Sunday, June 17, 2012

Wanafunzi walemavu Mafinga waipigia magoti Serikali

Wanafunzi walemavu Mafinga waipigia magoti Serikali

Na Joachim Mushi, Thehabari.com- Mafinga

WANAFUNZI wenye ulemavu anuai katika Shule ya Msingi Makalala wameiomba
Serikali na wadau wengine kuwasaidia kuwajengea mazingira bora ya
kujifunzia kwa watoto wenye ulemavu ili waweze kupata elimu bora kama
ilivyo kwa watoto wengine.

Kauli hiyo imetolewa katika risala ya wanafunzi hao iliyosomwa jana
Wilayani Mafinga kwenye maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika
kiwilaya kwenye Shule ya Msingi Makalala nje kidogo ya Mjini wa Mafinga.

Katika maelezo yao watoto hao wameiomba Serikali na wadau wengine
kuwatizama kundi la watoto wenye ulemavu anuai kwa jicho la karibu, hasa
katika uboreshaji wa mazingira jumuishi ya kujifunzia katika shule zenye
watoto wenye ulemavu.

Pamoja na hayo wanafunzi hao walemavu wameomba kuboreshewa mazingira ya
lijifunzia katika Shule yao ya Makalala, ikiwa ni pamoja na kuwajengea
chumba maalumu kwa ajili ya kujifunzia kitakachokidhi mahitaji ya kundi
hilo maalumu.

Akizungumza katika maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Mafinga, Bi. Farida Mwasumilwe alisema licha ya Serikali
kujitahidi kuboresha huduma mbalimbali kwa watu wenye ulemavu bado kuna
changamoto nyingi hivyo kuomba wadau kushirikiana kwa pamoja kuwasaidia
watu wenye ulemavu hasa watoto

Acheni Mafinga iitwe Mafinga duh!

 Wadau jana nilikuwa Mjini Mafinga kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika, nimejifunza kitu hivyo si vibaya tushirikiane. Mara nyingi kilio cha wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji vyake ni joto linalowakera wengi karibia kipindi kirefu cha mwaka, lakini kwa wanaokerwa na joto hilo si vibaya mnapokuwa mapumziko (likizo) mtembelee Mjini Mafinga kupima baridi mwanana inayopatikana eneo hilo kuanzia mwezi wa sita hadi wa nane. Leo baada ya mdau mkuu wa mtandao wa Thehabari.com kuwasili Mafinga pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha Habari Kuhusu Walemavu (ICD), tulilazimika kutafuta namna ya kuidhibiti baridi iliyokuwa ikivuma eneo hilo asubuhi kabla ya kuendelea na majukumu mengine yaliyotuleta.
Nililazimika kuvaa hivi pamoja na mdau kutoka ICD

MAADAM RITAH AJITOLEA DAMU KATIKA KITENGO CHA DAMU SALAMA MJINI DODOMA

Mkurugenzi Mtendaji wa Benchmark Production Ritha Paulsen akitolewa damu na Mkuu wa Kitengo cha Damu Salama kituo cha Dodoma Dk Leah Kitundya muda mfupi kabla ya kuanza kwa zoezi la kusaka vipaji vya wasanii chipukizi mkoa wa Dodoma, aliyeko pembeni yake ni Hawa Iche mkuu wa Mawasiliano wa Zantel

Majaji Maadam Ritah katikati Salama Jabir kulia na Paoul wakiwa kazini wakati wa kusaka vipaiji vya Bongo Star Search mjini Dodoma
Vijana wakionyesha vitu vyao mbele ya Camera wakati wa zoezi la kusaka vipaji vya washiriki wa Bongo Satr Search Mjini Dodoma

ZIARA YA NAPE KILOLO MKOANI IRINGA

  Katibu wa Halmashauti Kuu ya Taifa, CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa michezo mjini Ilula, wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
 Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa msaada wa fedha Mwalimu Beatrice Luoga, wakati alipozungumza na walimu wa mjini Mafinga, wilayani Mufindi mkoani Iringa, juzi.  Nape alimpa msaada huo kwa ajili ya kushughulikia matibabu ya maradhi yanayomsumbua mwalimu huyo, na alizungumza na walimu hao wa shule za sekondari na za msingi ili kujua changamoto zinazowakabili na jinsi CCM iliyounda serikali inavyoweza kuyatatua.
Wananchi wa Kilolo wakimshangilia Nape baada ya kuzungumza nao kwenye Ofisi ya CCM, Kilolo.
Nape akiwatuza wanakwaya wa CCM, Kilolo mkoani, Iringa walipoimba wakati wa mapokezi yake wilayani humo. Kulia ni Mbunge wa Kilolo, Profesa Peter Msolla (Picha na Bashir Nkoromo BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment