Sunday, September 16, 2012

SHIRIKA LAFANIKIWA KUIBUA VIPAJI 1000


NA MERY KITOSIO, MERU

SHIRIKA la Afrika Amini Alama kutoka nchini Austria limewakutanisha wanafuzi zaidi ya elfu moja kutoka  shule mbali mbali za msingi na sekondari  wilayani arumeru kwa  lengo la kutambua na kukuza   vipaji vyao walivyo navyo ili waweze kusaidiwa kielimu .

Akizungumza na upako wa habari meneja wa shirika hilo bw Willium Kinua alisema kuwa shirika hilo limeamua kuwakutanisha wanafunzi hao kwa kuwa wapo wanafunzi wenye vipaji lakini havitumiki ipasavyo.

Alisema kuwa kupitia tamasha hilo la kutambua wanafunzi wenye vipaji  litasaidia kwa kiwango kikubwa kuibua vipaji mbali mbali ambavyo wameshindwa kuviibua ambapo kupitia michoro ambayo watachora itawasaidia kupatiwa misaada mbali mbali ya  kielimu.

Aliongeza kuwa shirika hilo kwa sasa  limelenga kuwasaidia watoto kwa kuangalia vile vipaji muhimu walivyozaliwa navyo ikiwa ni wale wenye vipaji vya sanaa,uchoraji pamoja na mpira  ambapo  wanafuzi wengi wanashindwa kujitambua ni vipiji gani walivyo navyo.

“Afrika Amini Alama tumejipanga kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliopo haya maeneo wananufaika na elimu kwa kupitia vipaji vyao walivyo navyo kwa kuwa tumeona wako wanafunzi wengi wana vipaji vyao vya kuzaliwa lakini hawajitambui ni kipaji gani walicho nacho”alisema Kinua.

Kwa upande wake mratibu wa shirika hilo bw Jaffarson Severua alisema kuwa awali kabla ya kufanyika kwa tamasha hilo la kukuza vipaji shirika hilo liliwapatia kwanza wanafuzni hao semina kwa ajili ya kujua namna ya kuibua vipaji vyao ambapo mara bada ya kuibua vipaji hivyo kwa njia ya uchoraji picha hizo zitapelekwa Austria ambapo wafadhili wa shirika hilo ndio watawajibika kuwasaidia wanafunzi hao .
Aidha Severua alitaja maeneo waliyotokea wanafunzi hao kuwa ni  kata za 
Ngarenanyuki,Ngabobo,Kisimiri,Olkwang’ado,Momela,Lendoiya,pamoja na Miririn zote zikiwa za halmashauri ya Meru.

Hata hivyo aliiomba serikali kuwaunga mkono hasa pale wanapokwama hasa kielimu kwa kuwa wamejikita zaidi kusaidia zile jamii zisizokuwa na uwezo wa kuendeleza watoto kielimu ambapo hadi sasa wana mkakati wa kujenga shule nne za awali ambapo hadi sasa wameshajenga katika kata ya leguruki na ngarenanyuki shule zenye majaengo  yanayogahrimu zaidi ya shilingi milioni 300.

mwisho

No comments:

Post a Comment