Wednesday, September 5, 2012

WAUMINI WACHANGA MILIONI 5 KWA AJILI YA KUONGEZA ENEO LA KANISA,MCHUNGAJI WAO AWATAKA KAMWE WASIWE NI WATEGEMEA WAFADHILI WA NJE


Na Bety Alex, ARUSHA

WAUMINI WACHANGA MILIONI 5 KWA AJILI YA KUONGEZA ENEO LA KANISA,MCHUNGAJI WAO AWATAKA KAMWE WASIWE NI WATEGEMEA WAFADHILI WA NJE

MAKANISA ya leo yametakiwa kuacha tabia ya kuwategemea zaidi wafadhili  hasa katika kuchangia masuala mbalimbali ya maendeleo ya makanisa yao kwani hali hiyo husababisha kwa kiwango cha hali ya juu sana wafadhili hao kukomba baraka huku wenyeji wakiwa hawana baraka kutoka kwa Mungu.

Ni vizuri kama wakristo wao wenyewe wakawa ni wafadhili na kama watajijengea tabiaya kujichangia wao wenyewe basi kwa kiwango cha hali ya juu sana watasababisha hata kizazi cha watoto wao kukua katika msingi wa imani ambao unawataka wao wenyewe waweze kujitegemea zaidi

Kauli hiyo imetyolewa na Mchungaji Elinaisha Ayo wa kanisa la FPCT Sombetini Mkoani hapa wakati akiongea katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo mapema Wiki iliyopita ambapo pia ibada hiyo ya Harambee ilienda sambamba na Mahubiri ya kukataa kuwa tegemezi kwa wafadhili wa nje

Mchungaji huyo alisema kuwa ni vizuri sana kama Wakristo wakahakikisha kuwa wanaaachana na tabia ya kuwawazia wafadhili kuja kuwapa msaada ilihali wao wanaweza kujichangia na kama makanisa yataendelea kuwategemea zaidi wafadhili ni wazi kuwa hata kizazi kijacho nacho kitakuwa ni kizazi tegemezi zadii

Alisema kuwa kama wakristo wakiwa na Umoja wataweza kuchangia maendeleo ya makanisa yao na hivyo hali hiyo itafanya hata kazi ya injili kuwa raisi sana na hivyo hata wale ambao wanachangia huduma mbalimbali nao wataweza kupata baraka tofauti na pale ambapo wafadhili wanatoka nje ya nchi na kuja kusaidia makanisa

“leo unakuta kanisa lina uhitaji ili liweze kufanikisha zoezi hilo linawafikiria zaidi wafadhili na kama maandiko yanavyosema ni kuwa kila atakayefanya kazi ya bwana kwa umakini na kwa moyo ndiyon atakaye barikiwa sasa hapa hawa wafadhili wote wataondoka na baraka na sisi tutabaki kama tulivyo tuache kufikiria kusaidiwa bali tufikirie zaidi jinsi ya kujisaidia sisi wenyewe’aliongeza mchungaji Elinaisha

Pia aliongeza kuwa kama makanisa ya leo yatakuwa na desturi ya kujichangia basi hata watoto wadogo nao watakuwa na moyo wa kuweza kuchangia kwa kiwango kikubwa kazi mbalimbali za injili ambapo hata kwa kizazi chao nacho kitakuwa na Utoaji mzuri sana tofauti na pale ambapo wazazi na walezi wanapowafikiria sana wafadhili kuja kuwasadia

“Tunachokipanda ndicho kitakachokivuna na kama tukipanda mbegu bora ndio itakayoweza kuwasaidia hawa watoto wetu kwa maana hiyo basi kuanzia sasa tunaanza kujiopanga ndani ya makanisa yetu hasa hapa Sombetini na watoto nao wawe ni wachangiaji hasa wa harambee kama hizi kwa manufaa ya hapo baadaye”aliongeza Mchungaji Elinaisha

Akiongelea harambee hiyo ambayo ilifanyika kanisani hapo alisema kuwa Wakristo wa kanisa hilo wamefanikiwa kuchanga kiasi cha zaidi ya milioni tano ambazo zitatumika kwa ajili ya kupanua eneo la Kanisa hilo huku lengo halisi likiwa ni kueneza Injili ndani ya eneo hilo la Sombetini na Mkoa wa Arusha kwa ujumla

MWISHO

No comments:

Post a Comment