Monday, June 18, 2012

VIONGOZI WA DINI 2000 KUTOKA NCHI TANO KUTAFAKARI NA KUOMBEA CHANGAMOTO ZA TANZANIA




ZAIDI ya viongozi 2000 wa makanisa ya Intenational Evangelism kutoka kati nchi 5 wanatarajia kukutana jijini Arusha na kujadili changamoto mbalimbali za nchi ya Tanzania ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia za nchi,na hali ya maisha ya sasa kwa watanzania

Akiongea na waandishi wa habari mkoani hapa Askofu wa makanisa ya Intenational Evangelism Centre ya hapa nchini Bw Eliud Isangya alisema kuwa viongozi hao watakutana jijini hapa wiki ijayo

Bw Eliud alisema kuwa viongozi hao watajadili mambo mbalimbali ambayo kwa sasa yanaikabili sana nchi ya Tanzania ambapo changamoto hizo zinaweza kutatuliwa hata kwenye taasisi mbalimbali za dini badala ya kutegemea zaidi Serikali kwa kila kitu

Alisema kuwa mara mbali na kuweza kutatua changamoto mbalimbali ambazo zipo sana ndani ya jamii pia watafanya maombi kwa ajili yan kuombea nchi ya Tanzania pamoja na Zanzibar dhidi ya machafuko ambayo yanatokea kila mara.

“kwa sasa zipo changamoto kubwa sana ikiwemo changamoto ya mabadiliko ya tabia za nchi sasa kwa inawaasumbua wananchi wengi sana hasa wa vijijini lakini kama taasisi mbalimbali zikiwemo za dini zitawaamasisha hata waumini wake ni wazi kuwa jamii haitaweza kukumbwa na baa la ukame kwa maana hiyo tutajadili masuala kama hayo ambayo yanaitesa jamii za watanzania walio wengi”aliongeza Bw Eliud

Pia alisema kuwa taasisi mbalimbali za dini zinatakiwa kusaidia jamii kwa kuweza kuwa bunifu na kubuni vitu ambavyo ni mzigo kwa Serikali ili kuweza kuraisisha hata maendelo ya Miji na Majiji hapa nchini

‘kila siku wanasayansi wanabuni vitu vipya na vina uwezo wa kuwasaidia jamii kwanini sisi kama wadau wa nchi hii tusiwe wabunifu wa kusadia hata kuombea taifa katika majanga mbalimbali ambayo ni kikwazo cha maendeleo tunataka tufanye hivyo ili kurudisha hata vitu ambavyo vimepotea kwenye nchii hii ya Tanzania”aliongeza bw Eliud

Mbali na hayo bw Eliud alizitaka Taasisi nyingine za dini kuhakikisha kuwa kila mara zinayafanyia kazi changamoto ambazo zipo kwenye jamii kwa kuwa wao ndio wana nafasi kubwa sana ya kuweza kulikomboa taifa la Tanzania

mwisho


No comments:

Post a Comment