Saturday, November 17, 2012

JICHO LA LEO- KWELI MIAKA MINNE TEKNOLOJIA ZAZALISHWA KAMA PICHA ZASHINDWA KUWAFIKIA WAKULIMA KISA HAKUNA FUNGU KUTOKA SERIKALINI


JICHO LA LEO


 KWELI MIAKA MINNE TEKNOLOJIA ZAZALISHWA KAMA PICHA ZASHINDWA KUWAFIKIA WAKULIMA KISA HAKUNA FUNGU KUTOKA SERIKALINI

Wiki iliyopita nilitembelea Kituo cha Utafiti wa mazao ya kilimo kwa kanda ya kaskazini(SARI) lakini katika mahojiano hayo nilishangaa sana kwani Sera ya Kilimo Tanzania bado ni wimbo wa taifa tena kwa Wakulima wadogo wadogo

Katika kutetea Safu ya Jicho la Leo niliongea na Mkurugenzi wa kituo hicho Dkt Mboya Mgendi ambaye alikiri kuwa pamoja na kuwa Kituo hicho kinapambana na changamoto mbalimbali za kilimo kwanza lakini Serikali imefunga Macho kwa kushindwa kutoa fedha  kwa kituo hicho kwa muda mrefu sasa ambapo Teknolojia mpya thelathini zimeshindwa kuwafikia wakulima kwa muda wa miaka minne sasa

Kwa mujibu wa Dkt Mgendi alisema kuwa kutokana na ukosefu wa fedha kwa muda mrefu sasa kituo hicho ambacho ni muhimu sana kwa ajili ya kuzalisha teknolojia mbalimbali zimeshindwa kufika maeneo mbalimbali hasa vijijini ambapo ndipo kwenye huitaji mkubwa sana hivyo Teknolojia ambazo zinazalishwa kwa ajili ya kutoa msaada kwa Kilimo kwanza zinabaki hapo hapo

Lakini aliendelea kwa kusema kuwa Kituo hicho ambacho kwa sasa kinasikitisha sana kutokana na Serikali kushindwa kutoa fungu la kusafirishia teknolojia Vijini kwa sasa Mikoa ya kanda ya kaskazini ambayo ni Arusha,Kilimanjaro,na Tanga haina teknolojia ambazo zinazalishwa na kituo hicho hali ambayo inaonekana sana kuzorotesha sana maendeleo ya kilimo.
“tunasikitika sana kwa kuwa tuna buni teknolijia kila siku tena teknolojia ambazo ni mpya kabisa kisha zinashindwa kuwafikia walengwa kwa kuwa tunafikaje ni lazima fedha itumike kusafirisha hata hawa wataalamu, na kutokana na hilo tunabaki na hizi teknolojia wakati walengwa wa hizi teknolojia ni wananchi tena wa  chini sasa Serikali inatakiwa kuliangalia suala hili kwa undani sana ili kuweza kuboresha zaidi Kilimo kwanza”alionngeza Dkt Mgendi.


Pia aliiomba Serikali kuhakikisha kuwa inaangalia kwa undani sana umuhimu wa kituo hicho hassa kwa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini ambapo kuna changamoto kubwa sana ya Matumizi sahihi ya  utafiti  wa kilimo, Mbegu bora za kilimo,pamoja na dhana ambazo bado wakulima wanaitaji elimu zaidi kutoka kwa wataalamu hao  wa kilimo bora.

Mbali na hayo Kamera ya jicho letu inatafakari kuwa nini maana ya Kilimo Kwanza endapo kituo kama hiki cha utafiti wa mazao tena ya kilimo kitashindwa kufikisha teknolojia mpya tena thelathini kwa wakulima,je inakuwaje kwa wakulima ambao wanaangalia kwa jicho la huruma kwa kutegemea Teknolojia hizi mpya kwa kweli hii ni ajabu tena ya Musa,WADAU ANGALIENI KWA JICHO LA TATU SUALA HILI MKO WAPI MNAOTOA MISAADA KWENYE STAREHE HASA HARUSI,NA KITCHEN PATY, WASAIDIENI WAKULIMA WENU TEKNLOJIA 30 ZIWAFIKIE BIBI NA BABU ZETU KULE KIJIJINI.

No comments:

Post a Comment