Saturday, November 24, 2012

SIDO ARUSHA YAFANIKIWA KUTOA MKOPO WA ZAIDI YA MILION 544,KWA WAJASIMALI 2018


SIDO ARUSHA YAFANIKIWA KUTOA MKOPO WA ZAIDI YA MILION 544,KWA WAJASIMALI 2018

Na Queen Lema,Arusha

SHIRIKA la kuhudumia viwanda vidogo vidogo hapa nchini(SIDO)mkoa wa Arusha limefanikiwa kutoa elimu ya ujasiamali kwa wajasiamali 2,018 huku jumla ya Milioni 544 nayo ikitolewa kama Mkopo ili kuendeleza mitaji ya wajasiriamali hao kwa kipindi cha miaka miwili,

Hayo yameelezwa na Meneja wa shirika hilo mkoani hapa Bw Isidore Kayenzi wakati akielezea mafanikio ya Shirika hilo kwa Waziri wa Viwanda na Biashara hapa nchini Bw Abdalah kigoda mapema jana

Bw Isidore alisema kuwa Mikopo na elimu hiyo ambayo ilikuwa inatolewa kwa wajasiamali hao imefanikiwa kuwafikia wananchi wa Wilaya za Arumeru,Monduli,Karatu, longido, na Ngorongoro ambapo mpaka sasa mafanikio yameshaonekana

Aliongeza kuwa mafunzo ambayo wameweza kuwapa wajasiamali hao ni pamoja na Ujasiamali hasa katika Uongozi wa Kibiashara,utengenezaji wa sabuni,usindikajiwa ngozi na bidhaa za ngozi,usindikaji wa chakula  na matunda,pamoja na mafunzo mengine ambayo yameweza kutoa ajira huku yakichochea msukumo mkubwa wa Ujasiamali hasa kwa mkoa wa Arusha

‘hawa wajasiamali ambao tumewapa mafunzo asilimia 70 wameweza kutoa ajira hata kwa watu wengine nah ii imeongeza hata idadi ya  viwanda vidogo vidogo ambavyo tunavyo kwa mkoa wa Arusha ingawaje Sido kama Sido bado inakabiliwa na changamoto za hali ya juu san”aliongeza Bw Isidore.

Pia alisema kuwa kwa sasa changamoto kubwa sana ambayo inayokabili Shirika hilo pamoja na wajasiamali wa Mkoa wa Arusha ni Mahitaji makubwa sana ya wajasiamali wadogo na wakati hasa Mitaji kuliko uwezo ambao wanao hali ambayo inatakiwa kuangaliwa kwa undani sana

Alifafanua kuwa mbali na changamoto hiyo ya Ukubwa wa mahitaji wakati hakuna Mitaji ya kuendeshea shuguli za kijasiamali lakini pia bado kuna changamoto ya utoaji wa mkopo hasa kwa SIDO kwani kiwango chao cha juu cha utoaji wa Mikopo ni Milioni sita huku kiwango hicho nacho kikifanya baadhi ya wajasiamali washindwe kuvuka malengo yao ambayo wamejiwekea hasa ya kutoa katika daraja dogo na kuingia kwenye daraja la kati la ujasimali.

Naye Waziri wa Viwanda na Biashara hapa Nchini Abdallah Kigoda alisema kuwa pamoja na kuwa Shirika hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali lakini bado Tanzania ina tatizo kubwa sana la kutowapa wajasiamali wadogo na wakati fursa mbalimbali za kukuza na kuimarisha Uchumi wa Mkoa na Tanzania

Bw Kigoda alisema kuwa kwanza Sekta za umma na binafsi zinatakiwa kuanza kuwapa fursa wajasiamali wadogo na wakati vipaumbele mbalimbali kwa kuwa wajasiamali wana uwezo mkubwa sana wa kuweza kuimarisha hata uchumi ambao unayumbayumba huku ajira mbalimbali nazo zitaweza kuongezeka.

‘Hii ni Sekta ambayo inatakiwa kupewa kipaumbele kikubwa sana kwa kuwa ndiyo injayoshikilia mambo mbalimbali na pia nguvu za Ziada zinatakiwa kuelekezwa kwa wajasiamali wengi zaidi ingawaje hata uwepo wa viwanda vingi hapa Nchini unachangia sana kuweza kufanya watanzania kupata bidhaa zao kwa uraisi sana tofauti na sasa ambapo asilimia kubwa ya watanzania wanategemea zaidi bidhaa kutoka nje ya nchi wakati watanzania wana uwezo wa kutengeneza bidhaa hizo”aliongeza Bw Kigoda.

No comments:

Post a Comment