Tuesday, September 11, 2012

ASKOFU HOTAY APEWA KITI RASMI CHA UASKOFU

huyu ni askofu rasmi wa kanisa la Angilican dayosisi ya mt kilimanjaro Stanley Hotay alipokuwa kanisani mapema jana wakati akiongea katika ibada ambayo ilimpa kiti rasmi mara baada ya kushinda kesi iliyofunguliwiwa dhidi yake na waumini watatu


 

Na Queen Lema,ARUSHA

ASKOFU HOTAY WA KANISA LA ANGILIKANA DAYOSISI YA MOUNT KILIMANJARO AKABIDHIWA RASMI KITI CHA UASKOFU

WALIOSABABISHA NA KUFUNGUA KESI WASAMEHEWA MBELE YA KANISA

WAKATI zikiwa zimepita siku chache mara baada ya Mahakama kuu kanda ya Arusha kutupilia mbali pingamizi la waumini wa kanisa la Angilikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro juu ya Uaskofu wa Askofu wa kanisa hilo Stanley Hotay jana(Leo)kanisa hilo limemuweka rasmi kazini askofu huyo sanjari na kutangaza msamahaa kwa waumini hao watatu kwani wamechangia sana kanisa hilo kupoteza muda kwenye kesi hiyo pamoja na aibu kubwa kwenye masikio ya watu wengi

Akiongea katika ibada maalumu ya kuweza kumpa nafasi ya kuongoza Dayosisi hiyo Askofu mkuu wa kanisa hilo la Angilican Tanzania Dkt Valentino Mokiwa alisema kuwa mpaka sasa wameshatangaza Msamaha  kwa watu hao ambao walitia aibu kanisa hilo hivi karibuni

Askofu huyo alisema kuwa hapo awali baadhi ya waumini akiwemo yeye mwenyewe walikuwa katika wakati mgumu sana kutokana na  kesi hiyo lakini kutokana na ukweli na haki  ya Askofu Hotay aliweza kupata haki yake kupitia mahakama  Septembe  tano mwaka huu huku waliofungua kesi hiyo wakishinndwa kusonga mbele

“wakati Kesi hii inaanza mimi nilikuwa katika wakati mgumu sana kwani nilikuwa na Presha ambayo wakati mwingine ilinipelekea hata kushindwa kuona na huku kwa upande wa Askofu Hotay naye alishindwa kukaa kwa amani lakini kila mara saa nyingine alikuwa anahitajika hata kwenda mahakamani  lakini kwa sasa kweli ya Mungu imejulikana na imeonekana mahakamani wiki iliyopita”aliongeza Dkt Mokiwa

Mbali na hayo alisema kuwa kuna masaa mengi sana ambayo yamepotea katika Kesi hiyo ambayo ilifunguliwa na waumini watatu lakini kanisa kama kanisa linapswa kuhakikisha kuwa linatoa msamaha wa kweli ambao unatoka ndani ya Mioyo yao kwani watu hao walidanganywa na hata kufikia hatua ya kutoka nje ya Kundi bila kujua kuwa hali hiyo inachangia sana hata mmonyoko wa Kanisa na aibu sana

“kwa kweli hawa watu wametupa aibu ya hali ya juu sana lakini tunapswa kuhakikisha kuw tunawasamehe hawa watu kwani walikuwa hawajui wafanyalo ingawaje si hawa waumini watatu pekee yao bali ni nyuma yao kulikuwa na watu wengi sana ambao hata wengine nao walichangia kwa kuwapa fedha za kwenda kufungulia kesi na wao pia tumewasamehe wote kabisa na kanisa lihakikishe kuwa linawaombea Toba na kuwapenda sana”aliongeza  Dkt Mokiwa

Katika hatua nyingine alisema kuwa kanisa hilo limempa Nafasi ya kuongoza jimbo hilo kwa mujibu wa katiba ya Kanisa hilo na kutokana na hali hiyo kiti hicho ambacho alikuwa hakitumii kutokana na kesi ambayo ipo mahakamani sasa anaanza kazi rasmi kwa kuwa sheria inamruhusu huku waumini wa  kanisa hilo nao wanatakiwa kumpa ushirikiano na kukumbuka Viapo mbalimbali ambavyo vinatumika na kanisa hilo

Naye Askofu Stanley Hotay aliwaambia waumini wa kanisa hilo kuwa ili ufanikiwe ni lazima kwanza uhakikishe kuwa unatoa msamaha hata  kwa wale ambao wamekuwa ni vikwazo vya kushindwa kufikia katika malengo mbalimbali ambayo yanatakiwa kufikiwa ingawaje vikwazo ni vingi sana katika safari ya Ushindi

Askofu huyo alifafanua kuwa pamoja na kuwa amepita katika wakati mgumu sana hasa wa kuwa na kesi ya kutotambulika na waumini wake lakini bado ana nafasi kubwa sana ya kuweza kuwatumikia hao hao na kuwafanya wabadilishe fikra kwani hapo awali hawakujua wanachokifanya hali ambayo ilizaa aibu kubwa sana mbele ya kanisa la Angilikana dayosisi ya Mout Kilimanjaro.

“ingawaje mimi nilipita katika wakati mgumu sana lakini wao walikuwa ni zaidi sana kwani mtu akijiaanda kukupiga ngumi kubwa yeye ndiye anayetumia nguvu nyingi sana kuliko yule ambaye anatarajia kupigwa na mimi nataka kuwaambia kuwa wapo huru kabisa dhidi yangu na bado mimi nawatambua kama wanakondoo wangu”aliongeza Askofu Hotayi

Aliwataka waumini wa kanisa hilo kuhakikisha kuwa wanasahau hilo na kuanza kufikiria upaya kwani bado kanisa hilo lina muitikio mkubwa sana wa kuweza kuwasaidia waumini pamoja na jamii kwa kuweza kuhamasisha maendeleo ambayo ndiyo yana amani kwa maslahi ya Taifa la Tanzania

Mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika ukabidhiwaji wa kiti hicho kwa askofu huyo ambaye hapo awali alikuwa ameshasimikwa kama askofu wa kanisa hilo alisema kuwa wakristo wanatakiwa kujua hakuna dhambi mbaya sana kama dhambi ya kutamani madaraka kwani dhambi hiyo ndiyo inayochangia kwa kiwango kikubwa sana kuwepo kwa migogoro sana

Bw Mulongo aliongeza kuwa ni vema kama mtu anayetamani Madaraka hata kama ni ya Uaskofu basi kuomba Mungu kna wala sio kuwa chanzo cha kuanzisha Kesi ambazo hazina Tija na ambazo zinapotosha hata maana halisi ya Wokovu huku tamaa kama hizo zikiwa ni chanzo pekee cha kuweza kusababisha amani kutoweka

MWISHO

No comments:

Post a Comment