Tuesday, September 4, 2012

UGUMU WA MAISHA,NA UKOSEFU WA ELIMU YA MAZINGIRA VIJIJINI CHANZO CHA UHARIBIFU WA VYANZO MBALIMBALI VYA MAZINGIRA




Na Queen Lema,MERU

IMEELEZWA kuwa baadhi ya wananchi hasa wa Vijijini wanaharibu Mazingira na uoto wa Asili wa Vijiji kutokana na hali ngumu ya maisha huku wengine wakiwa wanafanya hivyo kutokana na ukosefu wa elimu mbalimbali hasa elimu ya Mazingira bora hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana Vijjiji vingi kukabiliwa na Ukame

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa kijiji cha Nkoanekoli wilayani Meru Mkoani hapa Bw Christphoer Palangyo wakati akiongea na “upako wa habari”mapema jana kuhusiana na hali ya uharibifu wa mazingira ambayo inafanyika ndani ya eneo hilo

Bw Palangyo alisema kuwa hali ngumu ndio chanzo pekee ambacho kinasababisha baadhi ya wananchi kuharibu mazingira hasa katika eneo hilo la Nkoanekoli hali ambayo kama haitachukuliwa tahadhari basi itasababisha Ukame wa hali ya Juu sana

Alifafanua kuwa asilimia kubwa ya wananchi hasa wa eneo hilo la Nkoanekoli wanajishugulisha na shuguli za uchimbaji wa udongo ili waweze kujikimu na hali ngumu za maisha ya kila siku huku wengine wakiwa wanafanya hivyo bila ya kujua na kutambua kuwa hali hiyo ni mbaya sana hasa kwa utunzaji wa Mazingira.

“Elimu ya utunzaji wa mazingira  ni muhimu sana hasa kwa maeneo ya vijijini kwa kuwa baadhi ya watu wanaharibu vyanzo  mbalimbali na malzingira kutokana na hali ngumu ya maisha na pia wengine hawajui madhara ambayo yanaweza kutokea lakini kama watu wangekuwa wanapewa elimu ya  kutosha basi wasingeweza kuendelea kuharibu mazingira ambayo ni chanzo kilimo kwanza ambacho nacho kwa sasa kimedorora sana hasa katika maeneo ya Vijijini”aliongeza Bw Palangyo.

Akiongelea hali ya uharibifu wa mazingira hasa katika maeneo ya Kijiji ckha Nkoanekoli alisema kuwa kwa sasa wananchi wengi wanachimba Udongo ili waweze kujikwamua na hali ya Maisha huku hali hiyo ikisababisha kwa kiwango kikubwa sana Mmonyoko wa udongo ndani ya Kijiji hicho.

 Hataivyo alisema kuwa kutokana na hali hiyo Uongozi wa kijiji hicho umelazimika kuingilia kati suala hilo ambapo mpaka sasa uharibifu ni mkubwa sana hasa katika maeneo ambayo yapo kwenye vyanzo vya maji(CHEMCHEM) huku hali hiyo pia ikichangia kwa kiwango kikubwa sana baadhi ya vyanzo hivyo kukauka na kubaki vikiwa na hali ya ukame sana.

“hawa wananchi wa kijiji hiki ambao wanachimba Udongo kwa sasa wamevamia hadi katika vyanzo vya maji na kuchimba bila kujua kuwa kvyanzo hivyo ni muhimu sana hata kwan kata nyingine sasa kwa hali kama hii imetulazimu kuanza kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa nguvu sanjari na kutunga sheria kali hasa kwa hawa watu ambao ni wachimba udongo kwani kama hali itaendelea kama hivi baada ya miaka mitano hapa Meru patakuwa ni jangwa kabisa”aliongeza bw Palangyo

Alimalizia kwa kusema kuwa ni Vema kama Serikali pamoja na asasi binafsi zikahakikisha kuwa zinajiwekeza zaidi vijijini ambapo ndipo kwenye uitaji mkubwa sana wa utunzaji wa mazingira na Endapo kama hawataweza kufanya hivyo basi baadhi ya wananchi kila mara wataharibu mazingira huku wakijua kuwa wapo sahihi na wanachokifanya kwenye uharibifu huo.

MWISHO

No comments:

Post a Comment