Tuesday, November 20, 2012

MUUMINI WA KWA GEOR DAVIE AKAMATWA AKIWA ANAREKODI MAHUBIRI KWA CHANNEL ARUSHA



Na Bety Alex,ARUSHA

MUUMINI WA KWA GEOR DAVIE AKAMATWA AKIWA ANAREKODI MAHUBIRI KWA CHANNEL ARUSHA

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Victor amekamtwa ndani ya huduma ya Maisha ya Yesu  ambayo inaongozwa na Mchungaji Joackim Channel iliopo Kisongo  ambapo kijana huyo alikuwa anarekodi Maahubiri ambapo baada ya kukamtwa alikiri kuwa ametumwa na Viongozi mbalimbali wa huduma ya Nabii Geor davie.

Tukio hilo limetokea jumapili iliyopita ambapo kijana huyo alionekana kuwa kama si miongoni mwa waumini wa huduma ya maisha ya yesu iliopo Kisongo mjini hapa

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ambao ni waumini wa huduma ya Maisha ya yesu walisema kuwa kijana huyo alikuwa anarekodi maahubiri lakini mara baada ya kuhisiwa alijifanya kama Kichaa hali ambayo iliwalazimu kumshika kwa nguvu

“huyu kijana alikuwa katika hali isiyokuwa ya kawaida kwa kuwa alikuwa hana amani hasa nyakati za maombi lakini sisi tulivyomuona kwa kuwa hata jumapili iliyopita tulimuona basi tukawa na wasiwasi mkubwa sana kuwa huenda yupo kinyume na ibada yetu na ndivyo ilivyokuwa ndani ya Ibada hiyo”waliongeza  waumini hao.

Pia walisema kuwa mara baada ya kukamatwa na kuhojiwa kwa kijana huyo alikubali kuwa hakuwa na lengo halisi la kuabudu ndani ya ibada hiyo ya maisha ya yesu bali alikuwa ametumwa na Viongozi mbalimbali wa huduma ya Geor Davie kwa manufaa yao.

‘Mimi sikuwa  na lengo la kuabudu hapa bali mimi nimetumwa nije kurekodi ibada hii na viongozi wa Geor davie kwa malengo ambayo wanajajua wao kama wao lakini naomba mnisamehee jamani msinipige’aliongeza Kijana huyo ambaye alikamatwa akiwa anarekodi mahubiri kutoka kanisa la Mchungaji  Channel Joackim

Hataivyo mara baada ya kukamatwa kwa kijana huyo na kukiri mbele ya madhabahu hiyo ya Mchungaji Channel kuwa alikuwa ametumwa kurekodi ibada kwa ajili ya matumizi ambayo hayajulikani ya viongozi wa kwa Geor davie alipelekwa katika vyombo vya usalama ili sheria ichukue mkondo wake.

Katika hatua nyingine siku za hivi karibuni watu wasiofahamika walijaribu kumteka mchungaji huyo kwa lengo la kumdhuru lakini hawakufanikiwa na badala yake vyombo vya usalama vilifanikiwa kumuokoa mchungaji huyo Joackim Channel.

Juhudi za kuwatafuta kiongozi wa juu wa huduma za kwa Geor Davie ambaye ni Nabii Geor davie hazikufanikiwa kwa haraka kutokana na kudaiwa kuwa  hawezi kuonekana kwa uraisi,hivyo kushindwa kujibu mashitaka ambayo yameelekezwa mbele zake ya kurekodi ibada kwa malengo ambayo bado hajajulikana.

1 comment:

  1. Muaminini Bwana Mungu wenu mtadhibitika, mwamimi Nabii wake mfanikiwe. Sote tunajua Nabii Geordavie ni Nabii wa kweli na sidhani kama huduma kubwa kama Geordavie Ministries inaweza kumtuma mtu arekodi mahubiri. Mahubiri anayefundisha Nabii Geordavie ni 'classic" haiwezekani kabisa hizo ni propaganda tu. watumishi wa Mungu wapige kazi za ufalme wa Mungu..sio kueneza propaganda zisizo na msingi.

    ReplyDelete