Saturday, November 24, 2012

WANAOANGUKA NYAKATI ZA MITHIANI WANAKABILIWA NA HOFU YA MAWAZO


NA MWANDISHI WETU,ARUSHA

IMEELEZWA kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi mbalimbali ambao wanahisiwa kukabiliwa na nguvu za giza hawana nguvu hizo na badala yake wanafunzi hao wanakabiliwa na hali ya uoga hasa nyakati za mithiani,hali ambayo inasababishwa na mazingira ya majumbani mwao pamoja na shule zao

Wakati wa Mithiani asilimia kubwa ya wanafunzi huwa wanaanguka na kushindwa kufanya mithiani lakini sio nguvu za giza bali ni uoga wa mithiani na msongamano mkubwa sana wa mawazo (STRESS)

Hayo yamebainishwa wiki iliyopita  na Bw  Japhet Mwanangombe ambaye ni mratibu wa  shirika lan Roots and Shoots la jijini hapa wakati akiongea katikia kongamano la wanafunzi wa shule mbalimbali mjini hapa ni wanamazingira kwa kanda ya kaskazini

Bw Japhet alisema kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi wanasumbuliwa na hali ya uoga mkubwa sana hasa nyakati za mithiani ya Mwisho wa Mwaka pamoja na mithiani ya Kitaifa huku wazazi, walezi, na walimu wakijua kuwa ni nguvu za giza hali ambayo inafanya hata baadhi ya maendeleo ya Taaluma kushuka sana hasa kwenye baadhi ya shule.

Aliongeza kuwa wanafunzi wengi huwa wanafikiria zaidi matokeo ya mithiani au hali duni za maisha yao majumbani mwao bila kujua na kutambua kuwa mawazo kama hayo ndiyo yanayochangia kupoteza fahamu huku watu wengine wakihisi kuwa wanakabiliwa na changamoto ya nguvu za giza ndani ya shule zao

‘kwa kweli uchunguzi ambao tumeufanya kwa baadhi ya shule hasa za kanda hii ya kaskazini ambazo zinakabiliwa na changamoto kama hiyo tumebaini kuwa hakuna hata chembe ya nguvu za giza ila kwa kuwa wazazi na walimu wamejiwekea utaratibu wa kudai ni nguvu za giza na watoto wanaamini hivyo ila sio kweli wengi wanaogopa mithiani na matokeo ya mithiani,pamoja na hali duni za majumbani mwao’aliongeza

Katika hatua nyingine alisema kuwa ili hali hiyo iweze kupotea kwenye baadhi ya shule hasa kwa kanda ya kaskazini wazazi pamoja na walimu wanatakiwa kuhakikisha kuwa kwanza wanawajengea uwezo wanafunzi wa kuwa wajasiri wa kukabiliana na mithiani pamoja na hali duni za maisha ambapo kama watafanya hivyo basi watachangia sana wanafunzi kuacha kuanguka anguka ovyo.

Alisistiza kuwa wazazi wanatakiwa kuwapa moyo watoto wao hasa nyakati hizo za mithiani na kuacha tabia ya kuwapa vitisho ambavyo ndivyo vinachangia baadhi ya shule kukumbwa na na kashfa ya kuangukaanguka huku pia hali hiyo nayo ikichangia matokeo mabaya sana hasa kwenye mithiani ya Kitaifa

‘wakati wa mithiani wapo watoto ambao wana uwezo wa kufanya vizuri kabisa lakini wanashindwa kufanya vizuri kwa kuwa wazazi na walezi wao wanawapa vitisho vikubwa sasa hapa unakuta kama mtoto hajaanguka na mawazo, basi anafanya vibaya hii ni hatari sana kwa maendeleo ya taaluma hapa nchini”aliongeza


 Awali wanafunzi wa klabu hiyo walisema kuwa idadi ya wanafunzia ambao wanadondoka hasa nyakati za mithiani(EXAMINITIONAL FEVER) inaongezeka siku hadi siku lakini shule za Msingi,Sekondari, na Vyuo vinatakiwa kuwa na kitengo maalumu cha kuwapa wanafunzi ushauri ili kuweza kuwajenga zaidi tofauti na sasa ambapo baadhi ya wakuu wa shule na walimu wanatoa vitisho kwenye mithiani ya Kitaifa

Mwisho

No comments:

Post a Comment