Tuesday, June 5, 2012

SERIKALI YAOMBWA KUBORESHWA SERA ZA VIJANA WASIO KWENYE SEKTA RASMI

SERIKALI imeombwa kuboresha sera amabazo zitaweza kuinua hali ya vijana wasio katika sekta rasmi ili ziwawezeshe kujikwamua kiuchumi sa njari na  kujiepusha  na vishawishi mbali mbali wanavyokumbana navyo.

Hayo yalisemwa na mkurugenzi wa shirika la kimataifa la maendeleo lisilo kla kimataifa (DSW)bw Peter Owaga alipokuwa akizungumza  na vijana wakati   wabunge wa Ujerumani walipotembelea miradi ya  vijana hao   jijini hapa.

Bw Owaga alisema kuwa sera za kuwalinda vijana wasio katika sekta isiyo rasmi ni muhimu kwa kuwa endapo itawekwa na kuboreshwa ni wazi kuwa itasaidia kupunguza makundi ya vijana wanaozurura ovyo  kutokana na kutopata ajira

“sekta iliyo rasmi ndio inayowatambua vijana wanaomaliza vyuo vikuu lakini hawa walioko kwenye sekta iliyo rasmi hawatambuliki hali inayopelekea vijana wengi kushawishika na anasa za dunia ,hivyo serikali a  ikiboresha sera  ya sekta iliyo rasmi ni wazi kuwa itawaondoa kwenye umaskini”alisema Owaga

Alieleza kuwa sekta zisizo rasmi zikitengewa bajeti zitaweza kuwasaidia vijana kujiepusha na mambo mbali mbali ambayo ndi chanzo cha kuharibikiwa katika maisha yao.

Mbali na hayo alisema kuwa viongozi nao wanapaswa kuwekeza kwa vijana na kuhakikisha kuwa wanatekeleza ahadi mbali mbali ambazo wamezikusudia kwa kuwa vijana wengi wanaumia kutokana na viongozi hao kutotekeleza ahadi wanazozitoa kwa wakati muafaka.

“endapo kama ahadi ziatatekelezeka ni wazi kuwa vijana nao watapata haki zao za msingi tofauti na sasa ambako ahadi zinatolewa tu kama kawaida na hazitekelezwi hali inayowafanya vijana kuona kwa hawathaminiwi”alisema

Hata hivyo wabunge hao ambao wako ziarani hapa Tanzania walisema kuwa wamefurahishwa na miradi ya  vijana hao walioko chini ya dsw kwa kuwa michango yao wanayoitoa inawafikia walengwa ambao ni vijana hao.
mwisho


chanzo cha habari na upako wa ufalme

No comments:

Post a Comment