Tuesday, June 5, 2012

HALMASHAURI YA ARUSHA VIJIJINI YATOA ELIMU YA KIHASIBU KWA WATENDAJI WA VIJIJI 71




HALMASHAURI ya Arusha vijijini Mkoani hapa imefanikiwa kutoa mafunzo ya kiuasibu  pamoja na Stadi za utunzaji wa vitabu vya mahesabu kwa watendaji wa vijiji 71 ili kuweza kuepusha halmashaurri hiyo dhidi ya  matumizi mabaya ya fedha hasa vijijini

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Bw Khalifa Idda wakati wa kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika Wiki iliyopita  wilayani humo

Bw Idda alisema kuwa  hapo awali kulikuwa na kasoro lukuki ambazo zilikuwa zinajitokeza hasa kwa watendaji hali ambayo ilikuwa inasababisha hasara na halmashuri hiyo kushindwa kufikia makusudio ambayo yalikuwa yamelengwa

Alisema kuwa baada ya Halmashauri yake kuanza kuona hali kama hiyo ililazimika kwa kiwango kikubwa sana kuhakikisha kuwa wanapuunguza tatizo hilo na kuanza mpango maalumu wa kutoa elimu hali ambayo imezaa mafanikio makubwa sana

“hapo awali tulikuwa tunashindwa kufikia malengo yetu mbalimbali kutokana na baadhi yetu kushindwa kuwa na elimu hali ambayo ni chanzo cha ukwamaji wa miradi mbalimbali lakini kwa sasa mambo yataenda vema kabisa  tofauti na vile ambavyo tulikuwa hapo awali:”alisema Bw Idda

Pia alibainisha kuwa pamoja na kuwapa elimu hiyo ili wasiwe chanzo cha kukwamisha malengo mbalimbali pamoja  na Miradi pia jamii hizo za vijijini nazo zitaweza kuwa na manufaa kwa kuwa watendaji hao sasa wataweza kuandaa mapato na matumizi ambayo hapo awali hayakuwepo kwa baadhi ya vijiji.

Alisema kupitia mapato na  matumizi pia nao wananchi wataweza kuwa kufuatilia fedha mbalimbali ambazo zinatolewa na Halmashauri hiyo kwa karibu sana tofauti na hapo awali ambapo wengi waalikuwa wanaingia katika migogoro kwa kuwa hawajui kuaanda mapato na matumizi.

Katika hatua nyingine alisema kuwa mpango huo wa kuendeleza watendaji wa kata na vijiji ni mpango wa kudumu ili kupitia watumishi hao Halmashauri hiyo iweze kufikia malengo yake ambayo walikuwa wamejiwekea ya kupambana na changamoto mbalimbali hasa za vijijini

Mwisho

No comments:

Post a Comment