mkuu wa wilaya ya Meru akifafanua jambo wakati wa mkutano wa TCRA na wadau wake jijini Arusha mapema leo

hawa ni wadau mbalimbali wa mkutano huo wakiwa wanafuatilia baadhi ya mada kwa makini sana ambapo baadhi yao ni madiwani wa manispaa ya Arusha,picha zote na Rose Jackson,Arusha

 HABARI NA ROSE JACKSON,ARUSHA
WAtanzania wametakiwa kujiandaa kuhama katika mfumo wa mabadiliko ya
anaelojia kwenda katika mfumo wa digital ambao hadi ifikapo desemba
31 mwaka huu matangazo ya anaelojia yatazimwa rasmi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa mkurugenzi mkuu wa
mamlaka ya mawasiliano Tanzania (tcra)bw Frederick Ntobi amaesma kuwa
kuanzia januari 2013 wananchi hawataweza tena kutumia mfumo uliopo wa
sasa wa anaelojia.
Amesema kuwa ili kwenda na utandawazi uliopo hadi ifikapo januari 2013
dunia nzima itakuwa imehama katika mfumo wa kutumia anaelojia katika
luninga zao hivyo ni vema wananchi wakaanza kujipanga mapema ili
kuhakikisha kuwa kila mtu anafikiwa na huduma hiyo.
Amengeza kusema ku wa ili mfumo huoi ukamilike ni vema jamii
ikahakikisha kuwa lazima inakuwa na kifaa kiitwacho kingamuzi ambacho
ndicho kinatumika katika kubadilisha mfumo ili kuweza kufanikiwa
katika ubadilishaji huo.
Bw ntobi ametaja faidsa ya kutumia mfumo huo kuwa ni pamoja kuwa na
matumizi bora ya masafa ,kupata huduma bora za ziada mfano kulipia
bili ya umeme,kutuma pesa pamoja na kupata intenet pindi uwapo kwenye
luininga zao
Pia alitaja faida ingine kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa ajira kwa
kuwa mfumo utachangia kuongezeka kwa makampuni nmengi ya utangazaji.


mwiosho .