Tuesday, April 29, 2014

ASKOFU ISANGYA ANENA NA VIJANA

IMEELEZWA kuwa ongezeko la vijana maeneo ya mijini chanzo chake kikubwa ni kuwa asilimia kubwa ya vijana hasa wa vijijini bado hawajaweza kutambua fursa za uchuni  walizonazo hali ambayo nayo inasababisha wimbi kubwa la watu mijini ambao hawana ajira za kutosha


Vijana wanaokimbilia mijini kutoka vijijini ni kutokana na kuwa kule vijijini hawahapata muongozo wa kutambua na kisha kutumia fursa za mali zilizopo jambo ambalo kwa sasa wadau ikiwemo serikali inatakiwa kuchukua tahadhari juu ya hilo.

Kauli hiyo imetolewa na askofu Dkt Eliud Isangya wa kanisa la Intenational evangelism Church  wakati akiongea na waandshi wa habari kuhusiana na fursa za vijana pamoja na changamoto ambazo zinawakabili vijana.

Aidha alidai kuwa inashangaza sana kuona kuwa wimbi kubwa la vijana wanakimbilia mijini wakati huko vijijini kuna fursa za kutosha na hazitumimiki wakati mijini fursa za ajira hazipatikani

Kutokana na hilo alisema kuwa kinachosabbisha waje mijini ni kuwa hawajaweza kutambua fursa zilizopo huku baadhi ya watumishi wa serikali wenye dhamana na vijana nao wakiwa wamesahu wajibu wao kwenye jamii wa kusaidia kundi hilo.

“hawa watendaji wa serikali wakati mwingine wanasahu wajibu wao hata wa kuweza kutangaza fursa za ajira kwa vijana na inasababisha vijana waweze kuona kuwa wapo pekee yao na hivyo wanaona bora waje mjini”aliongeza Dkt Isangya.

Hataivyo alidai kuwa kutokana na hilo asilimia kubwa ya vijana wanaokuja mijini wanasababisha madhara makubwa sana kwani wengi wao wajikuta wakiwa wanaangukia katika matukio ya kihalifu na matukio mabaya ya uharibifu wa amani ya nchi kwa hali hiyo ni changamoto kubwa sana kwa serikali, kwa vijana na hata wadau wa dini’aliongeza Dkt Isangya.
MWISH

NYUMBA ZAIDI YA 300 ZILIZOBOLEWA ARUSHA ZALETA DALILI YA WAWEKEZAJI WA KIMATAIFA

NYUMBA ZAIDI YA 300 ZILIZOBOLEWA ARUSHA ZALETA DALILI YA WAWEKEZAJI WA KIMATAIFA

Arusha

JIJI la Arusha limefanikiwa kuvunja nyumba zaidi ya 300 katika oparesheni maalumu ya kusafisha  jiji huku pia likiweza kuweka mikakati mbalimbali ya kuendelea kuboresha sehemu ambazo zimebomolewa nyumba hizo  huku pia Viongozi nao wakidai kuwa kuanzia kubomolewa kwa nyumba hizo kumeanza kuongeza idadi ya wawekezaji wenye nia ya kuwekza katika maeneo hayo.

Aidha nyumba hizo zilibomolewa siku chache zilizopita ambapo pia zoezi hilo liliweza kwenda sanjarai na ukamataji wa bidhaa ambazo zilikuwa zinauzwa nje bila mipangilio.

Hayo yamelelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela wakati akiongea na viongozi wa Majiji mbalimbali hapa nchini wakati akielezea mpango wa kuboresha jiji la Arusha

Mongelea alisema kuwa hapoa wali nyumba zilizobomelewa zilikuwa  katikati ya Jiji na zilikuwa zinalipa kodi ndogo sana ukilinganisha na hadhi yenyewe ya Jiji la Arusha hali ambayo ilisababisha waweze kuchukua hatua hiyo.

Hatiavyo Monngela alisema kuwa kabla ya hapo walilazimika kuburutwa mahakani ambapo wenye nyumba hzio walidia kuwa Jiji limewaonea na hivyo hawapaswi kuondolewa katika nyumba hizo.

“hawa walituburuza mahakamani na kudai kuwa tunawaonea sasa sisi tulishinda katika kesi hiyo na tuliweza kubomoa nyumba hizo ambazo walikuwa wanalipa kiasi cha kati ya elfu sita mpaka kumi kama kodi wakati kwenye majumba mengine watu wanalipa mpaka kiasi cha Mamilioni kwa ajili ya nyumba za biashara na nyumba za kuishi”aliongeza Mongela

Hataivyo Mkurugenzi mtendaji wa Jiji Juma Iddi alisema kuwa kwa sasa kuna mpango wa kuweza kuendeleza maeneo hayia mbayo yalikuwa kwanza na ujenzo holela lakini pia yalikuwa hayaingizi faida kubwa kwa Jiji

Iddi alisema kuwa toka nyumbha hizo kubomolewa Jiji la Arusha limekuwa katika taswira tofauti sana kwani kwa sasa hata wawezekaji nao wameanza kujitokeza tofauti na hapo awali ambapo kulikuwa na nyumba hizo

“hapo awali tulikuwa hatufanikiwi kwa lolote hata kodi yao kwetu ilikuwa ni ndogo sana lakini kwa sasa tumeweza kubomoa na sisi tutawekeza kwenye majengo makubwa yenye hadhi zake na wala sio yale”aliongeza Iddi.

Pia alisema kuwa mbali na kuwekeza majengo yenye hadhi ya Jiji na kimataifa kwenye maeneo ambayo nyumba hizo zimebomolewa lakini pia wanampango endelevu wa kuhakikisha kuwa nyumba za Jiji la Arusha zinajengwa kwenye hadhi ambayo inakubalika na wala sio ujenzi holela.

MWISHO

MANYARA WAPEWA CHANGAMOTO YA MABWENI

ILI kupambana na changamoto za elimu kwa watoto wa kike Mkoani Manyara, imeelezwa suluhisho ni kuwajengea mabweni ya kulala kwani hivi sasa wanasoma kwenye mazingira mabovu kutoka na mazingira ya mkoa huo.
 
Wito huo umetolewa Wilayani Mbulu na Mwenyekiti wa Mtandao wa asasi za kiraia mkoani Manyara, (Macsnet) Asia Lembariti, wakati akizungumza juzi kwenye Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo.
 
Lembariti alisema ili kuboresha elimu kwa mtoto wa kike shirika la WEGCC limejikita kufanya utafiti kwenye sekta ya elimu hasa ubora wa mazingira ya upatikanaji wa elimu kwa watoto wa kike katika shule za sekondari.
 
Alisema shule nyingi zipo mbali na kaya nyingi wanakotoka wanafunzi na uhaba wa miundombinu unachangia wanafunzi kutembea umbali mrefu mpaka kilometa 16 hadi 32 kwa siku, kwenda shule na kurudi nyumbani.
 
“Hii ni hatari zaidi kwa watoto wa kike na suluhisho ni mabweni, kwani huchangia mahudhurio hafifu, kuacha shule, kuchochea ubakaji na ujauzito kwani toka mwaka 2004 hadi 2010 watoto 45,256 waliacha masomo,” alisema.
 
Alisema ili kukabiliana na changamoto zote hizo zisababishwazo na kutembea umbali mrefu kwenda na kutoka shule, ujenzi wa mabweni ni muhimu, tofauti na kupanga kwenye magheto na matatizo kwenye vyombo vya usafiri kila siku.
 
Alisema Macsnet inatekeleza miradi minne kwa kushirikiana na wanachama wake ndani ya mkoa huo ikiwemo kuboresha elimu kwa watoto wa kike kuwajengea uwezo wa uandishi wa miradi, kuboresha ufugaji wa asili na kuboresha lishe.
 
“Katika kufanikisha miradi hiyo Wegcc imejikita kufadhili mradi wa kuboresha elimu kwa watoto wa kike na pia tunashirikiana na Usaid katika lishe, Care International kwa ufugaji na FCS utekelezaji miradi,” alisema Lembariti.
 
MWISHO.

WAFANYABIASHARA WAPEWA MBINU YA MABOMU

NA MWANDISHI WETU, ARUSHA


jeshi la polisi mkoa wa Arusha limewaomba wafanyabiashara pamoja na wanachi wote ambao wanakuwa kwenye mikusanyiko mara kwa mara kuhakikisha kuwa wanatumia camera aina ya CCTV ili kuweza kujiepusha na majanga hasa ya mabomu.

Hataivyo kauli hiyo inakuja siku moja mara baada ya kutokea kwa mlipuko wa bomu ambalo linadhani kuwa ni bomu la kienyeji na kisha kulipuka katika baa moja ijulikanayo kama Arusha Night  Park
Kauli hiyo imetolewa Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya Jinai Isaya  Mngulu wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya hatua ambazo wamezichukua mpaka sasa juu ya matukio hayo ya mabomu kwa mkoa wa Arusha.


Kamanda Isaya alisema kuwa watu wakichukua tahadhari basi wataweza kuwasaidia wengine kuepukana na vifo ambavyo sio vya lazima kwani kwa sasa magaidi wanaitesa sana jiji la Arusha.

Alidai kuwa kupitia camera hizo tahadhari inaweza kuchukuliwa tofautri na sasa ambapo kwa sasa asilimia kubwa ya mabomu ya kienyeji yanarushwa sana hasa kwenye mikusanyiko ya watu.


Hataivyo alishauri uongozi wa mkoa wa Arusha kuweka mikakati mbalimbali ya kuweka Camera hizo pande zote za Jiji kwani pia hilo nalo litaweeza kusaidia sana kupunguza uhalifu .


Kamanda Isaya alisema kuwa pamoja na kuwa wameweka mikakati mbalimbali ya kuweza kupunguza na kutokomeza uhalifu hasa wa mabomu katika maeneo ya mikusanyiko Polisi wanatarajia kufanya uchunguzi wa tukio hilo ambalo liliweza kujerui watu 15 ingawaje pia watatoa kitita cha Milioni 10 kwa mtu yeyote ambaye ataweza kutoa taarifa na kisha kufanikisha kukamtwa kwa mtuhumiwa.



Alimalizia kwa kusema kuwa katika tukio hilo la kurushwa kwa bomu la kienyeji katika nyumba hiyo ya kulala wageni hali za majerui zinaendelea vizuri na kwa sasa majerui nane wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Arusha.

Mbali na hayo Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amewataka wananchi wa Jiji la Arusha wasiwe na hofu juu ya mikusanyiko ila wachukue tahadhari ingawaje kwa sasa wamejipanga kulinda ipasavyo hasa msimu huu wa majira ya sikukuu ya Pasaka.

sabas alidai kuwa wanatarajia kufanya ulinzi wa kutosha kwa kutumia vifaa mbalimbali kama vile Mbwa, Farasi, pamoja na Polisi wenyewe ili kuweza kuwafanya wananchi waweze kusherekea siku hiyo ya Pasaka.

MWISHO

DAWA YA NJAA YAINISHWA

IMEELEZWA kuwa ili nchi ya Tanzania iweze kuepukana na majgana hasa ya baa
la njaa Nchi inapaswa kuzalisha kilimo kwa asilimia zaidi ya sita ambapo
chakula kinachozalishwa kitaweza kuwekwa hadi akiba tofauti na sasa ambapo
uzalishaji wa kilimo ni kwa asilimia 4 pekee.

Hataivyo uzalishaji huo wa asilimia sita pia utaweza kuongeza ufanisi wa
kilimo na kitakuwa ni cha kisasa zaidi hivyo majnga hasa ukosefu wa
chakula,umaskini nao utaweza kupungua kwa kiwango kikubwa sana .

Hayo yameelezwa na Bi Nkuvililwa Simkanga ambaye ni mkurugenzi wa sera na
mipango kutoka katika Wizara ya kilimo na ushirikia wakati akiongea kwa
niaba ya wizara hiyo mara baada ya kukabidhiwa kwa Jengo la kuhifadhia
mazao ambalo limejengwa chini ya uzamini wa  TAHA

Mkurugenzi huyo alidai kuwa kwa sasa Tanzania bado inazalisha Kilimo kwa
kiwango cha Asilimia 4 pekee hali ambayo bado inahitajika kuongezewa nguvu
zaidi kwani uwezekano wa kuendelea kuzalisha kwa wingi sana bado upo endapo
kama kutakuwa na umoja baina ya wakulima na wadai wengine wa Kilimo.

"tukizalisha kilimo chenye ubora na kiwango ambacho kinahitajika basi
tutaweza kupunguza tatizo la uhaba wa chakula na hata umaskini nao
utapungua kwani uwezo wa kufanya hivyo tunao kabisa ila changamoto bado
zinashindwa kutufikisha"aliongeza Bi Simkanga.

Mbali na hayo alisema kuwa Kilimo kinachangia uti wa mgongo wa taifa kwa
asilimia 24.7 huku wananchi nao wakiwa wanategemea kama ajira kwa asilimia
75 ambapo pia asilimia 95 ya chakula kinachotumika hapa nchini kinatokana
na kilimo

"Takwimu zinaonesha kuwa hali si mbaya sana na kilimo kinaendelea vizuri
sana ingawaje pia wakulima wana uwezo mkubwa sana wa kuzalisha chakula
kingi na hata kikaweza kupelekwa nje ya nchi hivyo jitiada za makusudi
zinahitajika kwa haraka sana"aliongeza

Wakati huo huo Mwenyekiti wa TAHA Erick Ngmario    erick alisema kuwa ili
wakulima waweze kufikia malengo yao ya kila siku wanatakiwa kuachana na
mila ambazo zimepitwa na wakati kwani wakati mwingine zinasababisha waweze
kulima kilimo cha umaskini

Erick alidai kuwa moja ya mila hizo amnazo zimepitwa na wakati ni pamoja na
mila za kulima kwa mazoea bila kulima kilimo cha kisasa hali ambayo wakati
mwingine husababisha umaskini ingawaje wanatumikia Kilimo kila mara

"kwa sasa wakulima wanatakiwa kujifunza kulima kilimo ambacho kinatija na
kamwe wasikubali kulima ili waweze kuonekana kama wamelima bali sheria,
taratibu na mbinu za kilimo zinaitajika kufuatwa"aliongeza Erick

Alimalizia pia kwa kuwataka wakulima hasa wa Eneo hilo la Midawi
wahakikishe kuwa wanatumia vyema jengo hilo kwa ajili ya kuhifadhi mazao na
kisha kuondokana na changamoto ya kuharibika kwa mazao.

MWISHO

SHULE YATOA UFADHILI WA MILIONI 90 KWA WANAFUNZI 90 KWA KILA MWAKA


SHULE YATOA UFADHILI WA MILIONI 90 KWA WANAFUNZI 90 KWA KILA MWAKA

SHULE ya Sekondari Edmund iliopo Sinon Mjini Arusha imetenga kiasi cha zaidi Milioni 90 kwa wanafunzi 90 kila mwaka kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaotokea katika mazingira magumu huku lengo likiwa ni kuwaepusha na mimba za utotoni lakini pia uvunjifu wa amani kwenye jamii
hataivyo fedha hizo zinatolewa na wafadhili wa nje ya nchi pamoja na mfuko wa shule hiyo ujulikanao kama Mfuko wa Edmund ambao pia huo unalenga kuhamasisha ufadhili wa ndani
Hayo yameelezwa na Mkwabi Francis ambaye ni mkuu wa shule hiyo wakati akiongea na wanafunzi, wazazi pamoja na walezi wa shule hiyo kwenye maafali ya nane ambapo jumla ya wanafunzi 240 wanatarajia kuhitimu katika shule hiyo.
Mkwabi alisema kuwa mpango huo wa kuwasidia watoto wanaotokea katika mazingira magumu umeweza kuwanufaisha watoto wanaotokea katika vijiji vya Murieth, Mkono,Nadosoito,Ungalmtd, na Sinoni ambapo walengwa ni wale wenye maitaji muhimu
alifafanua kuwa walengwa hao ni wale watoto wanaotokea katika familia ambazo hazina uwezo,na mayatima ambapo watoto hao huweza kukupewa ufadhili maalumu kwa ajili ya kusoma na kupata elimu ya Sekondari.
"wafadhili wetu wakubwa wanatokea katika Nchi za Ausralia, Newzeland,Iland, na Marekani na hawa wanatufanikikishia hawa watoto 90 kuweza kupata elimu yao bora sana ya Sekondari ingawaje na sasa sisi tumejipanga kuhakikisha kuwa na sisi hapa hapa shuleni tunatoa ufadhili kwa watoto wetu ili siku hata kama tukikosa wafadhili basi tunaweza kusaidia jamii'aliongeza Mkwabi
Pia alisema kuwa nao wazazi wanapaswa kujua na kutambua kuwa nao wana nafasi kubwa sana ya kuweza kuwasaidia watoto hasa wale ambao hawana uwezo wa kupata elimu ya sekondari kwani kupitia njia ya ufadhili wa ndani inawezekana kabisa
"kama wazazi, na walezi wakiwa na tabia ya kuchangia sekta ya maendeleo ya shule hasa mifuko ya shule  basi wataweza kusaidia jamii na hatutaweza kuwategemea zaidi wafadhili ambao wanatokea nje ya nchi kwani wakati mwingine wanapokatisha ufadhili wao wanasababisha watoto wawe kwenye hali ya uoga'aliongeza Mkwabi.
Wakati huo huo Wanafunzi wa shule hiyo ambao ni wahitimu waliwashauri walimu wa shule hiyo lakini pia wale wa shule nyingine kuachana na tabia ya kuwatenganisha wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha nne dhidi ya wale wa kidato cha tano na sita kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha wale wa vidato vya chini kutopata hamasa ya kujiunga au kufanya vema ili kuweza kujiunga na kidato cha tano na sita.
MWISHO

TAASISI ZA FEDHA ZAPEWA CHANGAMOTO

TAASISI  za kifedha zimetakiwa kangalia umuhimu  wa kwawezesha
wakulima  kuwakopesha mikopo kwa kutumia dhamana ya hatimiliki za
kimila ili waweze kulima kilimo cha biashara kwa kuwa ndio dhamana
pekee wakulima waliyo nayo.

Hayo yalisemwa jana  na mkuu  wa wilaya ya arumeru Munasa Nyerembe
alipokuwa akifungua maonyesho ya kilimobiashara ya  kuwaunganisha
wakulima na taasisi  kifedha  yanayofanyika katika viwanja vya AVRDC
tengeru mjini Arusha.

Munasa alisema kuwa asilimia kubwa ya ya wakulima wa vijijini
wanategemea dhamana ya hati miliki za kimila katika kujipatia mikopo
na hivyo taasisi zinapaswa kuhakikisha kuwa zinawawezesha wakulima hao
kwa kuwapatia mokopo ili waweze kuendeleza kilimo chao kiweze kuwa cha
manufaa zaidi.

Alieleza kuwa taasis zinazokataa kukopesha wakulima mikopo kwa kupitia
dhamana ya hati miliki za kimila zinachangia sana kuwanyima wakulima
kutofikia malengo yao ya kilimo cha biashara ambacho ndicho
kinachotegemewa kwa sasa.

Aliongeza kuwa taasisi zozote za kifedha zinazokataa kuwawezesha
wakulima kwa kupitia hati miliki za kimila zinavunja sheria na kwamba
watakaobanika kukataa dhamana hiyo watakchukuliwa hatua za kinidhamu.

“naombeni sana ninyi taasisi za kifedha wapeni wakulima mikopo kwa
kutumia dhamana ya hatimiliki za kimila na ni makosa makubwa sana
kuwanyima mikopo kwa dhamana hii maana ndio dhamana waliyo
nayo”alisistiza

Awali meneja uchumi   benki kuu ya Tanzania tawi la arusha Wilfred
Mbowe akizungumza na wakulima  katika maonyesho  hayo alisema kuwa
benki kuu itaendelea kushirikiana na wakulima kwa kuwapatia mikopo
mbali mbali kwa kuwa ndio benki mama ambayo imezaa taasisi nyinginezo
ambazo zimekuwa bega kwa began a wakulima .

Mbowe alisema benki hiyo itahakikisha kuwa inaendelea kutoa elimu kwa
wakulima na hata pia kusisitizia taasisi nyinginezo umuhimu wa
kushirikiana na wakulima ili kuhakikisha kuwa kilimo cha hapa Tanzania
kinakuwa cha manufaa makubwa zaidi.

Nae mkurugenzi wa chama cha wakulima wa mboga mboga,maua matunda na
viungo(TAHA) Jaqline Mkindi alisema kuwa maonyesho hayo yanachangia
kuwapa wakulima fursa za kuwafanya waweze kukopa katika taasisi za
kifedha kwa kuwa wakulima wengi wameshindwa kufikia malengo ya kilimo
chao kutoka na kukosa mitaji ya biashara.

Alieleza kuwa kupitia maonyesho hayo wakulima watapata elimu na mbinu
ambazo zitawafnya kilimo chao kuwa cha manufaa zaidi huku wakiwa
wanapata hata pembejeo za kilimo chao kwa kupitia taasis hizo ambazo
zitakuwa zinatoa mikopo kwa kupitia dhamana walizo nazo .
mwisho

WAFUGAJI WAASWA


JAMII za wafugaji zimeaswa kuhakikisha kuwa zinajijengea tabia ya kutafuta na kutumia fursa nyingi za mikopo kwani tafiti zinaonesha kuwa wengi wana fursa ila wanashindwa kuzitumia na hivyo kusababisha umaskini kuongezeka kwa asilimia kubwa mwaka hadi mwaka.
Aidha kama jamii hizo za wafugaji zitaweza kutumia vema fursa za mikopo ambazo zipo kwenye taasisi za fedha basi zitachangia sana ongezeko la uchumi tofautiu na sasa ambapo bado wafugaji wengi wanakwepa mikopo hiyo

Hayo yameelezwa na Afisa Ushirika Wilaya ya Longido ,Reginald Lyakurwa wakati akiongea na Wananchi Kitombeine mara baada ya shirika la World Vision kwa kushirikiana na Shirika la Vision Fund kutanga rasmi mradi wa mikopo kwenye jamii ya wafugaji hasa wa eneo hilo mapema jana

Lyakurwa alisema kuwa wafugaji wa sasa wanatakiwa kuachana na mila potofu za kukwepa mikopo na kisha kujiunga kwenye vikundi na kisha kukopa kwa ajili ya kuweza kunenepesha hata mifugo yao ambayo wakati mwingine hufa kutokana na ukosefu wa malisho

Alidai kuwa kama watajiunga kwenye vikundi na kisha kukopa wataweza kufanya kazi ya ufugaji kuwa raisi sana na hivyo wataweza kufuraia kazi zao za ufugaji tofauti na sasa ambapo wengi wanatumikia mifugo

"leo tumeweza kuleta fursa za mikopo hapa Kitombeine kuna fursa nyingi sana za mikopo ila hazitumiki sasa tunaomba wafugaji muweze kukopa na kisha hata muweze kunenepesha mifugo yenu ambayo kama itakuwa kwenye hali nzuri soko lipo karibu tu hapa Kenya ila kama mkiendelea kulea mifugo alafu ni dhaifu kwa kuwa hamna namna ya kuwasaidia ni wazi kuwa mtakuwa mnasumbuka sana na umaskini kamwe hauwezi kuisha"aliongeza Lyakurwa.


Wakati huo huo alidai kuwa kitu kikubwa ambacho kinawafanya wafugaji wengi washindwe kukopa ni kutokana na kuwa wengi bado wanafikra potofu juu ya mikopo hali ambayo wakati mwingine inachochea umaskini.

wakati huo huo Kaimu Mratibu wa mradi huo wa Mikopo katika eneo hilo Bw George Banyenza alisema kuwa mradi huo ni wa maendeleo na lengo lake halisi ni kuhakikisha kuwa wananchi wanaepukana na umaskini

Banyenza alisema kuwa waliweza kufanya tafiti kwa miaka mingi iliyopita na kisha kuweza kugundua kuwa endapo kama eneo hilo la Kitombeine litapata  miradi ya kukopa basi litaweza kuwa  balozi mzuri sana wa maendeleo kwa nchi za jirani

Alimalizia kwa kusema kuwa mradi huo utaweza kuwanufaisha wananchi zaidi ya 500 ambapo wataweza kupata fursa za mikopo na kisha kujinufaisha wao wenyewe na hata mifugo yao ambayo wanaitumia kama ajira kwenye maisha yao ya kila siku.

MWISHO

Zaidi ya wakulima 500 kupewa elimu ya rasilimali fedha.

Zaidi ya wakulima 500 kupewa elimu ya rasilimali fedha.
 ,Arusha.

ZAIDI  ya wakulima 500 kutoka katika kanda ya kaskazini wanatarajiwa kupewa elimu ya Rasilimali fedha,na kuongeza ufahamu na uelewa juu ya huduma mbalimbali za kifedha zitolewazo na Mabenki.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa chama cha wakulima wa mbogamboga,matunda na viungo(TAHA) JacKline Mkindi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maonesho ya kuunganisha kilimo biashara na taasisi za kifedha yatakayofanyika April 25 na 26 mwaka huu katika viwanja vya AVDRC Tengeru.

Alisema kuwa,kwa sasa asilimia kubwa ya taasisi za kifedha zimekuwa zikiwakandamiza wakulima kwa kuwatoza riba kubwa kwenye mikopo hali ambayo imekuwa ikiwasababishia wakulima hao kupoteza imani na mikopo kutoka katika taasisi hizo.
Alidai kuwa hali hiyo imekuwa ni changamoto kubwa sana kwa wakulima hao,kwani wakati mwingine imewawia vigumu kushindwa kufikia malengo yao waliyojiwekea kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha katika kuendesha miradi yao midogomidogo.

‘kutokana na changamoto hiyo sasa tumeamua kuandaa maonesho yatakayoweza kuwakutanisha taasisi za kifedha pamoja na wakulima ambapo hapo taasisi hizo zitaweza kutambua mahitaji ya wakulima,na jinsi ya kuweza kuwasaidia tofauti na hapo awali’alisema Jackline .

Pia alisema kuwa maonesho hayo yataenda sambasamba na uwasilishwaji wa mada mbalimbali ikiwemo uaandaji bora wa mipango biashara,umuhimu wa soko la hisa katika kuhakikisha upatikanaji wa mitaji wa muda mrefu,na matumizi bora ya mikopo katika biashara hususani za kilimo  ili walengwa waweze kujifunza zaidi juu ya mbinu bora za kufikia na kupata mitaji kwa kufanya biashara.
Kwa upande wake mratibu wa mtandao wa Agri-Hub Tanzania Bw Tom Ole Sikar alisema kuwa maonesho hayo yanalenga kuwawezesha wakulima pamoja na wamiliki wa biashara za kilimo kama vile wachuuzi,wauzaji wa pembejeo na wasindikaji kutambua fursa mbalimbali za mitaji pamoja na usalama wa kifedha zilizopo kwa biashara za kilimo.

Hata hivyo alisema kuwa wadau ambao wengi wao ni wakulima wataweza kupata fursa ya kutambua njia bora za kuboresha biashara na utoaji wa huduma kwa walengwa pamoja na kujifunza kutoka kwa wafanyabiashara wengine wa kilimo waliofanikiwa kutembelea maonesho yaliyopita.

MWISHO

VIJANA ZAIDI 1000 WA UVCCM MERU, WAFUNGA BARABARA, WAVAMIA OFISI ZA CCM MKOA WAKIDAI KUWA WAMECHOSHWA KUCHAGULIWA VIONGOZI NA MAKAO MAKUU

VIJANA ZAIDI 1000 WA UVCCM MERU, WAFUNGA BARABARA, WAVAMIA OFISI ZA CCM MKOA WAKIDAI KUWA WAMECHOSHWA KUCHAGULIWA VIONGOZI NA MAKAO MAKUU

Na Queen Lema, Arusha

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida vijana zaidi ya 1000 ambao ni wanachama wa umoja wa vijana chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Meru mkoa wa Arusha wamevamia ofisi za chama hicho kuanzia ngazi ya Wilaya hadi mkoa huku wakidai kuwa Makao makuu ya chama hicho wamewaonea kwa kutangaza uamuzi wao wa kuwachagulia viongozi tofauti na matakwa yao ambapo wao walimchagua Kamanda wao ambaye Ni John Palangyo ila CCM makao makuu walitofautiana nao.
hataivyo maandamano hayo ambayo yaliratibiwa na wajumbe wa UVCCM Meru yaliweza kusababisha shuguli mbalimbali za chama hicho kuanzia ofisi ya Wilaya hadi Mkoa kusimama kwa kuwa wajumbe hao walilazimika kuingia kwa nguvu ndani ya ofisi hizo na kisha kushinikiza kusikilizwa kwa madai yao
Akiongea kwa niaba ya wajumbe hao mmoja wa wajumbe hao Joshua Mbwana "Mwarabu"alisema kuwa kilichosababisha waweze kufanya maandamano hayo ambayo yalianzia kuanzia eneo la Usa River Mpaka Arusha ni kuelezea umma kuwa wapo baadhi ya viongozi katika chama hicho ambao wanawachagulia viongozi wa kuwaongoza bila kuwauliza
"hivi juzi tulikuwa na tulimchagua kamanda wetu ambaye ni John Palangyo na tulimpitisha lakini baada ya jina kufika mkoani ghafa jina lilibadilishwa kama haitoshi makao makuu wakasema kuwa wana mtu wao sasa je wao ndio wanatuchagulia mtu wa kutuongoza au sisi kamwe hatutakubali na badala yake tutapigana hadi mwisho hii tabia imetucosha sana"aliongeza Joshua

wakati huo huo alidai kuwa endapo kama hali hiyo itaendelea kufanyika ambapo wananchi, wajumbe, na wanachama watachagua kiongozi alafu makao makuu pamoja na uongozi wa Mkoa wakakataa basi mapambano yatakuwa makubwa sana.
Kutokana na hilo mjumbe huyo alisema kuwa pamoja na kuwa wamevamia ofisi za CCM wakiwa wanachama zaidi ya 300 bado kama hawatapewa majibu yha kuridhisha juu ya kamanda wa vijana ambaye amechaguliwa kwa kura zote na wajumbe wa baraza hilo basi ndani ya siku nne kutoka sasa huenda wakaandamana hadi makao makuu ya ofisi za CCM
"tumesharatibu maandamano hayo na yataenda vizuri itakuwa ni histori a kwa CCM kuchagulia viongozi kwa maslahi yao binafsi na matakwa ya viongozi wa ngazi za juu hasa wale ambao wana malengo ya kugombea nafasi za ubunge katika majimbo kwani ujumbe wetu ni lazima tutauweka wazi na kila mtu aweze kuosoma lakini hata kuingia ndani ya ofisi hizo bila taarifa wala kibali cha aina yoyote ile"aliongeza Joshua.
Hataivyo Katibu wa chama hicho Wilaya ya Meru, Langaeli Akyoo alisema kuwa mchakato wa kumpata kiongozi ambaye vijana hao wanamtaka ulienda vizuri na majina matatu yalifikishwa Dar es saalam makao makuu lakini baadaye hayakurudi kama ilivyoratarjiwa
Akyoo alisema kuwa majina mawili yalirudi majina mawili ambayo yana utata mkubwa ambapo utata huo ndio uliosababisha maandamano makubwa kuanzia Meru hadi Arusha
"jamani maombi yenu nimeyapata na ninapenda kuwaambia kuwa majina ambayo yalienda Dar es saalam makao makuu yalirudishwa mawili ambayo yana utata na wao walisema kuwa mchakato unatakiwa kuanza moja jambo ambalo sisi hatukubalini nalo kabisa"aliongeza Akyoo

Awali mwenyekiti wa umoja wa vijana Wilaya hiyo Bw Elirehema Mbisse alisema kuwa mchakato wa kumpata Kamanda huyo unaendelea na hivyo amewataka wawe na subira ili waweze kuangalia namna ya kutatua tatizo hilo ambalo limesababisha ofisi za CCM  kusimamisha kazi kwa muda.

Hataivyo Uongozi wa Uvccm kupitia kikao chake cha kamati ya utekelezaji kilipendekeza majina matatu ambayo ni John .D.Palangyo, Sioi Solomoni Sumari, na Daniel Mirisho Palangyo,na baadaye mutsari uliweza kupelekwa mkoani ambapo Mkoa ulijiridhisha na majina hayo na uliweza kuhoji na hatimaye waliweza kumpata John.D.Palangyo kama Kamanda wa Vijana Wilaya ya Meru,lakini baadaye barua ilikuja na kudai kuwa kamanda wa Meru siyo huyo jambo ambalo si la kweli.

MWISHO