Friday, September 28, 2012

RAISI KIKWETE ASISITIZA SERIKALI KUBORESHA VITUO VYA TAFITI ZA KILIMO ILI VITAFITI MAZAO MBALIMBALI YA KILIMO


RAISI KIKWETE ASISITIZA SERIKALI KUBORESHA VITUO VYA TAFITI ZA KILIMO ILI VITAFITI MAZAO MBALIMBALI YA KILIMO

Na Queen Lema,ARUSHA

RAISI Jakaya Kikwete amezitaka Nchi za bara la Afrika kuhakikisha kuwa zinaboresha vituo mbalimbali vya utafiti wa kilimo kwani kama kila kituo kitafanya vema tafiti zake basi zitachangia kwa kiwango kikubwa sana kuweza kuimarisha Kilimo na kukifanya kiwe cha kisasa zaidi ndani ya nchi mbalimbali ambazo bado mpaka sasa zinakabiliwa na changamoto kubwa ya kilimo duni

Raisi Kikwete aliyasema hayo jana(LEO)wakati akifungua mkutano wa wadau wa mapinduzi ya kijani ya  kilimo kwa nchi mbalimbali za Afrika(AGRA) ambapo alisema kuwa bado sekta ya kilimo katika nchi mbalimbali inakabiliwa na changamoto kubwa sana hali ambayo inatakiwa kutatuliwa kwa haraka sana kupitia vituo mbalimbali vya utafiti wa Kilimo

Alifafanua kuwa kwa sasa kunaitajika sana mapinduzi hasa kwenye taasisi za utafiti kwani hizo ndizo zitakazochochea sana mabadiiliko ya kilimo kutokana na uitaji mkubwa sana ambao upo ndani ya nchi mbalimbali kwa bara la Afrika

Pia alisema kuwa kama vituo hivyo vya tafiti vitapewa kipaumbele basi pia vitachangia kwa kiwango kikubwa sana kuweza kupunguza changamoto mbalimbali ambazo zinakabili sekta hiyo ya kilimo pamoja na wakulima ambao wanaitaji msaada mkubwa sana hasa wa wataalamu wa kilimo ambao wanatokea katika vituo hivyo vya utafiti.


"kwa sasa tuhakikishe kuwa tunajipanga ilivyo kwa kutoa kipaumbele kwa vituo hivi vya utafiti na hivi vituo navyo vinatakiwa kuhakikisha kuwa vinajiwekeza zaidi kwa kuwa bunifu na kutafiti hata mazao zaidi ya mawili kwa mwaka na kama Serikali zetu zitasimamia hivyo basi ni wazi kuwa zitchangia sana hata ongezeko la chakula na vipato vya wakulima hao kwa wingi sana"aliongeza  Dkt Kikwete

Katika hatua nyingine pia alisema kuwa  ili kukuza na kuimarisha sekta ya Kilimo hapa nchini na barani Afrika kwa ujumla wadau mbalimbali wa Kilimo wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanatoa mafunzo na elimu zaidi kwa wakulima hasa wale wa vijijini kwani kutokana na uhaba wa elimu asilimia kubwa ya wakulima wanafanya kilimo cha mila na desturi huku hali hizo zikiwa zinachangia kwa kiwango kikubwa sana kudidimiza mazao na kusababisha hata ukosefu wa chakula.

"kama tutawapa hawa wakulima wetu vipaumbele kwa kusisitiza zaidi elimu, na maitaji mengine kwa ajili ya kuboresha kilimo basi wataweza kupiga hatua kubwa sana kutokana na baadhi yao hawana elimu huku jambo hilo likiwa linachangia sana kilimo duni pamoja na umaskini miongoni mwa jamii za wakulima"aliongeza Dkt Kikwete

Naye aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa bw Koffi Annan alisema kuwa ni vema kama  wadau wa sekta binafsi na sekta za umma wakahakikisha kuwa wanawekeza zaidi katika Kilimo ambapo kama watafanikiwa kufanya hivyo basi watachangia kwa kiwango kikubwa sana kuimarisha zaidi kilimo sehemu mbalimbali duniani na hali hiyo itachangia hata uchumi wa Nchi zao
 `
Bw Annan alizitaka Serikali za Nchi za Afrika nazo kuhakikisha kuwa nazo zinakuwa miongoni mwa wawekezaji wakubwa katika kilimo sanjari na kuwa bunifu katika kuwasaidia wakulima wadogo na wakubwa  hasa kwenye maitaji yao muhimu ambayo mara nyingine wanayokosa huku hali hiyo ikifanya kilimo kiweze kudorora na kushindwa kufikia malengo yake mbalimbali.

MWISHO

No comments:

Post a Comment