Tuesday, June 5, 2012

BREAK NEWSSSSSSSSSSSSS EAC YAPATA SPIKA MPYA

  Arusha.
BUNGE la nchi za Jumuia ya Afrika mashariki .limemchagua ,Margret ZZiwa Nantongo, kutoka Uganda kuwa Spika wa bunge hilo baaada ya kupata kura 33 na kumshinda, mgombea mwenza, Dolla Byamkama nae kutoka nchini Uganda, aliyepata kura 12.
Uchaguzi huo ilibidi uingie awamu ya pili baada ya awamu ya kwanza kushindwa kumpata mshind ambapo katika a awamu hiyo ZZiwa alipata kura 27 na Dola Byamkama kura 18 hivyo hakufikia nusu ya kura.
Margeret Nantongo, na Dolla Byamkama, wote wanatoka nchini Uganda, hivyo anakuwa ni mbunge wa kwanza mwanamke kuwa Spika wa jumuia hiyo ya Afrika mashariki.
Mara baada ya uchaguzi huo Namtongo, amewashukuru wabunge wote kwa Imani kubwa waliyoionyesha kwa kumchagua na akaahidi kutoa ushirikiano kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya jumuia hiyo.
Mwisho 
chanzo cha habari na Queen Lema

No comments:

Post a Comment