Tuesday, September 25, 2012

mbunge Anjela Kairuki,amehaidi kuwasadia waongoza utalii



Na  Mustafa  Leu,  Arusha.

MBUNGE wa bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia kundi la wafanyakazi, Anjela Kairuki, ameahidi kuwasaidia waongoza utalii kupata stahili zao mbalimbali ikiwemo kuboreshewa maslahi na kuondokana na manyanyaso wanyaopata kutoka kwa wamiliki wa kampuzi za utalii.

Kairuki, ametoa ahadi hiyo jana baada ya kumalizika kwa kikao cha pamoja na Waongoza utalii katika hotel ya Naura, ambapo waongoza utalii hao walitoa kilio kwa mbunge huyo kutokana na manyanyaso wanayopata ikiwemo kulipwa ujira mdogo wa shilingi 80,000 kwa mwezi na kupewa posho ndogo ya shilingi kati 10,000 na 1500 ya   kujikimu wawapo safarini katika mbuga za wanyama  na kulala kwenye Hoel zisizokuwa na viwango huku wakila chakula kibovu..

Kairuki, ambae ni naibu waziri wa Katiba na Sheria,  alisema ameenda  kuwasilikiliza kama mbunge na kwa kutambua kuwa ametokana na  kundi la wafanyakazi hivyo atawasaidia ili kuona manyanyaso yanatoweka na waweze kufanya kazi kwa ufanisi ili kuboresha sekta ya utalii nchini.

Amesema  anasikitishwa na viwango wanavyolipwa kutokana na kazi ngumu ya kuongoza watalii wawapo mbugani  huku wakiwa hawana mikataba ya hiari ya ajira kama sheria ya kazi mpya ya mahusiano kazini ya mwaka 2004  inavyoelekeza kila mwajjiri awe na mkataba wa hiari na mfanyakazi wake ili aweze kupewa stahili zake.

Amesema atahakikisha kuanzia sasa atashirikiana na waziri wa kazi na vijana,waziri wa Maliasili na Utalii, kusimamia makampuni hayo  uwepo wa mikataba ya hali bora ya wafanyakazi wa makampuni ya utalii na sekta zingine ili kuywaondolea manyanyaso

Kwa upande wao waongoza utalii hao kupitia Chama chao cha Tanzania Tour guides associatio, TTGA ,walimwambia waziri kuwa hawana mikataba ya ajira, wanalipwa maslahi duni, hawana bima na wakipata ajali hufukuzwa kazi   hivyo wanaomba iwepo sheria ya kuwalinda na kuwabana waajiri.

Wamesema tatizo ni makampuni mengi ya Utalii nchini kumilikwa na baadhi ya mawaziri na viongozi wa serikali hivyo kuwafanya wao wasiweze kulipwa ujira mzuri na hawana pa kupeleka malalamiko yao.

Wamesema kuwa waongoza watalii ndio mabalozi wazuri wa kuelezea utalii hapa nchini kwa sababu wanatumia 80% ya muda wakiwa na watalii mbugani wanatoa maelezo sahihi kwa wageni  na wageni huwa wanapokwena makwao huwa wanarejea na kuleta wageni wengine.

Wamesema Sekta inayoongoza kwa utalii hapa nchini ni ya uopiga picha hivyo sekta hiyo ni muhimu lazima ipewe thamani zaidi .Maeneo mengine waliyolalamikia ni kufungwa kwa baadhi ya njia ndani ya hifadhi hivyo kuwasababishia usumbufu, ubabe wa askari wa hifadhi, kutozwa faini  hawaruhusiwi kula meza moja na wageni wawapo porini kitendo ambacho ni cha ubaguzi na dharau kwao .

Baadhi ya Hotel kutoa chakula kibovu, malazi duni matandiko yamechakaa vitanda vibovu vyumba visivyofaa kulala binadamu.kulipwa ujira mdogo huku wamekabidhiwa magari ya mamilioni ya fedha
```````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````````

No comments:

Post a Comment