Saturday, November 17, 2012

KAMWE SITALIPIZA VISASI-Dkt Kikwete

SITALIPIZA VISASI KWA MTU YOYOTE YULE-DKT KIKWETE


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiombewa dua na viongozi wa dini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa kilimanjaro leo Novemba 15, 2012 tayari kwa ziara ya siku tatu ya kikazi mkoani Arusha

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wa dini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa kilimanjaro  Novemba 15, 2012 tayari kwa ziara ya siku tatu ya kikazi mkoani Arusha
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wa dini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa kilimanjaro  Novemba 15, 2012 tayari kwa ziara ya siku tatu ya kikazi mkoani Arusha



Na Queen Lema, Arusha.

KAMWE SITALIPIZA VISASI-Dkt Kikwete

RAIS Jakaya Kikwete, amesema hawezi kulipiza visasi kwa watu wa aina mbalimbali wakiwemo watumishi wa serikali ambao hawaelewani nao bali watumishi wote watahukumumiwa kwa majungu  yao ndani ya jamii.

Rais Kikwete ameyasema hayo , jana jioni kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA) alipokuwa akizungumza na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini mkoa wa Arusha, waliofika kumpongeza kwa kuchaguliwa tena kuwa mwenyekiti wa CCM kwa kipindi kingine cha miaka mitano ijayo, alipowasili tayari kwa ziara ya kikazi mkoani Arusha.

Rais, amesema sio kweli kwamba watumishi wote serikalini ni marafiki zake la hasha bali wapo wengine sio marafiki lakini wanafanya kazi kutokana na sifa na uwezo wao na hivyo kila mmoja atahukumiwa kwa majukumu yake

Amesema hana moyo wa chuki  na mtu yeyote na kamwe hawezi kulipiza kisasi hata kama walivurugana kipindi kilichopita na akasisitiza kuwa watumishi wote watahukumiwa kwa majukumu yao tu

Akawataka watumishi wote kutimiza majukumu yao ipasavyo na kuwaonya watakaovuruga atawashughulikia

Kuhusu utekelezji wa ahadi mbalimbali rais, amesema atajitahidio kuzitekeleza ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake kilichobakia na endapo kama hazitakamilika zote basi rais ajaye atazitekeleza

Kuhusu ujenzi wa madaraja amesema serikali ya awamu ya kwanza iliweza kujenga daraja la Mto Kirumi lililopo wilayani Tarime, katika mto Mara, na serikali ya awamu ya tatu ilijenga Daraja la Mkapa, na sasa serikali yake inajenga madaraja mbalimbaIi yakiwemo  mto Malagarasi, Kilombero, na maeneo mengine nchini na tayari makandarasi wameshakabidhiwa kazi hizo

Aliongeza kuwa  viongozi hao wa dini kuiombea amani Tanzania na kueleza kuwa iwapo amani itatoweka kila kitu kitavurugika na maswala yote ya maendeleo yatakuwa hayapo tena.

Kwa upande wao viongozi hao weameahidi kuipa ushirikiano serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Dkta Jakaya Kikwete na kuahidi kuendelea kuomba amani  ya nchi idumu.

Wamesema, asijali kelele na kebehi na shutuma zinazotolewa na baadhi ya watu bali aendelee kutekeleza majukumu yake na kazi zake alizozifanya zinaonekana na ndizo zitawasuta wote wanaomshutumu.

Wamerejearea kauli ya Yusufu Makamba, aliyoitoa hivi karibuni katika mkutano mkuu wa CCM ulionmalizika mjini Dodoma na kusema kuwa rais sio malaika hivyo asihukumiwe bila sababu bali ahukumiwe kwa kazi alizozifanya wala asihukumiwe kwa  matendo ya watoto wake.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment