Tuesday, June 5, 2012

NIMEPITA LAKINI NASUSIWA JAMANI NDANI YA MASAA MACHACHE SANA

BIFU: Mbunge wa Uganda agoma kupongezana na Spika Mteule


 Spika wa Bunge la EALA Margaret Banbtonbg Zziwa
Kati Hali isiyokuwa ya kawaida ndani ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA) hii leo wakati Wabunge hao wakiendelea kuapa, aliyekuwa Mgombea wa Kiti cha Spika kutoka Uganda, Mwanasheria Dora Byamukama (40) amegoma kumkumbatia (hug) Spika Mteule wa Bunge hilo ambaye pia anatoka  nchini Uganda, Spika Margaret Banbtonbg Zziwa (49).

Ilikuwa ni kawaida ya wabunge wote waliokuwa wakiapa kukumbatiana au kupeana mikono ya pongezi na Spika huyo lakini Mbunge huyo aliyeanguka katika Uchaguzi wa Spika kuzira kufanya hivyo jambo lililozua mguno ndani ya Bunge na kwa wageni waalikwa kukumbwa na butwaa.

Safari hii ni zamu ya Uganda kuchukua kiti cha Spika baada ya Tanzania na Kenya kushika nafasi hiyo katika Bunge la Awamu ya Kwanza na Pili.

 Bunge hilo limezinduliwa leo na wabunge wake wakiendela kuapa hivi sasa katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha.
Zziwa ambaye ni Mchumi kitaaluma amemshinda mwanamke mwingine kutoka Uganda, Mwanasheria Dora Byamukama (40) baada ya uchaguzi huo kurudiwa mara mbili baada ya kura za awali kutokufikia idadi asiliamia 30 inayotakiwa ya wapiga kura wote.

No comments:

Post a Comment