Wednesday, November 21, 2012

MAJESHI YA SADC KUENDELEA KUTOA MSAADA KWA NCHI ZENYE MAJANGA,NA VITA


MAJESHI YA SADC KUENDELEA KUTOA MSAADA KWA NCHI ZENYE MAJANGA,NA VITA

Na Queen Lema,ARUSHA

UMOJA wa nchi zinazoendelea kusini mwa jangwa la Sahara(SADC)umesema kuwa utaendelea  kupeleka majeshi kwenye nchi zenye mitafaruku mbalimbali yakiwemo majanga na vita huku lengo likiwa ni kuepusha vifo.

Kauli hiyo imetolewa jana(Leo)na Kanali Gerson Sangiza ambaye ni mkuu wa kitengo cha ulinzi na mipango katika sektetarieti ya SADC wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mipango mbalimbali ya majeshi ya umoja huo

Kanali Sangiza alisema kuwa kwa nchi zenye majanga mbalimbali yakiwemo majanga ya vita,mitetemeko,pamoja na mafuriko ambazo ni wanachama wa umoja huo wataweza kusaidiwa kwa kupewa misaada na majeshi ya nchi kama kumi na tano

Alifafanua kuwa kupitia umoja huo wa majeshi kuweza kusaidia nchi zenye majanga kutaweza kuepusha nchi nyingine ambazo zipo jirani kupata matatizo mbalimbali ambapo kupitia matatizo hayo nayo yanachangia sana kukitihiri kwa majanga.

‘kama sisi SADC hatutashirikiana kwa pamoja katika kutetean amani ya nchi yenye vita kupitia kwenye majeshi yetu ni wazi kuwa matatizo mengi sana yataweza kuibuka kama vile vifo na hata wakimbizi,ingawaje kama kuna matatizo tukishirikiana kwa pamoja ni wazi kuwa tutaweza kuleta amani tena ya kudumu  na hiyo itafanya madhara mbalimbali ndani ya nchi yenye vita kukoma kabisa”aliongeza kanali huyo

Pia alisema kuwa mbali na kudumisha amani ndani ya nchi zenye vita pamoja na majanga mbalimbali kupitia umoja wa majeshi hasa ya nchi hizo za SADC majeshi hayo yanamikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa ndani ya karne ya sasa na karne ijayo hakuna mapigano ambayo ndiyo yanayochangia sana kukithiri kwa vita.

Katika hatua nyingine alisema kuwa pamoja na kuwa Majeshi ya nchi 15 yanafanya kazi kwa umoja mkubwa sana hasa kwa kusaidia nchi znye vita na majanga lakini bado wana mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kuwa kila Nchi mwanachama wa Umoja huo pamoja na majeshi yake yanakuwa katika viwango ambavyo vinahitajika

Alisema kuwa Mikakati hiyo ni pamoja na kubadilishana uzoefu baina ya Nchi na nchi ambapo hali hiyo inasaidia Vikosin mbalimbali vya Jeshi kuweza kufanya kazi kwa uzoefu wote ambao wao kwa wao wanaujua na hivyo kurahisisha kazi hasa pale inapotokea hasa ya Majanga, na Vita.

“kwa mfano hapa kwetu Tanzania tuna chuo cha TMA kipo Monduli pale wanajeshi kutoka Nchi mbalimbali wanasoma na kuendelea kujifunza mbinu mbalimbali lakini na sisi wanajeshi wetu pia na wao wanakwenda sehemu mbalimbali kujifunza nah ii inachangia sana kuweza kuwaandaa kuwa tayari kwa nyakati zozote zile’alisema

MWISHO

No comments:

Post a Comment