Saturday, June 9, 2012

Arusha wana meno yenye rangi na watoto kwa baadhi ya meneo wanasumbuliwa tatizo la matege.




Chanzo: Arusha255 Blog

Sababu ya dosari hizo kwa binadamu ni maji yanayopatikana ndani ya eneo hilo yanayoelezwa kuwa na kiwango kikubwa cha floride ambayo ndio inaaminika kuharibu meno kwa kutengeneza tabaka la nje kuwa rangi ya ‘brown’ na kulainisha mifupa, jambo linalopelekea mtu kuwa na matege.

Mamlaka ya Maji Arusha (Arusha Urban Water Supply Authority) iliungana na wataalamu toka Chuo Kikuu cha University of Dar-Es-salaam kufanya utafiti kuangalia kiwango cha kemikali ya ‘floride’ kilichomo kwenye vyanzo vyake vya maji na kutafuta mbinu za kukabiliana nayo.

Mkurugenzi wa AUWSA, Injinia Ruth Koya alisema, Mji wa Arusha una vyanzo vingi vya maji lakini vingi vina kiwango kikubwa cha floride na wakati huo huo maji yakianza kuonekana kama bidhaa adimu mjini hapa.
Kwa mujibu wa wataalamu, mtu anapoingiza mwilini kiwango kikubwa cha floride humsababishia kupata ugonjwa unaojulikana kama ‘dental flourisis’ kwa lugha ya kitaalamu.

AUWSA imeshagawa tenda kwa ajili ya kununulia dawa za kuondoa hiyo floride kwenye maji.
Wakati huo huo mtaalamu wa meno kutoka hospitali ya Saint Elizabeth ya Arusha (SEHA), Anna William Msuya anasema matatizo haya ya meno kwa wakazi wa Arusha mengine hutokana na kutokujua aina sahihi ya dawa za meno zinazofaa kwa mazingira ya Arusha.

Alisema maji yanayopatikana Arumeru na Arusha mjini tayari yana kiwango kikubwa cha madini ya floride na hivyo hakuna haja ya mtu kutumia tena dawa ya meno yenye madini hayo. kufanya hivyo ni kufanya tatizo liwe kubwa zaidi.
Anna anaeleza kwamba madini ya floride hupunguza kiwango cha madini mengine aina ya calcium ambayo ni muhimu kwa utengenezaji wameno imara na mifupa kwa binadamu.

Mtaalamu huyu anawaasa pia watu wanaodhania wakitumia maji ya viwandani wanaweza kuepukana na tatizo hili, na kuwakumbusha kuwa madini ya floride hupatikana pia kwenye mboga za majani zinazolimwa maeneo tofauti ya mji.
Kwa hiyo watu wa Arusha wanashauriwa kutumia zaidi dawa za meno zisizo na flouride, na hasa zenye mjumuisho wa clacium ili kupunguza tatizo kwa kiwango fulani.

Chanzo: Arusha255 Blog

No comments:

Post a Comment