Wednesday, November 28, 2012

KAMPUNI YA CHINA YA CHICO IMEJITOLEA KUTUMIA MILIONI 50

Na Joseph Lyimo,MANYARA

KAMPUNI ya Ujenzi ya China ya Chico imejitolea kutumia sh50 milioni kwa ajili ya ukarabati wa kituo cha magari ya kubeba abiria kilichopo mjini Babati Mkoani Manyara ili kumaliza kero iliyopo kituoni hapo mvua zinaponyesha.

Akizungumza juzi mjini Babati mbele ya viongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo wakati wakuanza kukarabatiwa kituo hicho,msemaji wa kampuni ya Chico,Yan Wangting alisema lengo lao ni kutoa msaada kwa jamii inayotumia kituo hicho.

Wangting alisema Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Babati,Mohamed Farah alizungumza naye na kuomba msaada wa kukarabatiwa kituo hicho ambacho wakati mvua zikinyesha kunakuwa na kero ya madimbwi ya maji.

Alisema kuwa ili kushiriki shughuli za maendeleo,kampuni ya Chico imejitolea kufanya kazi hiyo bure ili kuondoa adha ya wasafiri na magari yanayotumia kituo hicho hasa kero ya maji wakati mvua zinaponyesha.

“Lengo la kampuni ya Chico kukarabati kituo hiki ni kutoa mchango wetu kwa jamii ambapo tunatarajia kutumia siku tatu hadi nne katika kuhakikisha kuwa kazi hii imekamilika na kituo kinaendelea kutumika,” alisema Wangting. 

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa halmashauri ya mji huo,Mohamed Farah aliipongeza kampuni hiyo kwa kujitolea kukarabati kituo hicho cha mabasi cha mjini Babati ili kiweze kutoa huduma ipasayo ya usafiri mjini hapo.

“Tunaishukuru kampuni ya Chico kwa kuamua kutukarabatia stendi yetu na wananchi wasiwe na wasiwasi wala hofu ya kuona ukarabati ukiendelea ila mnapaswa kutambua huu ni msaada tu na siyo vinginevyo,” alisema Farah.

Alisema hivi sasa magari ya usafiri ya mji huo yanatoa huduma hiyo kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa Kwaraa kwa muda wote ambapo ukarabati wa kituo ukiendelea hivi sasa.

Naye,Kaimu Mkurugenzi wa mji wa Babati,Winnie Kijazi alisema ili kuunga mkono msaada huo uliotolewa na kampuni ya Chico,jamii inapaswa kutunza mradi huo pindi utakapokamilika.

“Tunaishukuru sana kampuni ya Chico kwa kutukarabatia kituo hiki na tunapaswa kuuenzi msaada huu kwa kuitunza miundombinu yetu ya kituo chetu ili kiweze kutunufaisha kwa muda mrefu zaidi,” alisema Kijazi.

Kampuni ya Chico ndiyo iliyojenga barabara ya Minjingu-Babati ambapo mwanzoni mwa mwezi huu,Rais Jakaya Kikwete aliizindua barabara hiyo ambayo imerahisisha usafiri wa kutoka mkoani Manyara hadi Arusha.

MWISHO.

Saturday, November 24, 2012

Diwani wa Chadema atimkia CCM



Katika hali isiyokuwa ya kawaida aliyekuwa diwani wa Chadema kata ya Olasiti viti maalumu mkoa wa Arusha Rehema Mohamed amekikacha chama chake na kurudi katika chama tawala

akiongea mara baada ya kupokelewa ndani ya chama tawala na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo Kinana,Nape.,Lowasa,Chatanda,alisema kuwa anazo sababu za msingi ambazo zimemfanya afanye mabadiliko

hatahivyo Malkia wa matukio Arusha amemtafuta rehema na akadai kuwa siku chache atafunguka zaidi kuhusiana na Chadema,

Ingawaje Rehema ni miongoni mwa madiwani walitakiwa kulipa kitita cha fedha baada ya kushindwa kesi iliyokuwa inawakabili ya kunyanganywa Unachama wa Chadema

VIJANA 200 WA VYUO VIKUU ARUSHA WAPEWA MBINU ZA KUTUMIA FURSA ZA SOKO LA PAMOJA LA AFRIKA YA MASHARIKI.


Na Queen lema,ARUSHA

VIJANA 200 WA VYUO VIKUU ARUSHA WAPEWA MBINU ZA KUTUMIA FURSA ZA SOKO LA PAMOJA LA AFRIKA YA MASHARIKI.

Zaidi ya vijana 200 kutoka katika vyuo vikuu vitano mjini Arusha wamefanikiwa kupewa elimu mbalimbali ikiwemo jinsi ya kutumia fursa za jumuiya ya Afrika ya mashariki ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko ya vitu mbalimbali

Akiongea mapema jana  katika mdahalo ambao  umewahusisha vijana kutoka vyuo vikuu vitano vya Arusha mratibu wa mdahalo huo  bw kanani chombara alisema kuwa lengo halisi la kuwapa vijana hao elimu ni kuhakikisha wasomi wote wa mkoa wa Arusha wanazijua na kutambua fursa za soko hilo   

Chombara alisema kuwa wameamua kufanya madahalo huo ambao unahusu fursa mbalimbali za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa kuwa asilimia kubwa ya wasomi bado hawajatambua umuhimu wa kutumia fursa zilizopo hasa upande wa ajira na badala yake wana vyuo wa Mkoa wa Arusha wanawaza kupata fursa za kuajiriwa

Alifafanua kuwa hatua hiyo inachangia sana kuweza kupoteza fursa mbalimbali huku kwa upande wa wasomi ambao hawana ajira nao wakiwa wanaongezeka mitaani ingawaje kuna fursa za kutosha

Pia alisema kuwa mara baada ya vijana hao 200  kuweza kupata fursa za kujua na kutambua umuhimu wa fursa za kuwa wasomi kwenye soko hilo na kupitia mdahalo huo ambao utachangia  sana kuongeza amasa kubwa kwa vijana wasomi hivyo kuweza kubuni hata aina mpya ya ajira

‘kwa sasa asilimia kubwa ya vijana wanabaki wakiwa wanalalamika kuhusu soko hilo lakini bado hawana mcheheto wa kutumia fursa zilizopo kwa kuwa wanasubiri Serikali iweze kuja kuwapa ajira sasa hali hiyo inachangia sana baadhi ya vijana kuweza kuwa wasomi jina huku vijana wa Nchi nyingine wakiwa wanatamia vema fursa ambazo zipo’aliongeza Bw Chombara

Naye mratibu wa shirika la kijerumani (GIZ)bathazar kitundu alisema kuwa shirika hilo limejipanga kuhakikisha kuwa asilimia kubwa ya vijana wanatakiwa kujipanga kuanzia wanapokuwa ndani ya Vyuo vyao na kuachana na tabia ya kulalamika.

Bw Kitundu alisema kuwa njia ya kulalamika pekee bado sio suluhisho la kufanikiwa hasa kwa upande wa ajira kwani suluhisho pekee ni kukagua fursa zilizopo na kuweza kuzitumia kulingana  na mahitaji ya Soko hilo ambalo mpaka sasa idadi ya vijana wa Kitanzania wanaotumia ni wachache sana

‘unajua kwa sasa asilimia kubwa ya vijana wanabaki wakiwa wanalalamika ovyo mitaani lakini wanashidwa kujua kuwa vijana wa n chi nyingine hawana tabia hiyo bali wanaangalia fursa zote sasa hapa kwetu wanataka watafutiwe kupitia elimu  na midahalo kama hii itasaidia vijana wa vyuo vikuu kuweza kufunguka kwa kutafuta fursa ambazo zipo lakini hazitumiwi na wasomi wa vyuo vikuu”aliongeza Bw kitundu.

Alimkalizia kwa kusema kuwa mpango huo wa kufanya midahalo kwa vijana wa vyuo vikuu ili waweze kutumia vema fursa zilizopo ni endelevu ingawaje kwa mkoa wa Arusha mpango huo umeanza na Vyuo vitano ambavyo ni Makumira,Nelson Mandela,Arusha,Tengeru na chuo Kikuu cha IAA.

MWISHO

WANAOANGUKA NYAKATI ZA MITHIANI WANAKABILIWA NA HOFU YA MAWAZO


NA MWANDISHI WETU,ARUSHA

IMEELEZWA kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi mbalimbali ambao wanahisiwa kukabiliwa na nguvu za giza hawana nguvu hizo na badala yake wanafunzi hao wanakabiliwa na hali ya uoga hasa nyakati za mithiani,hali ambayo inasababishwa na mazingira ya majumbani mwao pamoja na shule zao

Wakati wa Mithiani asilimia kubwa ya wanafunzi huwa wanaanguka na kushindwa kufanya mithiani lakini sio nguvu za giza bali ni uoga wa mithiani na msongamano mkubwa sana wa mawazo (STRESS)

Hayo yamebainishwa wiki iliyopita  na Bw  Japhet Mwanangombe ambaye ni mratibu wa  shirika lan Roots and Shoots la jijini hapa wakati akiongea katikia kongamano la wanafunzi wa shule mbalimbali mjini hapa ni wanamazingira kwa kanda ya kaskazini

Bw Japhet alisema kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi wanasumbuliwa na hali ya uoga mkubwa sana hasa nyakati za mithiani ya Mwisho wa Mwaka pamoja na mithiani ya Kitaifa huku wazazi, walezi, na walimu wakijua kuwa ni nguvu za giza hali ambayo inafanya hata baadhi ya maendeleo ya Taaluma kushuka sana hasa kwenye baadhi ya shule.

Aliongeza kuwa wanafunzi wengi huwa wanafikiria zaidi matokeo ya mithiani au hali duni za maisha yao majumbani mwao bila kujua na kutambua kuwa mawazo kama hayo ndiyo yanayochangia kupoteza fahamu huku watu wengine wakihisi kuwa wanakabiliwa na changamoto ya nguvu za giza ndani ya shule zao

‘kwa kweli uchunguzi ambao tumeufanya kwa baadhi ya shule hasa za kanda hii ya kaskazini ambazo zinakabiliwa na changamoto kama hiyo tumebaini kuwa hakuna hata chembe ya nguvu za giza ila kwa kuwa wazazi na walimu wamejiwekea utaratibu wa kudai ni nguvu za giza na watoto wanaamini hivyo ila sio kweli wengi wanaogopa mithiani na matokeo ya mithiani,pamoja na hali duni za majumbani mwao’aliongeza

Katika hatua nyingine alisema kuwa ili hali hiyo iweze kupotea kwenye baadhi ya shule hasa kwa kanda ya kaskazini wazazi pamoja na walimu wanatakiwa kuhakikisha kuwa kwanza wanawajengea uwezo wanafunzi wa kuwa wajasiri wa kukabiliana na mithiani pamoja na hali duni za maisha ambapo kama watafanya hivyo basi watachangia sana wanafunzi kuacha kuanguka anguka ovyo.

Alisistiza kuwa wazazi wanatakiwa kuwapa moyo watoto wao hasa nyakati hizo za mithiani na kuacha tabia ya kuwapa vitisho ambavyo ndivyo vinachangia baadhi ya shule kukumbwa na na kashfa ya kuangukaanguka huku pia hali hiyo nayo ikichangia matokeo mabaya sana hasa kwenye mithiani ya Kitaifa

‘wakati wa mithiani wapo watoto ambao wana uwezo wa kufanya vizuri kabisa lakini wanashindwa kufanya vizuri kwa kuwa wazazi na walezi wao wanawapa vitisho vikubwa sasa hapa unakuta kama mtoto hajaanguka na mawazo, basi anafanya vibaya hii ni hatari sana kwa maendeleo ya taaluma hapa nchini”aliongeza


 Awali wanafunzi wa klabu hiyo walisema kuwa idadi ya wanafunzia ambao wanadondoka hasa nyakati za mithiani(EXAMINITIONAL FEVER) inaongezeka siku hadi siku lakini shule za Msingi,Sekondari, na Vyuo vinatakiwa kuwa na kitengo maalumu cha kuwapa wanafunzi ushauri ili kuweza kuwajenga zaidi tofauti na sasa ambapo baadhi ya wakuu wa shule na walimu wanatoa vitisho kwenye mithiani ya Kitaifa

Mwisho

SIDO ARUSHA YAFANIKIWA KUTOA MKOPO WA ZAIDI YA MILION 544,KWA WAJASIMALI 2018


SIDO ARUSHA YAFANIKIWA KUTOA MKOPO WA ZAIDI YA MILION 544,KWA WAJASIMALI 2018

Na Queen Lema,Arusha

SHIRIKA la kuhudumia viwanda vidogo vidogo hapa nchini(SIDO)mkoa wa Arusha limefanikiwa kutoa elimu ya ujasiamali kwa wajasiamali 2,018 huku jumla ya Milioni 544 nayo ikitolewa kama Mkopo ili kuendeleza mitaji ya wajasiriamali hao kwa kipindi cha miaka miwili,

Hayo yameelezwa na Meneja wa shirika hilo mkoani hapa Bw Isidore Kayenzi wakati akielezea mafanikio ya Shirika hilo kwa Waziri wa Viwanda na Biashara hapa nchini Bw Abdalah kigoda mapema jana

Bw Isidore alisema kuwa Mikopo na elimu hiyo ambayo ilikuwa inatolewa kwa wajasiamali hao imefanikiwa kuwafikia wananchi wa Wilaya za Arumeru,Monduli,Karatu, longido, na Ngorongoro ambapo mpaka sasa mafanikio yameshaonekana

Aliongeza kuwa mafunzo ambayo wameweza kuwapa wajasiamali hao ni pamoja na Ujasiamali hasa katika Uongozi wa Kibiashara,utengenezaji wa sabuni,usindikajiwa ngozi na bidhaa za ngozi,usindikaji wa chakula  na matunda,pamoja na mafunzo mengine ambayo yameweza kutoa ajira huku yakichochea msukumo mkubwa wa Ujasiamali hasa kwa mkoa wa Arusha

‘hawa wajasiamali ambao tumewapa mafunzo asilimia 70 wameweza kutoa ajira hata kwa watu wengine nah ii imeongeza hata idadi ya  viwanda vidogo vidogo ambavyo tunavyo kwa mkoa wa Arusha ingawaje Sido kama Sido bado inakabiliwa na changamoto za hali ya juu san”aliongeza Bw Isidore.

Pia alisema kuwa kwa sasa changamoto kubwa sana ambayo inayokabili Shirika hilo pamoja na wajasiamali wa Mkoa wa Arusha ni Mahitaji makubwa sana ya wajasiamali wadogo na wakati hasa Mitaji kuliko uwezo ambao wanao hali ambayo inatakiwa kuangaliwa kwa undani sana

Alifafanua kuwa mbali na changamoto hiyo ya Ukubwa wa mahitaji wakati hakuna Mitaji ya kuendeshea shuguli za kijasiamali lakini pia bado kuna changamoto ya utoaji wa mkopo hasa kwa SIDO kwani kiwango chao cha juu cha utoaji wa Mikopo ni Milioni sita huku kiwango hicho nacho kikifanya baadhi ya wajasiamali washindwe kuvuka malengo yao ambayo wamejiwekea hasa ya kutoa katika daraja dogo na kuingia kwenye daraja la kati la ujasimali.

Naye Waziri wa Viwanda na Biashara hapa Nchini Abdallah Kigoda alisema kuwa pamoja na kuwa Shirika hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali lakini bado Tanzania ina tatizo kubwa sana la kutowapa wajasiamali wadogo na wakati fursa mbalimbali za kukuza na kuimarisha Uchumi wa Mkoa na Tanzania

Bw Kigoda alisema kuwa kwanza Sekta za umma na binafsi zinatakiwa kuanza kuwapa fursa wajasiamali wadogo na wakati vipaumbele mbalimbali kwa kuwa wajasiamali wana uwezo mkubwa sana wa kuweza kuimarisha hata uchumi ambao unayumbayumba huku ajira mbalimbali nazo zitaweza kuongezeka.

‘Hii ni Sekta ambayo inatakiwa kupewa kipaumbele kikubwa sana kwa kuwa ndiyo injayoshikilia mambo mbalimbali na pia nguvu za Ziada zinatakiwa kuelekezwa kwa wajasiamali wengi zaidi ingawaje hata uwepo wa viwanda vingi hapa Nchini unachangia sana kuweza kufanya watanzania kupata bidhaa zao kwa uraisi sana tofauti na sasa ambapo asilimia kubwa ya watanzania wanategemea zaidi bidhaa kutoka nje ya nchi wakati watanzania wana uwezo wa kutengeneza bidhaa hizo”aliongeza Bw Kigoda.

Wednesday, November 21, 2012

WALIOKUWA MADIWANI WA CHADEMA WALIPISHWA FAINI YA MILIONI 15 NA MAHAKAMA WAKISHINDWA KULIPA KWENDA MAGEREZA


WALIOKUWA MADIWANI WA CHADEMA WALIPISHWA FAINI YA MILIONI 15 NA MAHAKAMA WAKISHINDWA KULIPA KWENDA MAGEREZA

NI KWA KOSA LA KUKIUKA TARATIBU ZA CHADEMA NA KUINGIA KWENYE VIKAO VYA KUMTAMBUA MEYA WA CCM

Na Queen Lema,Arusha

HATIMAYE hukumu ya  kesi ya madai iliyokuwa ikiwakabili  waliokuwa madiwani watano wa  chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) hukumu yake imesomwa ambapo mahakama imeamuru madiwani hao kulipa kiasi cha shilingi milioni 15 kwa awamu mbili na endapo kama watashindwa kulipa fedha hizo basi watapelekwa magereza

Akitoa hukumu hiyo mbele ya Umati wa watu ambao walikuwa wamefurika mahakamaani hapo mapema jana katika mahakama kuu kanda ya Arusha Charlz Magesa alisema kuwa rufaa imefika mwisho

Magesa alisema kuwa washitakiwa hao ambao  walikuwa madiwani wa kata tano za jiji la Arusha wamekutwa na hatia hivyo mahakama imeamuru walipe kiasi hicho cha fedha haraka iwezekanavyo na endapo kama watashindwa kufanya hivyo basi watachukuliwa hatua kali ikiwemo kupelekwa magereza.

Aliongeza kuwa kwa sasa Madiwani hao wanatakiwa kulipa fedha hizo kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itakuwa ndani ya wiki mbili wakati awamu ya pili itakuwa ya mwisho na nibaada ya miezi miwili.

‘kwa sasa mnatakiwa muhakikishe kuwa mnalipa fidia kwa haraka sana na kama mtashindwa kufanya hivyo basi mahakama itachukua hatua na maambuzi makali zaidi ya haya’aliongeza Magesa

Wakiongea nje ya mahakama mara baada ya kukubaliana kulipa kiasi hicho cha fedha madiwani hao ambao walikuwa mahakamani hapo ambao ni Rehema Mohamed,Charlz Mpanda,na Rubeni Ngowi walidai kuwa Chadema haiyawatendea haki kwa kuwa fedha ambazo wanatumia kumlipa Wakili ili kuwakandamiza ndizo walizozitafuta kwa kipindi cha hapo awali.

Madiwani hao waliongeza kuwa wao wapo tayari kulipa hizo gharama kwa ndiyo haki ambayo Chadema walikuwa wanaililia hivyo wameomba Viongozi wa Taifa watafute njia nyingine ya kutatua migogoro na wala sio kufukuza  kwani inapoteza imani na chama

‘ukiangalia hapa tunaambiwa kuwa tulipe kiasi hiki cha fedha lakini nguvu zetu bado hazijalipwa na sisi ndio tuliotangaza Chadema kwa mkoa wa Arusha na mpaka sasa Kila mtu anaijua Chadema lakini malipo yake ndiyo haya sisi tunasema kuwa huu si mwisho wa siasa bado tupo na tutakutana katika gemu nyingine ‘waliongeza madiwani hao

Pia walisema kuwa pamoja na kuwa baadhi ya waliokuwa madiwani hawataki siasa lakini bado wengine wataendelea tena kwa kishindo kikubwa hata kama Chadema wanadai kulipwa fedha zao na kata zao zikiwa zinabaki hazina madiwani kwa muda mrefu sana.

Awali Kesi hiyo ilitokana na madiwani hao kufungua kesi ya kupinga kufukuzwa na kuvuliwa uanachama baada ya kudaiwa kukiuka sheria na kanuni za chama, zikiwemo sheria za kuwataka kutoingia katika vikao vya madiwani vya Jiji la Arusha kwa madai ya kutomtambua Meya wa Arusha Gaudence Lyimo wa Chama cha Mapinduzi(CCM)

CHADEMA YATETA JUU YA MADIWANI WALIOSHIRKI UZINDUZI WA JIJI


CHAMA cha demokrasia na maendeleo (Chadema) kimetoa onyo  kali kwa baadhi ya madiwani wake jijini Arusha walioshiriki  katika mchakato wa maandalizi ya uzinduzi wa jiji la Arusha kinyume na msimamo wa chama hicho.

Pia,chama hicho juzi kiliwaweka kiti moto madiwani hao na kuwahoji kuhusu tuhuma za kushiriki vikao vya baraza la madiwani la jiji hilo sanjari na kuchukua posho mbalimbali za vikao hivo ambapo walijieleza na maelezo yao kufikishwa katika ngazi za juu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, katibu mkuu wa Chadema ,Dk Willbrod Slaa alisema kuwa iwapo itabainika baadhi ya madiwani hao walijipenyeza na kushiriki mchakato wa uzinduzi wa jiji hilo pamoja na kuchukua posho za vikao mbalimbali wataadhibiwa kwa mujibu wa taratibu za chama hicho.
Dk, Slaa alisema kuwa msimamo wa chama hicho ni kutomtambua meya wa Arusha ,Gaudence Lyimo(ccm)kwa kile alichodai taratibu za kupatikana kwake hazikufuatwa,na kusisitiza kuwa iwapo madiwani wake wanajipenyeza na kushiriki vikao vya halmashauri vinavyoongozwa na meya huyo ni utovu wa nidhamu.
‘’kitendo cha kushiriki vikao vya halimashauri ni kuhalalisha kumtambua meya wa Arusha sasa sisi msimamo wetu ni kutoshiriki vikao na hata madiwani wanalijua hilo ila kama wanashiriki kinyemela na kuchukua posho tutapambana nao’’alisema Dk Slaa.
Aidha dkt Slaa alionya kuwa kitendo cha madiwani wake kushiriki vikao vya manispaa ni mwanzo mbaya wa kuambikizwa madhambi ya ufisadi yaliyopo ndani ya manispaa hiyo ukiwemo matumizi mabaya ya fedha za wananchi.
Hata hivyo mwandishi alipotaka kujua msimamo wa Chadema utaisha lini wakati wananchi wanaendelea kusota kwa kukosa wawakilishi kwenye kata zao,alisema kuwa diwani anapaswa kushiriki maendeleo kwenye kata yake na wananchi wake na si kushiriki vikao vya halmashauri.

Aliongeza kuwa diwani anapaswa kumfuata ofisini  mkurugenzi wa jiji na kumweleza matatizo yaliyopo kwenye kata yake bila kushiriki vikao vya baraza la madiwani.
Alipotafutwa mwenyekiti wa madiwani wa Chadema jijini hapa,Isaya Doita ambaye ni diwani wa kata ya Ngarenaro alikiri hatua ya wao kuhojiwa na Dk Slaa huku akisema kwamba kwa sasa hawana la kusema kwa kuwa wanasubiri maelekezo kutoka ngazi za juu za chama.
Hatahivyo,alikiri wao kushiriki mchakato wa uzinduzi wa jiji la Arusha hivi karibuni huku akidai ya kwamba suala la kushiriki na kupokea posho za vikao mbalimbali ni halali yao.


"sisi tulishiriki katika sherehe hizi za uzinduzi wa jiji kama viongozi wa wananchi na kikao cha kupanga bajeti kilikuwa sio kwenye baraza la madiwani bali tuliitwa katika kikao cha gafla ya madiwani tulivyofika ndo tukaambiwa kuwa ni kikao kwa ajili ya uzinduzi wa jiji na awali mkumbuke tulikaa chini na kuafiki kuwa jiji lizinduliwe mwezi wa kwanza tarehe moja mwakani sasa kwa kuwa watu walikaa na imeamuliwa jiji lizinduliwe tuliamua kushiriki ila sio kikao cha baraza"Doita
Itakumbukwa ya kwamba onyo lililotolewa na Dk Slaa limekuja siku chache baada ya madiwani wa CCM,Tlp na Chadema jijini Arusha kushiriki mchakato wa uzinduzi wa jiji hilo kitendo ambacho kimeibua gumzo jijini hapa huku ikikumbukwa ya kwamba madiwani wa Chadema waliweka msimamo wa kutomtatabua meya wa jiji la Arusha.
Baadhi ya madiwani wa Chadema walioshiriki mchakato wa uzinduzi wa jiji hilo hivi karibuni waliongozwa  na diwani wa kata ya Levolosi,Efatha Nanyaro ambapo alichaguliwa kuwa katibu wa maandalizi ya chakula cha Rais huku mwenyekiti wake akiwa ni diwani wa kata ya Moshono,Paul Matyhsen(CCM).
Vilevile itakumbukwa ya kwamba Chadema kiliwahi kuwatimua madiwani wake watano mwaka jana ambao ni John Bayo,Ruben Ngowi,Estomi Malah na Rehema Mohamed kwa kosa kuingia mwafaka wa   kumtabua meya wa jiji la Arusha.
MWISHO.
 

UTPC YATOA MSAADA APC

Na Gladness mushi, arusha

MUUNGANO wa Vyama vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC) uimeikabidhi Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) vifaa vyenye thamani ya Sh. Milioni 35.

Vifaa hivyo vilikabidhiwa jana Ofisa Utawala na Fedha wa UTPC Jackosn Uiso katika ofisi za Klabu ya APC jijini hapa na kushuhudiwa na viongozi na baadhi ya wanachama.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Uiso aliwahimiza viongozi kuhakikisha vinatumika kwa wanachama ikiwa ni pamoja na kuingizia fedha Klabu.

“UTPC inawahimiza mtumie vifaa hivi kwa uangalifu, lakini hakikisheni mnaweka utaratibu wa jinsi gani vitawaingizia fedha za Klabu badala ya kuendelea kuvifungia,” alisema Uiso.

Baadhi ya vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Mashine ya kudurufu, Televisheni ya Inchi 32, Kamera kubwa ya kisasa kwa ajili ya picha za mnato, mashine ya Projector, Desk Kompyuta na Laptop.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu aliwashukuru UTPC kwa kukabidhi vifaa hivyo na kuahidi kwamba vitatumika kwa uangalifu mkubwa.
“Vifaa hivi ni vya thamani na tunaahidi kuvitumia kwa uangalifu utakaoleta manufaa kwa Klabu na wanachama wake,” alisema Gwandu.

Naye Katibu Mkuu wa APC Eliya Mbonea kwa upande wake aliwashukuru UTPC kwa kufanyia kazi mawazo ya viongozi wa Klabu nchini waliopendekeza kutumiwa vifaa vinavyolingana na taaluma.

“Mapendekezo ya viongozi wa Klabu yamefanyiwa kazi, awali tulikuwa tunaletewa kamera ndigo zinazowapa wakati mgumu waandishi kupiga picha hususani viongozi wa kitaifa wanapokuja au tukio linapokuwa mbali,” alisema Mbonea na kuongeza:

“Mfano hii Kamera ya picha za mnato kweli hapa sasa hatuwezi kulalamika tena kwamba hatuna kamera ya kisasa kwani Kamera hii unaweza kupiga picha ukiwa mahali popote,” alisema.
Mwisho.




MAJESHI YA SADC KUENDELEA KUTOA MSAADA KWA NCHI ZENYE MAJANGA,NA VITA


MAJESHI YA SADC KUENDELEA KUTOA MSAADA KWA NCHI ZENYE MAJANGA,NA VITA

Na Queen Lema,ARUSHA

UMOJA wa nchi zinazoendelea kusini mwa jangwa la Sahara(SADC)umesema kuwa utaendelea  kupeleka majeshi kwenye nchi zenye mitafaruku mbalimbali yakiwemo majanga na vita huku lengo likiwa ni kuepusha vifo.

Kauli hiyo imetolewa jana(Leo)na Kanali Gerson Sangiza ambaye ni mkuu wa kitengo cha ulinzi na mipango katika sektetarieti ya SADC wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mipango mbalimbali ya majeshi ya umoja huo

Kanali Sangiza alisema kuwa kwa nchi zenye majanga mbalimbali yakiwemo majanga ya vita,mitetemeko,pamoja na mafuriko ambazo ni wanachama wa umoja huo wataweza kusaidiwa kwa kupewa misaada na majeshi ya nchi kama kumi na tano

Alifafanua kuwa kupitia umoja huo wa majeshi kuweza kusaidia nchi zenye majanga kutaweza kuepusha nchi nyingine ambazo zipo jirani kupata matatizo mbalimbali ambapo kupitia matatizo hayo nayo yanachangia sana kukitihiri kwa majanga.

‘kama sisi SADC hatutashirikiana kwa pamoja katika kutetean amani ya nchi yenye vita kupitia kwenye majeshi yetu ni wazi kuwa matatizo mengi sana yataweza kuibuka kama vile vifo na hata wakimbizi,ingawaje kama kuna matatizo tukishirikiana kwa pamoja ni wazi kuwa tutaweza kuleta amani tena ya kudumu  na hiyo itafanya madhara mbalimbali ndani ya nchi yenye vita kukoma kabisa”aliongeza kanali huyo

Pia alisema kuwa mbali na kudumisha amani ndani ya nchi zenye vita pamoja na majanga mbalimbali kupitia umoja wa majeshi hasa ya nchi hizo za SADC majeshi hayo yanamikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa ndani ya karne ya sasa na karne ijayo hakuna mapigano ambayo ndiyo yanayochangia sana kukithiri kwa vita.

Katika hatua nyingine alisema kuwa pamoja na kuwa Majeshi ya nchi 15 yanafanya kazi kwa umoja mkubwa sana hasa kwa kusaidia nchi znye vita na majanga lakini bado wana mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa kila Nchi mwanachama wa Umoja huo pamoja na majeshi yake yanakuwa katika viwango ambavyo vinahitajika

Alisema kuwa Mikakati hiyo ni pamoja na kubadilishana uzoefu baina ya Nchi na nchi ambapo hali hiyo inasaidia Vikosin mbalimbali vya Jeshi kuweza kufanya kazi kwa uzoefu wote ambao wao kwa wao wanaujua na hivyo kurahisisha kazi hasa pale inapotokea hasa ya Majanga, na Vita.

“kwa mfano hapa kwetu Tanzania tuna chuo cha TMA kipo Monduli pale wanajeshi kutoka Nchi mbalimbali wanasoma na kuendelea kujifunza mbinu mbalimbali lakini na sisi wanajeshi wetu pia na wao wanakwenda sehemu mbalimbali kujifunza nah ii inachangia sana kuweza kuwaandaa kuwa tayari kwa nyakati zozote zile’alisema

MWISHO

TUNATAMBUA MCHANGO WA SEKTA BINAFSI-SERIKALI


TUNATAMBUA MCHANGO WA SEKTA BINAFSI-SERIKALI

Na Mustapha leo,ARUSHA

SERIKALI imesema inatambua na kuthamini mchango wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambayo yamekuwa yakisaidia kutoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini ambako wananchi wamekuwa hawapati huduma ya moja kwa moja kutoka serikali.

Hivyo mashirika hayo ni mbia mwenza wa serikali katika kutoa huduma na serikali itaendelea kushirikiana nayo kwa ukaribu lengo ni kuwafikishia wananchi huduma mbalimbali ili waboreshe maisha yao

Rai hiyo imetolewa jana na Katibu tawala wa mkoa wa Arusha,bi Evereen  Itanisa, alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOS) na uongozi wa serikali mkoa wa Arusha katika Ukumbi wa Olasit Garden,  jijini Arusha.

Itanisa,aliongeza kuwa  hadi kufikia mwaka 2012 kuna mashirika yasiyo ya kiserikali 3600 yamesajiliwa hapa nchini ambapo mkoa wa Arusha una mashirika 385 ambayo yamekuwa yakifanya kazi nzuri za kuhudumia wananchi katika maeneo ambayo hasa huduma za moja kwa moja kutoka serikalini hazipo na mashiriuka hayo yamekuwa ni mbia katika maendeleo.

Alisema wilaya ya Ngorongoro ina mashirika 15, Karatu 15, Longido 21, Meru 52 , Arusha DC, 64  Monduli 52 na jiji la Arusha 166 .

Pia aliongeza kuwa hali hiyo imeyafanya mashirika hayo kuwa mkono wa pili wa serikali katika kufikisha huduma bora kwa wananchi hivyo serikali itaimarisha mahusiano na mashirika hayo katika kuwahudumia wananchi waweze kupata huduma stahiki..



Alisema kutokana na wingi huo wa mashirika hayo serikali ilitumnga Sera, Sheria na kanuni ambayo ndio mwongozo wa utekelezaji na usimamiz wa majukumu ya mashirika hayo ili kuboresha mahusiano kati ya serikali, jamii na wananchi

Itanisa alisema kuwa    kutokana na hali hiyo lazima mashirika hayo yafanye kazi zake kwa kuzingatia utekelezaji wa wa Dira ya taifa, ya maendeleo na mpango wa taifa  wa miaka mitano mpango mkakati wa mkoa na halmashauri ya Jiji na  wilaya

Amesema lengo la mkutano huo ni kufahamiana, nani anatoa huduma zipi na eneo lipi,  kuwezesha kupitia kwa pamoja Sera, Sheria na Kanuni za mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na vyombvo vlivyoundwa  vya kusimamia utendaji kazi kwa mashirika hayo,pia kupitia taarifa za  utekelezaji sanjari na kuangalia changamoto zinazoyakabili mashirika hayo.

Awali katibu tawala msaidizi Mipango na Uratibu, Anza _Amen Ndossa, amesema kuwa lazima mashirika yote yafuate Sera na mwongozo wa serikali  namna ya kufanya kazi na kuondoa migongano kati yao kwa kutoa huduma za aina moja katika eneo moja.

Amesema mashirika hayo yana kabiliwa na changamoto nyingi na mkutano huo unalenga kukimarisha mahusiano kati yao na serikali na kuondoa migongano kati yao na kupitia mkutano huo mashirika hayo yataelewa mipaka na majukumu yao na kutoa taarifa za utekelezaji wake kwa wakati bila kigugumizi pia mkutano huo utajenga kuaminiana kati ya Serikali na mashirika hayo..

Ndossa, akawakumbusha  maafisa Maendeleo ya jamii kila halmashauri kuwa wanalo jukumu kubwa la kushirikiana na mashirika hayo kwa kuyapangia maemneo ya kufanyia kazi ili kuondoa muinginiliano inayosababisha kukwama kwa miradi iliyokusudiwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.


Mwisho.

Tuesday, November 20, 2012

RAISI KIKWETE AZINDUA MKAKATI WA PILI WA NCHI WANACHAMA WA SADC

DKT JAKAYA KIKWETE AKIWASALAMIA WANANCHI,HAWAPO PICHANI HIVI KARIBUNI MKOANI ARUSHA,PICHA NA MAKTABA


RAISI KIKWETE AZINDUA MKAKATI WA PILI WA NCHI WANACHAMA WA SADC

WAANDISHI WETU,ARUSHA

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amezindua rasmi mkakati wa pili wa chombo cha nchi wanachama wa SADC ambapo chombo hicho kitashugulikia masuala mbalimbali kama vile Siasa,Ulinzi na Usalama (SIPO)

Akiongea na Waandishi wa habari mapema jana mara baada ya kuzindua chombo hicho Raisi Kikwete alisema kuwa chombo hicho kitasaidia sana kuweza kufanya mabadiliko ya hali ya juu sana hasa kwa nchi husika.

Alisema kuwa mkakati huo ambao ni mpya utasaidia sana kufanya mabadiliko makubwa sana hasa katika nyanja za Siasa,ulinzi, na usalama ambapo pia matarajio ya chombo hicho ni kuona kuwa mabadiliko yanachangia hata maendeleo

Alifafanua kuwa,kwa Nchi mbalimbali za SADC ambazo zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo vita mkakati huo utaweza kuwasaidia  hata katika  kutafuta muafaka na kuepukana na vita ambavyo  ni chanzo kikuuu cha vifo ambavyo havina hatia

‘tukiangalia suala la nchi zenye Vita hasa Demokrasia ya Kongo Mkakati huu utachangia sana kuweza kuleta Muafaka kwani tutahakikisha kuwa tunakaa meza moja na kumaliza vita kwa njia ya usuluhishi na hapo sasa ndio maana halisi ya chombo hiki’aliongeza Dkt Kikwete

Katika hatua nyingine alisema kuwa kupitia kweenye Chombo hicho cha kinachohusika na masuala ya Ulinzi,Usalama, na Siasa pia wataweza kuyuuunda Majeshi ya pamoja la kulinda amani katika nchi zenye vita ikiwemo Kongo.

Awali katibu mkuu wa Nchi wanachama wa SADC dr Tomaz Augusto alisema kuwa kupitia chombo na mkakati huo utasadia kuimarisha umoja ,maendeleo na mshikamano kwa nchi wanachama hali ambayo nayo itachangia sana kuweza kupunguza umaskini.

Dr  Tomaz  aliongeza kuwa mbali na hayo pia utaweza kujikita katika masuala mbalimbali hasa ya Uchumi ambapo chombo hicho kitaweza kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wanasiasa huku lengo likiwa ni kulinda amani

Katika  hatua aliwataka wanachama wa Nchi za SADC kuimarisha uhusiano ikiwa ni pamoja na kuuungana na kuwa kitu kimoja ili kuweza kufikia malengo mbalimbali ambayo wamejiwekea hasa katika nyanja ya kupambana na umaskini,pamoja na ukosefu wa elimu hali ambayo inasababisha vita mara kwa mara.

MWISHO

MUUMINI WA KWA GEOR DAVIE AKAMATWA AKIWA ANAREKODI MAHUBIRI KWA CHANNEL ARUSHA



Na Bety Alex,ARUSHA

MUUMINI WA KWA GEOR DAVIE AKAMATWA AKIWA ANAREKODI MAHUBIRI KWA CHANNEL ARUSHA

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Victor amekamtwa ndani ya huduma ya Maisha ya Yesu  ambayo inaongozwa na Mchungaji Joackim Channel iliopo Kisongo  ambapo kijana huyo alikuwa anarekodi Maahubiri ambapo baada ya kukamtwa alikiri kuwa ametumwa na Viongozi mbalimbali wa huduma ya Nabii Geor davie.

Tukio hilo limetokea jumapili iliyopita ambapo kijana huyo alionekana kuwa kama si miongoni mwa waumini wa huduma ya maisha ya yesu iliopo Kisongo mjini hapa

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ambao ni waumini wa huduma ya Maisha ya yesu walisema kuwa kijana huyo alikuwa anarekodi maahubiri lakini mara baada ya kuhisiwa alijifanya kama Kichaa hali ambayo iliwalazimu kumshika kwa nguvu

“huyu kijana alikuwa katika hali isiyokuwa ya kawaida kwa kuwa alikuwa hana amani hasa nyakati za maombi lakini sisi tulivyomuona kwa kuwa hata jumapili iliyopita tulimuona basi tukawa na wasiwasi mkubwa sana kuwa huenda yupo kinyume na ibada yetu na ndivyo ilivyokuwa ndani ya Ibada hiyo”waliongeza  waumini hao.

Pia walisema kuwa mara baada ya kukamatwa na kuhojiwa kwa kijana huyo alikubali kuwa hakuwa na lengo halisi la kuabudu ndani ya ibada hiyo ya maisha ya yesu bali alikuwa ametumwa na Viongozi mbalimbali wa huduma ya Geor Davie kwa manufaa yao.

‘Mimi sikuwa  na lengo la kuabudu hapa bali mimi nimetumwa nije kurekodi ibada hii na viongozi wa Geor davie kwa malengo ambayo wanajajua wao kama wao lakini naomba mnisamehee jamani msinipige’aliongeza Kijana huyo ambaye alikamatwa akiwa anarekodi mahubiri kutoka kanisa la Mchungaji  Channel Joackim

Hataivyo mara baada ya kukamatwa kwa kijana huyo na kukiri mbele ya madhabahu hiyo ya Mchungaji Channel kuwa alikuwa ametumwa kurekodi ibada kwa ajili ya matumizi ambayo hayajulikani ya viongozi wa kwa Geor davie alipelekwa katika vyombo vya usalama ili sheria ichukue mkondo wake.

Katika hatua nyingine siku za hivi karibuni watu wasiofahamika walijaribu kumteka mchungaji huyo kwa lengo la kumdhuru lakini hawakufanikiwa na badala yake vyombo vya usalama vilifanikiwa kumuokoa mchungaji huyo Joackim Channel.

Juhudi za kuwatafuta kiongozi wa juu wa huduma za kwa Geor Davie ambaye ni Nabii Geor davie hazikufanikiwa kwa haraka kutokana na kudaiwa kuwa  hawezi kuonekana kwa uraisi,hivyo kushindwa kujibu mashitaka ambayo yameelekezwa mbele zake ya kurekodi ibada kwa malengo ambayo bado hajajulikana.