Sunday, September 16, 2012

VIONGOZI WA CCM WATAKIWA KUTATUA KERO ZA WANANCHI


NA MERY KITOSIO, MERU

VIONGOZI mbali mbali wa chama cha mapinduzi kuanzia ngazi ya  kata ,vijiji na vitongoji   wametakiwa kushughulika na kero za wananchi na kuhakikisha kuwa wanazitatua kwa muda muafaka ili wananchi wao waone umuhimu wa chama na serikali .

Hayo yalisemwa  na katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya arumeru bw Langaeli akyoo alipokuwa akihutubia  wananchi  katika mkutano wa hadhara wa chama cha mapinduzi uliofanyika kijiji cha ngyeku kata ya kikatiti wilayani a rumeru.

Alisema kuwa kwa sasa ufike muda viongozi wasionekane kuwa wamepewa uongozi kwa ajili ya kustarehe na badala yake wajikite zaidi katika kusikiliza matatizo ya wananchi wao kwa kuwa uongozi wao ndio kimbilio la wananchi  kwa kuhakikishwa wanawasikiliza yale wanyohitaji.

Alieleza kuwa ili wananchi waweze kukiamini chama  cha mapinduzi ni vema viongozi hao wakadili na matatizo mbali mbali yaliyoko ndani ya jamii husika hususan kuwatatulia kero ya  maji kwa kuwa viongozi hao wao ndio suluhisho la wananchi .

Alifafanua kuwa kwa sasa hakuna tena haja ya kutafuta wa chawi wanaosababisha ccm kuchukiwa  bali viongozi watambue kuwa wenyewe ndio wasababishaji  kwa kuwa hawafuatilii ipasavyo kutatua kero zinazowakabili wananchi wao

“Ninawaagiza madiwani , wenyeviti wa vijiji na vitongoji kuhakikisha mnafuatilia  kero hizo ,tusitafute wachawi wanaosababisha CCM, kuchukiwa wakati wachawi ni nyie wenyewe”alisema Akyoo.
Mbali na hayo akyoo akielezea mafanikio ya serikali ya ccm katika kijiji hicho cha ngyeku alisema kuwa ni pamoja na kufanikiwa kujenga shule ya sekondari ngeku,zahanati pamoja na barabara iliyotengenezwa kwa mradi wa tasaf.

Aidha katika mkutano huo wananchi wa eneo hilo walitoa kilio chao cha maji wanachokabiliwa nacho  kwa katibu huyo ambapo alitumia fursa hiyo kumuagiza mara moja diwani wa kata hiyo kuhakikisha kuwa anatatua tatizo hilo kwa haraka iwezekanvyo.

Hata hivyo katika mkutano huo jumla ya wanachama  24 walijiunga na chama hicho ambapo watatu walitoka chama cha demokrasia na maendeleo huku wengine 21 wakiwa wananchama wapya.

No comments:

Post a Comment