Sunday, September 30, 2012

WAMILIKI, WAKUU WA SHULE WATAKIWA KUWA MFANO MZURI WA UTUNZAJI WA MAZINGIRA




WAMILIKI, WAKUU WA SHULE WATAKIWA KUWA MFANO MZURI WA UTUNZAJI WA MAZINGIRA



Na Queen Lema, ARUSHA

WAMILIKI na Wakuu wa shule mbalimbali kwa kanda ya kaskazini wameombwa kuwa mabalozi wazuri wa mazingira kwa kuhakikisha kuwa wanawapa fursa wanafunzi mbalimbali kuwa mabalozi  na waelimisha rika kuhusiana na Mazingira ili kuendelea kuhifadhi  mazingira ambayo yanaharibiwa kila mara kuanzia ngazi ya shule.

Mratibu wa shirika la Roots and Shoots la mkoa wa Arusha Bw Japhet Mwanangombe alitoa wito huo wakati wa maafali ya pili kwa waelimishaji rika 191 ambao wameitimu kwa kupata elimu ya sekondari pamoja na elimu ya uelimishaji rika mapema jana.

Alisema kuwa kwa sasa pamoja na kuwa wamejikita kuhakikisha kuwa kila shule inakuwa na vitalu kwa ajili ya kuwaelimisha wanafunzi umuhimu wa kuhifadhi mazingira lakini bado kuna baadhi ya walimu wamekuwa kikwazo kikubwa kwa kutowapa wanafunzi fursa mbalimbalin za kupambana na uharibifu wa mazingira.

Kufuatia hali hiyo alisema kuwa inachangia sana wanafunzi kukosa haki yao ya msingi hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana baadhi ya wanafunzi hao kuwa maadui wa mazingira badala ya kuwa marafiki wa mazingira kwa maslahi ya maisha yao ya baadaye na jamii ambazo zinawazunguka

“tunachoomba ni kuwa baadhi ya wamiliki wa shule pamoja na wakuuu wa shule ambao bado wanaona suala la kuwa na elimu ya mazingira si rafiki sana kwao kwa kweli wanakosea kwani wanasababisha sana hawa wanafunzi wawe na maadui wa mazingira kwa kuharibu hata vyanzo mbalimnbali lakini kutokana na hali hiyo kama shule itashirikiana na taasisi mbalimbali kama yetu  basi watachangia sana ufanisi katika suala la mazingira”alisema

Pia alisema,nazo shule ambazo zipo pembezoni mwa miji nazo hazipaswi kukaa bila ya kuwa na elimu ya mazingira hasa katika mchakato mzima wa Upandaji wa vitalu ndani ya shule zao wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatafuta elimu hiyo kwa haraka sana kwani hali hiyo ya ukosefu wa elimu ya mazingira ambayo inaanzia kuanzia ngazi ya Shule inasababisha sana  mazingira ya Vijijni kuendelea kuharibiwa.

Katika hatua nyingine alisema kuwa Shirika hilo limejipanga kuhakikisha kuwa linaendelea kuzalisha waelimisha Rika wengi zaidi hasa kwenye suala zima la Mazingira kwani mpaka sasa zaidi ya waelimisha Rika 235 wa  wilaya  22 za Kanda ya Kaskazini wameshanufaika na elimu hiyo ambapo hata hali ya uharibifu wa mazingira nayo imepungua ndani ya shule mbalimbali tofauti na hapo awali

“leo hawa Vijana wameitimu ambao pia ni wahitimu wa darasa la saba na kidato cha nne lakini pia wanaelimu hii sasa sisin tunachokifanya ni kuhakikisha kuwa tunawatuma ndani ya wilaya zetu 22 ili wakapunguze huko tatizo la uharibifu wa mazingira ambao unafanywa na baadhi ya wanajamii kutokana na uhaba wa elimu”aliongeza Bw Joseph

Kwa upande wa wahitimu wa uelimishaji rika ambao wameitimu kwa kupata elimu hiyo kwa zaidi ya miaka minne walisema kuwa pamoja na kuwa wamefanikiwa kupata elimu hiyo kwa uraisi sana lakini navyo vijiji hasa vya nje ya Miji vinatakiwa kuhakikisha kuwa wanawatumia ili kupunguza athari mbalimbali ambazo zinajitokeza mara kwa malra ndani ya jamii.

MWISHO

No comments:

Post a Comment