Tuesday, February 28, 2012

MCHUNGAJI JOKA KUU ALIA NA MATAMBO YA MATAJIRI WA DUNIA

Matajiri mbalimbali hapa nchini wametakiwa kuacha tabia ya kujisifu kutokana na mali zao na badala yake wahakikishe kuwa wanampa Mungu Utukufu kwa kuwapa mali, kwani baaadhi ya Matajiri, wenye Nguvu, na Hekima wamekuwa ni kikwazo kikubwa sana.


Katika jamii zetu wapo baadhi ya watu ambao wanajisifia sana kuhusuana na utajiri wao, hekima zao, na nguvu zao na kuona kuwa wao ni washindi katika maisha yao hali ambayo ni chukizo kubwa sana mbele za mungu.

Hayo yameelezwa na mchungaji Abati Joka kuu wa kanisa la MORIE  E.A.G.T lilopo katika maeneo ya Mbauda wakati akiongea na wauimini wa kanisa hilo mapema wiki hii.

Aidha Mchungaji Joka kuu alieleza kuwa kwa wale wenye tabia kama hizo wanatakiwa kuziacha kwa kuwa zinamkwaza sana Mungu na kwa hali hiyo inasababisha hata utukufu wa Mungu kushindwa kufanyika kwa wakati.

Aliongeza kuwa hao ambao wanatumia utajiri wao kwa kujisifia wanapata madhara mbalimbali katika maisha yao kwa kuwa Mkristo ambaye ana Mungu hashindwi na Jambo lolote wakati wale ambao wanajisifia mbele za Watu wanakosa hata maitaji yao

"Maandiko yanasema kuwa mwenye hekima asijifu, mwenye nguvu naye asijisifu kwa ajili ya hayo bali mimi ni bwana nitendaye wema, kwa maana hiyo tunapaswa kumpa Mungu peeke utukufu na wala sio Mali zetu"alisema Mchungaji Joka Kuu.

Alianisha kuwa pamoja na kuwa utajiri, nguvu, na hekima ni lazima ziwepo kwa Mwanadamu lakini wanadamu wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatumia vitu hivyo kwa kumrudishia Mungu utukufu na wala sio kujisifia mbele za Macho ya wanadamu.

katika hatua nyingine mchungaji huyo aliwataka wakristo kuhakikisha kuwa wanamjua Mungu kwanza na mengine ya dunia nayo yatafuata kwa kuwa ndani ya jamii pia  wapo baadhi ya watu ambao wanajali zaidi Mali kuliko kumjali Mungu wao.

Alitaja madhara ambayo yanaweza kumkumba mtu ambaye anajali zaidi mali, pamoja na kujisfia kuwa ni pamoja na kukosa amani ya roho pamoja  na uhuru ambapo kwa wale ambao wanamtanguliza Mungu na kumpa Mungu utukufu juu ya mali zao wanaweza kupata amani ya kudumu.

MWISHO 

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891

ARUSHA 
KIJANA AELEZA JINSI ALIVYOMPACHIKA MAMA YAKE UVIMBE, BABA AKAMPACHIKA PEPO LA ULEVI

Katika hali isiyokuwa ya kawaida kijana mmoja ambaye amejulikana kwa jina la Eriel Swai mkazi wa Ngaramtoni jijini hapa amekiri kumvika baba yake mzazi pepo la ulevi huku kwa upande wa mama yake mzazi  alimvisha tambara jeusi katika tumbo lake hali ambayo ilimfanya mama huyo kuwa na uvimbe mkubwa sana.

Akizungmza katika kanisa la uzima na ufufuo lilopo Maua Ungalmtd jijini hapa alisema kuwa aliamua kufanya hivyo kutokana na kuwa na nguvu za giza ambazo zilimuamuru kuwafanyia hivyo wazazi wake.

Kijana huyo alisema kuwa kwa zaidi ya miaka mitatu mfufulizo ameamua kuishi maisha ya nguvu za giza ambapo maisha hayo yalikuwa yakiwatumika hata wazazi wake bila ya wao wenyewe kujijua hali ambayo iliwasababisha waishi maisha ya mateso zaidi huku wakujua kuwa ni halali

Alibainisha kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu mfufulizo alilazimika kuishi katika maisha ya ufalme wa  nguvu za giza huku kivuli chake kikibaki duniani hali ambayo nayo iliweza kuwafanya watu wengi kujua kuwa ni yeye jambo ambalo lilikuwa si kweli.

“katika ufalme huo wa nguvu za giza mimi nilikuwa huko nikichimba makaburi lakini huku nyumbani ni kivuli ambacho kina sura ya mgomba ndicho kilichobaki pekee na wakati huo hicho kivulko killikuwa kikifanya mambo mbalimbali ambayo yalisababisha hasara kubwa sana”alisema kijana huyo.

Hataivyo alisema kuwa njia ambayo aliitumia yeye kama yeye kuenda katika ufalme huo wa nguvu za giza ni kupitia kwa bibi yake ambaye hapo awali alionekana kama amekufa lakini katika ufalme huo wa nguvu za giza hakuwa amekufa.

Naye Askofu wa kanisa hilo Bw Stanley kilima alisema kuwa kwa nyakati za sasa wazazi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanawaweka watoto wao katika msingi wa imani kwa kuwa adui kwa sasa anawawinda sana watoto ambao ndilo taifa la Dunia

Alibainisha kuwa kama watoto watajali na kutoa kipaumbele zaidi katika msingi wa neon la Mungu ni wazi kuwa kamwe shetani hataweza kuwafanya wawe katika njia ambazo si sahihi ambazo ndizo chanzo pekee cha mateso ndani ya familia zao.

MWISHO 

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891
ARUSHA 
WACHUNGAJI ARUSHA WALIA NA JESHI LA POLISI DHIDI YA MORANI
 
WACHUNGAJI wa kata ya Elerai mkoani hapa wamelitaka jeshi la polisi kuhakikisha kuwa wanachukulia sheria kali baadhi ya vijana wa kimasai”Morani”ambao wanawatembeza mitaani watu wakiwa utupu pamoja na kuwavisha magunia, na endapo kama jehi hilo halitaweza kufanya hivyo wao kama kanisa watafikiria mbinu nyingine ya kukabilana na Morani ambao wanawasumbua wananchi.
 
Akiongea na “NYAKATI” mapema leo kwa niaba ya wachungaji wa kata ya Elerai Sakina mchungaji Noel Urio alisema kwa muda mrefu sana vijana hao wamekuwa kikwazo kikubwa sana cha kufanya baadhi ya wakristoi kukosa amani.
 
Mchungaji Urio alibainisha kuwa Morani hao wamekuwa wakivamia makazi ya watu na kuchukua mali bila idhini na kisha kuwatembeza mitaani uchi huku wakiwa wamewavisha magunia huku jeshi la polisi likiwa na mbinu za kuweza kuwakamata Morani hao.
 
Waliongeza kuwa Jeshi la polisi ndilo lenye nafasi pekee ya kuweza kuwasaidia wananchi na kurudisha amani lakini mpaka sasa bado watuhumiwa hata wa sehemu nyingine hawajaweza kukamatwa na kutiwa mbaroni.
 
“hawa  Morani wamekuwa wakisumbua sana jamii kwa kuwa hata wale wa kipindi cha nyuma hawajatiwa mbaroni kwa maana hiyo sisi tunaomba ushirikiano dhidi ya hawa morani na kama hili litashindikana sisi tutajua kitu cha kufanya kama kanisa kwa kuwa na sisi wakristo tunahaki ya kuhakikisha kuwa tunaishi kwa amani”aliongeza Bw Urio.
 
Pia alisema kuwa Polisi pekee ndio wenye uwezo wa kuhakikisha kuwa wanatuliza gasia zote ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa wananchi wanaishi kwa amani bila kufuata sheria au mila ambazo wanaona zipo kinyume na imani zao.
 
Alibanisha kuwa pamoja na Morani hao kutaka mila zifuatwe za Kimasai lakini kimsingi mia hizo zina madhara makubwa sana kwa kuwa hata njia ambazo zinatumika ni hatari sana kwa Afya.
 
Aliongeza kuwa Njia ambazo zinatumika katika kufanya tohara si njia njema kwa kuwa hata vifaa ambavyo vinatumika na vyenyewe havina ubora ambao unatakiwa kwa ajili ya afya ya mwanadamu hususani kwa nyakati hizi ambazo kuna maambukizi ya magonjwa mengi.
 
Naye mzee wa bomaBw Robert Elias  ambaye alitembezwa umbali mrefu yeye pamoja na mwanaye alisema kuwa katika siku ya tukio polisi walikuja lakini wakashindwa kumuokoa
 
Alilitaka Jeshi la polisi kuhakikisha kuwa wanawachukulia hatua kali na kisheria wale wote ambao wamehusika katika matukio hayo kwa kuwa mila ambazo Morani hao wanataka zifutwe tayari zimeshapitwa na wakati na ni hatari kwa afya ya Mwanadamu.
 
MWISHO 

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891

ARUSHA 
NABII MALISA AWATAKA WAKRISTO KUTOA MAFUNGU YA KUMI, KUWA NA IMANI ILI KUONDOKANA NA UMASKINI

IMEELEZWA kuwa asilimia kubwa ya watu ambao ni maskini wanashindwa kuinuka katika umaskini na kuingia kati hadhi ya utajiri kutokana na wao kujithaminisha sana na baadhi ya mali zao huku wakishindwa hata kumpa Mungu Fungu la Kumi

Umaskini uliopo kwa sasa ni fumbo kubwa sana baina ya watu na watu lakini chanzo kikubwa ni kutokuwa na maagano na mungu, pamoja na kushindwa kutoa mafungu ya kumi.

Hayo yameelezwa jijini hapa na Nabii Boniphace Malisa kutoka katika huduma ya Ukombozi ,Ministry for al Nationals wakati alipokuwa akiongea na wakristo wa mji wa Arusha mapema wiki hii.

Aidha Nabii Malisa alisema kuwa hakuna sehemu ambayo Mungu alisema wanadamu wawe maskini bali Mungu alisema kuwa  wanatakiwa kutawala vitu vyote vya duniani hali ambayo inaonesha wazi kuwa Mungu aliweka maagano .

Alisema kuwa katika nyakati za sasa asilimia kubwa ya watu wanalia kuwa wao ni maski ni bila kujua na kutambua kuwa umaskini walio nao wamejitakia wao wenyewe hata kwa njia ya kukiri na kukataa maagano na Mungu, pamoja na kutoa Mafungu ya kumi.

Alibainisha kuwa mkristo anapotoa Fungu la Kumi ni wazi kuwa anarudisha matoleo na sadaka ambazo amezipata kwa mungu lakini wanaoteswa na roho ya umaskini kwa sasa ni wale ambao hawana mambo mbalimbali kama vile Imani, Maagano ya kimungu, Mioyo ya kujitolea hali ambayo inatumika kama kigezo na Muovu shetani hasa pale mtu anapodai haki yake

“leo unakuta mtu anadai kuwa Mungu hamuonoi lakini ukiangalia hana hata agano lolote lile ambalo ameliweka yeye pamoja na Mungu sasa Mungu atasimamaje lakini mtu huyohuyo akienda kwa mganga anaweka agano na mganga Kwa Mungu inashindikana  je umaskini utaisha au utaongezeka mara dufu”alisema Nabii Malisa.

Pia amesema kuwa kanuni za maagano ya Mungu ni za msingi kwa mtu yoyote yule ambaye anataka utajiri kwa maana hiyo ni vema watu wakatafiuta maagano ya Kimungu na wala sio maagano ya Kidunia(ZABURI 50.5)

Katika hatua nyingine amewataka hata wale ambao wanaweka maagano dhidi ya Mungu kuhakikisha kuwa wanawajibika Vema na kukumbuka maagano hayo kwa kuwa hata katika jamii wapo baadhi ya watu ambao wanaweka maagano lakini wanashindwa kuyatekeleza.

MWISHO 

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891
 ARUSHA 
MANABII MSIGEUZE HUDUMA HIYO YA UNABII KAMA BIASHARA- ASKOFU YONA


Manabii mbalimbali hapa nchini wameshauriwa kuhakikisha kuwa wanatumia karama hiyo vema ikiwa ni pamoja na kuacha kutumia karama hiyo kama kipato mojawapo cha kuweza kupata fedha.

Endapo kama watategemea kumtabiria mtu kitu na kisha kudai fedha ni wazi kuwa watakuwa wanafanya huduma hiyo kwa maslahi yao na  wala sio kwa maslahi ya Mungu ambayo wameitiwa.

Kauli hiyo imetolewa mjini hapa na Askofu Yona Suleman kutoka  Singida wakati alipokuwa akitoa neno katika kanisa la  all National  for Christian centre lilopo katika maeneo ya Jakaranda ndani ya manispaa ya Arusha, ambapo pia huduma hiyo ilienda sanjari na usimikwaji wa Viongozi mbalimbali katika kanisa hilo.

Aidha alisema kuwa hduuma ya utabiri sio mbaya kwa kuwa hata pindi Bwana yesu alipokuwa hapa duniani aliweza kufanya tabiri mbalimbali ambazo zilikwenda sambamba na uponyaji lakini hakudai fidia yoyote ile.

Aliongeza kuwa ili huduma yoyote ile iweze kukua ni lazima iende sambamba na utabiri na unabii lakini unabii huo pia uwe ni bure na ambao unalenga kuimarisha zaidi maisha ya mwanadamu ambaye ndiye anayetegemea Kanisa katika maisha yake.

"wapo baadhi ya watu na mimi nimeshawaona kabisa wanatoa unabii kwa mtu kisha wanadai malipo sasa hali hiyo ni mbaya sana kwa kuwa wanafanya hata kiwango cha imani za watu kushindwa kukua kwa kiwango ambacho kinaitajika"alisema Bw Yona.

Pia aliongeza kuwa na wale ambao wanapewa unabii juu ya mambo mbalimbali wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanapokea unabii huo vema ambapo pia mara baada ya kupokea unabii huo wanapswa kufanya toba

Alisisitiza kama toba hazitafanyika tena kwa wakati ni wazi kuwa wakristo hao watakuwa wanahama hama makanisa kwa ajili ya kutafuta Miujiza ambayo inatolewa na manabii hao wakati Mungu anapatikana mahala popote pale.

MWISHO                         

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891

ARUSHA 

WASHAURIWA KUTUMIA NISHATI YA BIOGESI

WAFUGAJI wanaofuga mifugo mbali mbali hapa nchini wameshauriwa kutumia
nishati bora ya bioges badala ya kutumia nishati za kuni ambapo tafiti
zinaonyesha kuwa nishati za kuni zimechangia kwa asilimia kubwa uharibifu
wa mazingira ambao umesababisha mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo yalisemwa na mkuu wa wilaya ya Mwanga bw Athuman Mdoe alipokuwa katika
ufunguzi wa teknolojia wa mtambo maalum wa bioges kwa ajili ya maeneo yenye
hali ya ukame uliozindiliwa rasmi mwanga mkoani kilimanjaro.

Aidha alisema kuwa nishati ya bioges ni nishati ya gharama nafuu
ukilinganisha na nishati nyinginezo kama vile umeme,gesiza viwandani ,mkaa
na kuni ambapo pia nishati hii inapunguza kwa kiwango kikubwa cha uharibifu
wa mazingira.

Aliongeza kuwa faida za nishati ya bioges haziishii hapo bali husaidia
katika uhifadhi wa mazingira ,hutoa mbolea bora kwa ajili ya kilimo
,hupunguza mudawa akina mama unaotumika katika utafutaji kuni na pia
hupunguza maradhi yotokanayo na matumizi ya kuni na mkaa.

Alieleza kuwa teknoloja hiyo ambayo kwa kitaalamu inajulikana kama Solid
State Biodgester(SSB)ambayo ndio iliyotumia katika ujenzi wa mtambo huo
utaweza kuwanufaisha wakazi waishio kwenye maeneo ya hali ya ukame ikiwemo
wilaya hiyo hivyo kuwataka wafugaji walioudhuria katika ufunguzi huo
kuitumia fursa hiyo pekee kuweza kjinufaisha na teknolojia hiyo..

Nae mratibu wa programu ya uenezi wa mitambo ya bioges kwa ngazi ya
kaya(TDBP)bw .Lehada Cyprian alisema kuwa programu hiyo imefanikiwa
kuhamasisha ujenzi wa mitambo katika maeneo yenye urahisi wa upatikanaji wa
maji .

Bw Cyprian aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu kwa kushirikiana
na wadau wengine imefanikiwa kujenga mitambo 2568 katika maeneo tofauti
tofauti hapa nchini.

Alieleza kuwa pia programu imepanga kujenga mitambo 50 kwa mwaka huu w
fedha kwa kutumia teknoloja ya SSB katika maeneo tofauti hapa nchini ikiwa
ni pamoja na mwanga,arusha na hanang lengo halisi likiwa ni kuwafikia
wafugaji wa ng'ombe asili ili nao waweze kunufaika na teknolojia hiyo ya
bioges.

mwishoo

CHANZO CHA HABARI NA QUEEN LEMA

0758907891

ARUSHA