Friday, September 7, 2012

BONDIA MAUGO KUPAMBANA ARUSHA 28 0CTOBER NA KUSAKA VIPAJI


BONDIA MAUGO KUPAMBANA ARUSHA 28 0CTOBER NA KUSAKA VIPAJI

NA QUEEN LEMA,ARUSHA

Kampuni ya Mnyalu Entertiment kwa kushirikiana na Bondia maarufu hapa nchini Mada Maugo watarajia kuibua vipaji vingi kwa kanda ya kaskazini hususani ndani ya mkoa wa Arusha October 28 mwaka huu  ambapo pia mabondia mbalimbali watapimana uzito akiwemo yeye mwenyewe na Bondia Gavad Zohrenvard wa Iran huku wanamichezo wengine kama vile diwani na mfanyabishara maarufu Mjini Arusha Bw Justin Nyari naye atashiriki

Kwa mujibu wa bondia Mada Maugo alisema kuwa Onyesho hilo ambalo litafanyika katika viwanja vya Triple A litakuwa ni moja ya michezo ambayo mbali na kuburudisha pia litachangia kwa kiwango kikubwa sana hata kuibua vipaji ambapo naye diwani wa kata ya Mirerani naye atashiriki na kiongozi yeyote wa Upinzani

Bondia Maugo alisema kuwa mpaka sasa ndani ya mkoa wa Arusha kuna Vipaji vya hali ya juu sana lakini jambo la kushanga za mpka sasa vipaji hivyo havijawaeza kubebwa na kuonekana hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa wapiganaji hao kupoteza vipaji

Akiongelea vipaji hivyo alisema kuwa yeye anatarajia kucheza na bondia  wa Iran ambapo mbali nay eye kucheza pia ataweza kuwapa fursa hata wengine kutoka Arusha na kuweza kushiriki ambapo katika kufufua Vipaji watacheza  watu mbalimbali

“Mimi nitashiriki katika michuano hiyo siku hiyo na nitapambana na  bondia wa Iran lakini pia mpaka sasa na wadau wengine akiwemo diwani wa Mererani Simanjiro naye amedhibitisha kushiriki na kuchuana vema na mwanasiasa yeyote hasa wa  upinzani nah ii itachangia kwa kiwango kikubwa sana kuweza kuboresha na kuendelea kuibua vipaji mbalimbali kwani ndani ya mkoa wa Arusha kuna vipaji vya hali ya juu sana”aliongeza  Bw Maugo

Pia alisema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano kama sita hivi ambapo ni ya utangulizi na bondia wa Arusha Robert Mroso atapambana na bondia Selemani Tall kutoka Dar,chini ya uzito wa kilo 72 na watacheza kwa Raundi nane na pia tuna bondia mwingine ambaye ni Abasi Ally wa Arusha naye atapamnbana na Joseph Marwa kutoka Zanzibar chini ya uzito wa kilo 80.

Mbali na hayo alisema kuwa mabondia hao watachuana kwa hali na mali ambapo pia wataweza kuburudishwa na makundi mbalimbali ya wanamuziki kama vile Dogo janja,Ras Lion,John Oka, na makiundi mengine mengi huku mgeni rasmi akiwa anatarajiwa kuwa Mzee Edward Lowasa

Katika hatua nyingine alisema kuwa kwa sasa kuna umuhimu mkubwa sana wa wadau mbalimbalui kuhakikisha kuwa wanawekeza zaidi katika Michezo hasa kwa kuwa una hamasa kubwa sana na unaweza kutumika kama njia ya kuweza kuwasaidia waepukane na matizo mbalimbali ambayo yapo kwenye jamii hasa ya ukosefu wa ajira

MWISHO

No comments:

Post a Comment