Tuesday, September 4, 2012

MERU KUWAPA WAZEE MATIBABU BURE





baadhi ya watendaji wa wa wizara ya afya wakiwa katika picha ya pamoja.



Na Mery Kitosio,MERU

VIONGOZI mbalimbali hasa ngazi za Vijiji na Kata Wilayani Meru mkoani hapa  wametakiwa kuhakikisha kuwa wanasimamia vema sera za wazee ambapo kwa sasa Halmashauri hiyo inahudumia huduma za afya bure wazee wote wenye umri wa miaka 60.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw Goodson Majola wakati akiongea katika kikao cha baraza la madiwani(FULL COUNCIL) mapema jana wilayani humo.

Aidha Bw Majola alisema kuwa kwa sasa halmashauri hiyo imeaanza rasmi mpango mkakati wa kutekeleza sera za wazee ambao wana umri wa zaidi ya miaka 60  na kwa hali hiyo ni jukumu la kila kiongozi kuhakikisha kuwa wazee wanapata huduma bora za afya

Pia alisema kuwa ili zoezi hilo liweze kufanikiwa kwa kiwango cha hali ya juu viongozi hao wa Kata wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa na idadi ya wazee ambao wapo katika jamii zao ambapo pia hali hiyo itaweza kuwasaidia kwa kiwango kikubwa sana.

“kwa kiongozi ambaye hatausika na kuwasaidia hawa wazee katika kupata haki zao za msingi au kuwapa garama hawa wazeee basi sisi tutahakikisha kuwa tunawachukulia hatua kali na za kisheria kwani ni tunachikiitaji ni kuhakikisha kuwa kila mzee hapa  Meru anapata haki matibabu bure kabisa”aliongeza bw Majola

Awali alibainisha kuwa mpango huo ni endelevu sana kwa Halmashauri hiyo ambapo kwa sasa wana mpango wa kuhakikisha kuwa Sera zote ambazo zipo chini ya Wizara mbalimbali zinatekelezwa tena kwa wakati kwani uwezo wa kutekeleza sera hizo upo ingawaje mara nyingine sera hizo zinaachwa huku wananchi nao wakiwa wanapata taabu katika shuguli za kila siku..

“Ni Muhiumu sana kwa kila sera kutekelezwa kwa kiwango cha juu sana kwani kukwepesha sera mbalimbali za kijamii ndio chanzo cha matatizo makubwa sana kwenye taifa la leo na kwa maana hiyo kila Sera itatekelezwa tena kwa wakati kwani ni haki ya jamii kupata huduma zitokanazo na Halmashauri zetu kama ilivyo sera ya wazee kwa sasa”aliongeza Bw Majola.

Hataivyo viongozi  mbalimbali wa Wilaya ya Meru walisema kuwa kama Sera hiyo itatekelezwa basi itaweza kupunguza  matatizo mbalimbali ambapo kwa sasa hata  wengine wanashindwa kujua na kutambua kuwa wazee wote wanatakiwa kupewa matibabu bure kwani Tayari Serikali imeshaona umuhimu huo kutokana na hali halisi na magonjwa amnbayo yanawakabili wazee wengi kwa sasa

Wazee hao walibainisha kuwa mbali na Halmashauri hiyo kuanza kutangaza kuwa wanawapa bure wazee huduma za afya pia nao watumishi wa afya wanatakiwa kujua na kutambua kuwa wazee nao wanapaswa kuhudumiwa vema pasipokuwa na masumango ya aina yoyote kwani zipo baadhi ya hospitali ambazo zinawanyanyasa sana wazee hasa wenye magonjwa nyemelezi.

MWISHO

No comments:

Post a Comment