Tuesday, November 20, 2012

PUNGUZENI IDADI YA MBWA MITAANI KWA KUWAFUNGA VIZAZI



PUNGUZENI IDADI YA MBWA MITAANI KWA KUWAFUNGA VIZAZI

Na Queen Lema,Arusha

WAFUGAJI wa Mbwa kwa mkoa wa Arusha wametakiwa kuwafunga Mbwa wao vizazi ili kuweza kupunguza wimbi kubwa la Mbwa ambao wanazagaa ndani ya Mitaa huku baadhi ya Mbwa hao wakiwa na Ugonjwa wa kichaa,hali ambayo inafanya madhara ya Ugonjwa huo kwa Jamii kuwa makubwa zaidi.

Hapo awali Serikali ilikuwa inapunguza idadi ya Mbwa kwa kuwapiga Risasi lakini njia hiyo si nzuri sana kwani inawafanya wanyama hao kukosa haki ya kuishi kinyume cha Sheria na haki za wanyama duniani.

Hayo yamebainishwa Mjini hapa na Bw Livingstone Masija ambaye ni Mratibu wa Mradi wa chama cha kulinda na kutetea haki za wanyama mkoani hapa(ASPA) wakati akiongea na wakazi wa Kijiji cha Nadosoito kuhusu umuhimu wa kufuata sheria ,kanuni,haki  na taratibu za wanyama hasa Mbwa wa mkoa wa Arusha.

Alisema kuwa ndani ya Mkoa wa Arusha hususan Manispaa ya Arusha kuna ongezeko kubwa sana la Mbwa ambao wanazagaa Mitaani huku Mbwa hao wakiwa hawana makazi rasmi hali ambayo ni hatari sana kwa Afya za wana jamii hasa watoto ambao mara nyingi sana wanaonekana kupenda Mbwa kwa ajili ya michezo yao

Alifafanua kuwa ili kuweza kupunguza kasi ya Mbwa hao kuzaliana na kuongezeka mara kwa mara basi wamiliki wa Mbwa wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanawafunga vizazi Mbwa hao ili wasiweze kuzaliana ovyo na kuendelea kusababisha madhara makubwa sana kwa jamii ambayo kila mara inapata matatizo kutokana na Ugonjwa huo wa kichaa cha Mbwa

“kama wamiliki au wafugaji wa Mbwa wataendelea kuwaachia Mbwa wao wazaliane Ovyo mitaani basi watakuwa ni sababu mojawapo ya kusababisha hata vifo vya watu ambao hawana hatia kwa kwua hawa mbwa wanapochanganyana na mifugo mingine ni raisi sana kuwaambukizia vichaa lakini kama wapo wachache itakuwa ni raisi sana kuweza kuwaweka chini ya Uangalizi wa hali ya Juu sana tofauti na pale ambapo wanaporandaranda Mitaani bila kujua na kutambua kuwa mmiliki halisi ni yupi’aliongeza Bw Livingstone

Pia alisema kuwa nao wamiliki wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanafuta sheria za wataalamu za kuwalinda Mbwa hao kwa kuwapa vyumba maalumu vya kuishi na kisha kuwafungulia kwa nyakati maalumu hasa nyakati za usiku ambapo hata kwa njia hiyo itaweza kupunguza kasi ya madhara ya Mbwa kwa binadamu ambayo kila siku inazidi kukua na kuongezeka kwa Mkoa wa Arusha.


Hataivyo alisema kuwa mbali na kuweza kuwasaidia Mbwa kwa kuwaVyumba Maalumu vya kuishi pia wafugaji na wamiliki nao wanatakiwa kuhakikisha kuwa kila mara wanawapa tiba ya kuweza  kuwakinga na magonjwa hasa Chanjo ya kila wiki ambayo nayo itaweza kuwalinda Mbwa hao dhidi ya Magonjwa yenye madhara hasa kwa Binadamu.

MWISHO

No comments:

Post a Comment