Wednesday, November 21, 2012

TUNATAMBUA MCHANGO WA SEKTA BINAFSI-SERIKALI


TUNATAMBUA MCHANGO WA SEKTA BINAFSI-SERIKALI

Na Mustapha leo,ARUSHA

SERIKALI imesema inatambua na kuthamini mchango wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambayo yamekuwa yakisaidia kutoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini ambako wananchi wamekuwa hawapati huduma ya moja kwa moja kutoka serikali.

Hivyo mashirika hayo ni mbia mwenza wa serikali katika kutoa huduma na serikali itaendelea kushirikiana nayo kwa ukaribu lengo ni kuwafikishia wananchi huduma mbalimbali ili waboreshe maisha yao

Rai hiyo imetolewa jana na Katibu tawala wa mkoa wa Arusha,bi Evereen  Itanisa, alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOS) na uongozi wa serikali mkoa wa Arusha katika Ukumbi wa Olasit Garden,  jijini Arusha.

Itanisa,aliongeza kuwa  hadi kufikia mwaka 2012 kuna mashirika yasiyo ya kiserikali 3600 yamesajiliwa hapa nchini ambapo mkoa wa Arusha una mashirika 385 ambayo yamekuwa yakifanya kazi nzuri za kuhudumia wananchi katika maeneo ambayo hasa huduma za moja kwa moja kutoka serikalini hazipo na mashiriuka hayo yamekuwa ni mbia katika maendeleo.

Alisema wilaya ya Ngorongoro ina mashirika 15, Karatu 15, Longido 21, Meru 52 , Arusha DC, 64  Monduli 52 na jiji la Arusha 166 .

Pia aliongeza kuwa hali hiyo imeyafanya mashirika hayo kuwa mkono wa pili wa serikali katika kufikisha huduma bora kwa wananchi hivyo serikali itaimarisha mahusiano na mashirika hayo katika kuwahudumia wananchi waweze kupata huduma stahiki..



Alisema kutokana na wingi huo wa mashirika hayo serikali ilitumnga Sera, Sheria na kanuni ambayo ndio mwongozo wa utekelezaji na usimamiz wa majukumu ya mashirika hayo ili kuboresha mahusiano kati ya serikali, jamii na wananchi

Itanisa alisema kuwa    kutokana na hali hiyo lazima mashirika hayo yafanye kazi zake kwa kuzingatia utekelezaji wa wa Dira ya taifa, ya maendeleo na mpango wa taifa  wa miaka mitano mpango mkakati wa mkoa na halmashauri ya Jiji na  wilaya

Amesema lengo la mkutano huo ni kufahamiana, nani anatoa huduma zipi na eneo lipi,  kuwezesha kupitia kwa pamoja Sera, Sheria na Kanuni za mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na vyombvo vlivyoundwa  vya kusimamia utendaji kazi kwa mashirika hayo,pia kupitia taarifa za  utekelezaji sanjari na kuangalia changamoto zinazoyakabili mashirika hayo.

Awali katibu tawala msaidizi Mipango na Uratibu, Anza _Amen Ndossa, amesema kuwa lazima mashirika yote yafuate Sera na mwongozo wa serikali  namna ya kufanya kazi na kuondoa migongano kati yao kwa kutoa huduma za aina moja katika eneo moja.

Amesema mashirika hayo yana kabiliwa na changamoto nyingi na mkutano huo unalenga kukimarisha mahusiano kati yao na serikali na kuondoa migongano kati yao na kupitia mkutano huo mashirika hayo yataelewa mipaka na majukumu yao na kutoa taarifa za utekelezaji wake kwa wakati bila kigugumizi pia mkutano huo utajenga kuaminiana kati ya Serikali na mashirika hayo..

Ndossa, akawakumbusha  maafisa Maendeleo ya jamii kila halmashauri kuwa wanalo jukumu kubwa la kushirikiana na mashirika hayo kwa kuyapangia maemneo ya kufanyia kazi ili kuondoa muinginiliano inayosababisha kukwama kwa miradi iliyokusudiwa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.


Mwisho.

No comments:

Post a Comment