Thursday, September 20, 2012

WANAWAKE WA KIMERU WAMTAHADHARISHA MBUNGE WAO DHIDI YA KAULI ZAKE


WANAWAKE WA KIMERU WAMTAHADHARISHA MBUNGE WAO DHIDI YA KAULI ZAKE


Na Queen Lema,ARUSHA

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida wanawake wa eneo la kisambare Usariver Wilyani Meru mkoani Arusha wamesema kuwa kamwe hawatavumilia kauli za mbunge wa jimbo hilo bw Joshua Nasari badala yake watalazimika kuingia barabarani hata kwa vita na kumpinga hadharani  Mbunge huyo  kwani kauli zake hazijengi hoja za kutetea shida za wananchi na badala yake kauli zake zinachochea Malumbano pamoja na Migogoro huku wanawake wa Vijijini wakiwa wanakabiliwa na shida mbalimbali

Wanawake hao waliyasema hayo jana wilyani humo wakati wakizungumza na Viongozi mbalimbali ambao waliwatembelea Kijijini humo sanjari na kuongea na wanachama wa chama cha mapinduzi
Wanawake hao walisema kuwa kauli za Mbunge Nassari sio kauli za kujenga bali ni kauli za kubomoa na kuchochea malumbano makubwa sana ambapo pia kwa sasa mbunge huyo angepswa kuongelea changamoto mbalimbali ambazo zimo kwenye jamiii

Walifafanua kuwa mbunge huyo anapaswa kujua na kutambua kuwa alipewa jimbo hilo kwa hasira kutokana na kukithiri kwa changamoto lukuki ambazo zimo kwenye jamii hasa za Wameru na kwa hali hiyo huu ndio muda muafaka wa mbunge huyo kuhakikisha kuwa anatatua kero na wala sio kutoa matammko ambayo hayana tija na jamii

Waliongeza kuwa kauli hizo lzimekuwa na madhara makubwa sana hasa kwa vija na kwa kuwa mpaka sasa wapo baadhi yao wanaofanya makosa kwa visingizo vya Mbunge huyo hali ambayo ni chanzo kikubwa sana cha uharibifu wa Amani

“tunachotaka kujua ni kuwa tunatatuliwa kero zetu lakini badala mbunge afikirie suala zima la maendeleo yeye anafikiria kuzima mwenge wakati sisi hatuna shida na mwenge na mwenge unapita lakini shida zetu hasa sisi wakina mama wa Nkoakirika hatujui hata majira ya saa sasa tueleweje kwani tukimbia CCM kutokan a na changamoto lakini hii ya sasa ni kali na kama huyu mbunge ataendelea hivi basi ipo siku matatizo makubwa sana yatatokea”waliongeza wakina mama hao huku wakiwa wanalia

Mbali na hayo waliongeza kuwa nao viongozi wa siasa watakiwa kkukumbuka ahadi mbalimbali ambazo wamezitoa kwa jamii hasa nyakati za kampeni kwani baadhi ya viongozi hasa wa Mkoa wa Arusha wakishapata nafasi ya kuongoza basi wanakuwa na matamko ambayo hayana tija kwa jamii na badala yake matamko hayo yanasabahbisha hata baadhi ya vijana kushikwa shikwa ovyo na Polisi

Awali Katibu wa CCM Wilaya ya Meru bw Langaeli Akyoo alikiri kuwa chama cha mapinduzi kilikuwa na kasoro hali ambayo iliwafanya wananchama wake kukopesha jimbo la Arumeru Mashariki lakini kwa sasa chama hicho kimejipanga hata kwa Watendaji wa huduma zote za kijamii kuhakikisha kuwa wanatekeleza Sera za wananchi

Bw Akyoo alifafanua kuwa hasira ambazo  ndio chanzo  pekee cha wananchi kutoa kura kwa upinzani kwa sasa zitapunguzwa kwa kiwango cha juu  huku jamii hasa za vijijini zenye maitaji maalumu nazo zikiweza kupatiwa ufumbuzi wa matatizo yao  kwani uwezekano wa kuwasaidia bado ni mkubwa sana.

No comments:

Post a Comment