Friday, September 28, 2012

NAIBU WAZIRI ASHIKWA NA BUTWAA JUU YA MALIPO YA MKANDARASI UWANJA WA NDEGE KISONGO


NAIBU WAZIRI ASHIKWA NA BUTWAA JUU YA MALIPO YA MKANDARASI UWANJA WA NDEGE KISONGO 

NA ASHURA MOHAMED,ARUSHA

Naibu waziri wa Uchukuzi mhandisi dkt.Charles Tizeba ameiagiza mamlaka ya Viwanja vya ndege(TAA) kukaa pamoja na mkarandarasi wa kampuni ya Harising and Sons ili kukubalina namna ambavyo wanaweza wakafanya marekebisho ya kipande cha barabara cha mita 420 ili mkandarasi huyo aweze kumaliziwa malipo yake.

Ameyasema hayo mara baada ya kufanya ukaguzi katika barabara hiyo ya kurushia na kutua ndege iliyopo ndani katika kiwanja kidogo cha ndege kilichopo kisongo nje kidogo mwa jiji la Arusha.

Dkt.Tizeba amesema kuwa ni vyema kama pande hizo mbili zikakaa pamoja ili kupata muafaka kwa kuwa Mhandisi Mshauri alipendekeza marekebisho yafanyike baada ya msimu wa mvua kumalizika na wamiliki wa viwanja wanahitaji marekebisho yasisubiri msimu kumalizika.

Aidha amefafanua kuwa endapo pande hizo mbili zitakubaliana basi ni wazi kuwa mkandarasi atapatiwa fedha zake zote zilizobakia ambapo amesema kuwa mpaka sasa tayari ameshapatiwa malipo kwa asilimia 60 tu.
naibu waziri wa uchukuzi amesema kuwa mradi huo tayari umeshakamilika kilichokuwa kinasubiriwa ni makabidhiano tu ambapo mkandarasi anaona amefanya kazi vizuri huku mwenye kiwanja anaona hajakamilishiwa uwanja wao.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya viwanja vya ndege injinia White Majula amesema kuwa kuotokana na ubovu wa miundombinu uliokuwepo mamlaka ya viwanja vya ndege imekuwa ikifanya ukarabati wa barabara ya kuruka na kutua ndege kwa kiwango cha lami ambapo kwa mwaka 2011-2012 wamekarabati meta 420 kwa kiwango cha lami ili kukamilisha urefu wa meta 1620 zilizopo.

Pia ametaja baadhi ya changamoto ambazo bado zinahitaji kupatiwa marekebisho mara moja kuwa ni pamoja na Mwiingiliano wa barabara ya magari Arusha-Minjingu na miundo mbinu ya kiwanja ambayo imejengwa ndani ya eneo la kiwanja hivyo kutishia usalama wa kiwanja ambapo licha ya kujadiliwa na Mkoa wa Arusha,TAA,TANROADS na Wizara ya Uchukuzi, bado suala la kuhamisha barabara hiyo halijapatiwa ufumbuzi.

Lakini hata hivyo Injinia Majula amesema kuwa kutokuwepo kwa jengo la Abiria kumeathiri huduma ya kiwanja kutokana na ufinyu wa bajeti,Mmlaka ya Viwanja vya Ndege inaendelea kutafuta wabia kupitia sekta binafsi ili kufanikisha mpango huu.

Kiwanja cha ndege cha Arusha kilianzishwa mwanzoni mwa miaka ya 1950,kikiwa kinamilikiwa na mjasiriamali wa kizungu na kilimilikishwa rasmi serikalini mwishoni mwa miaka ya 1960 ambapo kina barabara moja ya kuruka na kutua ndege ya kiwango cha lami yenye urefu wa meta 1620 na upana wa meta 30 inayotumika kwa ndege zenye ukubwa na uwezo wa kubeba abiria 70 mfano ATR 72.

Mwisho…………………………….

No comments:

Post a Comment