Thursday, June 7, 2012

AUWA NA KISHA KUNYOFOLEWA UUME, NA MIKONO


 KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA LIBERATUS SABAS



HABARI NA UPAKO


,ARUSHA

Mtu mmoja ambaye hajajulikanan jina lake amefariki dunia huku baadhi ya viungo vyake hasa sehemu za uume wake zikiwa zimechomolewa  pamoja na mikono yake

Akiongea na waandishi wa habari mapema leo kamanda wa polisi mkoa wa arusha Sabas Liberatus alisema kuwa tukio hilo lilitokea  may 26 majira ya saa tni asubuhi katika eneo la Mto Nambala wilyani Arumeru

Kamanda Sabas alisema kuwa katika siku ya tukio mytu mmoja mwenye jinsia ya kiume ambaye hajatambulika mpaka sasa anakadiriwa kuwa na miaka25-30 alikutwa akiwa amefariki

Kamanda huyo aliongeza kuwa mara baada ya wapita njia kumkuta akiwa amefariki waligundua kuwa pia hana viungo mbalimbali ndani ya mwili wake hali ambayo ilizua tafrani kubwa

‘hawa watu walipomuangalia kwa undani sana waliweza kujua na kutambua kuwa baadhi ya viungo vyake havipo na ndipo walipota taarifa kwa jeshi la polisi na sisi tulipoofika ndani ya eneo la tukio tuliyakuta hayo hayo”alisema Kamanda Sabas

Pia aliongeza kuwa baada ya polisi kufika katika eneo la tukio walikuwa mwili huo ukiwa na suruali  aina ya jeans ambayo ilikuwa imeshushwa hadi chini ya magoti na viungo vyake vikiwa vimenyofolewa

Hataivyo jeshi hilo linaendela na upelelezi juu ya tukio hilo na upelelzi wa kumfahamu chanzo cha umati huo huku mwili wa marehemu ukiwa umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mount Meru

mwisho

No comments:

Post a Comment