Tuesday, September 25, 2012

TUME YA KUDHIBITI UKIMWI YASHAURIWA KUONGEZA KASI

 Na Mustafa Leu. ARUSHA

TUME ya taifa ya kudhibiti Ukimwi nchini Tacaids, imeshauriwa  kuongeza kasi zaidi ya mapambano hayo   dhidi ya maambukizi mapya  kwa kutoa elimu  zaidi  kwa jamii iweze kuchukua hatua za kujiepusha  na maambukizi na kusathiri nguvu kazi ya taifa inayotegemewa.

Hayo yameelezwa jana na Afisa tawala mkoa wa Arusha, Exaud Mwanga,alipokuwa akifungua kikao cha siku moja cha viongozi wa madhehebu ya dini mkoani Arusha  kuhusu mwitikio na usahiriki wao  katika mapambano ya ugonjwa wa ukimwi  kilichoaandaliwa na tume ya taifa ya kudhibiyi ukimwi nchini Tacaids.

Mwanga, amesema kuwa serikali inatambua juhudi kubwa  zinazofanywa na madhehebu ya dini  kwa kushirikiana na tacaids   na wadau wengine kwa kutoa ushauri wa kiroho kwa watu waishio na ukimwi ushauri unaowawezesha waliokwisha ambukizwa kuishi kwa matumaini ..

Amesema mchango unaotolewa na madhehebu ya dini  katika kupunguza ongezeko la maambukizi ya ukimwi  ni mkubwa sana ,pamoja na mchango huo kuwa mkubwa bado mahitaji ya elimu ni makubwa  hasa ngazi za kata, vijiji na jamii  na familia yanahitajika ili kupunguza ongezeko la maambukizi mapya  ambapo kwa mijini kiwango cha maambukizi ni asilimia 8.7 na vijini ni asilimia 4.7

Awali Kamishina wa tume ya ukinmwi nchini Askofu mstaafu wa KKKt, Peter Lukumbusho Mwamasika , amesema taasisi za dini  zina wajibu mkubwa  kutoa misaada ya kimalezi, kiafya, kielimu, kiushauri,  kisheria  kwa waathirika  ambao ni waumini wao  ili waepuke kupata maambukizi mapya.

Amesema taasisi hizo za dini  lazima zitambue kuwa zina wajibu wa kuwatunza  yatima na wajane  wasiokuwa na uwezo ambao wanatokana na vifo vya ukimwi ili kuwaanzishia miradi ya kiuchumi na kuachana na tabia ya  kuwaombea dua na kuwaacha waende zao  bila kuwawezesha

Amewaambia viongozi hao kuwa Tacaids ina jukumu kubwa la kuhamasisha watu waeleze mahitaji yao kuhusu mapambano dhidi ya ukimwi  na kuwaepushia kupata maambukizi mapya na kupitia Tacaids, serikali inzifikia taasisi za dini ili ziweze kusaidia kutoa elimkwa wananchi kuhusu madhara ya ukimwi na hatua za kuchukua ili kujikinga na maambukizi mapya.

mwisho

No comments:

Post a Comment