Tuesday, June 5, 2012

TANZANIA YAFANIKIWA KUVUNA KILO MILIONI 224 KWA MWAKA 2011,1012




TANZANIA imefanikiwa kuvuna pamba kilo millioni 224  kwa kipindi cha mwaka 2011/2012 wakati katika msimu wa miwaka 2010/2011 kilo Milioni 163 ziliweza kuvunwa kwa mwaka hali ambayo imefanya zao hilo kuongeza thamani ya zao hilo zaidi kwa wakulima katika maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yameelezwa na Bw Marko Mtungu ambaye ni Mkurugenzi wa bodi ya pamba hapa nchini wakati akiongea na wadau mbalimbali wa zao la pamba mapema jana jijini hapa.

Bw Marko alisema kuwa ongezeko hilo la kilo za pamba linatokana na juhudi mbalimbali ambazo zinafanywa na wadau wa zao hilo kwa kushirikiana na nchi nyingine za Afrika hali ambayo imeonekana kuzaa matunda.

Aidha aliongeza kuwa kuongezeka kwa mavuno kwa zao hilo la pamba pia kumekuwa na faida kubwa sana kwa wakulima wa zao hilo kwa kuwa  wameweza kufanya zao hilo la Pamba kuwa na thamani hali ambayo nayo imechangia kwa kiwango kikubwa sana kuongezeka hata kwa ulimaji, na mauzo.

“kwa sasa nchi  hii imeweza kupata mavuno mengi sana kutokana na juhudi mbalimbali lakini pamoja na hayo yote pia kama jitiada zitaongezwa ni zaidi kuwa zao hili litaweza kuzalishwa kwa hali ya juu sana tofauti na sasa’alisema Bw Marko.

Hataivyo alitaja Nchi ambazo zinaongoza kwa kulima sana pamba kuwa ni pamoja na Nchi ya Tanzania ikifuatiliwa na nchi ya Zimbabwe wakati kwa upande wa mikoa ni Mkoa wa Shinyanga.

Naye Mkurugenzi wa shirika la viwango hapa nchini(TBS) bw Charles Ekelege alisema kuwa ili kufanya zao hilo la Pamba liwe na ubora wa kimataifa wakulima wa zao hilo wanapswa kuhakikisha kuwa wanatumia na kufuata utaratibu wa kuhakikisha kuwa wanatumia maabara za upimaji wa zao hilo

Bw Ekelege aliongeza kuwa kwa kutumia utaratibu wa kupima zao hilo utaweza kuwafanya watanzania walima zao hilo kuuza kwa ubora ambao unatakiwa katika masoko mbalimbali ya dunia.

‘ili hili zao la pamba liweze kuwa katika viwango vya kimataifa ni lazima kwanza walimaji wa zao hilo kuhakikisha kuwa wanapima ubora wa zao hili kwa kutumia njia za kisasa zaidi na wala sio kwa kutumia njia za macho kwani njia hizi za macho zinachangia sana wakulima kuuza mazao yao bila kuwa na bei maalumu hasa katika masoko ya kimataifa kwa kuwa pale wanaambiwa kuwa wauze kwa bei yoyote’aliongeza bw Ekelege.

Katika hatua nyingine alisema kuwa watanzania wanatakiwa kujiwekea utaratibu wa kuhakikisha kuwa wanapima na kutoa ubora wa mazao yao kabla ya kuingiza sokoni hali ambayo itachangia kwa kiwango kikubwa sana kukuza hata uchumi wa nchi.

Nao wadau mbalimbali wa zao hilo la pamba walisema kuwa pamoja na kuonekana kukuwa kwa kiwango cha uvunaji wa zao hilo la pamba lakini bado kuna umuhimu mkubwa sana wa Serikali kuhakikisha kuwa inatatua matatizo ambayo yapo kwenye zao hilo kwa kuwa bado kuna uwezo  kuongezeka kwa mavuno katika zao hilo


HABARI NA UPAKO WA HABARI

No comments:

Post a Comment