Friday, September 28, 2012

KAMPENI ZA CHADEMA KWA KATA ZA DARAJA MBILI NA BANGATA KUANZA OCTOBER 3


KAMPENI ZA CHADEMA KWA KATA ZA DARAJA MBILI NA BANGATA KUANZA OCTOBER 3

Na Mery Kitosio, ARUSHA

CHAMA cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) kinatarajia kuanza rasmi kampeni zake katika kata za daraja mbili manispaa ya Arusha  na kata ya Bangata Wilayani Meru mkoani Arusha ambapo kampeni hizo zinatarajiwa kuwa kuanza rasmi October tatu na kuongozwa na  ya aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini Goodbles Lema na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari

Hayo yamelezwa mjini hapa na Katibu wa mkoa wa chama hicho  Amani Golugwa jana ambapo alisema kuwa mpaka sasa wameshafanikiwa kupata wagombea watakosimama katika kinyanganyiro hicho ambacho kitahusisha vyama mbalimbali vya siasa kwa mkoa wa Arusha.

Golugwa alisema kuwa ndani ya chama hicho wamesharidhia wagombea wawili kuweza kusimama ambao ni bw Prosper Msofe ambaye atasimama kama mgombea Udiwani kwa tiketi ya chama hicho  katika kata ya daraja mbili huku kata ya Bangata Meru nayo ikiwakilishwa na Erick Samsoni ambapo pia kampeni za kuchukua kata hizo nazo zitaendeshwa kwa njia ya kitaalamu na kidemokrasia sana.

“hawa watu wawili mpaka sasa chama kimeshawapa baraka zote za kuweza kugombea kwa kata hizi mbili lakini kwa sasa tunatarajia kuhakikisha kuwa kamwe demokrasia ya watanzania haibakwi na baadhi ya viongozi walafi na badala yake tutahakikisha kuwa kila mtu anatumia vema demokrasia yake ili kupata haki zake za msingi”aliongeza  Golugwa

Hataivyo aliongeza kuwa ndani ya kampeni hizo ambazo zinatarajiwa kuanza wiki ijayo chama hicho kamwe hakitamvumilia kiongozi yoyote yule ambaye atakuwa anatoa Rushwa ya aina mbalimbali zikiwemo Rushwa za kutumia magari ya Serikali ndani ya kampeni na badala yake kiongozi atakayefanya hivyo watamuhisha na Rushwa na hivyo chama hicho kitasimamia ukweli kwa kuwafikisha ndani ya Magareza

Awali alisema kuwa mbali na kuanza rasmi kampeni kwa kata za Daraja mbili na Bangata pia chama hicho kimelazimikka kuwapa waraka muhimu chama cha Wananchi Cuf juu ya mapungufu mbalimbali ambayo yanaendelea kutokea katika mji wa Arusha hasa katika harakati zao za mikutano ya Hadhara ambayo inaendelea ndani ya Mji wa Arusha

Golugwa alisema kuwa chama hicho kimekuwa kikitoa malalamiko kadhaa  baadhi ya wanachama wa Chadema wamewafanyia vurugu huku vurugu hizo zikihusishwa na aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini bw Goodbless Lema hali ambayo inasababisha muendelezo wa Siasa chafu ambazo ndizo chanzo kikubwa sana cha ubakaji wa  Demokrasia hadharani.

“Sisi kamwe hatuwezi kuwafanyia hawa Cuf vurugu kwa kuwa tunajua kuwa hilo ni suala la uvuinjifu wa amani ndani ya nchi yetu na kwa maana hiyo tunapenda kuwaambia kuwa tunawapenda na pia tunawakaribisha ndani ya mji wa Arusha ila wasitafute visngizio vya hapa na pale ila watafute hoja ambazo zinajenga na kuimarisha hata Maslahi ya Nchi”alibainisha  Golugwa

Mbali na hilo katibu huyo pia alisema kuwa Cuf inatakiwa kuhakikisha kuwa inakuwa na Matamko ambayo yanalenga kumkomboa Mtanzania na wala sio kuwa na matamko ambayo hayana tija mbele za jamii kama ambavyo wamefanya kupitia Kwa Naibu  Mkurugenzi wa habari uenezi na haki za binadamu, Abdul Kambaya ambaye alitoa matamko ambalo lilikuwa na matisho na lugha isiyofaa kwa nchi na jamii za kitanzania

MWISHO

No comments:

Post a Comment