Tuesday, November 20, 2012

TAASISI ZA FEDHA ZASHAURIWA KUPELEKA HUDUMA VIJIJINI



Na Queen Lema, Arusha

TAASISI ZA FEDHA ZASHAURIWA KUPELEKA HUDUMA VIJIJINI

TAASISI za Fedha zimeshauriwa kuhakikisha kuwa wanapeleka huduma zao hata Vijijini kwa kuwa asilimia kubwa ya wananchi wa Vijijini hawana uelewa wa kutosha juu ya matumizi ya Taasisi hizo za fedha hali ambayo nayo inachangia kukithiri kwa changamoto mbalimbali zikiwemo za matumizi mabaya ya fedha na mali

Kauli hiyo imetolewa mjini hapa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru Trasias Kagenzi wakati alipokuwa akiongea na Walimu mbalimbali ambao ni wadau wa Benki ya NMB katika Siku ya Mwalimu iliyoazimishwa na Benki hiyo.

Kagenzi alisema kuwa kwa sasa Taasisi nyingi sana za fedha zimejikita zaidi kwenye maeneo ya Mijini huku kwa upande wa Vijijini wakiwa wamesahulika ingawaje kijijini ndiko kwenye fursa nyingi sana za Fedha ambazo zimesahulika sana hali ambayo nayo inachangia sana Umaskini.

Aliongeza kuwa Taasisi hizo za Fedha zinatakiwa kubadilisha na kuimarisha mifumo zaidi hasa Vijijini ambapo kuna fursa nyingi lakini hazitambuliki kutokana na wananchi kushindwa kujimudu kimaisha lakini kama Taasisi za Fedha zingejikita zaidi basi hata uchumi wa vijiji pamoja na Mikoa ingeweza kuimarika sana na kufanya hata kiwango cha uzalishaji kuwa kikubwa sana.

“kwa sasa hasa ndani ya Mkoa wa Arusha Mjini unakuta kila mahali ni benki lakini ukija vijijini hakuna hata benki ya kugeresha maisha sasa hawa Wamiliki wa Mabenki  na Taasisi za Fedha wanasahau kuwa ambaye anaweza kujikwamua zaidi kiuchumi ni mtu wa Kijijini kwa kuwa ndani ya Vijiji kuna fursa Nyingi sana hasa za Kilimo, na Ufugaji hivyo basi napenda kuwakumbusha kuwa mnatakiwa kuwakumbuka hata wananchi wa Vijijini hata kwa kuwapa elimu ya kumiliki fedha”aliongeza Bw Kagenzi

Pia alisema kuwa mbali na Mabenki hayo kuweza kuwekeza zaidi Vijijini lakini nao wafanyakazi hasa ambao ni waajiriwa wa Serikali wanatakiwa kuijiendeleza kwa kuhakikisha kuwa wanatumia fursa mbalimbali za Mabenki hasa NMB kwa kuhakikisha kuwa wanakopa na kisha kufanyia Mikopo yao kazi za maendeleo kwa manufaa ya Jamii zao.

Awali Meneja wa Benki hiyo kwa kanda ya Kaskazini bi Vicky Bishubo alisema lengo halisi la kuwakutanisha walimu wa shule mbalimbali ni kuweza kuwapa elimu mbalimbali ikiwemo huduma zinazotolewa na Benki hiyo hali ambayo itawafanya wadau hao kuweza kufikia malengo yao mbalinbali ya Kimaisha.

“kama tunavyojua ni kuwa benki yetu mpaka sasa imeshatoa mikopo mingi sana kwa walimu na walimu ni wadau wetu wa muhimu sana sasa tunapowakutanisha hivi katika siku ya Mwalimu ndani ya benki hii tunaweza kuwaongezea uwezo wa kutumia fursa zilizopo ambazo kama nazo watazitumia vema basi wataweza kufikia malengo yao mbalimbali’aliongeza Bi Vicky

MWISHO

No comments:

Post a Comment