Sunday, September 30, 2012

VYAMA VYA SIASA ARUSHA VYATAKIWA KUTOA ELIMU YA URAIA NA DEMOKRASIA KWA VIJANA ILI KUEPUSHA UHARIBIFU WA MALI

VYAMA VYA SIASA ARUSHA VYATAKIWA KUTOA ELIMU YA URAIA NA DEMOKRASIA KWA VIJANA ILI KUEPUSHA UHARIBIFU WA MALI


Na Queen Lema, ARUSHA
VYAMA vya siasa hasa kwa mkoa wa Arusha  vimeombwa kuhakikisha kuwa vinatoa elimu ya Uraia pamoja na umuhimu wa demokrasia  kwenye siasa kwani kutokana na hilo asilimia kubwa ya Vijana wanaharibu sheria hizo bila kujua na kutambua kuwa wanafanya kosa
Hayo yameelezwa na Bi Cristanta  Mwinyi ambaye ni Katibu wa CCM Kata ya Ngararenaro wakati akiongea na vyombo vya habari mara  baada ya kuvamiwa na vijana wa  Chama cha demokrasia na Maendeleo(CHADEMA)na kuharibu mali zenye thamani ya zaidi ya Laki tano
Bi Mwinyi alisema kuwa pamoja na kuwa wamevamiwa na vijana hao wenye itikadi tofauti hapo juzi bado kuna nafasi kubwa sana ya kuweza kuhakikisha kuwa vijana hao wanajua na kutambua maana halisi ya Demokrasia
Aliongeza kuwa vijana hao ambao si mara ya kwanza kufanya matukio kama hayo wanafanya hivyo kwa kujua kuwa wanashabikia baadhi ya vyama na kuharibu mali ya chama kingine wanavunja hata sheria na taratibu za nchi na pia ni chanzo hata cha mauji ambayo hayana  tija kwa jamii
Alifafanua kuwa endapo vyama vya siasa vingekuwa na tabia ya kuwaonya vijana wake kuacha kuharibu au kufanya fujo kwa vyama pinzani basi siasa ya mkoa wa Arusha ingekuwa inaenda vema tofauti na sasa ambapo siasa imegeuka kama uwanja wa mapambano makali kutokana na itikadi kali
“hawa vijana wanapotoka katika mikutano yao si mara mara ya kwanza kuharibu ofisi hii sasa kama wataendelea hivi kuharibu mali za ofisi hii ni wazi kuwa ipo siku na vijana wetu nao watainuka na hawatakubali na hayo yatakuwa ni mauji ya hali ya juu sasa ni wakati wa Vyama vya siasa kuhakikisha kuwa wanaliangalia suala hili kwa undani sana ili kuepusha madhara kama hayo”aliongeza Bi Mwinyi
Alifafanua kuwa endapo kama Siasa itaenda kistaarabu hasa pale ambapo baadhi ya vijana hao watakuwa wamepata elimu ya Uraia na Demokrasia basi itachangia kwa kiwango kikubwa sana hata kuweza  kuwapa wananchi wengine fursa ya kutumia Demokrasia vema tofauti na pale wenye itikadi moja kwenda nyingine kwani uharibifu huo nao unachangia sana hata Umaskini.
MWISHO

No comments:

Post a Comment