa ajali hizo zinapungua kwa kiwango kikubwa sana kwa kuwachukulia hatua kali na za kiesheria wale wote ambao wanasababisha ajali hizo za mara kwa mara.

Awali aliongeza kuwa pamoja na kuwa na mikakati imara ambayo itasababisha Ulemavu wa ajali pamoja na vifo kupungua kwa kiwango kikubwa sana lakini bado kuna changamoto kubwa sana hasa upande wa Manispaa ya Arusha ambapo napo changamoto hizo zinatakiwa kutatuliwa kwa haraka sana lili kupunguza hata tatizo hilo

Katika hatua nyingine Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha bw John Mongela alisema kuwa ajali inafanya nguvu kazi ya Taifa kupungua sana na hivyo ni jukumu la kila mtu kuanzia ngazi ya familia kuhakikisha kuwa anawapa hata watoto elimu hiyo ili kupunguza hata kasi ya Ajali

MWISHO

KIFO CHA BABA MZAZI WA TUNDU LISU,NA ALUTE MUGWAI AMBAYE NI MAWAKILI KATIKA KESI YA LEMA CHASABABISHA KESI KUHARISHWA


KIFO CHA BABA MZAZI WA TUNDU LISU,NA ALUTE MUGWAI AMBAYE NI MAWAKILI KATIKA KESI YA LEMA CHASABABISHA KESI KUHARISHWA

Kesi ya Rufaa iliyokuwa inamkabili Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Bw Goodbless Lema imeharishwa mpaka October 2 kutokana na Mawakili wawili ambao ni Alute Mugwai na Tundu Lisu kufiiwa na baba yao mzazi na mazishi kufanyika Kesho kutwa

Kesi hiyo ya Rufaa ambayo inaendeshwa na Majaji watatu ambao ni Othaman Chande,Natalia Kimaro,na Salum Masati pia  mahakama imeamuru baadhi ya walengwa kuhakikisha kuwa wanakamilisha taratibu zote ili kesi hiyo iweze kusikilizwa

Aidha ilidaiwa mahakani hapo mbele ya Jaji Mkuu Othaman Chande ambaye alitoa ufafanuzi huo kwa niaba ya majaji wenzake alidai kuwa kesi hiyo itasikilizwa October 2 ambapo Wajibu rufaa nao wanatakiwa kuhakikisha kuwa walete hoja zao zote ili kuraisisha masuala mbalimbali ndani ya kesi hiyo ya Mbunge wa Arusha Mjini

“hawa mawakili ambao ni ndugu na wapo pande zote mbili ni ndugu na kwa maana hiyo wamempoteza baba yao mzazi kwa hali hiyo watamzika siku ya Jumamosi lakini pamoja na hayo yote taratibu mbalimbali nazo zinazohusu hii kesi zinatakiwa kuboreshwa na kuwasilishwa hapa October 2 mwaka huu nah ii ni kwa wahusika wote”aliongeza Jaji Chande

Hataivyo Jaji huyo aliamuru mahakama kuhakikisha kuwa Mahakama ihakikishe kuwa wajibu rufaa wawasilishe hoja zao za awali kabla ya September  26 mwaka huu,huku naye muomba Rufaa na Mwanasheria wa Serikali naye anatakiwa kuhakikisha kuwa wanaleta majibu kabla ya September 29.

Katika hatua nyingine ilidaiwa mahakamani hapo naye Mwanasheria  wa upande wa walamikaji wa naye alete hoja zake kuhusu rufaa kabla ya September 28 ili kuweza kuruhusu  kesi hiyo kusikilizwa kwa uraisi hapo October 2 ndani ya Mahakama hiyo.

Hataivyo kwa upande wa mawakili wa Serikali atawakilishwa na wakili Timothy Vitalisi ambapo kwa upande wa Majaji wataongozwa na Jaji Othmani  Chande

Katika hatua nyingine mara baada ya Kesi hiyo kuharishwa mamia ya wananchi wa mji wa Arusha walilazimika kutembea miguu na kufunga baaadhi ya barabarani za mji wa Arusha kutoka katika eneo hilo la mahakama hadi kufikia katika Ofisi za chama hicho zilizopo katika eneo la Makao Mapya.

MWISHO

NAIBU WAZIRI AZISIFU TAASISI ZA DINI



na gladness mushi,arusha

Naibu waziri wa  mawasiliano sayansi na teknolojia,January Makamba amesema kuwa taasisi za dini hapa chini zimekuwa na mchango mkubwa kwa jamii katika kuchangia maendeleo ya taifa pamoja na kuisaidia serikali  kwa kutoa ufadhili mbalimbali wa elimu kwa jamii yenye uhitaji pamoja na kuhubili amani.
Makamba aliyasema hayo jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe za kidini na utamaduni zinazoadhimishwa kila mwaka na dhehebu la dini ya wahindu wa jamii ya kilala kutoka jimbo la kusini nchini India,ambao wanaasili ya kiasia waishio hapa nchini, kwa kutoa shukrani wakati wa mavuno  .
Alisema kuwa sherehe  hiyo inamanufaa makubwa hapa nchini katika kuwaunganisha watanzania kiutamaduni ,kiimani na wenzao wanaotoka madhehebu ulimwenguni katika kudunisha amani,ambapo alieleza kuwa serikali kwa kutambua umuhimu wa taasisi za dini hapa nchini,itaendelea kutoa misamaha ya kodi kwa taasisi hizo kwenye vifaa mbali mbali vinavyokuwa na manufaa kwa wananchi ili kuweza kuwasogezea  maendeleo.

Aidha alizihakikishia taasisi hizo kuwa serikali itaendelea kutoa ushirikiano wa karibu ikiwa ni pamoja na kuheshimu imani ya kila dhehebu bila kuingilia na kuzitaka taasisi hizo kuendelea kuisaidia serikali katika kudumisha amani kupitia Nyanja mbalimbali .
Naye msemaji wa chama cha Arusha Meru Maalayelee Assiociation(AMMA),Prem Cheriam alisema kuwa AMMA imeanzishwa hapa nchini miaka 6 iliyopita ikiwa na lengo la kuwaunganisha waumini wa dini hiyo ya wahindu  na wenzao waishio hapa nchini na nje ya nchi.
Alisema lengo la ni kumshukuru mungu kwa kutoa sehemu ya mavuno yao kwa kuisaidia jamii kama shukrani yao kwa mwenyezi mungu kwa kufoa sadaka na kwamba mwaka huu wameamua kusaidia katika Nyanja ya elimu kwa kufadhili wanafunzi 7 kusoma masomo ya kompyuta nje na ndani ya nchini.
Prem alisema kuwa mpango huo utawanufaisha zaidi wanafunzi wasio na uwezo ambao wanalelewa kwenye vituo vya watoto yatima  na kwamba AMMA imeahidi  kujenga bwawa moja kwenye shule  moja wapo ya msingi katika  jiji la Arusha litakalosaidia kuwaimarisha vijana kimichezo ya kuogelea .
Katika sherehe hizo watu mbalimbali walihudhuria wakiwemo wabunge wa Mikoa ya Arusha na Manyara na viongozi wa ngazi mbali mbali serikalini pamoja na wenzao wa jamii hiyo kutoka mataifa mbalimbali na kwamba sherehe hizo zilipambwa na kunakshiwa na vikundi mbalimbali vya utamaduni  na sanaa kutoka  Nchi ya India .
Mwisho

WANAWAKE WA KIMERU WAMTAHADHARISHA MBUNGE WAO DHIDI YA KAULI ZAKE


WANAWAKE WA KIMERU WAMTAHADHARISHA MBUNGE WAO DHIDI YA KAULI ZAKE


Na Queen Lema,ARUSHA

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida wanawake wa eneo la kisambare Usariver Wilyani Meru mkoani Arusha wamesema kuwa kamwe hawatavumilia kauli za mbunge wa jimbo hilo bw Joshua Nasari badala yake watalazimika kuingia barabarani hata kwa vita na kumpinga hadharani  Mbunge huyo  kwani kauli zake hazijengi hoja za kutetea shida za wananchi na badala yake kauli zake zinachochea Malumbano pamoja na Migogoro huku wanawake wa Vijijini wakiwa wanakabiliwa na shida mbalimbali

Wanawake hao waliyasema hayo jana wilyani humo wakati wakizungumza na Viongozi mbalimbali ambao waliwatembelea Kijijini humo sanjari na kuongea na wanachama wa chama cha mapinduzi
Wanawake hao walisema kuwa kauli za Mbunge Nassari sio kauli za kujenga bali ni kauli za kubomoa na kuchochea malumbano makubwa sana ambapo pia kwa sasa mbunge huyo angepswa kuongelea changamoto mbalimbali ambazo zimo kwenye jamiii

Walifafanua kuwa mbunge huyo anapaswa kujua na kutambua kuwa alipewa jimbo hilo kwa hasira kutokana na kukithiri kwa changamoto lukuki ambazo zimo kwenye jamii hasa za Wameru na kwa hali hiyo huu ndio muda muafaka wa mbunge huyo kuhakikisha kuwa anatatua kero na wala sio kutoa matammko ambayo hayana tija na jamii

Waliongeza kuwa kauli hizo lzimekuwa na madhara makubwa sana hasa kwa vija na kwa kuwa mpaka sasa wapo baadhi yao wanaofanya makosa kwa visingizo vya Mbunge huyo hali ambayo ni chanzo kikubwa sana cha uharibifu wa Amani

“tunachotaka kujua ni kuwa tunatatuliwa kero zetu lakini badala mbunge afikirie suala zima la maendeleo yeye anafikiria kuzima mwenge wakati sisi hatuna shida na mwenge na mwenge unapita lakini shida zetu hasa sisi wakina mama wa Nkoakirika hatujui hata majira ya saa sasa tueleweje kwani tukimbia CCM kutokan a na changamoto lakini hii ya sasa ni kali na kama huyu mbunge ataendelea hivi basi ipo siku matatizo makubwa sana yatatokea”waliongeza wakina mama hao huku wakiwa wanalia

Mbali na hayo waliongeza kuwa nao viongozi wa siasa watakiwa kkukumbuka ahadi mbalimbali ambazo wamezitoa kwa jamii hasa nyakati za kampeni kwani baadhi ya viongozi hasa wa Mkoa wa Arusha wakishapata nafasi ya kuongoza basi wanakuwa na matamko ambayo hayana tija kwa jamii na badala yake matamko hayo yanasabahbisha hata baadhi ya vijana kushikwa shikwa ovyo na Polisi

Awali Katibu wa CCM Wilaya ya Meru bw Langaeli Akyoo alikiri kuwa chama cha mapinduzi kilikuwa na kasoro hali ambayo iliwafanya wananchama wake kukopesha jimbo la Arumeru Mashariki lakini kwa sasa chama hicho kimejipanga hata kwa Watendaji wa huduma zote za kijamii kuhakikisha kuwa wanatekeleza Sera za wananchi

Bw Akyoo alifafanua kuwa hasira ambazo  ndio chanzo  pekee cha wananchi kutoa kura kwa upinzani kwa sasa zitapunguzwa kwa kiwango cha juu  huku jamii hasa za vijijini zenye maitaji maalumu nazo zikiweza kupatiwa ufumbuzi wa matatizo yao  kwani uwezekano wa kuwasaidia bado ni mkubwa sana.