Friday, September 14, 2012

MUINJILISTI WA EAGT ATUMIA MSTARI WA ZAKARIA 4.6 KATIKA UCHAGUZI WA UVCCM NA AIBUKA MSHINDI KAMA MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA MANISPAA YA ARUSHA



hapa ni mwenyuekiti huyo ambaye pia ni muinjilisti wa kanisa la EAGT Sinoni akiwashukuru vijan a wa ccm kwa kumpa dhamana ya kuongoza





MUINJILISTI WA EAGT ATUMIA MSTARI WA ZAKARIA 4.6 KATIKA UCHAGUZI WA UVCCM NA AIBUKA MSHINDI KAMA MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA MANISPAA YA ARUSHA


Na Be ty Alex, ARUSHA

MUINJILISTI wa kanisa la EAGT Sinoni mjini hapa amefanikiwa kushinda kinyanganyiro cha mwenyekiti wa umoja wa Vijana (UVCCM)na kuweza kuweka historia kuwa hata viongozi mbalimbali ndani ya makanisa wana nafasi kubwa sana ya lkushiriki chaguzi mbalimbali ndani ya Nchi

Akiongea na nyakati mara baada ya kushinda mwenyekiti huyo ambaye ni Martin Munisi alisema kuwa ameamua kushiriki katika chaguzi hizo kwani bado kuna uwezekano mkubwa sana hata watu wanaomjua Mungu kuweza kuchukua nafasi ya uongozi

Bw Martin alieleza kuwa hapo awali alilazimika kutumia biblia ambayo ina mistari imara na kuweza kuomba nafasi kwenye chama hicho ambapo alipinzana na watu wengi ambao walikuwa wanaonekana kama wana uwezo mkubwa sana lakini baadaye Mungu alimtetea zaidi

“Unajua wartu wengi sana wanaogopa Siasa lakini kama sisi ambao tunajua kweli ya mungu tutafanya siasa tutaweza kuokoa walio wengi zaidi kwani tutaweza kuhubiri kweli na kweli hiyo ikaweza kuwaweka watu huru tofauti na pale watu wa mungu watakapokuwa wanaogopa siasa na huu ni muda mzuri sana kwa Kanisa kusimama na kutafuta nafasi mbalimbali za uongozi wan chi”aliongeza bw Martin


Alifafanua kuwa  lengo halisi la kugombea ilihali yeye ni muinjilisti ni kuhakikisha kuwa anawavutia hata watu wengine nafasi ya kugombea huku wakiwa wanamjua Mungu na kutokana na hili wataweza kufanya asilimia kubwa sana ya Viongozi kujikwepa na dhambi ambayo ni tishio kubwa sana.

Aliendelea kusema kuwa kwa watu ambao wanamjua Mungu wana uwezo mkubwa sana wa kuweza kupata nafasi za uongozi kwani Muongozo mzuri ni biblia na sasa bado kuna changamoto kubwa sana katika kutetea haki za taifa la Tanzania ya leo

Alibainisha kuwaendapo kama wana wa Mungu watajitokeza kwa wingi basi watasaidia kuwapa changamoto ya kufanya hata vema baadhi ya viongozi ambao wapo maldarakani lakini wanatumia vibaya nafasi zao za uongozi hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana madhara ya Umaskini, na Umwagaji wa damu ambazo hazina hatia mbele ya macho ya Mungu

“Nawasihi sana watu wa mungu kuhakikisha kuwa pindi mpapokweda kugombea mtumie Biblia na imani zenu ziwe juu tukiwa wengi ambao tunamjua Mungu itaweza kutusaidia sana sisi kuweza kupata nafasi ya kupambana na maadui mbalimbali ambao ndio chanzo cha kuyumba kwa maisha ya mtanzania kwani mimi nilitumia kitabu cha Zakaria 4.6 na nikapata ambacho ninakipata”aliongeza Bw Martin

Pia alisema kuwa ili kufanikisha kazi ya Mungu na siasa ana mikakati mbalimbali yan kuhakikisha kuwa Vijana wa kitanzania hususani wa mkoa wa Arusha wanainuka Kiimani sanjari na kuongeza na kuimarisha chama cha kuweka na kukopa ili waweze kujikwamua kimaisha kwani wengi wao hawana hata mitaji ya kujiendesha wao kwa wao.

MWISHO

No comments:

Post a Comment