Tuesday, August 27, 2013

WAKULIMA WATAKIWA KUTUMIA KILIMO CHA UMWAGILIAJI KULIKO KILIMO CHA MAJIRA YA MWAKA



Na Queen Lema, Arusha


Wakulima wa Kanda ya kaskazini wameshauriwa kuhakikisha kuwa wanaanzisha utaratibu maalumu wa kutegemea zaidi kilimo cha umwagiliaji kuliko kutegemea kilimo cha majira ya mwaka kwani aina hiyo ya kilimo kwa sasa inaonekana kupitwa na wakati.

Kauli hiyo imetolewa mjini hapa na Bw Elias Mshiu ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha wakulima Tanzania(TFA)wakati akiongea na gazeti hili kuhusu hali ya kilimo kwa kanda ya kaskazini mapema jana

Aidha Bw Mshiu alisema kuwa inashangaza sana kuona kuwa asilimia kubwa ya wakulima hasa wa kanda hii ya kaskazini bado wakiwa wanategenea kilimo cha mvua za Vuli lakini pia mvua za masika hali ambayo ndiyo chanzo cha ukame

Alibainisha kuwa endapo kama wakulima watatumia zaidi aina ya kilimo cha umwagiliaji ni wazi kuwa hata mazao nayo yatawweza kuongezeka tofauti na sasa ambapo wapo baadhi ya wakulima ambao wanafanya kama kubahatisha tu

Alisema, Kilimo cha umwagiliaji kina tija kubwa sana kwa wakulima wa kanda hii hivyo basi ni vema hata kama nayo wizara ikahakikisha kuwa inatoa elimu zaidi  na fursa mbalimbali ili wakulima wazoeee kuliko kutumia kilimo cha majira ya mwaka ambacho wakati mwingine kinakataa kabisa.

Pia alisema katika Chama hicho cha TFAkwa sasa wameweza kugundua changamoto hiyo ya wakulima wengi kutegemea zaidi kilimo cha majira ya mwaka hivyo wamebuni mbinu na njia mbadala ambazo zitaweza kuifanya jamii iweze kuondokana nacho kwa malengo ya kuongeza zaidi chakula

Alitaja Mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuweza kuwakopesha lakini pia kuwawezesha wakulima vifaa mbalimbali kwa ajili ya umwagiliaji ili waweze kufikia malengo yao ambayo wamejiwekea.

“tulikaa na kisha kuona kuwa kuna umuhimu wa kuwasaidia hawa wakulima ili wawe na elimu hii ya umwagiliaji lakini waweze kukopa hata vifaa kwa ajili ya umwagiliaji katika mashamba yao na kwa kweli kama wote wataitiika hata kuja kuchukua elimu hii basi kilimo kwa kanda hii kitaimarika sana”aliongeza Bw Mshiu.

Alimalizia kwa kusema kuwa nao wakulima wanatakiwa kubadilika na wanatakiwa pia kuachana na kilimo cha mazoea ambacho mara kwa mara ndiocho kinachisababisha waonekane ni wakulima lakini faida hawana na badala yake wafuate sheria,kanuni, na taratibu mbalimbali za Kilimo.

MWISHO

MAASKOFU NA WASIMAMIZI WA MAKANISA FUATILIENI MAADILI YA WACHUNGAJI WENU ILI WASIWABISHE-ASKOFU MGONJA





IMEBAINIKA kuwa kutokana na tabia ya Maaskofu na wasimamizi mbalimbali wa makanisa kushindwa kuwafundisha wachungaji wao jinsi ya kuitumikia jamii ya kikristo ndio chanzo pekee cha baadhi ya viongozi wa dini kupata dharau ambazo haziwahusu.

Kauli hiyo imetolewa mjini Arusha na Askofu Aminiel Mgonja wa kanisa la Arusha Praise centre lilopo Sekei wakati akiongea na waumini wa kanisa hilo juu ya maadalizi ya mahafali ya wachungaji 30 wa kanisa hilo yatakayofanyika mapema wiki ijayo

Askofu Mgonja alisema kuwa wasimamizi wa makanisa lakini pia maskofu wanatakiwa kuwa na utaratibu a kuwafundisha mambao mbalimbali wachungaji wao ili nao watakapofundisha waumini wawe na umoja na wala sio mgawanyiko

Alisema, kupitia mafundisho ambayo yatakuwa yanatolewa mara kwa mara juu ya wachungaji yartaweza kuwajenga kiimani lakini pia kiroho kwani asilimia kubwa ya wachungaji wa sasa wanakabiliwa na mambo mengi sana

Alibainisha kuwa watakapojijenga kiroho na kiimani kutaweza kuruhusu hata kazi ya bwana iweze kutendeka kwa wepesi zaidi kuliko pale ambapo kazi ya kulinda na kuwahifadhi kondoo itakapofanywa na wachungaji pekee yao.

“kama wachungaji wakiharibu kazi ya bwana basi sifa chafu haibaki kwao tu bali inabaki kwenye kanisa zima lakini pia inabaki kwa maaskofu sasa kabla hatujakubali kuchafiliwa ni lazima sisi kama maaskofu tujiwekee taratibu za kuwafunidhs kila mara hata kama wanaelimu ya uchungaji”aliongeza Askofu huyo

Wakati huo huo alidai kuwa hata nao wachungaji wa sasa wanatakiwa kuangalia zaidi msingi wa maandiko kuliko msingi wa mambo ya dunia ambayo wakati mwingine wanasababisha wawe wachungaji wa shetani

Alisema ni vema kama wakawa na tabia ya kufuata zaidi maadili na kuangalia ni aina ya huduma gani ambayo wanaitoa kwa mkristo kuliko kuacha maadili na kisha kujikuta wakiwa wameshazama ndani ya dhambi hivyo kusababisha madhara ya madharau ndani na hata nje ya kanisa

Kanisa hilo linataarajia kuwafanyia maafali wachungaji wake 30 ambao wamehitimu kozi na mafunzo ya uchungaji huku somo kubwa kwao likiwa ni maadili ya uchungaji kwa jamii yote hapa duniani

Monday, August 26, 2013

POLISI YAWAKAMATA MAJAMBAZI WANNE WALIOPORA MADINI YA MILIONI 40 NA FEDHA KIASI CHA MILIONI 5

KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,PICHA NA MAKTABA




POLISI YAWAKAMATA MAJAMBAZI WANNE WALIOPORA MADINI YA MILIONI 40 NA FEDHA KIASI CHA MILIONI  5
, Arusha

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limefanikiwa kuwatia nguvuni majambazi wanne ambao walifanya tukio la wizi wa mfanyabiashara wa madini na kisha kumpora madini yenye thamani ya Milioni 40 pamoja na fedha taslimu Milioni 5.
aidha majambazi hayo yalifanya tukio hilo la kumvamia na kumjerui mfanyabiashara wa madini aliyejulikana kwa jina la Abeli Musa(35)mnamo Agust 23 majira ya saa nane na nusu mchana.
Akiongea na waandishi wa habari mapema leo Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa kukamwatwa kwa majambazi hayo kunatokana na taarifa za raia wema pamoja na kikosi kazi cha Jeshi la Polisi ambao waliingia kazini rasmi kwa ajili ya kuwasaka majambazi kuanzia siku ya tukio.
Sabas alisema kuwa Majambazi hayo ambayo yamefahamika kwa majina ya Shangai William(38)mkazi wa Sokoni one, Ally Habibu au dogoo (23)mkazi wa Tabata Dar es saalam, Eugine Donas(28)mkazi wa makao Mapya pamoja  na  Josephat Jerome(29)mkazi wa Sombetini ambapo walikamatwa Agust 24 katika maeneo ya nyumba za kulala wageni Makao Mapya
Wakati huo huo alidai kuwa mara baada ya kuwamata majambazi hao pia walifanikiwa kukamata vifaa walivyotumia katika tukio hilo na matukio mengine ya uuaji yaliyotokea Jijini arusha
Ametaja Vifaa hivyo pamoja na silaha kuwa ni pamoja na Bastola aina ya Browing Model 83 Cal 9 yenye namba 4738 huku ikiwa na risasi 10 pamoja na bastola ya LAMI ikiwa na Risasi 12.
Vifaa vingine ni pamoja na Gari aina ya Vist yenye namba za usajili T 368  AUH huku pikipiki aina ya Skygo yenye namba T352CBW pamoja na pikipiki nyingine yenye namba T 464 APH aina ya Honda nazo zikimatwa kwani majambazi hayo yalitumia vifaa hivyo kwa ajili ya uporaji maeneo mbalimbali.

MWISHO