Tuesday, September 4, 2012

WAJASIAMALI 4000 WAPEWA ELIMU YA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO VIDOGO PAMOJA NA VIWANDA VYA KATI


Kikundi cha vijana cha KIPENET kikimba nyimbo za kuishukuru UN kwa kuwaonyesha Mwanga wa Maisha na Maendele baada ya kupata elimu ya ujasiriamali


Na Queen Lema,Arusha

WAJASIAMALI 4000 WAPEWA ELIMU YA KUANZISHA VIWANDA VIDOGO VIDOGO PAMOJA NA VIWANDA VYA KATI

Kampuni inayojihusha na Utengenezaji wa shuguli za Biashara Tanzania (TBCC)imefanikiwa kutoa elimu kwa wajasimali zaidi ya 4000 kutoka maeneo mbalimbali Nchini ambapo baadhi yao kwa sasa wanamiliki Viwanda Vidogo Vidogo pamoja na Viwanda vya Kati  huku wakiwa ni sehemu ya kuchangia Pato la Taifa.

Akiongea na “Majira”jana Jijini hapa Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni hiyo Bw Mchau Elibariki alisema kuwa Wajasiriamali hao wamepata elimu hiyo kuanzia mwaka 2009 ambapo baadhi yao kwa sasa wanamiliki Viwanda Vidogo Vidogo

Bw Elibariki alisema kuwa  Kampuni yake imeamua kufanya hivyo kutokana na Nchi kuwa na Wafanyabiashara wengi  ambapo bila kujua kuwa wao ni wachuuzi hali ambayo nayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana hata baadhi ya wadau wengine wakiwemo wafanyakazi kutopata ajira

Aliongeza kuwa kupitia wajasiamali hao 4000 ambao wameweza kupata elimu hiyo wengi wao wamekuwa na faida kwa Nchi ya Tanzania kwani wameweza kuongeza hata idadi ya watu ambao wameajiriwa tofauti na pale ambapo Nchi inakuwa na wachuuzi wengi kuliko wafanyabiashara

Alifafanua kuwa pamoja na kufanikiwa kuwapa elimu na mbinu mbalimbali kwa  wanajamii bado Kampuni hiyo ina dhamiria kuendelea kuwapa wananchi fursa za kumiliki Viwanda Vidogo Vidogo  pamoja na Viwanda vya Kati ambapo hapo napo patakuwa na manufaa makubwa sana kwani hata pato la Taifa nalo litaweza kuongezeka sana huku Maitaji muhimu ndani ya jamii nayo yakiweza kutatulika kwa Uraisi kutokana na kipato ambacho kinapatikana.

“Tumedhamiria  kuwepo na Viwanda vya kutosha kila mahali kwani tunao huo uwezo wa kutengeneza bidhaa zetu na kuachana na tabia ya kuwa tegemezi kwa kusubiria zaidi bidhaa za nje na pia kupitia hata viwanda hivyo vidogo vidogo na vya kata pia Tunatarajia hawa wafanyabiashara wawe na Mtaji ambao haupungui kiasi cha Shilingi Bilioni Moja”aliongeza Bw Elibariki

Pia alisema kuwa ili kuweza kuwa na wafanyabiashara ambao watamiliki Viwanda Vidogo na Viwanda vya kati wamedhamiria kwa kipindi cha miaka Mitano Mitano mfululuzo watakuwa na wafanyabiashara 25 ambao wataweza kumiliki Viwanda hivyo huku wakiwa na Mtaji wa kiasi cha shilingi Bilioni Moja kwa kila Mmoja ambapo nao hawa wataweza kuendesha viwanda vyao ambavyo vitakuwa ni viwanda venye manufaa kwa jamii.

“tukishafanikiwa kuwapa hawa watu wenye Mitaji ya kiasi cha Shilingi Bilioni moja itakuwa ni raisi sana kwetu kuweza hata kulipa Kodi za Nchi kwa uraisi tofauti na pale kila mtu anapokuwa na biashara yake ndogo ndogo ya Uchuuzi na kwa hali hiyo tutaweza kusogeza Nchi kutoka sehemu moja ya ulipaji wa kodi hadi sehemu Nyingine”aliongeza Bw Elibariki

Bw Elibariki alimnalizia kwa kusema kuwa kwa sasa ni vema kama kila Mtanzania akafikiria jinsi ya kupata elimu ya ujasiamali ili aweze kujikomboa dhidi ya Umaskini kwani kupitia masomo ya Ujasiamali yana uwezo wa kuwafanya walio wengi zaidi kuinuka na kuachana na ktabia ya kuwa Tegemezi.

MWISHO

No comments:

Post a Comment