Tuesday, June 5, 2012

MANISPAA YA ARUSHA YAPANDA MITI 2000



Halmashuri ya manispaa ya jiiji la Arusha inatarajia kupanda miti zaidi ya 2000 katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo huku lengo halisi likiwa ni kutunza na kuthamini mazingira .

Kauli hiyo imetolewa mjini hapa na Meya wa jiji hilo Gauydence Lyimo wakati wa zoezi la upandaji miti katika bonde la mto Naura mapema jana.

Lyimo alisema kuwa pamoja na kuwa hii ni wiki ya mazingira lakini bado kuna jitiada mbalimbali ambazo zinafanywa ili kuweza kuboresha zaidi jiji la Arusha kwa kuwa yapo maeneo mengi sana ambayo miti yake imekatwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

Alifafanua kuwa ili mji wa Arusha ukae katika muonekano mzuri n Iazima kwanza kuwepo na mpangilio mzuri wa mazingira ambapo mpangilio huo utaweza kuwanufaisaha hata watanzania hasa wakazi wa Arusha wenyewe.

Alibainisha kuwa mara nyingi zoezi la ukataji wa miti linakuwa na madhara makubwa sana hasa kwa wakazi wa mji huu kwa kuwa wanapoteza vitu muhimu ambavyo ni kwa ajili ya maslahi yao wenyewe

Alitaja vitu hivyo kuwa ni pamoja na kukosa maji sanajari na mvua za uhakika kwa kuwa  ambazo ndizo zinazozalisha vyakula kwa mpangilio hali ambayo wananchi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajifunza kutokana na hali ya ukame ambayo inaikumba baadhi ya familia

Awali alisema kuwa mbali na hayo yote pia nayo makampuni mbalimbali yanatakiwa kuhakikisha kuwa yanaboresha mji wa Arusha kwa kupanda aina mbalimbali za miti ambazo zitachangia kwa kiwango kikubwa sana kuboresha hata uoto wa asili

Aliyataka makampuni yote hata kama ni makampuni ya Kitalii kujiwekea utaratibu na kama makampuni yote ndani ya Jiji hilo watapanda miti pembezoni mwa jiji basi huenda hali ya jiji ikarudi kama ilivyokuwa hapo awali.

No comments:

Post a Comment