Tuesday, June 5, 2012

RC ARUSHA AWATAKA WATALAAM, WA MIAMBA KUPEWA MBINU MBADALA

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Magesa  Mulongo  amewataka wataalamu  wa Miamba na madini Migodini, kusaidia  wachimbaji wadogowadogo wa madini  hususani wa madini ya Tanzanite yaliopo Mererani, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kwa kuwapatia mbinu bora na za kisasa za kufanikisha uchimbaji bora.
Ameyasema jijini Arusha  wakati alipokuwa akifungua mkutano wa Chama cha Wajiolojia Tanzania (TGS), na kuongeza kuwa mbinu bora, zitaleta ufanisi zaidi katika kupata madini bora yatakayoleta  tija  kuzuaia uharibifu wa mazingira.
Mulongo alisema kuwa mbali na kufanikisha hayo Pia Jiji litanufaika na wataalamu hao kukutana Mkoani hapa, kwa sababu wanaamini watapatiwa utatuzi wa matetemeko ya ardhi, milipuko ya volkeno na uchafuzi wa maji unaotokana na kemikali za miamba na gesi za volkeno zinazotokana na  bonde la ufa kuupitia mkoa wa Arusha.
Aidha alisema kuwa hivyo ni vema wataalamu hao wakaelimisha wakazi wa Arusha namna  bora ya kukabiliana na athari hizo.
Aidha Mulongo alisema ili Tanzania iweze kunufaika na rasiliamli zilizopo kwamanufaa ya Taifa, serikali ya Tanzania  iliandaa mkakati madhubuti wa muda mrefu kwa kusomesha wazawa taaluma mbalimbali, ili wawe na uwezo unstahili wa kusimamia na kuendeleza sekta hizo za madini, nishati na maji kwa ufanisi na kwa faida ya nchi kw aujumla.
Alisema baadhi ya wazawa walionufaika na mkakati huo ni wataalamu wa Wana-jiosayansi ambao wengi wao  wamekutana katika mkutano huo, hivyo vema wakaleta changamoto  kw akuelimisha wananchi ili kukuza na kuendeleza sekta hizo ambazo kw akiasi kikubwa ni baadhi ya mihimili ya uimarishaji wa uchumi na maendeleo ya kijamii.
Pia aliomba waibue mikakati ya kukabiliana ipasavyo na majanga ya asili ya kijiolojia hususani matetemeko ya ardhi, milipuko ya volkeno na gsi chafu zitokanazo na vokeno,kemikali zinazotokana  kwenye miamba na kuchafua maji, pamoja na mionzi ya asili.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini na Nishati Tanzania,  Joseph  Kahama, alisema kuwa  sekta hiyo inakabiliwa na changamoto lukuki, lakini kubwa wamejikita kuzalisha dhahabu na vito vingine kama vile madini aina ya Alili ambayo inasemekana  Tanzania ni ya pili duniani kuw ana madini hayo kwa wingi
 Pia changamoto kubwa waliyonayo ni ile ya kuanzisha  Chuo Kikuu cha  Madini ili kuzalisha wataalamu wengi zaidi ya hawa waliopo, lakini hilo litafanikiwa iwapo serikali itasaidia kusukuma kwa haraka suala hilo.    
Alisema kuwa ili hayo yote yafanikiwe kw aharaka, ni lazima serikali kuboresha miundombinu ya reri na barabara iboreshwe ili  kurahisisha usafirishaji.
Mwisho

HABARI NA ASHURA MOHAMED ARUSHA

No comments:

Post a Comment