Thursday, November 15, 2012

UGONJWA WA KISUKARI NI TISHIO

NA MWANDISHI WETU,MERU

UGONJWA wa kisukari Duniani umekuwa tishio, ambapo watu milioni 300
wanaugua ugonjwa huo, kati yao milioni 14.7 wanatoka nchi za Afrika.

Hayo yalisemwa juzi na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha, Anzamen
Ndossa, wakati alipokuwa akizungumza kwenye  maadhimisho ya ugonjwa wa
kisukari yaliofanyika Kimkoa eneo la Tengeru, Wilayani Arumeru.

Ndossa alisema kuwa inakadiriwa ifikapo mwaka 2030, watu watakaokuwa
wanaugua ugonjwa huo Afrika, wataongezeka na kufikia milioni 28,000,
sawa na ongezeko la asilimia 9.

Alisema kuwa kwa Dunia nzima inakadirwa watu milioni 500 wataongezeka
na kuugua ugonjwa huo ufikapo mwaka 2050 na idadi hiyo itatokana na
rika baada rika.

“Kutokana na ugonjwa huu kuwa tishio na idadi ya watu kuongezeka,
nashauri watu wajenge bia ya kupima afya zao mara kw amara na kufuata
masharti wanayopatiwa na wataalamu,”alisema.

Aidha aliwaasa wananchi kujenga tabia ya kufanya mazoezi  na kubadili
mfumo wa ulaji wa vyakula, ili kuepukana na ugonjwa huu,”alisema
Ndossa.

Naye Mratibu wa maadhimisho hayo, Dk. Clement Makule, alisema ugonjwa
huo ni tishio, ambapo kwa Mkoa wa Arusha mwaka 2011 vituo vya
Hospitali ya rufaa ya Mount Meru (MMH), Meru na Monduli vilitembelewa
na wagonjwa 4,730 ambao ni wastani wa wagonjwa 394 kwa mwezi.

Alisema kati yao watu 3,716 sawa na asilimia 78.6  waligundulika
katika hospitali ya Mkoa Mount Meru na kufanya ongezeko la asilimia
84.5  ukilinganisha na mwaka 2010 iliyokuwa na wagonjwa 2,014.

“Vile vile ni sawa na asilimia 170 ukilinganisha na takwimu za mwaka
2009, ambapo wagonjwa waliotembelea  hospitali hiyo walikuwa 1,375 ni
wazi mkumbo huu wa  ongezeko la kisukari duniani limefika
Tanzania,”alisema.

Alisema kuwa kisukari kinaathiri zaidi maskini na wenye hali duni na
hakuna nchi itakayoepuka mkumbo huo na inakadiriw akila kwenye watu
wanne wenye kisukari ni watatu wanaoishi  kwenye nchi maskini na zenye
uchumi wa kati.

Dk. Clement alisema Kisukari kimeongezeka kwa kasi zaidi kwenye nchi
maskini na kukisiwa kuw aongezeko  la kisukari nchi za Afrika miaka 20
ijayo itakuwa asilimia 98 na kubw akuliko bara lingine lolote Duniani.
Mwisho

No comments:

Post a Comment