Friday, July 20, 2012

MABALOZI WA NYUMBA KUMI KUMI WAHAMASISHENI WENYE WATOTO WALEMAVU WAJITOKEZE KATIKA SENSA

Na ROSE JACKOSON , Arusha

SERIKALI imeombwa kutoa elimu zaidi hasa kwa mabalozi wa nyumba kumi kumi maeneo ya Vijijini hasa kwa upande wa walemavu kwani baadhi ya wananchi wa vijijini bado wana uelewa mdogo kwa walemavu na hali hiyo huenda ikasababisha wasishirikishwe katika zoezi la Sensa ya watu na makazi.

Hayo yameelezwa na Bi Yunisi Urasa ambaye ni Katibu wa shirikisho la vyama wenye ulemavu(SHIVYAWATA) mapema jana wakati akiongea na wakufunzi ambao watashirikishi katika zoezi la Sensa.

Aidha bi Yunisi alisema kuwa ni vema kama zoezi hilo liweze kuwafikia watu wote kama sheria inavyosema lakini wapo baadhi ya watu ambao hawataweza kufikiwa kutokana na uelewa mdogo , pamoja na Imani mbaya dhidi ya walemavu.

Aliongeza kuwa endapo kama Serikali kwa sasa ikiwashirikisha viongozi wa nyumba kumi kumi katika zoezi hilo la Sensa itachangia kwa kiwango kikubwa sana watu wenye ulemavu hasa watoto wa maeneo ya vijijini  kuweza kushiriki katika zoezi hilo la  Sensa.

 “kama tunavyoona ni kuwa zoezi hili linasonga mbele zaidi hasa hapa mijini lakini sisi tunajiuliza kuwa je Kijijini itakuwaje na kwa maana hiyo basi kama hawa mabalozi wa nyumba kumi kumi watahamasisha watu hasa wenye ulemavu watakuwa  ni kichocheo  kikubwa sana hasa kwa Serikali hasa kufikia kwenye malengo yake ya Sensa na watu kwa kipindi hiki”aliongeza Bi Yunisi.

Pia alisema kuwa mbali na Mabalozi kuhamasisha watu juu ya umuhimu wa Sensa ya watu na makazi hasa maeneo ya Vijijini  nao wanawake wana nafasi kubwa sana ya kusaidia na kuraisisha  zoezi hilo kwa kuachana na mila potofu za watoto walemavu kwa kuwa nao wana haki ya msingi kabisa.

“Wanawake wa Vijijini wanatakiwa kujua na kutambua kuwa Sensa ina umuhimu mkubwa sana kwa maendeleo ya jamii ambapo kupitia hata Sensa hiyo itaweza kusaidia Jamii hizo za Walemavu katika mahitaji muhimu ikiwemo huduma za Msingi kwenye maisha ya kila siku”aliongeza Bi Yunisi

Awali Mratibu wa zoezi hilo la Sensa kwa Mkoa wa Arusha Bi Magret Martin alisema kuwa mpaka wamejipanga kuhakikisha kuwa makundi yote kwenye jamii yanafikiwa katika zoezi hilo la Sensa kwa kuwa Sensa ina umuhimu mkubwa sana kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.

Bi Magret aliongeza kuwa ndani ya mafunzo yanayoendelea mjini hapa wamejipanga kuhakikisha makundi maalumu katika jamii nayo yanafikiwa na jamii kwa kuwa nayo yana nafasi kubwa sana katika kuraisisha zoezi hilo ndani ya jamii ya Kitanzania.

MWISHO

WAIMBAJI WATAKIWA KUACHA KUENDEKEZA ZAIDI MASLAHI

WAIMBAJI WATAKIWA KUACHA KUENDEKEZA ZAIDI MASLAHI

WAIMBAJI wa nyimbo za injili wametakiwa kufanya kazi hiyo ya uimbaji kama njia ya kutangaza injili hasa katika maeneo ya vijijini na kuacha kufanya kazi ya injili kwa maslahi kwa kuwa wapo wachungaji  na makanisa yao ambayo yanashindwa kufikiwan na huduma ya  uimjbaji kwa kuwa hayana fedha za kuwalipa waimbaji

Kauli hiyo imetolewa mjini Arusha na Mchungaji Anthony Albert “Joka Kuu”katika kania la EAGT Moria wakati akizungumza na waumini wiki iliyopita mara baada ya kuweka wakfu  cd ya waimbaji wa kanisa hilo inayojulikana kwa jina la Bado Kitambo

Mchungaji Anthony alisema kuwa wapo baadhi ya waimbaji wa nyimbo za injili ambao kwa sasa wameendekeza zaidi maslahi ya uimbaji na kusahau kuwa uimbaji ni wito na hali hiyo inachangia kudidimiza hata maisha ya wakristo ambao hawana uwezo

Alifafanua kuwa kwa sasa makanisa ambayo yanaonekana kuwa na uwezo wa kuwaita waimbaji hao  ni makanisa yale ambayo yanaweza kuwalipa lakini kwa makanisa hasa ya vijijini huwa hayana nafasoi ya kuita na kuwatiumia waimbaji hao maarufu

Aliongeza kuwa hali hiyo si makusudio ya Mungu na kwa hali hiyo waimbaji wanatakiwa kuwa makini na kuhakikisha kuwa wanarudi katika fasheni za biblia na wala sio fasheni za maslahi kama walivyo baadhi ya waimbaji kwa sasa

“unakuta kanisa au huduma inamujita muimbaji lakini kwa kuwa kanisa lile halina uwezo wa kumuita Muimbaji  sasa kama hawa waimbaji wameitwa kwa ajili ya watu wenye fedha je hawa maskini wanakwenda wapi ni lazima waimbaji wafike mahali wajue na kutambua kuwa wao wapo kwa ajili ya kueneza injili na wala sio kwa ajili ya kuangalia maslahi”alisema Mchungaji Anthony.

Awali alisema kuwa nao wanakwaya wa makanisa mbalimbali wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajikita zaidi katika maisha ya kiroho na kuachana na tabia ya kuwa Moto Baridi ndani ya makanisa na badala yake wanatakiwa kuimba kwa mujibu wa biblia inavyosema na kudai

Aliongeza kuwa nao  wanakwaya wa sasa baadhi yao huwa wanaaimba kwa mazoea hali ambayo inawafanya wengi kila mara kujikuta wakiwa wanaanguka katika dhambi kubwa ikiwemo dhambi ya uzinzi  ambayo inawatesa walio wengi sana.

”nawasihi sana ninyi wanakwaya hakikisheni kuwa kamwe hamrudi nyuma hakikisheni kuwa hamshindani  kimavazi kwa kuwa mnaposhindana kwa mavazi hamfikii hata malengo yenu ya kuifikisha injili panapotakiwa”alisema Mchungaji Anthony

MWISHO

MAKANISA,OMBENI TOBA ILI MPATE UPAKO

,ARUSHA
 
IMEELEZWA kuwa mipango pamoja na mikakati mbalimbali ndani ya makanisa inashindwa kufikiwa kwa uraisi zaidi kwa kuwa baadhi ya wadau wa kanisa hawana tabia ya kufanya toba ya kweli
 
Hayo yamebainishwa na mchungaji Mariamu Mbisse wakati alipokuwa akifundisha neno la Mungu katika kanisa la FPCT Sombetini mkoani hapa Juma lilopita
 
Mchungaji Mbise alisema kuwa asilimia kubwa ya watu wanajijengea tabia ya kusahau sana Toba hali ambayo inafanya kanisa la leo lishindwe kufikia malengo na mikakati yake mbalimbali ambayo wamejiwekea
 
Alifafanua kuwa hali hiyo ndiyo inayochangia sana hata baadhi ya watu kushindwa kufanikiwa kwa uraisi sana hali ambayo inafanya baadhi ya watu kuona kama makanisa hayana upako wa kweli
 
Alisema kuwa ni vema kama kila mkristo akahakikisha kuwa anaishi maisha ya Toba na kila mara kutafuta Toba ili aweze kufungua hata milango ya baraka kutoka kwa mungu kwani Dhambi nazo ni kikwazo cha kutopata mafanikio
 
“kwa sasa kuna mambo mengi sana huku duniani kwa maana hiyo kila mara ni vema kama watu wakajitokeza kwa wingi na kuweza kuomba kwa pamoja maombi ya toba ambayo ndiyo yanayofungua lakini kama kanisa kama kanisa litaomba juu ya toba basi hata upako utaweza kushuka”alisema Mchungaji Mariam
 
Awali mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Bi Elinaisha Abraham alisema kuwa  ili upate mafanikio ya aina yoyote ile hapa duniani ni lazima uombe na utubu kwa toba ya kweli kwa kuwa kwa Mungu kuna misamaha
 
Mchungaji Elinaisha alibainisha kuwa ni vema kama kila kanisa likahakikisha linakuwa na utaratibu wa toba ili makanisa hayo yaweze kufikia hata hatua mbalimbali ambazo wamejiwekea.
 
mwisho

MAKANISA YATAKIWA KUOMBEA MASLAI YA WAFANYAKAZI WAKE

,ARUSHA

WITO umetolewa kwa makanisa mbalimbali hapa nchini kuhakikisha kuwa yanajiwekea utaratibu wa kuombea mapato ya wafanyakazi wake kwa kuwa wengi wamekuwa wakipoteza hata haki zao  za msingi

Kauli hiyo imetolewa mjini Arusha na mchungaji Joel Kessoi  katika kanisa la Ngome ya Yesu lilopo Kisongo

Aidha mchungaji huyo alisema kuwa kwa sasa maslahi ya wakristo wengi sana wanaibiwa ovyo kwa kuwa baadhi ya waajiri wanashindwa kuwalipa na baadaye wakristo hao wanaishia kuteseka

Alisema kuwa endapo kama kanisa litasimama katika nafasi yake na kuanza maombi yake basi waajiri hasa wa viwanda ambao wananyima haki zao  na badala yake kuanza kuwakata wafanyakazi makato ambayo hayastaili.

“ukiangalia hawa wafanyakazi wa Viwanda kila siku wanalia na shida lakini wa nahaki sana ya kuweza kufanya kazi zao na kupewa wanachokitaka lakini kwa sasa kazi zao nyingi sana zimeingiliwa na shetani na wanakatwa hata makato ambayo hayastaili kwa kweli”aliongeza mchungaji Joel

Pia alisema kuwa kama kanisa litaendelea kuangalia suala hilo ambalo ndilo chanzo cha umaskini wa makanisa ya leo basi nafasi ya maombi inatakiwa kuanza kutumika katika kuombea wafanyakazi na makato yao

Alifafanua kuwa kwa kuanza kanisa hilo limeanza na mchakato wakuombea  wafanyakazi wa kiwanda cha A- Z ambao nao wamekatwa sana makato mengi ambayo hayana faida na wafanyakazi

Alisema kuwa kila mara watakuwa wanaombea wafanyakazi wa makampuni na viwanda mbalimbali katika maombi maalumu ili wawezen kufikia malengo yao ya msingi ambayo wamejiwekea na kuacha kuonewa hasa wakati wa kupewa haki zao

MWISHO

MARUFUKU MASHOGA WA KIKE KUONGOZA FAMILIA ANAYEONGOZA FAMILIA HATA KAMA NI DUNI NI MWANAUME PEKEE – ASKOFU NGOY NGOY

HABARI NA QUEEN LEMA,Arusha

WANAWAKE wa kikristo wametakiwa kuacha tabia ya kuwatumia marafiki kwenye ndoa zao kwani takwimu zinaonesha kuwa ndoa nyingi sana za kikristo zinakufa kutokana na marafiki kuwa ndio vichwa badala ya Mume

Hayo yamebainishwa na Askofu Nassor Ngoy Ngoy wa kanisa la Reboth Victory Church lilopo Maeneo ya Mianzini wakati akiongea na waumini  wa kanisa hilo katika ibada ya ndoa iliyofanyika kanisa hapo jumapili iliyopita

Askofu huyo alisema kuwa wanawake wanapswa kujua na kutambua kuwa hakuna kichwa cha familia bila ya mwanaume na kutokana na hali hiyo alisema kuwa kwa sasa ndoa nyingi zinaongozwa na marafiki wa kike hali ambayo inachangia sana kuvunjika kwa ndoa.

Alifafanua kuwa hali hiyo ambayo ni chukizo na ndio chanzo kikubwa sana cha kuvunjika kwa ndoa zilizo nyingi zinapswa kuachwa mara moja na badala yake wanawake wakahakikisha kuwa wanakuwa na vifua ambavyo vitatunza Siri,

“inasikitisha sana kuona marafiki wanakuwa wao ndio baba na wao ndio mama kwenye ndoa wakati hata maandiko hayasemi hivyo sasa hali hii inachangia kwa kiwango kikubwa sana baadhi ya watoto kuteseka na wengine wanakesha wakiwa wanamtafuta shetani wakati shetani wanamkaribisha wao wenyewe”aliongeza Askofu Ngoy Ngoy

Pia aliongeza kuwa endapo hata kama ndoa ina shida kwa kiasi kikubwa sana basi siri ya ndoa ile anatakiwa kuijua na kutambua ni baba mlezi ambaye ni mchungaji na wala sio Shoga kwani ataweza kukupitisha katika mpango wa Mungu  ambapo ndiko kuna chimbuko kubwa sana la misingi ya ndoa

Aliongeza kuwa ili ndoa idumu ni lazima kila mwanandoa hasa wanawake wawe na uwezo wa kujiwekea tabia ya siri sanjari na kutafuta kweli ya mungu na wala sio kuongea ili kuweza kuwafuraisha marafiki walio wengi wakati ndio msingi wa kuvunjika kwake

Aidha aliwataka wana ndoa ambao wanatofauti za kidunia kuendelea kuwaombea wenzao kwa maombi ambayo yatasababisha imani zao za kidunia kubalika na kuja kwenye mfumo wa kimungu kwa kuwa chanzo cha ufalme wa mungu pia kinaanzia kwenye ndoa

“ndani ya ndoa unaweza kukuta mtu mmoja ameokoka lakini kwa kuwa mwenzako wako bado hajamjua Mungu kila mara unamdharau na kumuona hafai au unakuta hata wengine wanadiriki kuwakimbia na kutaka wapate wake au wanaume waliokoka sasa hii siyo suluhisho la ndoa ambazo ni imara bali ndoa imara ni ile inayomjua na kumtafakari zaidi Mungu”aliongeza Askofu Ngoy Ngoy.

MWISHO

MABALOZI WA NYUMBA KUMI KUMI WAHAMASISHENI WENYE WATOTO WALEMAVU WAJITOKEZE KATIKA RUSHWA

habari na Rose Jackson,  Arusha

SERIKALI imeombwa kutoa elimu zaidi hasa kwa mabalozi wa nyumba kumi kumi maeneo ya Vijijini hasa kwa upande wa walemavu kwani baadhi ya wananchi wa vijijini bado wana uelewa mdogo kwa walemavu na hali hiyo huenda ikasababisha wasishirikishwe katika zoezi la Sensa ya watu na makazi.

Hayo yameelezwa na Bi Yunisi Urasa ambaye ni Katibu wa shirikisho la vyama wenye ulemavu(SHIVYAWATA) mapema jana wakati akiongea na wakufunzi ambao watashirikishi katika zoezi la Sensa.

Aidha bi Yunisi alisema kuwa ni vema kama zoezi hilo liweze kuwafikia watu wote kama sheria inavyosema lakini wapo baadhi ya watu ambao hawataweza kufikiwa kutokana na uelewa mdogo , pamoja na Imani mbaya dhidi ya walemavu.

Aliongeza kuwa endapo kama Serikali kwa sasa ikiwashirikisha viongozi wa nyumba kumi kumi katika zoezi hilo la Sensa itachangia kwa kiwango kikubwa sana watu wenye ulemavu hasa watoto wa maeneo ya vijijini  kuweza kushiriki katika zoezi hilo la  Sensa.

 “kama tunavyoona ni kuwa zoezi hili linasonga mbele zaidi hasa hapa mijini lakini sisi tunajiuliza kuwa je Kijijini itakuwaje na kwa maana hiyo basi kama hawa mabalozi wa nyumba kumi kumi watahamasisha watu hasa wenye ulemavu watakuwa  ni kichocheo  kikubwa sana hasa kwa Serikali hasa kufikia kwenye malengo yake ya Sensa na watu kwa kipindi hiki”aliongeza Bi Yunisi.

Pia alisema kuwa mbali na Mabalozi kuhamasisha watu juu ya umuhimu wa Sensa ya watu na makazi hasa maeneo ya Vijijini  nao wanawake wana nafasi kubwa sana ya kusaidia na kuraisisha  zoezi hilo kwa kuachana na mila potofu za watoto walemavu kwa kuwa nao wana haki ya msingi kabisa.

“Wanawake wa Vijijini wanatakiwa kujua na kutambua kuwa Sensa ina umuhimu mkubwa sana kwa maendeleo ya jamii ambapo kupitia hata Sensa hiyo itaweza kusaidia Jamii hizo za Walemavu katika mahitaji muhimu ikiwemo huduma za Msingi kwenye maisha ya kila siku”aliongeza Bi Yunisi

Awali Mratibu wa zoezi hilo la Sensa kwa Mkoa wa Arusha Bi Magret Martin alisema kuwa mpaka wamejipanga kuhakikisha kuwa makundi yote kwenye jamii yanafikiwa katika zoezi hilo la Sensa kwa kuwa Sensa ina umuhimu mkubwa sana kwa maslahi ya Taifa la Tanzania.

Bi Magret aliongeza kuwa ndani ya mafunzo yanayoendelea mjini hapa wamejipanga kuhakikisha makundi maalumu katika jamii nayo yanafikiwa na jamii kwa kuwa nayo yana nafasi kubwa sana katika kuraisisha zoezi hilo ndani ya jamii ya Kitanzania.

MWISHO

Tuesday, July 17, 2012

WANANCHI WAGOMEA MRADI WA BENKI YA DUNIA

MRADI wa ujenzi  dampo la kisasa wenye thamani ya shilingi bilioni 3 unofadhiliwa na benki ya dunia katika jiji la Arusha, upo hatari  kuyeyuka kufuatia wananchi wa kata ya Muriet manispaa ya Arusha kugoma kupisha eneo la  mradi huo licha ya kulipwa stahili zao .

Aidha mradi huo ambao ulikuwa uanze tangu april mwaka jana umeshindwa kuendelea kutokana na mvutano mkali ulipo kati ya wananchi zaidi ya 200 na manispaa ya jiji la Arusha ,ambapo wananchi hao wameilalamikia manispaa hiyo kwa kushindwa kuwalipa fidia ya maeneo yao waliyoyaendeleza ,huku manispaa hiyo ikidai imeshawalipa.

Akizungumzia swala hilo , Mkurugenzi wa manispaa ya Arusha, Bw Estomih Changa’h alikiri wananchi hao kuwa kikwazo cha kuanza kwa mradi huo huku akidai kuwa wafadhili wa mradi huo ambao tayari walionyesha nia na kuja na kupima katika eneo hilo wameanza kukata tamaa.

Alifafanua kuwa , baada ya kufanya tathmini ya awali mwaka jana walibaini kuwa wananchi 42 ndio  waliopo ndani ya  eneo husika la mradi ,hivyo manispaa ya Arusha ilifanya tathimin na kukubali kuwalipa  kiasi cha shilingi milioni 252 kama fidia ya makazi yao.

‘’tulipofanya tathimini ya makazi yao tulikubaliana kuwalipa wakazi hao 42,na kila mtu alipigwa picha akiwa amesimama mbele ya eneo ama nyumba yake,sasa tunasikitika sana kuona wakiendelea kunga’ng’ania huku kundi lingine la watu zaidi ya 200 wakiibuka kutaka nao walipwe fidia’’alisema Bw Chang’ah

Alisisitiza kuwa,tayari manispaa imeshawalipa wananchi 33 kati ya 42 kwa kiwango tofauti na kubaki wananchi tisa tu ambao walikuja kurubuniwa na kugomea malipo hayo.

Aliongeza kuwa, wananchi hao wamekuwa wakifika katika ofisi ya manispaa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha kudai fidia zao ambapo wamekuwa wakijaribu kuwaelewesha na uendesha vikao kadhaa, lakini wamekuwa wagumu kuelewa .

Mwenyekiti  wa kamati ya waathirika hao ,Jackson Japhet alisema kuwa, wao wanachotaka ni kutaka kulipwa fidia stahili ya makazi yao kwani  wengi wa wananchi wamekuwa wakiishi hapo muda mrefu na wamekuwa na makazi ya kudumu ,hivyo ni ngumu sana wao kuondoka katika eneo hilo.

Wakizungumza katika kikao cha hadhara katika eneo hilo la Muriet mwishoni mwa wiki, wameazimia kwenda mahakamani kusimamisha uanzishaji wa mradi huo  hadi manispaa hiyo itakapofanya tathimini upya kwa kuwashirikisha wananchi hao na kuwalipa fidia stahili bila kuwapunja.

Mwisho
SERIKALI imesema kuwa ipo kwenye mchakato wa kuviboresha viwanja mbalimbali vya ndege hapa nchini ukiwemo uwanja wa ndege wa Arusha kwa kuufanyia matengenezo makubwa uweze kuruhusu kutua kwa ndege kubwa za kimataifa.

Waziri wa uchukuzi ,dkt Harisson Mwakyembe aliyesema hayo jana baada ya kupokea taarifa fupi wakati akiongea na wafanyakazi wa kiwanja cha ndege cha Arusha baada ya kufanya ziara fupi mkoani hapa.

Dkt Mwakyembe alisema kuwa uwanja wa ndege wa Arusha unaumuhimu wa kipekee katika kuendeleza utalii wa ndani na kueleza kuwa serikali itafanya kila njia kuhakikisha kuwa uwanja huo unapanuliwa na kuwa na uwezo wa kutua ndege kubwa.

Alisema amekuwa akipata malalamiko mengi kuwa uwanja huo umekuwa ukitumika kunyangánya wateja wa uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) huku maombi hayo yakitaka uwanja huo ufungwe.

‘’nimepata taarifa za kutaka kufungwa kwa  uwanja huu wa ndege wa Arusha kwa kuwa unatumika kunyangánya abilia wa uwanja wa KIA ,nimejiridhisha kuwa kiwanja hiki kina umuhumu wa kipekee na serikali itaangalia uwezekano wa kukiboresha’’alisema Mwakyembe.

Alisema serikali itatenga fedha zaidi  kwa ajili ya kukiboresha kiwanja hicho ili kiwe cha kisasa zaidi ,ikiwa ni pamoja na kuviboresha viwanja vingine vya Songwe,Kigoma na Mwanza.

Awali Kaimu mkurugenzi wa kiwanja cha ndege cha Arusha,Mhandisi Suleiman Suleiman alisema kuwa kiwanja hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa eneo la maegesho ya ndege, jengo la abilia na jengo  la zima moto.

Alisema changamoto zingine ni pamoja na kutokuwa na taa zinazowaka majira ya usiku hivyo kutoruhusu ndege kutua ama kuruka nyakati za usiku,kituo cha umeme ,Mnara wa kuongozea ndege ,Jengo la hali ya hewa ,jengo la Mizigo  pamoja na miundombinu yake.

Aidha alisema kuwa ukarabati wa kiwango cha lami wa barabara ya kuruka na kutua yenye urefu wa mita 420 uliogharimu kiasi cha shilingi bilioni  1.7umefanya urefu wa barabara hiyo kufikia mita 1620 hivyo kuwezesha  ndege zenye ukubwa wa kubeba abilia 70 kuweza kutua katika kiwanja hicho.

Mhandisi Sulemeni aliongeza  kuwa kwa sasa kiwanja hicho kinahudumia wastani ndege 1700 kwa mwaka na abilia wanaohudumia kwa mwezi ni 12,000.

Alisema kuwa mpango wa sasa ni kuhamisha barabara ya Arusha Babati na tayari wamemweleza wakala wa barabara mkoani Arusha(Tanroads).

Aliongeza kuwa hatua hiyo itasaidia kuondoa msongamano uliopo sasa, pamoja na kuhamisha barabara ya sasa ya kuingia kiwanjani hapo kwani inaingiliana na maegesho.

ACHENI KUOMBA MAOMBI YA HASIRA DHIDI YA WALE WALIOJIBIWA

AMBAO  hawajibiwi maombi yao wametakiwa kuanza upya kuomba kwa kuwa wapo ambao hawajibiwi maombi yao kwa kuwa wanaomba maombi ya kukomoa na wala sio maombi ya unyenyekevu kama ambavyo Mungu aliagiza katika maandiko yake

Rai hiyo imetolewa na mchungaji Joseph Msengi alipokuwa akiongea  na waumini wa kanisa la FPCT Miembeni Usa River Wilayani Meru Mkoani hapa mapema wiki iliyopita

Mchungaji Msengi alisema kuwa watu wanatakiwa kujua jinsi ya kuomba kwa Mungu na hata kama maombi hayajibiwa hawapaswi kwenda kinyume cha mapenzi  kwa kuwa Mungu ana makusudio ya kila hitaji na kila ombi

“kuna watu ambao wanaomba maombi kwa kejeli mbele za Mungu na maombi ambayo wanayaomba ni maombi ya hasira kwa kuwa baadhi ya wengine pia wanaomba kwa kuwa baadhi ya majirani au ndugu zao  wamefanikiwa sasa je tunampangia Mungu kazi za kufanya jamani’aliongeza mchungaji huyo

Pia alisema kuwa kwa wale ambao hawajajibiwa wanatakiwa kuacha kuomba kwa hasira au kutoa maneno ambayo yanamfanya kazi za Mungu ziwe chini na badala yake wanatakiwa kuangalia ni yapi mapendekezo ya Mungu katika maisha ya kila siku ili maombi yajibiwe kwa haraka sana.

Hataivyo  aliongeza kuwa ni vema hata wakristo wakahakikisha wanafuatilia kwa karibu sana matakwa ya Mungu hasa kwenye biblia ambapo ndio muongozo wa maisha ya kila siku ingawaje kwa sasa biblia zinaoneka kubebwa kwa muda wa mara moja kwa wiki

‘jamani basi tuhakikishe kila sekunde na dakika tunaangalia mapenzi ya Mungu na kwa maana hiyo ukiangalia hata ndani ya makanisa yetu yeyote yule ambaye anafuatilia kwa karibu sana biblia hayumbi na imani wala haombi kwa hasira sasa kwa maana hiyo kwa nini tunaacha hili na kujiongoza wenyewe hii ni mbaya sana na ukiwa hivi utaoimba mpaka ‘alisema mchungaji Msengi.

Aliwataka wakristo kuhakikisha kuwa wanajitafakari kwa kina na kuanza kuomba hata toba hasa kwa wale ambao wanaomba maombi ya hasira ya kulipizana mali na vitu vya kidunia kwani maombi ya hasira ndio chanzo pekee cha kushindwa kujibiwa

MWISHO

ACHENI KUWAZIA UTAJIRI NA MALI ZA KIDUNIA BALI ANGALIENI UTUKUFU WA MUNGU KWANZA

IMEBAINIKA kuwa asilimia kubwa ya wakristo wanashindwa kufikia malengo yao mbalimbali kwa kuwa wameweka mawazo yao zaidi kwenye vitu vya kidunia kuliko kwa Mungu  hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana Umaskini wa leo

Hayo yameelezwa na Mchungaji Japhet Nanyaro wa kanisa la T.A.G Patmo Nkoanekoli  wilayani Meru  mkoani hapa wakati akiongea na waumini wa kanisa hilo wiki iliyopita

Alisema kuwa asilimia kubwa ya watu wanawaza sana fedha na utajiri wa dunia kuliko kuwaza na kutafakari utukufu wa Mungu hali ambayo inachangia sana kushindwa kusonga mbele zaidi katika matarajio yao mbalimbali

Aliongeza kuwa zipo hasara ambazo zinachangia kwa kiwango kikubwa sana ambazo zinatokana na kutafakari maisha ya kimwili kuliko maisha yale ya kiroho ambayo ndiyo yanayodumu zaidi hata baada ya maisha ya hapa duniani.

“ndani ya maisha ya leo unakuta kila mtu anatafakari jinsi atakavyoweza kupokea mali na fedha lakini hata kuchukua dakika moja na kumrudishia Mungu utukufu hamna sasa je tunasahau kuwa ambaye ametupa nguvu zaidi ya kuwaza tunamuacha wakati yeye ndiye muamuzi wa kila kitu ni vema sasa tukabadilika”alisema Mchungaji Nanyaro.

Awali alisema kuwa ni vema kama mawazo ya watu wa sasa wakabadilisha mtizamo wao na kumrudia mungu kwani hata hali ambazo zinawakabili watu wengi kwa sasa  kama vile Umaskini zinachangiwa  sana na kutafakari maisha ya kimwili kuliko yale ya Kiroho

Pia alisema kuwa ukiwa unataka utajiri wa kudumu hapa duniani ni lazima kwanza umtumike Mungu kwa moyo wako wote ili uweze kuzidishiwa yale yote ambayo unayataka ambapo ndio kusudio la mungu kumbariki yeyote yule ambaye analenga kumtegemea katika maisha yake yote ya hapa duniani

“Maandiko yanasema kuwa tunapswa kujua na kutambua kuwa tunatakiwa kusumbukia kwanza ufalme wa Mungu ili mengine yote tuweze kuzidishiwa na unapomsumbukia Mungu unapata hata kwa njia ambazo hauzijui sasa kwa nini usumbukie maisha yako wakati Mungu anaweza kukusumbukia kwa moyo wake wote”aliongeza Mchungaji Nanyaro

MWISHO

WILAYA YA MERU KUANZA KUWAPA VIJANA FURSA ZA KUIMARISHA UCHUMI WAO

WILAYA  YA MERU KUANZA KUWAPA VIJANA FURSA ZA KUIMARISHA UCHUMI WAO

WILAYA ya Meru Mkoani Arusha inatarajia kuanza kuwapa vijana wote wa Wilaya mbinu mbalimbali za kuweza kujikomba dhidi ya umaskini ambapo mbinu hizo zitachangia sana vijana kuacha kulalamika na kuona kama Serikali imewatenga huku wilaya hiyo ikiwa ni miongoni mwa Wilaya zenye rasilimali nyingi.

Hayo  yamebainishwa wilayani humo na Mkuu wa Wilaya hiyo Bw Munasa Nyirembe wakati wa zoezi la kumuaga aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo Bi Mecy Silla mapema jana Wilayani humo

Bw  Munasa alisema kuwa mpaka sasa kuna kila dalili za kuweza kuokoa uchumi wa kijana wa Meru kwa kuwa vitenda kazi muhimu vikiwemo Ardhi vipo vya kutosha na kutokana na hali hiyo sasa Serikali imeshajiwekea utaratibu a kuhakikisha kuwa vijana wanaanza kunufaika mapema hivi sasa

Alifafanua kuwa mbali na hilo pia wilaya hiyo itaaza kwa kuwapa mawazo ya kijisariamali vijana wa maeneo hayo ambapo zoezi la kuwapa mawazo pia litaenda sanjari na zoezi la kuwakuzia zaidi Uchumi wao kwa kupitia fursa mbalimbali ambazo wanazo

“tunaamini kuwa hawa vijana wa hapa Meri wakipatiwa hata elimu ya ujasiamali basi wataweza kujikomboa na Maisha mabaya ambayo wengi wanaishi huku fursa nazo zikiwa ni nyingi sana na kutokana na hali hiyo basi tunataka kuona kuwa kila kijana anapiga hatua kwenye uchumi na mtu wa kuweza kuwasaidia ni sisi Serikali kwa kuwa hata wanapofanya maovu sisi ndio tunakuwa katika heka heka Sasa kila mmoja wetu akikishe kuwa anakuwa na mchanganua hata wa idadi ya vijana aliona na kisha aweze kufikiri  pamoja nasi”aliongeza Bw Munasa

Pia alisema ili kuendelea kuboresha zaidi maisha ya vijana ambao ni wazawa wa Meru kuanzia sasa wawekezaji wote wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaachana na tabia ya kutoa ajira kwa vijana wan chi za nje na kuaawacha vijana wa Kimeru wakiwa wanaranda randa Mitaani

Alifafanua kuwa kila muwekezaji ndani ya Wilaya hiyo anatakiwa kuanza utaratibu wa kuhakikisha kuwa vijana wananufaika na utendaji kazi wao na kutokana na hilo pia litachangia sana maendeleo na hata uchumi wa Wilaya ya Meru

“Nawasihi sana wawekezaji ambao wapo kwenye wilaya hii ya Meru kuhakikisha kuwa wazawa ambao ni vijana wananufaika na uwekezaji wao ni vema hata wakarudisha fadhila kwa vijana kwa kuwa wanapowachukua wafanyakazi kutoka nje ya nchi je hawa vijana waende wapi kama sio kuwaonea jamani”Aliongeza Bw Munasa

Awali aliye kuwa mkuu wa wilaya hiyo ambaye kwa sasa ni mkuu wa Wilaya ya Mkuranga  bi Mecy Silla alisema kuwa hilo linatakiwa kuchukuliwa kama changamoto  na watu wote ndani ya Wilaya hiyo kwa kuwa vijana ndio taifa la kesho.

SERIKALI IJISAFISHE KWA KUWAKAMATA WALIOHUSIKA NA KIPIGO CHA DKT ULIMBOKA-

Na Queen Lema, ARUSHA

Askofu wa kanisa la KKKT dayosisi ya kaskazini Kati,Dkt Thomas Laizer ameyataka makanisa kujiwekea utaraibu wa kufanya maombi kila mara kwa kuwa sasataifa linapoteza rasilimali watu kutokana na migomo ambayo inaendelea kila mahala.

Dkt Laizer aliyasema hayo wakati wa ibada ya kuweka wakfu gari la kanisa la KKKT usharika wa Kimandolu mapema jumapili iliyopita jijini hapa.

Askofu huyo alifafanua kuwa kwa sasa Taifa la Tanzania lina ingia kwenye migogoro ya aina mbalimbali hali ambayo kama kanisa haitaliangalia kwa undani sana basi itaweza kupoteza mambo mengi

Alifafanua kuwa ni vema kuhakikisha kuwa kila mara maombi yanafanyika na kuliombea taifa kwa kuwa hiyo ni kazi mojawapo ya kanisa la leo na kanisa kama kanisa linanguvu kubwa sana ya kuweza kutetea jambo hilo

“leo madaktari wameingia kwenye migogoro na wamegoma lakini ukiangalia suala zima la vifo hasa kwa wanawake na watoto nalo linaongezeka sana sasa hali hii ni mbaya sana na kama hatutaomba rehema za Mungu juu ya nchi yetu basi hata kesho utasikia wengine nao wamegoma ingawaje kwa madaktari wanachokidai ni halali kabisa”alifafanua Dkt Laizer

Alisema kuwa ingawaje madaktari  hao wana haki ya kugoma lakini wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakumbuka kuwa na huruma ya Mungu kwa kuwa wanaokufa hawana hatia bali yenye hatia ni Serkali na kwa hali hiyo wanatakiwa hata kukumbuka amri za Mungu ambazo zinadai na kusema kuwa watu wanatakiwa kupendana.

Awali dkt Laizer aliongeza kuwa endapo kama kanisa litafanya maombi mbalimbali kwa taifa pia linatakiwa kuomba juu ya haki kwa kuwa kwa sasa kuna baadhi ya maeneo ambayo hayatoi haki kwa watanzania hali ambayo ndiyo chanzo kikubwa sana cha Rushwa.

“kwa sasa hivi rushwa imejaa kila mahali watu wananyimwa haki zao za msingi na hili limejitokeza hata kwenye uchaguzi wa EAC ambapo kulikuwa na rushwa nje nje na vyombo vy a usalama vilikuwa pale lakini hawaliangalia hilo na sisi kama tutaruhusu hilo ni wazi kuwa hata jamii zitakosa haki zao za msingi”aliongeza Dkt Laizer.

Katika hatua nyingine mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Bw Solomon Masangwa alisema kuwa mchakato wa kununua gari hilo  ulianza toka miezi michache iliyopita kutokana  na uitaji uliokuwepo

Bw Solomon alifafanua kuwa uitaji huo ulisababisha washarika waweze kuchanga zaidi ya Milioni 40 ili waweze kununua gari hilo ambalo wamenunua kwa ajili ya shuguli mbalimbali za kueneza injili.

Alizitaka sharika nyingine kuiga mfano kama huo ambapo waumini kama waumini wana uwezo mkubwa sana wa kununua vifaa maalumu kwa ajili ya kuendesha injili na kuacha kuwategema zaidi wafadhili.

TUMIENI MBINU ZA KISASA ZAIDI KATIKA ZOEZI LA SENSA ILI MSIWE CHANZO CHA HASARA KWA SERIKALI- RC ARUSHA

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA,ARUSHA

WAKUFUNZI  wa Sensa ya watu na makazi pamoja na wadau mbalimbali ambao watahusika katika zoezi la kuhesabu watu kwa mkoa wa Arusha wametakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia mbinu za kisasa zaidi ili kuwezesha zoezi hilo kufanikiwa kwa uraisi kwani kama halitafanikiwa litasababishia Serikali hasara kubwa sana.

Hayo yameelezwa na mkuu wa mkoa wa Arusha Bw Magesa Mulongo mapema jana wakati akifungua mkutano wa Wakufunzi wa Sensa kwa Mkoa wa Arusha

Bw Mulongo alisema kuwa endapo kama watalaamu hao watatumia utaalamu wao vizuri kutokana na mafunzo ambayo wameyapata basi wataweza kuokoa Serikali dhidi ya hasara mbalimbali ambazo zinaweza kutokea hasa pale zoezi hilo litakapokwama.

Alifafanua kuwa zoezi hilo lina umuhimu mkubwa sana na kwa hali hiyo ni vema kama watendaji wakuu wakawa makini kwa kuhakikisha kuwa wanakabiliana na Vikwazo ambavyo vinaweza kutokea wakati  wa zoezi hilo la Sensa ya watu na makazi linaloanza hivi karibuni.

“kama zoezi hili litakwama ni hasara kubwa sana kwa Serikali na hata kwa maendeleo ya jamii sasa nawasihi sana ninyi wadau hakikisheni kuwa mnakuwa makini na kama mdau hanaona kuwa atakuwa moja ya kikwazo cha Sensa ni bora akasema mapema na ajitoe kuliko kuwa chanzo cha kushindwa kufikia malengo”aliongeza Bw Mulongo

Pia alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanachangia maendelo ya nchi hasa kwenye zoezi hilo la Sensa kwani Serikali inapojua idadi ya watu wake inaweza kuraisisha shuguli mbalimbali za maendeleo ya Kijamii.

Awali Mratibu wa zoezi la Sensa kwa Mkoa wa Arusha Bi Magret Mutaleba alisema kuwa mpaka sasa maandalizi ya muhimu kwa ajili ya shuguli hizo za Sensa kwa Mkoa wa Arusha zimeshakamilika ambapo pia wanaendelea kutoa elimu kwa wahusika mbalimbali wa zoezi hilo ambalo linatarajia kuanza hivi karibuni.

Bi Magret aliongeza kuwa kwa sasa Wakufunzi  158 wanapata  elimu  juu ya kukabiliana na zoezi hilo ndani ya Mkoa wa Arusha ambapo wanatokea katika Halmashauri zote za jiji la Arusha na watapata mafunzo hayo kwa siku 12 huku lengo likiwa ni kuboresha zoezi hilo

“hawa Wakufunzi 158 ambao leo wamepewa mafunzo ni kwa ajili ya kuweza kuwapa na wengineo mafunzo ambapo na  wao watawapa watu kama vile makarani ambao nao watahusika katika zoezi hilo la Sensa na tunaamini kuwa kwa kutumian njia hii ya mafunzo basi itachangia sana kuraisisha zoezi hilo kwa uraisi zaidi”aliongeza Bi Magret

            MWISHO

WILAYA ZA LONGIDO,NA KARATU ZAONGOZA KWA KUWA NA WANAWAKE WAJAWAZITO WENYE VIRUSI VYA UKIMWI WENGI.

CHANZO CHA HABARI Na Queen Lema, ARUSHA

Imeelezwa kuwa idadi ya wanawake wajawazito waliohudhuria vituo vya afya  kwa mwaka 2011  na kupima virusi vya ukimwi walikuwa 48375  ambapo kati yao 1677 walikuwa wameathirika na Ukimwi huku wilaya za longido na Karatu zikiwa zinaongoza kuwa na idadi kubwa sana kwa mwaka 2011 mkoani Arusha.

Hayo yamebainishwa na Mganga mkuu wa hospitali ya mkoa wa Arusha(Mount Meru) Dkt Omary Chande wakati akiongea katika mahojiano maalumu  na vyombo  vya habari mapema jana mkoani hapa.

Aidha Dkt Chande  alisema kuwa  walifanikiwa kujua na kutambua kuwa idadi hiyo ya wanawake imeathirika mara baada ya kufanya vipimo maalumu ambavyo vinafanywa kabla ya kufikia hatua ya uzazi ili kuepusha madhara ya maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

“leo tunaweza kusema ,kuwa ndani ya wanawake hawa ambao wamefanikiwa kupimwa Ukimwi ambao ni kama asilimia 3 wameonekana kuathirika lakini ili kuokoa maisha ya mama na mtoto tulichokifanya ni kuhakikisha kuwa tunawapa elimu ya kujikinga na kuwalea watoto wao vema”aliongeza Dkt Chande.

Awali alisema kuwa zipo wilaya ambazo zinaongoza katika maambukizi ya Mama wajawazito ambapo Wilaya za Longido, na Karatu, na Manispaa ya Arusha zilionekana kukithiri kwa waathirika kutokana na kuwepo kwa migongano ya kijamii ambayo ndiyo chanzo kikubwa sana cha Magonjwa hayo

“hapa ukiangalia ndani ya Wilaya ya longido kuna maambukizi ya Ukimwi kwa kiwango cha asilimia 14, ikifuatiliwa na Karatu, kwa asilimia 4.7, huku nyingine ikiwa ni Manispaa kwa asilimia ni  asilimia 4 hali ambayo kwa kweli ni tishio kubwa sana lakini tunajikita sana kuhakikisha kuwa hawa watoto wanaozaliwa wanakuwa katika hali ya usalama zaidi”aliongeza Dkt  Chande

Katika hatua nyingine alisema kuwa kwa mwaka 2011 pia watoto zaidi ya 928 walikutwa wakiwa na virusi vya ukimwi ambapo kati yao asilimia 82 walinyosnyeshwa maziwa ya mama zao ambapo asilimia 18 walikuwa wanatumia njia mbadala  ili kuendelea kuishi.

Pia alifafanua kuwa kwa kipindi cha mwaka 2011 takwimu zinaonesha kuwa waki mama ambao wamejifungua hospitalini ni 33,643 ambapo kati ya hao 1907 hawakuwai kufika katika vituo vya afya wakati wakiwa wajawazito na hivyo hii kupelekea kuwepo kwa asilimia 6 ya wanawake ambao hawaeleweki kuwa kama wana maambukizi au hawana

Dkt huyo aliongeza kuwa kati ya hao asilimia 4 walikutrwa wakiwa tayari na maambukiz ya Ukimwi mara baada ya kupimwa huku wakiwa na ujauzito hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana kuwepo kwa changamoto hasa kwenye idara ya uzazi salama.

Hataivyo alitaja changamoto kubwa sana ambayo inaikabili idara lhiyo kuwa ni pamoja na kuwepo kwa amasa ndogo sana ya wanaume  ambao wamekuwa wakijitokeza kupima virusi vya ukimwi wakifuatana na wake zao katika vituo mbalimbali vya Afya,

Alifafanunua kuwa changamoto hiyo imekuwa ikichangiwa na mambo mbalimbali ndani ya jamii za kitanzania ikiwemo ukosefu wa elimu kwa makundi hayo, mila na desturi zilizopo katika jamii mbalimbali,pamoja na  hali ya uchumi hivyo juhudi za lazima zinahitajika kutoka kwa wadau mbalimbali katika kutoa elimu hiyo ili kuondokana na changamoto hizo

Mwisho

Wednesday, July 4, 2012

MTUME ARUSHA ADAI KUWA WAPO WAMILIKI, WACHUNGAJI,NA MAASKOFU WENYE HUDUMA KUBWA AMBAO WANAJIHUSISHA NA FREEMASONS ILI WAPATE FEDHA

HUYU NI MTUME HERBON AMBAYE ANA MAMBOZAIDI YA ELFU MOJA AMBAYO YANA HUSU MANABII WA UONGO NA VIONGOZI AMBAO WAPO KWENYE UTAWALA WA NGUVU ZA GIZA LAKINI WANATUMIA KOFIA YA YESU

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mtume mmoja wa jijini Arusha amesema kuwa kwa sasa zipo huduma kubwa za watumishi mashuhuri Tanzania ambao wanajihusisha na Nguvu za giza huku wakiwa wanatangaza Injili

Mtume huyo ambaye anatokea katika kanisa la Yesu ni bwana na mwokozi wa mataifa yote Bw Herbon Kisamo aliyasema hayo jana wakati akiongea na “UPAKO WA HABARI”mapema wiki hii jijini Arusha

Mtume huyo allisema kuwa Wamilikiu hao wa makanisa na wakuu wa huduma ambao wapo wengi sana na huku wengine wakiwa ni watu mashuhuri sana hapa nchini wanajiingiza kwenye ufalme wa Ki Freemasons ili waweze kupata fedha na waumini wengi sana

Aliongeza kuwa mpaka sasa ana ushaidi dhidi ya watumishi wa mungu wakubwa ambao wapo Kuzimu lakini wanaongoza ibada na kutoa ushuhuda wa uongo na bila kujua na kutambua kuwa wana mkasirisha sana Mungu

“hawa watumishi ambao wengine wanaonekana kama ni watumishi wa ukweli wanajiambatanisha na nguvu za giza na kisha wanatoa damu zao ili waweze kupata fedha na hata kwenye mitandao ya ki freemasons wanaonekana je hii ndio kazi ya Mungu kweli”alihoji Mtume huyo

Mbali na hayo aliongeza kuwa Mungu amempa ufunuo wa kuwasema hadharani wale wote ambao wanatumika kuzimu lakini wanashika biblia ya Mungu huku wakidai kuwa wanampenda na hatimaye wanawapeleka waumini wao kuzimu bila ya wao kujua

Alifafanua kuwa hapo awali alishawai kusema lakini Majeshi ya Kishetani ambayo yanaongozwa na watumishi hao yakaibuka lakini kwa kuwa ametumwa na Mungu hakuogopa hali kabisa

Alibainisha kuwa nao wakristo wanatakiwa kuhakikisha kuwa kila mara wanajilinda na kuomba sana Uweza wa Mungu uweze kuwatala kwa kuwa wengi wamekufa macho ya rohoni na ndio chanzo cha kupelekwa kwenye utawala  mwingine wa giza

Aliongeza kuwa mbali na ,kuwa na macho ya rohoni pia wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajijengea tabia ya kuwachunguza zaidi viongozi wao kwa njia ya roho mtakatifu na pia kujua kweli ya Mungu

“wapo baadhi ya wakristo ambao kila mara wanakimbilia zaidi muujiza bila kujiuliza muujiza huo umetoka wapi na sasa hawa  ambao wanakimbilia zaidi muujiza ndio hawana ambao wanatekwa na mambo kama haya”aliongeza Mtume Hebron

Ujangili mazao ya misitu KINAPA bado ni tatizo Kilimanjaro

Ujangili mazao ya misitu KINAPA bado ni tatizo Kilimanjaro

Hifadhi ya Kilimanjaro (KINAPA)
Na Mwandishi wa Thehabari.com-Moshi
TATIZO la ujangili wa mazao ya misitu katika Hifadhi ya Kilimanjaro (KINAPA) limeelezewa kukwamisha jitihada za Serikali ya Mkoa wa Kilimanjaro na hifadhi hiyo za kulinda na kuhifadhi mazingira.
Kutokana na matukio hayo ya ujangili katika hifadhi hiyo kuendelea kushika kasi takwimu zinaonyesha kuwa jumla ya majangili 921 wamekamatwa katika kipindi cha mwaka 2009 hadi juni 2012 wakiwa wanajihusisha na uharibifu wa mazao ya misitu ikiwa ni pamoja na ukataji wa miti ya asili kwa matumizi ya fito, kuni, Nguzo, Mbao na uchomaji moto katika misitu ya hifadhi.
Hayo yalibainishwa na mhifadhi wa Hifadhi ya Kilimanjaro KINAPA, Amani Shipella wakati akitoa mada juu ya ulinzi wa rasilimali za asili kwenye kikao cha wadau wa usimamizi wa sheria katika rasilimali za asili iliyohusiha maofisa maliasili, wanyamapori na vyombo vingine vya sheria wakiwemo Polisi na wanasheria.
Shipella alisema tatizo hilo la ujangili limeonekana kushamiri zaidi katika maeneo ya Longido mkoani Arusha, Siha na Hai mkoani Kilimanjaro ambapo wananchi wamekuwa wakiingia ndani ya hifadhi bila kibali na kufanya uharibifu wa mazao ya misitu.
Alisema ili kuweza kumaliza tatizo la ujangili ni vema wasimamizi wote wa sheria wakatoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kusimamia sheria za mazingira na rasilimali za asili kikamilifu.
Awali akifungua kikao hicho katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Dk. Faisal Issa alisema pamoja na jitihada mbalimbali ambazo zinafanywa na serikali ya mkoa wa Kilimanjaro bado kumekuwepo na uharibifu mkubwa wa mazingira ambao unafanywa na binadamu hali ambayo imesababisha kukauka kwa mazao katika kipindi cha msimu wa kilimo wa Masika kutokana na kukosekana kwa mvua.
Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya KINAPA, Erastus Lufungulo alisema lengo la kikao hicho ni kuweka nguvu za pamoja katika kudhibiti tatizo la uharibifu wa mazingira kutokana na kwamba kwa sasa hali ya uharibifu wa mazingira katika hifadhi hiyo bado ni kubwa.
Naye Oscer Ngole mwanasheria kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu Kanda ya Moshi ameishauri KINAPA kuweka utaratibu wa kuwashirikisha wananchi wanaozunguka hifadhi katika kulinda na kuhifadhi mazingira ili kuimarisha ujirani mwema.
“Kuna wananchi ambao wamekuwa wakikamatwa katika hifadhi kwa kosa la kukutwa wakikata majani, Kinapa iangalie namna ya kujenga ujirani na watu hawa ili kuhakikisha wanakuwa walinzi wa rasilimali za misitu,” alisema Ngole.

Polisi Kilimanjaro wakamata wahamiaji haramu 42

Polisi Kilimanjaro wakamata wahamiaji haramu 42

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Said Mwema
Na Mwandishi Wetu, Moshi
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia wahamiaji haramu 42 kutoka nchini Ethiopia na Somalia kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha sheria.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Robert Boaz alisema wahamiaji hao walikamatwa Julay mbili majira ya saa kumi jioni katika eneo la Kilototoni Himo wilayani Moshi.
Kulingana na taarifa ya kamanda Boaz Raia hao wa Ethopia na Somalia waliingia nchini kinyemela kupitia njia za panya na kwamba walikuwa wamejificha kwenye nyumba ya mtu mmoja ambaye hajafahamika kwa jina.
Alisema Raia hao waliingia nchini bila kuwa na vibali vya kuwaruhusu kuingia nchini na kwamba walikamatwa baada ya wananchi wema kutoa taarifa polisi kuhusiana na raia hao kuwepo maeneo hayo.
Alisema katika kundi hilo la wahamiaji haramu 39 ni Raia kutoka nchini Ethiopia na wengine watatu ni kutoka nchini Somalia. Aliwataja wahamiaji hao kuwa ni Abahamu Lamango, Dauji Elius, Terepes Lombebo, Eliso Ashe, Wolde Abuye, Muluneh Warko, Endele Mekengo, germelo Adero, Adamsu Yoikobo wote (25)
Wengine ni Ahamdin Mohamed, Tamraji anor, Fanus Krew, Dive Man, Taganye Phawuls, Tamama mekeyo, Masale Cufomo wote wakiwa na umri wa miaka 24 na Taregna Mengehah, Dembalo Adrea, Tarefa Abulee, Biranus Yohanis, Melese Gemeda, Denekel Kebeda, Mulunhe Danabo, Abyenh Landebi wote wenye umri wa miaka 22.
Abaine Lomore, Mesifin Mundido, Rebeba kofiso, Maratu Kabiro, Kasahun Acio, Fayhisa Lete, Budeta Beketa wote wakiwa na umri wa miaka 23 na kuongeza kuwa Bayonse Gernagano, Abeda Livanso, Seleman Himranm, wote wakiwa na umrei wa miaka 26.
Kamanda Boaz aliwataja wewngine kuwa ni Mamushi De Sita (28), na Keboda Mudamo, Yohanis Watharo ro(30) Kadri Amiri (18) wote raia wa Ethiopia na Raia wa Somalia ni pmoja na Mohamed Hasani (24) Mohamed Alii (28) na Rawud hasani (26).
Hata hivyo Kamanda Boaz hakuweza kuweka wazi kuwa raia hao waliingia nchini lini licha ya kueleza kuwa wameingia kwa kupitia njia zisizo sahihi na kwamba taratibu za kisheria zinafanyika ili kuweza kuwafikisha mahakamani.

MATUKIO YA UKUSANYAJI MAONI YA KATIBA MPYA MKOA KUSINI UNGUJA.

MATUKIO YA UKUSANYAJI MAONI YA KATIBA MPYA MKOA KUSINI UNGUJA.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ukusanyaji wa Maoni ya Katiba mpya Mohd Yussuf Mshamba akitoa Ufafanuzi wa namna ya Utoaji wa maoni unavyotakiwa huko katika kijiji cha Kibuteni Mkoa wa Kusini Unguja ikiwa ni siku ya Pili tokea kuanza kwa mchakato huo huko Zanzibar kushoto yake ni Mjumbe wa Kamati Salim Ahmed Salim na kulia yake ni Mjumbe wa kamati Richard Lyimo.
Mjumbe wa Kamati ya Ukusanyaji wa Maoni ya Katiba mpya Richard Lyimo akifahamisha nmna ya mchakato mzima wa kukusanya na kutoa maoni kwa wananchi unavyotakiwa huko katika Kijiji cha Kibuteni Mkoa wa Kusini Unguja kushoto yake ni Mwenyekiti wa Kamati hio Mohd Yussuf Mshamba.
Mwananchi wa Kijiji cha Kibuteni Riziki Wakili Haji akipeleka maoni yake kwa njia ya Barua  mbele ya kamati ya ukusanyaji maoni huko katika kijiji hicho Mkoa wa Kusini Unguja.
Wajumbe wa Ukusanyaji Maoni ya Katiba Mpya wakiwa katika Kazi ya kuandika maoni ya Wananchi mbalimbali waliokuwa wakitoa maoni yao huko katika kijiji cha Kibuteni Mkoa wa Kusini Unguja.
 
PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

TUPO PAMOJA KAMA MBINGU NA ARDHI

KAZI NA DAWA BWANA NIPO  RAFIKI YANGU KIPENZI KUSHOTO ROSE JACKSON KATIKA MJENGO MMOJA HIVI MAENEO YA KISONGO TUKIPERUZI YALIJOJIRI KATIKA MITANDAO MBALIMBALI

MAKANISA YATAKIWA KUOMBEA MASLAI YA WAFANYAKAZI WAKE

HUYU NI MCHUNGAJI JOEL KESSOI AKIWA ANATOA NENO LA KINABII KATIKA KANISA LA NGOME YA YESU KISONGO A-Z

MAKANISA YATAKIWA KUOMBEA MASLAI YA WAFANYAKAZI WAKE

WITO umetolewa kwa makanisa mbalimbali hapa nchini kuhakikisha kuwa yanajiwekea utaratibu wa kuombea mapato ya wafanyakazi wake kwa kuwa wengi wamekuwa wakipoteza hata haki zao  za msingi

Kauli hiyo imetolewa mjini Arusha na mchungaji Joel Kessoi  katika kanisa la Ngome ya Yesu lilopo Kisongo

Aidha mchungaji huyo alisema kuwa kwa sasa maslahi ya wakristo wengi sana wanaibiwa ovyo kwa kuwa baadhi ya waajiri wanashindwa kuwalipa na baadaye wakristo hao wanaishia kuteseka

Alisema kuwa endapo kama kanisa litasimama katika nafasi yake na kuanza maombi yake basi waajiri hasa wa viwanda ambao wananyima haki zao  na badala yake kuanza kuwakata wafanyakazi makato ambayo hayastaili.

“ukiangalia hawa wafanyakazi wa Viwanda kila siku wanalia na shida lakini wa nahaki sana ya kuweza kufanya kazi zao na kupewa wanachokitaka lakini kwa sasa kazi zao nyingi sana zimeingiliwa na shetani na wanakatwa hata makato ambayo hayastaili kwa kweli”aliongeza mchungaji Joel

Pia alisema kuwa kama kanisa litaendelea kuangalia suala hilo ambalo ndilo chanzo cha umaskini wa makanisa ya leo basi nafasi ya maombi inatakiwa kuanza kutumika katika kuombea wafanyakazi na makato yao

Alifafanua kuwa kwa kuanza kanisa hilo limeanza na mchakato wakuombea  wafanyakazi wa kiwanda cha A- Z ambao nao wamekatwa sana makato mengi ambayo hayana faida na wafanyakazi

Alisema kuwa kila mara watakuwa wanaombea wafanyakazi wa makampuni na viwanda mbalimbali katika maombi maalumu ili wawezen kufikia malengo yao ya msingi ambayo wamejiwekea na kuacha kuonewa hasa wakati wa kupewa haki zao

MWISHO

MTUME AWATAJA MANABII WA KIUNGO HAPA NCHINI

HUYU NDIYE MTUME HERBON MWENYE MAMBO ZAIDI YA 1000 YENYE KUSISIMUA AKILI JUU YA NCHI NA HUDUMA AMBAZO ZINAIBUKA KWAN WENGIN WAMEITWA KWENYE UTAWALA MWINGINE LAKINI WANATUMIA JINA LA YESU

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mtume mmoja wa jijini Arusha amesema kuwa kwa sasa zipo huduma kubwa za watumishi mashuhuri Tanzania ambao wanajihusisha na Nguvu za giza huku wakiwa wanatangaza Injili

Mtume huyo ambaye anatokea katika kanisa la Yesu ni bwana na mwokozi wa mataifa yote Bw Herbon Kisamo aliyasema hayo jana wakati akiongea na “UPAKO WA HABARI”mapema wiki hii jijini Arusha

Mtume huyo allisema kuwa Wamilikiu hao wa makanisa na wakuu wa huduma ambao wapo wengi sana na huku wengine wakiwa ni watu mashuhuri sana hapa nchini wanajiingiza kwenye ufalme wa Ki Freemasons ili waweze kupata fedha na waumini wengi sana

Aliongeza kuwa mpaka sasa ana ushaidi dhidi ya watumishi wa mungu wakubwa ambao wapo Kuzimu lakini wanaongoza ibada na kutoa ushuhuda wa uongo na bila kujua na kutambua kuwa wana mkasirisha sana Mungu

“hawa watumishi ambao wengine wanaonekana kama ni watumishi wa ukweli wanajiambatanisha na nguvu za giza na kisha wanatoa damu zao ili waweze kupata fedha na hata kwenye mitandao ya ki freemasons wanaonekana je hii ndio kazi ya Mungu kweli”alihoji Mtume huyo

Mbali na hayo aliongeza kuwa Mungu amempa ufunuo wa kuwasema hadharani wale wote ambao wanatumika kuzimu lakini wanashika biblia ya Mungu huku wakidai kuwa wanampenda na hatimaye wanawapeleka waumini wao kuzimu bila ya wao kujua

Alifafanua kuwa hapo awali alishawai kusema lakini Majeshi ya Kishetani ambayo yanaongozwa na watumishi hao yakaibuka lakini kwa kuwa ametumwa na Mungu hakuogopa hali kabisa

Alibainisha kuwa nao wakristo wanatakiwa kuhakikisha kuwa kila mara wanajilinda na kuomba sana Uweza wa Mungu uweze kuwatala kwa kuwa wengi wamekufa macho ya rohoni na ndio chanzo cha kupelekwa kwenye utawala  mwingine wa giza

Aliongeza kuwa mbali na ,kuwa na macho ya rohoni pia wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajijengea tabia ya kuwachunguza zaidi viongozi wao kwa njia ya roho mtakatifu na pia kujua kweli ya Mungu

“wapo baadhi ya wakristo ambao kila mara wanakimbilia zaidi muujiza bila kujiuliza muujiza huo umetoka wapi na sasa hawa  ambao wanakimbilia zaidi muujiza ndio hawana ambao wanatekwa na mambo kama haya”aliongeza Mtume Hebron

MWISHO

KANISA LA KKKT KIMANDOLU LAFANIKIWA KUNUNUA GARI JIPYA LENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 40

ASKOFU THOMAS LAIZER AKIWEKA WAKFU GARI LA KANISA KIMANDORU

  Askofu wa Kanisa la Kiinjili Kilutheri tanzania
dayosisi ya kaskazini kati Dr Thomas Laizer akizindua rasmi gari la
usharika wa kimandolu uliopo mijini hapa ,mapema leo hii .
Gari ambalo lilizinduliwa rasmi  ambalo ni gari aina
ya Rord Renger  namba za usajili T 474 BRS lenye thamani ya
shilingi milioni 40 ambapo waumini wa usharika huo  walitoa michango
yao  kwa ajili ya kununua gari hilo ili limwezeshe mchungaji wa kanisa
hilo kufanya kazi yake kiufanisi.Picha na Queen Lema, Arusha

WAUMINI WANUNUA GARI AINA YA FORD RANGER LA ZAIDI YA MILIONI 40 KWA AJILI YA SHUGULI ZA INJILI