Tuesday, September 11, 2012

TAZANIA KUPUNGUZA KEMIKALI ZA TABAKA LA ORIZONI KUTOKA TANI 254 HADI TANI 36.2 KWA MWAKA

TAZANIA KUPUNGUZA KEMIKALI ZA TABAKA LA ORIZONI KUTOKA TANI 254 HADI TANI 36.2 KWA MWAKA





Na Queen Lema na Pamele Mollel, Arusha

TANZANIA imefanikiwa kupunguza matumizi ya kemikali zinazomong'onyoa tabaka la hewa la orizon angani kutoka tani 254 kwa mwaka hadi kufikia tani 36.2 sawa na asilimia 86 huku ikiwa ni nchi ya kwanza kwa bara la Afrika kuweza kufikia malengo yake kwa kiwango kikubwa ingawaje bado kuna changamoto kubwa hasa kwenye majokofu na viyoyozi.

Hayo yalielezwa na waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira dr Terezya Huvisa wakati alipokuwa akiongea katika mkutano wa baraza la mawaziri wa mazingira kwa nchi za Afrika mapema jana jijini hapa.

Dr Terezya alisema kuwa tanzania imefanikiwa kufikia hatua hiyo ktokana na juhudi mbali mbali ambazo zinafanyawa na wizara yake kwa kushirikiana na taasisi nyingiena hali ambayo imetoa sifa kubwa sana kwa nchi za bara la afrika na kusababisha kuwa miongoni mwa nchi ambazo zimepunguza madhara ya tabaka la ozoni.

"kama tunavyojua ozoni ni hewa iliyoko kwenye anga hewa juu takribani kilomita 10-50 juu ya ardhi na kwa hali hiyo tabaka la ozoni linapoharibuiwa uchangia kuruhusu mionzi zaidi kufika kwenye uso wa dunia na ndio maana kuna ongezeko kwa magonjwa mbali mbali kama vile saratani ya ngozi ,uharibifu wa macho,kwa hali hiyo sisis tumepiga hatua kubwa sana kuliko nchi nyingene barani afrika "alisema dr Terezya.

Pia aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo ya nchi ya tanzania kuwa miongoni mwa nchi zilizopiga hatua kwa zaidi ya asilimia 86 ya kupunguza kasi hiyo ya kemikali alisema kuwa mnamo septemba 16 mwaka huu tanzania itaungana na jumuiya ya kimataifa ya kuazimisha siku ya hifadhi tabaka la ozoni ambapo mgeni rasmi ambaye ni makamu wa rais atakabidhiwa tuzo kama mshindi wa kwanza wa kupoambana na tabaka la hewa ya ozoni .

Alifafanua kuwa makamu wa rais atapewa zawadi hiyo kama mshindi wa kwanza miongoni mwa nchi zote za bara la afrika ambapo kutokana na tuzo hizo zitachangia kwa kiwangi kikubwa kwa watanzania kuweza kupunguza na kepukana na vifaa mbali mbali ambavyo vinacdhangia kukithiri kwa kemikali hiyo ambayo ina madhara makubwa sana kwa maisha ya kawaida .

Wakati huo huo waziri huyo alisemam kuwa miongoni mwa changamoto nkubwa ambayo wanayo ni pamoja na changmaoto ya matumizi ya majokofu na viyoyozi ambapo baadhi ya vifaa hivyo vinachangia kwa kiwango kikubwa sana kuwepo kwa gesi ambayo ndio chanzo cha magonjwa mbali mbali pamoja na uharibifu wa mazingira.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa ni vema kama watanzania wakahakikisha kuwa wanafuata taratibu mbali mbali ambazo zinatolewa na serikali ikiwa ni pamoja na kuachana na kununua vifaa ambavyo vimetoka nnje ya nchi (mitumba) ambapo baadhi yake ndivyo vyenye gesi yenye madhara kwa binadamu.

"nawasihi sana watanzania wezangu kuepuka  kutupa ovyo majokofu ya zamani ama vifaa vya kuzima moto vyenye kemikali zinazomongonyoioa tabaka la ozoni aina ya CFCs na halon bali hakikisheni mnapata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa mafundi ama mamlaka zinazousika"alisisistiza

No comments:

Post a Comment