Friday, September 28, 2012

JAJI NYERERE ASISITIZA WANANCHI KUJITOKEZA KATIKA MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Na Ashura Mohamed,Arusha

JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Jaji Aisha Nyerere,amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuweza kujitokeza kwa wingi katika kutoa maoni juu ya katiba mpya.

Aidha mashirika,taasisi zilizo za kiserikali au zisizokuwa za kiserikali kutumia nafasi zao kuisaidia serikali kuhamasisha umma juu ya umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika mchakato huo.

Jaji Nyerere aliyasema hayo juzi mjini hapa wakati alipokuwa akizindua vitabu vya uwajibikaji wa makampuni kwa jamii pamoja na kitabu kinachohusu haki za jamii katika maeneo ya uwekezaji,uzinduzi ulioenda sambamba na maadhimisho ya miak 17 ya Kituo cha sheria na haki za binadamu(LHRC).

“Napenda niwakumbushe watanzania kuwa kwa sasa taifa letu lipo katika mchakato wa kutunga katiba mpya,mchakato huu upo katika hatua za mwanzo kabisa ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi,hivyo kwa kuzingatia hayo napenda kuwahimiza ninyi na raia wengine kushiriki kikamilifu kikamilifu kutoa maoni yenu”

“Kituo cha sheria na haki za binadamu pamoja na watu wengine wenye nafasi na uwezo wa kutoa elimu kwa uumaa kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima,mnapaswa kutumia vema nafasi zenu”alisema na kuongeza
Jaji huyo alisema kuwa watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali hivyo wanapaswa kuungwa mkoni kwani utetezi wa haki za binadamu ni wajibu wa jamii nzima.

“Watetezi wa haki za binadamu wanaweza kuisaidia serikali katika uendelezaji na kulinda haki za binadamu na ni nafasi pekee kutengeneza misingi imara ya kuwatetea na kuwalinda watetezi wa haki za binadamau na kuna nafasi nzuri kama wakati huu wa mchakato wa kuhakikisha kuwa haki za binadamu na matamko mbalimbali ya kimataifa yanaridhiwa na kuwekwa katika katiba mpya kwani hii itakuwa na mchango mkubwa sana katika kulinda haki za binadamu na watetetzi wa haki hizo”alisema Jaji Nyerere

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Dk.Hellen Kijobisimbo alisema kuwa baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa ziliwakabili katika kutekeleza majukumu yao ni pamoja na sheria kwua kandamizi,hata wanapokuwa wanapokuwa wanamsaidia mtu kisheria,sheria zimekuwa zikiwakandamiza.

Alitaja changamoto nyingine kuwa ni tatizo la mfumo wa mahakama ambapo mashauri yamekuwa yakichukua muda mrefu hadi kukamilika,wasaidizi wa kisheria kutokutambulika.
Dk.Hellen aliongeza kuwa vyombo vya dola navyo vimekuwa ni tatizo kwao kwani wakati mwingine wao wakiwa katika majukumu yao ya utetezi,vyombo vya dola vimekuwa vikiwaona wao ni wapinzani wakati wao ni wasaidizi wa serikali.

Naye Mratibu wa Kitengo cha uwajibikaji wa makampuni na mazingira(LHRC) Wakili Flaviana Charles akizungumza wakati wa uzinduzi wa vitabu hivyo alisema kuwa sheria ya uwekezaji hapa nchini haina vifungu vyenye kutoa wajibu wa wawekezaji kwa wananchi jambo linalosababisha jamii kutokunufaika na miradi ya uwekezaji inavyotekelezwa katika maeneo husika.

Aliongeza kuwa ukosefu wa sheria inayosimamia uwajibikaji wa makampuni kwa jamii umepekelea kuwepo kw augumu wa kuzichukulia hatua za kisheria kampuni zinazoshindwa kutimiza wajibu wake kwa jamii,ambayo imesababisha uwepo kwa migogoro isiyoisha ndani ya jamii.

No comments:

Post a Comment