Thursday, June 7, 2012

AMUUA MKEWE KWA KUHOFIA UJAUZITO SI WA KWAKE

STORY NA DOTO MZAVA,ARUSHA



Mtu mmoja na mkazi wa kijiji cha Olkeijulongishu,aliyefahamika kwajina la bi Neisisiri Mokoroo (25),amefariki dunia mara baada ya kupigwa na mumewe ndani ya tumbo lake kwa tuhuma za kubeba ujauzito usio wake


Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Arusha bw Liberatus Sabas leo(jana) alisema tukio hilo lilitokeajuni 6 mwaka huuhuko katika wilaya ya Longidokatikakijiji cha Olkeijulongishu nakata ya Olkeijulongishu majira ya saa11;00 jioni.

Kamanda Sabas aliongeza marehemu alikutwa na mauti baada ya mume wake aitwaye KapaitoNaanjarati,kumshambulia mkewe kwa kumpiga nafimbo sehemu mbalimbaliza mwili wake hali iliyomsababishia umauti.

Aliongeza kuwa kwa mujibu wa taarifa za awali zinasema kuwa,tukio hilolilitokea baada ya wawili hao kwenda shambani kukata nyasi na
walipofika huko,ndipo mtuhumiwa ambaye ni mume wa marehemu
aliopomtuhumu mkewe kwamba ujauzito alionao si wa kwakebaliamepewa na mwanamume mwingine.

Hata hivyo Kamanda Sabas alisema kufuatia hali hiyo ilisababisha mumewe aanzekumpiga kwa fimbo na kumsababishia kifo chake baada ya muda mfupi.

Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikimbia na kuelekea kusiko julikana nakusema jeshi la polisi mkoani hapa,bado linamtafuta mtuhumiwa napindiatakapopatikana atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Kamanda Sabas alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Longido na uchunguzi unaendelea

MWISHO.

No comments:

Post a Comment