Sunday, September 30, 2012

Mchungaji Dr. Emmanuel Kandusi, manusura, mwathirika ahudhuria kongamano la saratani ya tezi dume Washington DC

Katika picha ni Dr. Kandusi akimkabidhi magazeti ya MAN Rais na Mwanzilishi wa Prostate Health Education Network Ndugu Thomas Ferington. Ndugu Farrington naye ni manusura, mwathilika na mhanga wa saratani ya tezi dume.
…………………………………………..
Mchungaji Dr. Emmanuel Kandusi, manusura, mwathirika na mhanga wa saratani ya tezi dume (prostate cancer) na mwanzilishi wa Tanzania 50 Plus campaign akiwa Washington DC nchini Marekani kwenye Kongamano (Summit) la saratani ya tezi dume linaofanyika katika jengo la Maseneta wa Marekani Russell Hall Capitol Hill.
Katika kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa na waathilika na wanaharakati wa saratani ya tezi dume na baadhi ya Maseneta na Wabunge (Members of Congress) ulijadili pamoja na mambo mengi umuhimu wa kutoa elimu katika jamii juu ya saratani ya tezi dume na umuhimu wa kutoa tiba ya kisasa kwa watu wote na mahali popote.

Kongamano liliohudhuriwa na washiriki takribani mia moja, liliandaliwa na shirika la hiari Prostate Health Education Network la Marekani na lenye makao makuu huko Boston. Shirika hilo linakazia “Knowledge is the best defense against prostate cancer”.
Kongamano liligundua kuwa kwa kutoa elimu katika jamii utawezesha kupunguza magonjwa ya saratani (prevention is better than cure) kwa watu wengi. Watu wakielimika na kupata elimu juu ya hali hatarishi, umuhimu wa kubadili maisha yao kwa kula vyakula asilia, kufanya mazoezi, kujiepusha na utumiaji wa tumbaku wa aina yote, kupiga vita unene hatarishi itapunguza sana watu kupata saratani.
Hii itaokoa nguvu kazi na kuokoa pesa nyingi ambazo zinaweza kutumika kwa maendeleo mengine.

No comments:

Post a Comment