Monday, December 16, 2013

VIJANA WA MERU WATAKAOKIUKA MAADILI NA KUIGA TAMADUNI ZA NJE YA NCHI KUCHAPWA VIBOKO 60 HADHARANI

VIJANA WA MERU WATAKAOKIUKA MAADILI NA KUIGA TAMADUNI ZA NJE YA NCHI KUCHAPWA VIBOKO 60 HADHARANI
 
Na Queen Lema, Meru
 
UONGOZI wa Kimila ujulikanao kama Rika la Kilovio kutoka katika kabila la Kimeru
 umepitisha sheria kali ya kudhibiti maadili kwa vijana wa kike na wa kiume hasa wale ambao wanaiga tamaduni  za mataifa ya nje ya nchi ambapo kwa kijana atakayebainika kuiga au kukiuka maadili ya Kitanzania basi atalazimika kuchapwa viboko 60 hadharani
 
Hatua hiyo inakuja mara baada ya baadhi ya vijana katika eneo hilo la Meru kuanza tabia ya kuiga tamaduni lakini hata madili ya mataifa ya nje hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa maadili kuendelea kuporomoka.
 
Hayo yameelezwa na Bw Akundaely Mbisse ambaye ni kiongozi wa marika ya vijana katika kabila hilo wajulikao kama “Kilovio”wakati wakimsimika na kumuingiza rasmi kiongozi wa vijana katika eneo hilo la Mareu Bw Herieli Mafie mapema jana.
 
Mbisse alisema kuwa utaratibu huo wa kuwapa vijana adhabu ya viboko 60 utaweza kurudisha maana halisi ya kijana wa kabila hilo ambapo kwa sasa jamii ya Mkoa wa Arusha bado inaonekana kuendelea kulelemewa na tatizo la vijana wengi kuiga tamaduni za nje ya nchi huku hali hiyo nayo ikichangia sana hata ubaribifu wa amani ya Kaya,hadi mkoa.
 
Alifafanua kuwa adhabu hiyo ya viboko 60 hadharani itaenda sanjari na vijana wote wenye tabia mbalimbali ambazo hazina tija kwenye jamii hiyo ya Meru kama vile Uzinzi, ulevi wa kupindukia saa za kazi, wizi, Mavazi yanaonesha maumbile,ukosefu wa adabu pamoja na makosa mengine ambayo chanzo chake ni kuiga maadili yasiyokuwa na tija kwennye jamii.
 
“tumejipanga kuhakikisha kuwa wilaya hii ya Meru inakuwa na utofauti wa hali ya juu sana kwani tunao uwezo wa kuwaweka vijana wetu wawe katika maadili mazuri, na masuala kama vile uvaaji wa nguo za ajabu utaisha na kwa hali hiyo jamii itaweza kupungza hata ujinga unaofanywa na baadhi ya vijana wachache huku wakisingizia umaskini’aliongeza Mbisse.
 
Hataivyo Mgeni rasmi katika sherehe hizo ambaye ni Mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa Arusha John Palangyo alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa maadili ya kila kabila kurudiwa ili kuweza kuwajengea vijana uwezo wa kufanikiwa zaidi kwenye maisha yao ya kila siku.
 
Palangyo alisema kuwa suala hilo la ulindaji wa maadili lina manufaa sana sio kwa vijana kwani hata kwa taifa kwani kwa sasa wapo baadhi ya vijana ambao wanaharib na kuvunja amani ya Nchi kwa kuwa hawana maadili ambayo yanaanzia ngazi za marika hadi taifa.
 
‘hili jambo la kuweza kuwaweka vijana katika mazingira mazuri ya kimaadili linawezekana kabisa na sisi watanzania tunatakiwa kuondokana na dhana potofu kuwa eti vijana wa sasa hawana maadili wa kuwafundisha maadili ni sisi wazee wa ukoo,rika, na hata wana siasa hivyo basi kila mtu anatakiwa kuzingatia hili lakini pia kuona kuwa kijana wa mwenzake ni wa kwake na hata kama ataharibikiwa basi atachangia uharibifu bila kujali anaharibu kwa nani”aliongeza Palangyo.
 
MWISHO

`WIVU WA KIMAPENZI WASABABISHA MWALIMU KUMWAGIWA MAJI YA MOTO MITHILI YA KUKU

PICHANI NI MWALIMU NEEMA AKIWA AMELALA KWENYE CHUMBA CHA MAJERUI KWENYE HOSPITALI YA MKOA WA ARUSHA MT MERU,PICHA NA QUEEN LEMA

MWALIMU AMWAGIWA MAJI YA MOTO NA KUUNGUWA VIBAYA KWA KUHOFIWA KUWA ANAMAHUSIANO NA MUME WA MTU

Na Queen Lema, Arusha

KATIKA hali isiyokuwa ya awaida Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Neema Teti ambaye pia ni mwalimu,mkazi wa Shangarai mkoa wa Arusha amepata majeraha makubwa sana mara baada ya kumwagiwa maji ya moto sehemu zote za mwili wake mara baada ya kuhofiwa kuwa anatembea na mume wa mtu

Aidha tukio hilo lilitokea December tisa majira ya asubui katika eneo la Shangarai ambapo  Bi Neema alimwagiwa maji ya moto na rafiki yake kwa kuhofiwa kuwa anatembea na mume wake

Akiongea na “MALKIA WA MATUKIO ”mapema jana katika hospitali ya Mt Meru ambapo anapatiwa matibabu Bi Neema alisema kuwa siku hiyo ya December tisa rafiki yake ambaye bi Tatu  Msuya alienda nyumbani kwake na kumuomba kuwa waweze kwenda kwa pamoja kwani kuna matatizo na hivyo yeye ndio anatakiwa kusimamia familia yake.

Neema alidai kuwa mara baada ya kufika nyumbani kwa rafiki yake  kwa malengo ya kumsaidia shida aliyonayo ambayo alidai ni msiba lakini walipofika mambo hayakuwa hivyo

Aliongeza kuwa mara baaada ya hapo rafiki yake ambaye ni Bi Tatu alimtaka aingie ndani ili waweze kupanga mambo yao ya jinsi ya kusaidia familia kwa kipindi hicho cha msiba jambo ambalo hakuwa na wasiwasi nalo kwa kuwa walikuwa wanaaminiana sana

“baada ya hapo nilishangaa sana kwani alifunga milango yote na kuongeza makofuli jambo ambalo lilinipa shida kwa haraka kwani niliwaza labada anataka mazungumzo yawe siri”aliongeza Neema

Alidai kuwa mara baada ya tukio hilo la kufungwa milango,yote ya nyumba ya rafiki yake ndipo alipomtaka aweze kunywa soda lakini alikataa kwani ilikuwa ni asubui sana  lakini pia soda hiyo ilikuwa na chupa ndogondogo jambo ambalo halikuwa na ishara nzuri

“niloishangaa kwa kuwa aliniletea soda ambayo ilikuwa na chupa ndogondogo ndani lakini nilijiuliza kwanini huyu rafiki yangu ananilazimisha zaidi ninywe soda asubui na inaonekana inasumu machale yalinicheza lakini sikuweza kutoka kwa kuwa alikuwa tayari ameshafunga milango yote huku baadhi ya watu wa familia yake nao wakiwa wamefungiwa ndani”aliongeza zaidi Neema

Pia alidai baaada ya muda  mfupi rafiki yake alikuja na maji ya moto ambayo yamechemka sana na kuanza kumwagia bila kujali kuwa ni rafiki yake jambo ambalo pia lilifanya ashindwe kupata msaada wa haraka kwa kuwa milango yote alikuwa ameifunga

“alinimwagia maji ya moto kama kuku bila hata kunionea huruma huku akidai kuwa analipiza kwa kuwa ameambiwa mimi natembea na mume wake na nina mimba ya mume wake jambo ambalo sio kweli na alidai anachotaka ni kunitoa roho”aliongeza Neema

Alidai kuwa baada ya tukio hilo alifungua mkilango na kisha kuchukua mizigo yake haraka na kisha kukimbia kusikojulikana jambo nalo liliwafanya majirani wa eneo hilo kuweza kukusanyika na kisha kumpa msaada wa kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa lakini pia kumfikisha hospitalini

Awali Muuguzi wa zamu katika hospitali hiyo ya Mte Mt Meru  ambaye ni Bi Neema Baya alisema kuwa hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri japokuwa bado ana maumivu makali na pia ametoa wito kwa wanawake wengine kuacha tabia ya ukatili kama hiyo kwani inaweza kusababisha vifo.

Wakati huohuo Jeshi la polisi mkoa wa Arusha kupitia Kitengo cha dawati la jinsia limedai kuwa bado linamtafuta Bi Tatu kwa kosa ambalo amelifanya kwani tukio hilo ni la kinyama na nituykio ambalo halipaswi kutokea tena kwenye jamii

Akiongea kwa niaba ya Jeshi hilo Maria  alisema kuwa kwa kuwa jeshi hilo lina mkono mrefu basi litahakikisha kuwa linamtafuta Bi tatu na kisha kumfikisha mahakamani kwa kuwa amefanya kitendo kibaya sana kwa mwenzake baada ya kumuhisi kuwa anamahusiano ya kimapenzi na Mume wake

MWISHO


UKOSEFU WA HUDUMA ZA MAJI ZA UHAKIKA CHANZO CHA NDAO NYINGI KUVUNJIKA, PIA CHANZO CHA MIMBA ZA UTOTONI





IMELEZWA kuwa ukosefu wa huduma za uhakika za maji hasa maeneo ya vijijini ni chanzo mojawapo cha ongezeko la mimba  za utotoni lakini pia uvunjikaji wa ndoa nyingi huku hali hizo zikisababisha pia ongezeko la watoto mitaani ndani ya mji wa Arusha

Pia hali hiyo ya ukosefu wa maji kwenye kaya pia inasababisha umaskini wa hali ya juu sana ingawaje Serikali kwa sasa inaweka mikakati mbalimbali ya kupambana nao.

Hayo yameelezwa na Bi Asha Shabani ambaye ni Katibu wa Mradi wa maji ujulikanao kama Mangole uliopo maeneo ya Kisongo jijini hapa,wakati akielezea mradi huo lakini pia umuhimu wa miradi ya uhakika ya maji hasa kwa maeneo ambayo yapo nje ya miji

Asha alisema kuwa ukosefu wa maji ya uhakika hasa katika maeno ambayo yapo nje kidogo ya miji ni changamoto kubwa sana kwa wanawake kwa kuwa asilimia kubwa huambulia uchovu lakini pia hata kipigo kutoka kwa wenza wao kwa kuwa hutumia muda mrefu kwa ajili ya kusaka maji

Mbali na hayo alisema kuwa ukosefu huo hauathiri pekee wanawake bali hata mabinti wadogo ambao baadhi ya vijana hutumia mwanya huo katika kuwadanganya ili waweze kuwapa maji au kuwasaidia kubeba maji kwa uraisi jambo ambalo nalo ni chanzo kikubwa cha mimba za utotoni lakini pia mdondoko wa elimu kwa watoto wa kike

Akiongelea Mradi huo wa MANGOLE ambao unawasaidia wananchi kutoka katika kata za Matevesi,Ngorobobu, na Lemguru alisema kuwa umekuwa ni faida kubwa sana kwenye jamii hiyo kwani hapo awali kulikuwa na matatizio mengi sana

Alitaja matatizo hayo ni pamoja na baadhi ya wanawake kukosa ndoa,huku wengine wakiambulia wajukuukabla ya wakati kutokana na udanganyifu ambao ulikuwa uanendelea kwa watoto wa kike na vijana pia.

“hapo awali tulikuwa tunalazimika kwenda kilomita mpaka 20 kwa siku ili kutafuta maji lakini toka mradi huu uletwe kwa hisani ya Word Vision umekuwa na faida kubwa sana na hivyo tunataka tuhakikishe kuwa hata wanawake wa maeneo mengine ndani ya mkoa wa Arusha nao wanaweza kufaidika na miradi kama hii ili waweze kuepukana na changamoto za uhaba wa maji”aliongeza Asha

Wakati huohuo Mwenyekiti wa Mradi huo ambaye ni Profesa Calvin Marealle alisema kuwa pamoja na kuwa mradi huo umekuwa ni faida kubwa sana kwa jamii lakini bado unakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile Ukosefu wa umeme wa uhakika hali ambayo wakati mwingine inasababisha baadhi ya wananchi kutoka katika vijiji hivyo vitatu kukosa maji ya uhakika

Profesa Marealle aliongeza changamoto nyingine ni pamouja na baadhi ya wananchi kuiba na kuharibu miundombinu ya maji hali ambayo ni chanzo kikubwa sana cha hasara kwenye miradi hiyo.

MWISHO

WATENDAJI 17 KUTOKA KATIKA KATA 17 MERU HAWANA SIFA ZA KUWA NA CHEO HICHO

WATENDAJI 17 KUTOKA KATIKA KATA 17 MERU HAWANA SIFA ZA KUWA NA CHEO HICHO


IMEELEZWA kuwa watendaji wa kata 17 kutoka katika Wilaya ya Meru mkoa
wa Arusha hawana sifa za kuwa watendaji kutokana na kuwa na elimu
chini ya kiwango hivyo wanatakiwa kuacha kukaidi amri ya Serikali
iliyowataka waende shule kwa ajili ya kujiendeleza



Aidha Serikali ilishatoa waraka toka July mosi mwaka 2003 kuwa
watendaji wanatakiwa kwenda shule lakini mpaka sasa watendaji hao
hawajaweza kwenda shule kutokana na sababu mbalimbali



Hayo yameelezwa na Afisa utumishi wa Wilaya hiyo Anord bureta wakati
akielezea kazi mbalimbali za watendaji hao kwenye baraza la madiwani
wa Halmashauri hiyo kwa malengo ya kuelezea changamoto mbalimbali
ambazo zinawakabili watendaji hao mapema jana


Bureta alisema kuwa July Mosi 2013 Serikali iilitoa tamko ambalo
liliwataka watumishi hao kuweza kwenda mashuleni lakini mpaka sasa
tunaweza kusema kuwa agizo hilo halijaweza kutimizwa jambo ambalo ni
madhara makubwa kwa ajili ya utendaji kazi lakini pia hata kwa ajili
ya maslahi ya umma



Pia alisema kuwa ili kuweza kukabiliana na hali hiyo kwa sasa wameweka
utaratibu wa watendaji hao kuweza kwenda kusoma ili kuweza kukidhi
matakwa ya sheria hiyo ambayo inawataka kuwa na elimu lakini kuweza
kwenda sanjari na mpango wa serikali wa sasa yaani Big Result


Akiongelea suala hilo kwa niaba ya madiwani wa halmashauri hiyo Makamu
Mwenyekiti Frida Kaaya alisema kuwa  ni lazima watendaji hao waweze
kwenda shule lakini pia hata Halmashauri ihakikishe kuwa inasimamia na
kutatua changamoto zao ambazo zinajali maslahi


‘hapa ni lazima tujiulize kuwa hawa watendaji walikosa fedha au fursa
za kwenda kusoma au walikaidi agizo hilo lakini pia kuanzia sasa
maslahi ya watendaji yawekwe hadharani na pia waweze kupewa kwa
wakati ili nao pia waweze kupata moyo wa kufanya kazi”aliongeza Frida



Pia  Bi Frida alidai kuwa kama Halmashauri lakini pia Serikali
itashindwa kuwajali watendaji ni wazi kuwa lawama zitakuwa nyingi sana
kwani wao ndio wapo na wananchi kila siku ingawaje kwa sasa zipo
changamoto lukuki ambazo zinasababishwa na watendaji hao.



MWISHO

WANAWAKE 200,WATOTO 1000 WAFANIKIWA KUPEWA ELIMU PAMOJA NA UWEZESHWAJI KIUCHUMI KWA AJILI YA KUPAMBANA NA UMASKINI



Na Queen Lema, Arusha

ZAIDI  ya watoto elfu pamoja na wanawake mia mbili kutoka jijini
Arusha wamefanikiwa kuwezeshwa kiuchumi pamoja na kupatiwa elimu
mbalimbali ili kupunguza kasi ya ongezeko la watoto mijini lakini pia
kwenye vituo vya kulelea watoto yatima

Hataivyo watoto hao pamoja na wanawake hao wamefanikikiwa kupatiwa
elimu pamoja na uwezeshwaji hali mabyo mpaka sasa imeweza kuonesha
mafanikio ya hali ya juu sana.

Wanawake hao pamoja na watoto wamewezeshwa na Kijiji kinachotoa malezi
mbadala ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu(SoS)chini ya mradi
wa kuimarisha familia(FSP)unaotekelezwa sehemu mbalimballi nchini.

Hayo yamelezwa na Mratibu wa utetezi kutoka katika kijiji hicho cha
SOS ambaye ni John Batista wakati akiongea kwenye maazimisho ya
ukatili wa kijinsia kwa wanwake na watoto yaliyofanyiika katika eneo
la Kimnyaki Jijini Arusha mapema wiki hii

Batista alisema wanawake hao 200 pamoja na watoto elfu moja wameweza
kusaidiwa kutokan ana kampeni ambayo inaendeshwa chini ya SOS ya
kupinga nakutokomeza suala zima la unyanyasaji kwenye kwenye jamii.


Alisema kuwa kwa kuwawezesha wanawake hao pamoja na watoto kutasaidia
sana kupungua kwa umaskini kwenye jamii kwani umaskini unapokithiri
basi unachangia hata suala zima la malezi nalo kuwa duni sana.


Mbali na hayo Batista pia alitoa wito kwa jamii kuhakikisha kuwa
wanachana na ukatili dhidi ya wanawake lakini pia kwa watoto kwani
hali hiyo ndiyo chanzo cha ongezeko la watoto wa mitaani

SHULE ZA SEKONDARI AMBAZO ZINA MAABARA KUPEWA HUDUMA YA INTERNET BURE

SHULE ZA SEKONDARI AMBAZO ZINA MAABARA KUPEWA HUDUMA YA INTERNET BURE

Na Queen Lema, Arusha

KAMPUNI ya Smile ya mawasiliano ya Smile imeweka mikakati ya kusaidia
shule za Serikali ambazo zina maabara kwa kutoa huduma ya
mawasiliano(internet)bure itakayowawezesha wanafunzi waweze kusoma kwa
kupitia mitandao.

Hayo yameelezwa na Deo Ndejembe ambaye ni meneja kitengo cha mauzo
katika kampuni hiyo wakati akiongea kwenye uzinduzi wa mtandao wa
smile kwa mkoa wa Arusha mapema leo.

Deo alisema kuwampango huo unalenga kuimarisha huduma za maabara
katika shule za sekondari za serikali kwani wanafunzi wakiwa na huduma
hizo wataweza kusoma na kwenda pamoja na soko la dunia ambalo
linategemea zaidi huduma za mitandao.

Alidai kuwa mpango huo utaweza kuwanufaisha zaidi shule ambazo zina
maabara pamoja na kompyuta hivyo basi hata kwa shule ambazo hazina
maabara zinatakiwa kuweka mara moja ili ziweze kunufaika na mpango huo
ambao umeshaanza

“tunataka kuona kuwa lile lengo la serikali ambalo lililenga shule
ziwe na maabara linatimia lakini pia maabara ziwe za kisasa zaidi na
ziweze kupata teknolojia ya mawasiliano bure kwani itasaidia hata
ufaulu wa masomo kama sayansi kuweza kuongezeka’alisisitiza Deo

Wakati huo huo alidai kuwa mpango huo wa kutoa huduma za Tekonlojia
umeshaanza kwa shule 10 ndani ya Jiji la Dar es saalam lakini kwa mkoa
wa Arusha shule ya Arusha School tayari imeshanufaika na mpango huo
ambao ni bure

Naye Afisa mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania
(TCRA)Innocent Mongi alidai kuwa bado mkoa wa arusha unahitaji huduma
za mawasiliano zaidi kutokana na mwingiliano wa huduma kama vile
uchumi, na utalii

Mongi alidai kuwa uwepo wa mtandao huo wa Smile kwa mkoa wa arusha pia
utachangia wafanyabiashara  wakubwa na wadogo kuweza kufanya biashra
kutoka katika masoko mbalimbali duniani .

“napenda kuwasihi wakazi wa Arusha kuhakikisha kuwa wanatumia vema
mtandao huo ili kuraisisha shuguli mbalimbali za maendeleo kwa mkoa wa
arusha na kutokana na hili tunaamini kuwa Arusha itapata mabadiliko
makubwa”alisema Mongi

WAZIRI AZITAKA NCHI ZA AFRIKA ZIUNGANE ILI KUPAMBANA NA RUSHWA


WAZIRI wa nchi ofisi ya rais anayeshughulikian utawala bora George
Mkuchika amezitaka nchi za Afrika  kujenga umoja na kupeana uzoefu
katika vita vya kupambana na rushwa huku  nchi hizo z ikitakiwa
kujenga sera za uwazi kwenye sekta nzima ya rasilimali ili waweze
kunufaika nazo ikiwa ni pamoja na kupaza sauti moja kuomba kurejeshwa
kwa fedha zilizoko nje ya bara la afrika.

Mkuchika alitoa kauli hiyo jana  alipokuwa akifunga na kusherehekea
maadhimisho ya siku ya umoja wa mataifa ya mapambano dhidi ya rushwa
yaliyofanyika jini hapa

Alisema kuwa umoja una  nguvu katika kupambana na rushwa hivyo ili
kuhakikisha kuwa swala hilo linatokomezwam nchi za afrika zinapaswa
kutekelza kwa vitendo mkataba wa umoja wa afrika dhidi ya rushwa kwa
kila nchi kujiunga moja kwa moja kwa kutoa uzoefu juu ya mapambano
dhidi ya rushwa ambayo yameonekana kurudisha nyuma maendeleo ya bara
la afrka.

Alieleza kuwa pamoja na chi za Ulaya kuwa mstari wa mbele katika
mapambano dhidi ya rushwa lakini nchi hizo zimekuwa zikikumbatia
Uhamishaji wa fedha kutoka bara la afrika na kukaa kimya
kilawanapotakiwa urejeshwaji wa fedha zilizopo kwenye mataifa hayo


Aidha alifafanua kuwa nchi 30  zimesaini mkataba wa umoja wa mataifa
wa mapambano dhidi ya rushwa kati ya nchi 44 zinazotakiwa kusain
mkataba huo hivyo kuzitaka nchi zilizobaki kujiunga na umoja huo ili
kuliletea maendeleo bara la afrika na kuwa na sauti moja ya mapambano
dhidi ya rushwa huku akizitaka nchi za bara la afrika kutambua kuwa
mapambano si ya rushwa si ya mtu moja bali ya watu wote.

Nae mkurugenzi wa takukuru nchini Drt Edward Hosea alisema kuwa bara
la afrika bado lina safari ndefu katika mapambano ya vita vya rushwa
kwani kati ya nchi za afrika 34 kati ya 44 ndizo amabzo zimesaini
mkataba wa mapambano ya rushwa huku akidai kuwa mikataba mingi
inaingia kwenye rasilimali za nchi za bara la afrka haina uwazi na
sheria zinazotumika  hazimnufaishi mwananchi wa kawaida dhidi
yamapambano ya rushwa.

Aidha aliitaka serikali kuweka sera ya uwazi kwenye mikataba ya
wawekezaji wa rasilimali ya gesi ili iweze kuwanufaisha watanzania na
sheria zitakazotungwa iwe ya uwazi na yenye faida kwa watanzania
hukuakizishawishi nchi ambazo hazijatakeleza mkataba wa umoja wa
mataifazifanye hivyo mara moja kwani bara la afrka ndilo linalohitaji
maendeleo makubwa hivyo bila kuungana hawataweza kufanikiwa.

MWISHO.

KIKUNDI CHA OLGILAI CHANGAMKENI YOUTH GROUP CHAFANIKIWA KUTOA MSAADA WA MADAWATI,NA VIFAA VYA SHULE YA OLGILAI


KIKUNDI CHA OLGILAI CHANGAMKENI YOUTH GROUP CHAFANIKIWA KUTOA MSAADA WA MADAWATI,NA VIFAA VYA SHULE YA OLGILAI

Na Queen Lema, Arusha


KIKUNDI cha Olgilai Changamkeni Youth Group kilichopo maeneo ya Olgilai mkoani Arusha kwa kushirikiana na wadau wengine wa elimu wameweza kutoa msaada wa madawati zaidi ya 50 pamoja na vifaa vingine kama vile meza, kabati, na viti  kwa shule ya msingi Olgilai huku lengo likiwa ni punguza changamoto za kielimu shuleni hapo

Hataivyo msaada huo ambao ulitolewa mapema jana ulienda sanjari na uzinduzi wa kikundi hicho ambacho kimelenga kutatua changamoto mbalimbali katika kijiji hicho cha Olgilai na Mkoa wa Arusha kwa ujumla.

Akiongea mara baada ya kukabidhi msaada huo kwa shule ya msingo Olgilai Mwenyekiti wa kikundi hicho Benjamini Justin alisema kuwa wameamua kuchangia zoezi zima la elimu ili kwenda sanjari na mpango wa serikali wa matokeo ya haraka(BRN)

Benjamini alidai kuwa hapo awali shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na changamoto kubwa sana ya ukosefu wa madawati na vifaa vingine hali ambayo ilifanya wazazi wa eneo hilo ambao ni wanakikundi kuhakikisha kuwa wanatafuta mbinu ya kukabiliana na changamoto hiyo.

Alifafanua kuwa baada ya kuweka mikakati mbalimbali waliweza kuwashirikisha wadau wengine ambao nao waliweza kuungamkono na kuhakikisha kuwa wanapunguza tatizo la uhaba wa madawati kwenye shule hiyo ya Olgilai.


Wakati huo huo alidai kuwa pamoja na kuwa wameweza kufanikisha kutoa msaada huo wa madawati, meza,viti, madaftari, na kalamu lakini bado wanakabiliwa na changamoto lukuki ambazo wakati mwingine zinakwamisha jitiada zao

Alitaja changamoto hiyo kuwa ni pamoja na baadhi ya fursa za mikopo ni finyu kwa kuwa taasisi hizo hazitoi mikopo kwa vikundi jambo ambalo linakwamisha jitiada za maendeleo ya vikundi hasa vile vya mitaa.

“pamoja na kuwa leo tumeweza kutoa msaada huu kwa shule hii pamoja na kuzindua rasmi kikundi chetu bado changamoto hii tunaifikiria sana hivyo basi tunaomba taasisi za Fedha kuhakikisha kuwa zinatuangalia ili nasi tuweze kusaidia jamii kama tulivyofanya leo”aliongeza Benjamini

Wakati huo huo akiongea kwa niaba ya wanafunzi ambao ndio walengwa wa msaada huo Irene Peter alidai kuwa msaada huo wa madawati utasaidia sana kuongeza ufanisi wa elimu kwani hapo awali wanafunzi shuleni hapo walikuwa wanalazimika kuandika Miandiko mibaya kwa kuwa hawakuwa na madawati.

WAZEE ARUSHA WAPATIWA MSAADA


Asasi ya Informal Sector team(INSERT)imefanikiwa kutoa msaada wa Mablanketi yenye thamani ya zaidi ya milioni moja na nusu kwa Jukwaa la wazee wa mkoa wa Arusha (JUWA)huku lengo halisi likiwa ni kuhakikisha kuwa wazee wote wanaendelea kusihi maisha ya upendo na amani

Akiongea na wazee hao mara baada ya kuwapa msaada mratibu wa asasi hiyo ya INSERT,Japhet Saruni alisema kuwa msaada huo unalenga kuhakikisha kuwa afya za wazee zinaendelea kuboreka zaidi

Aidha Saruni alisema kuwa kwa sasa wazee wengi sana wamekuwa wakisahulika kwenye maslahi yao hali ambayo inachangia sana kuzorotesha hata afya zao ingawaje sera za wazee bado zipo

Alifafanua kwa kusema kuwa hali hiyo imechangia kwa kiwango kikubwa sana wazee wengi kupoteza maisha kabla ya siku zao hivyo basi ndio maana Asasi hiyo ya INSERT ikaweza kuona kuwa kuna umuhimu wa kuwasaidia wazee

Pia alisema kuwa kuna umuhimu wa jamii kuhakikisha kuwa wanatatua kero za jamii kila mara kwani kwa sasa jamii imeacha kabisa kuwasaidia wazee huku wazee nao wakikabiliwa na changamoto kubwa sana

Hataivyo alifafanua kuwa kama jamii itaweza kuwakumbuka wazee kila mara basi kasi ya ongezeko la vifo visivyo vya lazima hasa vya wazee vitaweza kupungua kwa kiwango kwani takwimu zinaonesha kuwa wazee wengi wanakufa kutokana na kuwa hawana msaada wa kuwasaidia.


Awali wazee waliopewa msaada walisema kuwa pamoja na kuwa wamepewa msaada huo bado kuna umuhimu wa sera za wazee kuweza kutekelezwa hasa kwenye sekta muhimu kwani sera hizo zipo lakini hazitekelezwi na baadhi ya watendaji tena wwa Serikali.

MWISHO

WASANII ARUSHA WAHIDIWA NEEMA


KAMPUNI ya Mkundi Production yenye makao makuu Jijini Arusha imeahidi kuibua lakini pia kuwezza kuendeleza vipaji vya  mbalimbali vya vijana ikiwa ni pamoja na kuweza kuwasaida kurekodi na kusambaza kazi zao

Aidha kwa sasa asilimia kubwa ya vijana wenye vipaji vya uimbaji wanashindwa kufikia malengo yao mbalimbali kwa kuwa hawana uwezo wa kuingia studio lakini pia kutoa na kughramikia baadhi ya gharama hali ambayo inachangia sana kupoteza vipaji vingi

Hayo yameelzezwa na mkurugenzi jmtendaji wa kampuni hiyo Carlos Mkundi mapema jana mara baada ya kuzindua Album ijulikanayo kama “NIMETOKA  MBALI”ambayo imejumuisha vijna mbalimbali wa mkoa wa Arusha

Mkundi alisema kuwa kampuni yakeimejidhatiti kuhakikisha kuwa kila msanii mwenye uwezo wa kuimba aweze kunufaika na kipaji chake na kamwe kisingizo kuwa ghrama ni chanzo kisiwepo

Aidha alidai kwa sasa wasanii wa nyimbo mbalimbali ndani ya mkoa wa Arusha wanashindwa kuimba na kutoa album zao kwa kuwa kuna changamoto lukuki sana ambazo ndizo chanzo kikubwa cha wao kushindwa kufanya vema zaidi

Wakati huo huo alisema kuwa kwa kipindi cha mwaka huu Kampuni yake tayari imeshwaweza kuwasaidia wasanii saba kuweza kurekodi album zao na hivyo mikakati zaidi bado itaendelea kuwekwa

Pia alidai kwa kila mwaka wasanii saba kutoka Jijini Arusha wataweza kurekodi kwa msaada wa kampuni hiyo lakini hata wale ambao bado hawajaweza kurekodi basi watapewa misaada mbalimbali ambayo inalenga kuinua vipaji vyao zaidi

MWISHO

Wednesday, December 4, 2013

HALMASHARI YAURARUSHA VIJIJINI WAFANIKIWA KUKUSANYA MILIONI 682 KUTOKA KATIKA VYANZO VYAKE VYA MAPATO


Wilaya ya Arusha Vijijini imefanikiwa kukusanya kiasi cha Milioni 682
sawa na asilimia 31.8 kutoka katika vyanzo vyake vya mapato ingawaje
kwa kipindi cha mwaka 2013,2014 wanatarajai kukusanya kiasi cha zaidi
ya bilioni mbili sanjari na kuibua vyanzo vya mapato ambavyo
vitaimarisha zaidi uchumi wa wananchi wake.

Hayo yamelezwa mapema jana na Kaimu mweka wa Halmashauri hiyo bw
Munguabela Kakulima wakati akielezea Vyanzo vya mapato ambavyo
vitakwenda sanjari na mpango wa matokeo makubwa (Big Result Now)kwenye
wilaya hiyo

Kakulima alidai kuwa kupatikana kwa fedha hizo kunatokana na jitoada
mbalimbali ambazo zinafanywa na idara yake ambapo ndipo zilipochangia
mafanikio hayo

Aidha alidai mpaka mwaka wa fedha wa sasa uweze kuisha wanatarajia
kuvuka hata lengo ambalo walikuwa wameliweka na hivyo kukusanya fedha
nyingi zaidi hali ambayo itachangia shuguli mbalimbali za maendeleo
kuweza kufanyika kwa haraka

Mbali na hayo alidai kuwa kwa sasa wanamikakati mbalimbali ya
kuhakikisha kuwa wanaweka uwezekano wa kubaini vyanzo vipya vya mapato
ambavyo navyo vitaweza kuweka halmashauri hiyo kwenye kiwango cha juu
sana

Mkakati mwingine ambao nao aliweza kuutaja ni pamoja na kuweza kuwapa
wananchi elimu ya kuweza kulinda vyanzo vya mapato lakini kuweza
kuonesha umoja baina ya watendaji wa halmashauri hiyo ili kuweza
kuharakisha shuguli mbalimbali za ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri

Awali alisema kuwa pamoja na mikakati na jitiada ambazo zinafanywa na
idara ya fedha katika Halmashauri hiyo zipo changamoto ambazo nazo
zinachangia kukwamisha malengo mbalimbali ya ukusanyaji wa mapato
kutoka katika vyanzo

Kakulima alidai kuwa changamoto hizo ni pamoja na baadhi ya wanasiasa
kuingilia shuguli pamoja na vyanzo vya mapato hali ambayo wakati
mwingine inasababisha waone kuwa halmashauri hiyo inachangia sana
kuwadidimiza.

Naye mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alisema kuwa ili matokeo ya
haraka yaweze kuja katika Halmashauri hiyo vyanzo vya mapato
vinatakiwa kulindwa lakini nao watendaji wa idara ya fedha wanatakiwa
kufuata wajibu wao wa kulinda na kuitetea halmashauri hiyo.

MWISHO

ACHENI UKIRITIMBA USIOKUWA WA LAZIMA

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, amewataka watumishi wa
serikali na taasisi zake kuondoa ukiritimba usio wa lazima katika
kutoa huduma kwa wadau wa maendeleo, hususani, wanaowafundisha
wakulima wadogo wadogo  kilimo cha kibiashara ili waweze kujipatia
maendeleo.




Alitoa maagizo hayo wakati akifungua maonesho ya vikundi vya wakulima
zaidi ya 21 kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, yaliyoandaliwa na
Shirika lisilo la kiserikali la Farm Concern International (FCI)
wakishirikiana na World Vision Tanzania, World Vision Canada na
Shirika la Maendeleo la Canada (CIDA), jijini hapa jana.




Mkurugenzi wa FCI Afrika, David Richiu, alisema shirika lake ambalo ni
wakala wa masoko kwa wakulima wadogo wadogo, limejikita kuwafundisha
kilimo cha kibiashara, uongozi katika vikundi kupitia mfumo kijiji
biashara, wanawapa mbinu za kutafuta masoko ya mazao, utunzaji wa
mazingira, elimu ya lishe bora kwa familia, uhifadhi wa mazao,
huwaunganisha na watu wa pembejeo na huduma za ugani.



Alisema maonesho hayo ya kilimo yenye kauli mbiu, “Jua mahitaji ya
soko zalisha kibiashara,” yamedhaminiwa na mradi wa SMART (Sustainable
Market led Agriculture Resource) na wanafanya kazi katika wilaya za
Arusha, Monduli, Siha, Arumeru na Hai.



Baadhi ya miradi ambayo shirika lake linatekeleza nchini ni pamoja na
kukuza uzalishaji na ulaji wa mboga mboga za kiasili unaotekelezwa
katika wilaya za Arusha, Arumeru, Hai, Siha, Same na Karatu, lishe kwa
wakulima wa kahawa unaotekelezwa wilaya za Arusha, Arumeru, Siha na
Hai.



Mingine ni mradi wa muhogo ulioanzia kijiji cha Mbuguni wilayani
Arumeru, mradi wa ndizi na viazi vitamu hasa viazi lishe vyenye
asilimia nyingi ya vitamin A ambao wanatarajia kuupanua kwenye mikoa
mingine nchini.



Kwa upande wake, Kiongozi mkazi wa FCI nchini, Wiston Mwombeki,
alisema ili mkulima aweze kupata soko yampasa kwanza ajue mahitaji ya
soko kama vile mazao yanayohitajika sokoni, ubora, mahali walipo
wanunuzi, kiwango kinachotakiwa, ufungashaji, uhifadhi na usafirishaji
wa mazao, kilimo bora na pembejeo bora.


MWISHO.

OFISI ZA CHADEMA ARUSHA ZACHOMWA MOTO NA WATU WASIOFAHAMIKA

Na Queen Lema, Arusha



KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida watu wasiofahamika jana(leo)wamevamia ofisi ya Chadema Kanda ya kaskazini iliopo Jijini Arusha na kisha kuanza kuwasha moto ambao ulisababisha hasara kubwa sana.

Akizungumza na “Majira”katibu wa kanda ambaye pia ni katibu wa mkoa wa Arusha Chadema, Amani golugwa alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya asubuhi katika ofisi za kanda zilizopo eneo la Ngarenaro mjini Arusha.

Golugwa alisema kuwa watu hao waliingia mara baada ya mlinzi kutoka zamu ya kulinda usiku ambapo walilazimika kuvunja kioo kikubwa na kisha kuingia ndani ili kufanya lile walilolikusudia.

Aliendelea kwa kusema kuwa baada ya kuingia ndani walipanda kwenye dari la nyumba hiyo ambapo walianza kutafuta uwiano wa chumba ambacho kinahifadhi nyaraka mbalimbali za Chama na kisha kuwasha moto

Alidai kuwa wakati wanawasha moto huo ghafla uliweza kulipuka hivyo lengo halisi halikuweza kutimia kwa haraka na badala yake walishuka na kuanza kukimbia wakati jingo letu likiwa linateketea kwa moto
Pia alisema baada ya watu hao kuona kuwa hawawezi kuchoma chumba hicho walitengeza shoti kubwa ya umeme ambayo iliweza kusababisha vyumba vya choo na bafu kuunguwa na hatimaye walishuka wakiwa wanakimbia huku moto ukiendelea kutapakaa kwenye jingo la ofisi hiyo.

“kilichofanya tuweza kusema kuwa walikuwa na lengo la kuchoma chumba hiki ambacho kinahifadhi nyaraka muhimu za chama ni baada ya kuona kuwa wameacha maeneo yote na kisha kuingia hapa na inavyoonekana lengo lao ni kupoteza ushahidi wa vitu mbalimbali ambavyo tunapambana navyo”aliongeza Golugwa

Katika hatua nyingine Golugwa alisema kuwa tukio hilo la kuchoma ofisi linaonesha kuwa wapo baadhi ya watu ambao wanatumia muda na fikra zao nyingi kuwawinda viongozi wa Chadema na kuingilia hata kwenye maisha yao ya kila siku

Aidha aliwataja watu ambao wanawindwa sana kwa ajili ya kujeruliwa ni pamoja nay eye ,mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Goodbless Lema, pamoja na mwenyekiti wa wilaya ambaye ni Ephata Nanyaro
‘mpaka sasa tunawahisi watu watatu katika sakata hili na kwa maana hiyo tumesharipoti polisi ili waanze mara moja upelelezi wao lakini jingo letu tumeliwekea ulinzi mkubwa sana na kumbukumbu zote zipo ingawaje mpaka sasa bado hatujaweza kujua kwanza ni hasara ya shilingi ngapi tumeipata’aliongeza Golugwa

POLISI ARUSHA WASHIKILIA SILAHA ILIYOKUWA IKITUMIKA KWENYE MATUKIO YA UHALIFU



JESHI la Polisi mkoani Arusha,linashikilia silaha aina ya short gun
WINCHESTER  yenye namba za usajili c.056900 pamoja na mmiliki wake
ambaye alikuwa anaitumia kwenye matukio mbalimbali ya uhalifu kwa mkoa
wa Arusha na nje ya mkoa wa Arusha

Pia Polisi mkoa wa Arusha ilifanikiwa kumkamata mmiliki wa silaha hiyo
ambaye ni Jumanne Abadlaha(25) maarufu kama babu G

Akiongea na vyombo vya habari mapema leo kamanda wa polisi mkoa wa
Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa silaha hiyo pamoja na jambazi
huyo walifanikiwa kumkamata September 27 majira ya asubuhi.

Sabas alisema kuwa Polisi waliokuwa katika doria waliweza kumkamata
jambazi huyo na silaha yake  katika eneo la Ungalmtd ambapo ndipo
makazi ya jambazi huyo mara baada ya kupewa taarifa na raia wema kuwa
anamiliki silaha kinyume cha sheria lakini pia anatumia kwenye matukio
mbalimbali ya uhalifu.

Aidha alidai kuwa mara baada ya kumkamata jambazi huyo na silaha yake
waliweza kugundua kuwa silaha hiyo tayari ilikuwa imeshakatwa kitako
lakini ndani ilikuwa na risasi 13

Sabasi aliendelea kwa kusema kuwa mara baada ya kumkamata jambazi huyo
pamoja na silaha yake waliweza kumuhoji na alikiri kuwa amehusika na
matukio mbalimbaliya uhalifu kama vile unyanganyi wa kutumia nguvu na
silaha, lakini pia anamiliki silaha hiyo kiyume cha sheria.

Pia alidai kuwa mbali na kuweza kugundua kuwa anamiliki silaha hiyo
kinyume cha sheria lakini pia silaha hiyo imekuwa ikitumika kwenye
matukio mbalimbali  ya uhalifu ambayo yameweza kutokea katika mkoa wa
Arusha na nje ya mkoa wa Arusha.

Hataivyo kamanda huyo amedai kuwa upelelezi zaidi bado unaendelea na
mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.

Wakati huohuo kamanda huyo aliwataka wakazi wa mkoa wa Arusha
kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa za siri hasa za wale wananchi wasio
waaminifu wanaojihusisha na matukio ya uhalifu kwani matukio hayo ya
ualifu yamechangia sana kushuka kwa amani ya nchi ya mkoa wa Arusha.
Mwisho.

SHULE ZA SEKONDARI AMBAZO ZINA MAABARA KUPEWA HUDUMA YA INTERNET BURE



Na Queen Lema, Arusha

KAMPUNI ya Smile ya mawasiliano ya Smile imeweka mikakati ya kusaidia
shule za Serikali ambazo zina maabara kwa kutoa huduma ya
mawasiliano(internet)bure itakayowawezesha wanafunzi waweze kusoma kwa
kupitia mitandao.

Hayo yameelezwa na Deo Ndejembe ambaye ni meneja kitengo cha mauzo
katika kampuni hiyo wakati akiongea kwenye uzinduzi wa mtandao wa
smile kwa mkoa wa Arusha mapema leo.

Deo alisema kuwampango huo unalenga kuimarisha huduma za maabara
katika shule za sekondari za serikali kwani wanafunzi wakiwa na huduma
hizo wataweza kusoma na kwenda pamoja na soko la dunia ambalo
linategemea zaidi huduma za mitandao.

Alidai kuwa mpango huo utaweza kuwanufaisha zaidi shule ambazo zina
maabara pamoja na kompyuta hivyo basi hata kwa shule ambazo hazina
maabara zinatakiwa kuweka mara moja ili ziweze kunufaika na mpango huo
ambao umeshaanza

“tunataka kuona kuwa lile lengo la serikali ambalo lililenga shule
ziwe na maabara linatimia lakini pia maabara ziwe za kisasa zaidi na
ziweze kupata teknolojia ya mawasiliano bure kwani itasaidia hata
ufaulu wa masomo kama sayansi kuweza kuongezeka’alisisitiza Deo

Wakati huo huo alidai kuwa mpango huo wa kutoa huduma za Tekonlojia
umeshaanza kwa shule 10 ndani ya Jiji la Dar es saalam lakini kwa mkoa
wa Arusha shule ya Arusha School tayari imeshanufaika na mpango huo
ambao ni bure

Naye Afisa mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania
(TCRA)Innocent Mongi alidai kuwa bado mkoa wa arusha unahitaji huduma
za mawasiliano zaidi kutokana na mwingiliano wa huduma kama vile
uchumi, na utalii

Mongi alidai kuwa uwepo wa mtandao huo wa Smile kwa mkoa wa arusha pia
utachangia wafanyabiashara  wakubwa na wadogo kuweza kufanya biashra
kutoka katika masoko mbalimbali duniani .

“napenda kuwasihi wakazi wa Arusha kuhakikisha kuwa wanatumia vema
mtandao huo ili kuraisisha shuguli mbalimbali za maendeleo kwa mkoa wa
arusha na kutokana na hili tunaamini kuwa Arusha itapata mabadiliko
makubwa”alisema Mongi

KANISA LATANGAZA NEEMA KWA WAHUDMU,WAHADIWA KUPEWA MASAMBA YA KILIMO KWA AJILI YA MSIMU MPYA WA KILIMO UJAO

NA BETY ALEX, ARUSHA


HUDUMA ya Maisha ya Yesu iliopo maeneo ya Kisongo jijini Arusha imesema kuwa kwa kutambua mchango wa wahudumu lakini pia wazee wa kanisa hilo wanatarajia kuwagawia mashamba ya kulima ili waweze kujiendeleza kwenye maisha yao ya kila siku na kuachana na tabia ya kuwa tegemezi

Aidha mpango huo unakuja mara baada ya kanisa hilo kuanza kutoa na kusisitiza masomo ya upendo ambayo yanalenga kumuinua zaidi Mungu kuliko mwanadamu

Akitangaza msimamo huo wa kuwasaidia wahudumu hao mchungaji kiongozi wa huduma hiyo Eliakimu molel”Channel”alisema kuwa mpango huo utasaidia sana kuongeza ufanisi wa kazi za kila siku lakini hata za kanisa

Alisema kuwa kwa kufanya hivyo wahudumu hao hasa wale ambao hawana kazi wataweza kuepukana na dhambi mbalimbali ambazo zinasababishwa na ukosefu wa kazi za kufanya

“ukiwa kama muhudumu hapa kanisani kwangu nilazima nihakikishe kuwa mnatoka siwezi kutoboa mimi mwenyewe halafu ninyi mkabaki mkiwa hamna lolote nasema nitagawa mashamba ya kulima na kila atakayweze akulima katika mashamba hayo ni lazima atoke”aliongeza Channel

Pia alisema kwa kanisa lolote lile ili liweze kusimama vema wahudumu lakini pia hatawazee wa kanisa wanapaswa kuwa makini kuanzia kiroho hadi kimwili hivyo ni wajibu wa viongozi wa makanisa kuhakikisha kuwa wanawaangalia makundi hayo

Alidai kuwa kama wakiwa dhaifu kwenye nyanja yoyote ile ni lazima kuwepo na kasoro kwenye huduma hiyo na badala yake badala ya kusonga mbele kwenye wokovu basi hata waumini watakuwa wanarudi nyuma kwenye wokovu

“wahudmu, wazee wa kansiani watu muhimu sana kwenye maendeleo ya kanisa la leo tusiwaache wakawa legelege bali tuwainue juu hata hali zao za maisha ziweze kubadilika ni faraja sana kama mhudumu wa kanisa akapanda daraja kwenye kiwango cha juu alafu pia akawa na imani basi hata mimi mchungaji nitafanya kazi yangu bila shaka ila kama akiwa legelege pepo likija linaanza nay eye kwanza”aliongeza Channel

Wakati huo huo alisema kuwa pia kanisa hilo limejiwekea hata utaratibu wa kuweza kuwasaidia wale wasiojweza kwa kuwa msaada wa vyakula ili wasiwe wakrisro wenye imani lakini pia wawe na uwezo kuamini kuwa hata kama hawana kitu bado mchungaji wao anawapenda na anaweza kufunga na kuomba juu yao ili hali za maisha ziweze kubadilika.

MWISHO